Msanii wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ anadaiwa kulipasua Kundi
la Bongo Movie kutokana na uchaguzi wa kundi hilo unaotarajiwa
kufanyika leo katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar, Ijumaa
lina habari kamili.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, baadhi ya wasanii wa filamu wanaounda
kundi hilo wanadai Ray hafai kuliongoza kutokana na skendo ya
kuwagonganisha mademu inayomtafuna huku wengine wakimuunga mkono.
“Kuna baadhi yetu wamekuwa wakikaa vikao ili kutaka kumweka pembeni
Ray kwa kuwa ameshindwa kuleta umoja ndani ya Bongo Movie na amekuwa
akifanya mambo yasiyokubalika…” alisema mmoja wa wasanii ambaye hakutaka
kutajwa jina lake gazetini.
Chanzo hicho kimesema kwamba wasanii wasiomtaka Ray wamekuwa wakiweka
vikao usiku katika kumbi mbalimbali za burudani za jijini Dar kwa ajili
ya kumng’oa kwenye cheo hicho.
Wasanii wanaomkubali Ray wanadai anastahili kuendelea kuliongoza
kundi hilo kwa kuwa ana msimamo thabiti na hakuna mwingine anayeweza
kuliongoza.
Msanii wa filamu za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere, amesema
uongozi wa Ray unafika kikomo na wanatakiwa kumchagua kiongozi mpya au
kuendelea naye na jukumu hilo liko mikononi mwa wasanii wenyewe.
“Kimtazamo Bongo Movie linaenda vibaya na hii siyo kwa sababu ya Ray,
bali wasanii wote ni jukumu letu kulijengea heshima kundi hilo, katika
uchaguzi wa leo Ray anaweza kuchaguliwa au asichaguliwe kwani kura ni
demokrasia…” alisema Steve Nyerere.
Ray hakuweza kupatikana mara moja kuuzungumzia mpasuko huo ndani ya Kundi la Bongo Muvi.