STAA wa Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ juzikati ameweka wazi nia yake ya kusaka mtoto, Risasi Mchanganyiko linakushushia.
Akizungumza na mwandishi wetu Desemba 9, mwaka huu jijini Dar, Linah
alisema tangu alipoingia kwenye muziki hakuwahi kufikiria kushika
ujauzito kwa kuwa alikuwa bado hajajiandaa kufanya hivyo.
Nyota huyo ambaye aliwahi kuzama katika penzi zito la staa
mwenzake, Amin Mwinyimkuu alisema kuwa kwa sasa hali ni tofauti na
anataka kuzaa iwapo atashika ujauzito.
“Nilipokuwa katika uhusiano wangu wa kwanza hakuna hata siku moja
niliyohisi kama nitakuja kutamani kupata mtoto maana mwenzangu
aliponiambia tuzae nilimkatalia tofauti na leo hii natamani nishike
mimba na ulimwengu wote ujue kwamba nina mimba,” alisema Linah.
Hata hivyo Linah alikwepa kuweka wazi uhusiano wake wa sasa na hakutaka kumwongelea Amin.