Facebook, Twitter na Instagram ndio
mitandao ya kijamii inayotawala maisha ya mtandaoni kwa watu wengi
duniani. Hadi sasa Facebook ina watumiaji bilioni 1 duniani kote,
Twitter ikiwa na watumiaji milioni 250 na Instagram ikiwa na watumiaji
milioni 150.
Hata hivyo, takwimu zinazonesha kuwa
Instagram inakua haraka zaidi kuliko Twitter na utumiaji wake kwa sasa
ni mkubwa kuliko Twitter. Ikumbukwe kuwa vita kati ya Twitter na
Instagram ilianza December mwaka jana baada ya Instagram inayomilikiwa
na Facebook, kuacha kushirikiana na Twitter.
Kabla ya hapo, watu walikuwa na uwezo wa
kuona picha za Instagram kirahisi kupitia Twitter hivyo Twitter ilikuwa
inapata watumiaji wengi Instagram. Baada ya urahisi huo kuondelewa,
watumiaji wengi wa Twitter wamejikuta wakiitumia zaidi Instagram.
Kwa mujibu wa ripoti, Twitter inapata
shida zaidi kwa kupigwa chini na Instagram ambayo imeendelea kuneemeka
tu. Kuna ubadilishanaji picha wa asilimia 59 tu kwenye Twitter
ukilinganisha na asilimia 98% kwenye Facebook.
Tangu Instagram iache kusupport picha
kwneye Twitter, mtandao huo umepata pigo kubwa kwa kupungua kwa matumizi
ya picha huku Instagram kwa upande mwingine ikiendelea kukua ambapo
ongezeko la followers limefika 41%.
Kwa utafiti wa kawaida tu na hata hapa Tanzania, utagundua kuwa kumekuwepo na watumiaji wengi mno wa Instagram.
Mastaa wa Tanzania wameonekana kuvutiwa zaidi na kuwa ‘active’ kwenye mtandao huo kuliko Twitter wala Facebook.
Kuna mastaa wengi ambao huwezi kuwaona
Facebook wala Twitter lakini wako active zaidi Instagram. Kwa mfano kuna
waigizaji wachache sana wa filamu Tanzania wanaotumia mtandao wa
Twitter lakini wakiwa na followers wengi Instagram.
Sababu kubwa zinazochangia Instagram
kupendwa zaidi ya Twitter na Facebook kwa mazingira ya Tanzania ni ule
urahisi wa kuweka picha nyingi bila ulazima wa kuweka maelezo mengi na
ile imani kuwa picha huongea maneno mengi kuliko maandishi kama ilivyo
kwenye Twitter na pia Facebook ikiwa imetawaliwa na watu aina mbalimbali
wakiwemo wakorofi na wanaopenda kutukana watu.
“Mi naweza kusema kwamba Instagram ni
sehemu unayoweza kuona how crazy stars can be,” anasema Wema Sepetu
kujibu swali la kwanini anapenda kutumia zaidi Instagram kuliko Twitter.
“Watu wengi ambao nawafollow on Instagram ni macelebrities wa nje. So I
follow people like Ellen Degeneres, I follow Soulja Boy, I follow 50
Cent, I follow Kim Kardashian, I follow the Kardashians, Nicole Ritchie,
Rihanna. This is the only place ambayo ninaweza kuwaona how crazy they
can get, it’s kila mtu amekuwa an ‘Instagram freak’ right now. Through
profile ya mtu ya Instagram, unamjua mtu alivyo. It’s very hard to tell
from Twitter cause it’s just mtu anaandika tu, ‘sasa hivi niko wherever’
anaweza akadanganya. Lakini kwenye Instagram, you can actually tell
‘Yeah nimeenda sehemu fulani nimepiga picha I’m here, nimepiga picha
chakula changu, I am eating’ it’s just interesting.”
Kwa upande wake muigizaji wa filamu,
Irene Uwoya anaamini kuwa mtandao wa Facebook ni kama daladala ambako
kuna fujo za kila aina na ndio maana anaipenda zaidi Instagram kwakuwa
watuamiji wake wengi ni waelewa.
“Facebook imechafuka sana,”anasema.
Matusi, watu waandika vitu vya ajabu yaani changanyikeni, kila mtu yupo
Facebook. Naweza nikatolea mfano kama usafiri, basi Facebook ni
daladala. Instagram ni latest, kama ni gari basi ni Range new model,
kama langu. Watu wanaoingia Instagram ni watu wa ukweli, watu wanaoingia
huko ni wenye akili zao timamu, japokuwa kuna wachache waliotoka huko
huko kwenye Facebook wanakuja kuchafua Instagram.
Irene anasema maudhi ya Facebook yalimfanya ajiondoe muda mrefu uliopita na wala hana akaunti tena.
“Kuna watu wanajifanya mimi sasa kwenye
Facebook, wakati mimi sipo Facebook toka siku nyingi. Kuna akaunti kama
saba za kwangu kila mtu ananiambia ‘nimekutumia meseji Facebook’
nawaambia ‘bwana mimi Facebook nilishatoka.”
Kwa upande wa Jokate Mwegelo, Twitter, Facebook na Instagram yote ni mitandao muhimu kwake.
“Mimi kotekote. Twitter napenda zaidi
kuongeza mambo ya current affairs etc. Instagram picha zaidi na Facebook
natoa mawaidha,” anasema.
Hata hivyo wataalam wanasema ingawa
namba zinaonesha kuwa ni vizuri kuitegemea Instagram kwa sasa, watumiaji
wa mtandao hawapaswi kusahau kuwa vitu vingine muhimu vinavyofanywa na
Twitter. Mtandao huo hutoa vifaa zaidi ya kusambaza picha. Kwa biashara
na watumiaji wa kawaida kuweza kuwafikia vizuri walengwa wao, wanatakiwa
kupitia tena mikakati yao kwa kuchunguza mitandao mbalimbali ya kijamii
kwa matumizi yanayofaa.
Pamoja na watu wengine kuanza kuikimbia
Facebook kwa kuwepo na watu wengi wanaoitumia vibaya, bado imeendelea
kuwa jukwaa muhimu linalotumiwa na makampuni, mashirika, viongozi na
watu mashuhuri kuwasiliana na wateja ama mashabiki wao kwa haraka na kwa
njia inayowafikia watu wengi.