Search in This Blog

TASWIRA YA MJI WA MWANZA BAADA YA WAMILIKA WA MADUKA KUGOMA KUFUNGUA MADUKA YAO, KISA MASHINE ZA TRA

Maduka mengi ya jijini Mwanza jana yalikuwa yamefungwa kutokana na mgomo wa wafanyabiashara waliokuwa wakipinga mashine za kielektroniki kutoka TRA.
Kamera ya GPL jana ilinasa maduka mengi ya jijini Mwanza yakiwa yamefungwa kutokana na mgomo wa wafanyabiashara wakigomea mashine za kielektroniki kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kama ilivyokuwa maeneo ya Kariakoo jijini Dar katika miezi michache iliyopita, hali imekuwa hivyohivyo katika mitaa ya Mwanza ambapo pia wafanyabiashara wameamua kuingia kwenye mgomo wa kufunga maduka yao kushinikiza kushuka kwa bei za mashine hizo za Elektroniki.
Maeneo yaliyoathirika zaidi kwa mgomo huo ni maeneo yote ya Mwanza mjini na maeneo yote yanayozunguka jiji hilo.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger