Search in This Blog

WHITE HOUSE YAZUIA TALAKA YA OBAMA KWA MKEWE



Obama akiwa 'busy' na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt wakati wa mazishi ya Mandela Afrika Kusini.
WASHINGTON, Marekani
NDOA ya Rais Barak Obama na mkewe Michelle haitaweza kuvunjika kwa sasa kwa vile mke huyo mrembo atatakiwa kuendelea kuishi katika Ikulu ya White House hadi mumewe atakapomaliza muhula wake wa pili wa uongozi mwaka 2016.

Kwa mujibu  wa vyanzo mbalimbali, Michelle, mama wa watoto wawili, Sasha na Malia, hata kama ataachika atalazimika kuendelea kubakia ikulu kwa ajili ya mahitaji ya kuwa pamoja na mumewe katika hafla za kiserikali zinazohitaji uwepo wa mke. Hiyo ndiyo sera ya Ikulu ya Marekani.
Juzi, Gazeti la The Nation la Marekani liliripoti kuparaganyika kwa ndoa hiyo iliyowahi kutajwa kama ndiyo bora zaidi duniani, kwa kile kilichoelezwa kuwa kuchukia kwa Michelle baada ya kumwona mumewe akishoboka na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt  wakati wa shughuli za kumuaga rais wa zamani wa Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela ‘Madiba’.
Vyanzo katika mitandao mbalimbali vilisema ndoa hiyo ilikuwa inawaka moto kwa muda mrefu na kwamba hata kabla Michelle hajaanza kuishi katika jengo la peke yake katika viwanja hivyo vya ikulu, walikuwa wakilala ‘mzungu wa nne’.
Mwaka 2012, uvumi ulisambaa kwa kasi duniani ukielezea kutengana kwa watu hao wawili maarufu zaidi, hali iliyosababisha Ikulu ya Marekani kukanusha taarifa hizo.
Hata hivyo, hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na ikulu, Obama wala Michelle juu ya madai ya kutengana kwao.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger