Search in This Blog

MZEE SMALL NI MZIMA, TETESI ZA KIFO CHAKE NI ZA UONGO

KUNA taarifa zilizagaa kuwa msanii mkongwe wa vichekesho na maigizo nchini, Said Ngamba ‘Mzee Small’ amefariki dunia. Taarifa hizo ni za uongo na uzushi maana mwandishi wetu ameongea na mke wa Mzee Small pamoja na Mzee Small mwenyewe ambaye ni mzima kabisa!  Mke wa Mzee Small anadai usiku kucha hajalala maana alikuwa anapokea meseji za pole kutoka kwa watu mbalimbali kuhusu taarifa hizo za uzushi. Mzee Small mwenyewe amesema: "Mimi ni mzima kabisa japo bado nasumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi (stroke)"
Mzee Small akiwa na mkewe.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger