KWA
takribani wiki tatu sasa tumekuwa tukijadili kuhusu tabia ya baadhi ya
walimu kujihusisha kimapenzi na wanafunzi, hasa wa kiume. Nashukuru
kwamba nimepata mrejesho mzuri kutoka kwenu.
Lakini kuna mwalimu mmoja msomaji mzuri wa safu hii, yeye ni msichana
anayefanya kazi mikoani. Alinitumia ujumbe mmoja ambao ulinivutia sana,
nikabadilishana naye maneno mawili matatu na kujikuta nimepata kitu
ambacho ni lazima tushirikiane pia kujadili.
Kwanza alinipongeza kwa makala ile, lakini baadaye akaniambia kuwa
mara nyingi wanafunzi wa kike ndiyo wanaoanza kujitongozesha kwa walimu
ambao wanachokifanya wao ni kama kumalizia tu.
Aliniambia kwamba wanafunzi wa kike wakiwa mbele ya walimu wa kiume
hujishaua, wakati mwingine hata kupandisha juu sketi zao, kurembua macho
na viuchokozi vingine ili mradi tu walimu wausome mchezo.
“Sasa
anko kwa hawa walimu wenyewe vijana unategemea nini? Lakini ngoja
tuwaite sisi walimu wa kike, wanakuja wamebetua midomo, wanaonyesha
ishara ya dharau na vitu kama hivyo, mimi kwa kweli siwalaumu walimu,
mara nyingi wanalazimishwa,” alisema mwalimu huyo.
Katika kukolezea na kuniaminisha anachokisema, alinipa mchapo mmoja unaomhusu yeye mwenyewe kiasi cha kuniacha hoi kabisa.
Aliniambia kuwa hapo awali, aliishi kinyumba na mwalimu mwenzake na
walijaaliwa kupata mtoto mmoja. Kumbe jamaa kimya kimya akawa anajipigia
kabinti kamoja ka darasa la sita hapo shule waliyokuwa wakifundisha.
Dada akashtukia, ikawa bonge la msala. Huku na huku soo likafika kwa
wazazi wa mtoto ambao nao hawakukubali, ikibidi sheria ichukue mkondo
wake!
Polisi wakaipeleka mahakamani, kesi ikaanza kunguruma.
Katikati ya shughuli, mtoto wa kike akatoa mpya. Akasimama mbele ya
hakimu na wazazi wake, akawaambia kuwa yeye anampenda mwalimu, akawataka
waachane na ile kesi na kama wataendelea nayo, atajiua!
Mchezo ukaishia hapo na dada yangu akaamua kumwachia mwanafunzi wake aendelee na mzigo, yeye akashusha manyanga!
Huo ni mfano ulio hai, lakini wanafunzi huko mashuleni wanaelewa zaidi.
Ninakumbuka katika moja ya matoleo yaliyopita nilizungumzia kuhusu
hili.
Wasichana wa aina hii mashuleni wako wa aina nyingi, lakini sana
utakuta ni wale ambao hawana kitu kichwani au ambako kiasili ni wahuni.
Mungu bwana wa ajabu sana, hawezi kuwanyima vyote wanadamu. Wasichana
wasio na akili darasani hujaaliwa uzuri wa sura na umbo.
Nao hutumia uzuri wao kujiegemeza kwa walimu kwa mategemeo ya
kusaidiwa mambo wanayoamini hawayawezi. Si rahisi kukuta mwanafunzi
mwenye akili zake darasani na anayejua kitu alichokifuata shule,
akambania pua mwalimu wake kwa lengo la kumteka kimapenzi.
Na kuna hawa wanafunzi vicheche wa asili, mtaani ana mabwana, shuleni
anao, kwa ndugu zake anao ili mradi tu kila anapokwenda lazima apate
mtu. Hawa ndiyo wanaoingia katika lile kundi la kujitongozesha, ingawa
hata hivyo, wakati mwingine, mwanafunzi anaweza kumpenda mwalimu kama
binadamu ye yote anavyoweza kufanya.
Labda niwaase maanko zangu
kwamba pamoja na kuwa uhusiano wa kimapenzi haupendezi wakati ukiwa
bado shule, hasa hizi za msingi na sekondari, ni vibaya zaidi kushiriki
tendo hilo ovu na mwalimu wako.
Ni lazima tukubali kwamba kwa kufanya hivyo, moja kwa moja ni kwamba
hakutakuwa na heshima baina yenu na hapa ndipo mkazo wa masomo kwa
mwanafunzi unapowekwa kando. Mwalimu badala ya kumsisitiza mwanafunzi
wake kujisomea, atataka muda ambao alistahili kuwa akijisomea, autumie
kwa mambo yao ya mapenzi.
Nirudie tena wito wangu ambao nimekuwa
nikiutoa kila mara. Tutumie vizuri muda wetu wa shule, tukiuchezea,
tutakuja kushtuka muda umeenda. Haya mambo yote mnayotaka kuyafanya
sasa, yapo, mtayakuta na kuyaacha.
JIUNGE NA UKURASA WETU WA FACEBOOK KUPITIA HAPA >>MDADISI MAMBO