ACHANA na mabifu yaliyotangulia, hili ni jipya kabisaa! Msanii wa
sinema na Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ameingia kwenye bifu zito na
Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ na kudai staa huyo wa Wimbo wa
Number One ni mzinzi ‘fuska’, Amani lina mkanda mzima.
Bila kumung’unya maneno, mapema wiki hii, Baby Madaha alimvaa Diamond
ambaye ni Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB) akimtuhumu kuwa na tabia za
kifuska.
Baby Madaha alidai hata muziki anaoufanya Diamond kamwe
hauwezi kulingana na mafanikio makubwa ya jina lake zaidi ya kubebwa na
skendo tu.
CHOKOCHOKO ZILIVYOANZA
Kupitia mitandao ya
kijamii, ilivuja posti ambayo ilidaiwa kutoka kwa Baby Madaha ikimpaka
Diamond kuwa siyo mwanamuziki kama ilivyo kwa wasanii wengine wenye
uwezo mkubwa, akitolea mfano Elias Barnaba wa THT.
Sehemu ya posti
hiyo ilionesha kuwa, Diamond si msanii wa muziki bali ni mzinzi f’lani
hivi anayefanya biashara ya muziki kupitia mapenzi.
“Siku wanawake maarufu nchini Tanzania watakapojitambua na kuacha
kulewa penzi la Diamond, huo ndiyo utakuwa mwisho wa maisha yake
kimuziki kwa sababu hatakuwa na jipya na hivyo soko lake litaporomoka,”
ilisomeka posti hiyo.
UKWELI NI UPI?
Baada ya ishu hiyo kugeuka habari
ya mjini na kuibuka kwa makundi mawili yanayokinzana, Amani lilimtafuta
Baby Madaha ili kujua ukweli wa posti hiyo ndipo akatiririka aya za
kuthibitisha kuwa picha haziivi, hamkubali Diamond na kudai hata
kimuziki hamkubali kwani anaamini wapo wanamuziki wanaofanya vema katika
gemu kuliko yeye.
“…tuseme ukweli, Diamond ni mfanyabiashara siyo mwanamuziki. Kuhusu
hiyo posti iwe ni mimi nimeandika au si mimi lakini kimsingi hayo maneno
yanamstahili kabisa. Mzinzi tu.
“Diamond anabebwa na media (vyombo vya habari). Kuna wanamuziki wengi wazuri sembuse yeye? Ana nini haswa?” alihoji Baby.
AMANI LAMGEUKIA DIAMOND
Baada ya kusikia maelezo
ya Baby kwa kifupi, Amani lilimuweka ‘pending’ kwa muda na kumwendea
hewani Diamond ili liweze kujua upande wake analizungumziaje bifu hilo
ambalo lilikuwa likienea mitandaoni kama moto wa kifuu.
Tofauti na
matarajio ya mapaparazi wetu kwamba huenda angejibu mashambulizi makali
kwa Madaha, Diamond au ‘Sukari ya Warembo’ aling’aka huku akimponda
mwanadada huyo na kumshangaa:
BOFYA HAPA KUMSIKIA
“Daaah! Huko ni
kunishusha…mimi na huyo (Baby) wapi kwa wapi kamwe huwezi kunilinganisha
na mtu ambaye yupo chini yangu sana, nikijibizana naye nitajishusha tu.
Ingekuwa ni mtu mkubwa mwenye levo yangu hapo ningesema natakiwa kusema
neno.
“Hana lolote huyo anatafuta ‘kiki’ tu kupitia mimi, nipo na
dili zangu za maana nipoteze muda kwake? Atafute wa levo yake na wala si
mimi.”
UZINZI VIPI?
Alipoulizwa kuhusu suala la uzinzi
ambalo Baby Madaha aliumaanisha katika posti yake, Diamond aliendelea
kukazia kuwa hana muda wa kupoteza kwa mtu kama Baby Madaha ambaye
kimsingi ni kama ardhi na mbingu.
“Huyo anatafuta kiki tu, aachane
na mimi…mbona hatufanani kabisa mimi na yeye wapi kwa wapi?” alikazia
Diamond a.k.a Weka Mbali na Watoto Wazuri wa Kike.
BABY AREJEA HEWANI
Wakati mapaparazi wetu
wakimalizana na Diamond, kilongalonga kimoja cha paparazi wetu kilikuwa
kikionesha kinaita, ilivyokatika ya Diamond, Baby akapanda hewani kwa
mara nyingine.
Safari hii alimchana laivu: “Nimeisoma upya posti yenyewe, kilichopo
humu ni ukweli mtupu. Hakuna hata tone la uongo, wewe utamlinganisha
Diamond na mtu kama Barnaba? Huyu ni mfanyabiashara tu, hajui kuimba kwa
kutumia vyombo kama mimi.
“Diamond hawezi kupiga chombo hata kimoja cha muziki atajiitaje mwanamuziki? Anastahili kabisa ujumbe huu.”
UFUSKA
Mapaparazi wetu walilazimika kumtwanga
swali Baby Madaha kuhusiana na ufuska ambao ulikuwa umetajwa katika
maelezo ya awali, kama endapo Diamond ni mzinzi au yeye ndiyo mzinzi.
Katika maelezo yake, Baby Madaha aliwashangaza mapaparazi wetu kwa kutaja namna gani anaweza kumuita Diamond mzinzi. Sikia:
Amani: “Umesema Diamond si mwanamuziki, je, suala la uzinzi ni nani analo kati yako na yeye?”
Baby: “Mimi si mzinzi. Diamond ndiyo mzinzi tena sana tu.”
Amani: “Uzinzi wake upo wapi?”
Baby: “Kitendo cha kubadilisha wanawake, kufumaniwa na Wema Sepetu akiwa na Jokate Mwegelo ndiyo uzinzi wenyewe huo.”
Amani: “Kwani wewe hujawahi kuwa na wanaume tofauti? Hujawahi kufumaniwa?”
Baby: “Mimi sijawahi, yeye amewahi na hakuwahi kukanusha hivyo
inadhihirisha kuwa ni kweli. Kwangu mimi kila aliyetajwa kutoka na mimi
kama haikuwa kweli, nilikanusha mara moja yeye mbona hakanushi?”
Amani: “Kwani Diamond alifumaniwa na nani?”
Baby: “Acha hizo, kwani hukumbuki kipindi cha Wema? Mara alinaswa na Aunt mara na… yule ndiyo mzinzi sasa.”
KWANI WALITONGOZANA?
Kuhusu suala la kutongozwa,
Baby alisema Diamond hajawahi. Cha kushangaza zaidi, alisema hata kama
ikitokea siku staa huyo akamtongoza kamwe hawezi kumkubalia kwani
hawaendani hata kidogo.
Alisema yeye ni mtu wa kutembea na vigogo na si vitoto kama Diamond.
“Hana hela, kamwe siwezi kumkubalia. Ni mtu ambaye ana vihela mbuzi
sasa mtu kama yeye mimi wa nini? Ndiyo maana aliwahi kukimbiwa na
mwanamke kwa kuwa hana hela.
“Tena yule mwanamke akaenda kwa kigogo
mwenye hela, mimi na yeye ni mbalimbali kabisa. Hata muziki ninaofanya
hauwezi, mimi ninaimba RnB yeye anafanya Pop, tuko tofauti kabisa,”
alisema Baby pasipo kumtaja mwanamke aliyemkimbia Diamond.
TUJIKUMBUSHE PANDE ZOTE
Diamond aliwahi
kuripotiwa kutoka kimapenzi na ‘totoz’ kibao wakiwemo yule wa mwanzo
aliyemzingua aitwaye Sarah, Rehema Fabian, Jacqueline Wolper, Upendo
Mushi ‘Pendo wa Maisha Plus’, Wema Sepetu, Natasha (Video Queen wa Wimbo
wa Moyo Wangu), Najma (aliwahi kuwa mpenzi wa Mr. Blue), Jokate
Mwegelo, yule demu wa Kenya na aliyekuwa mwigizaji aliyefulia ambaye ni
mke wa mtu.
Kwa upande wake Baby Madaha anayekimbiza na ngoma yake ya Summer
Holiday naye si haba kwani aliwahi kuripotiwa kuminya kimapenzi na yule
mtoto wa mwanasiasa maarufu Bongo (jina lipo), Mwisho Mwampamba, Dokta
Pakir, Juma Nature na Joe Kairuki aliye naye sasa ambaye ni mume wa mtu.