Search in This Blog

"WASANII WA BONGO WAMESHINDIKANA KWA KILA KITU".....MAYA

 
Mayasa Mrisho ‘Maya’.
MSANII wa filamu, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amejikuta ‘akiponyokwa’ na sentensi tata kwa kudai wasanii wengi linapokuja suala la ‘kuponda’ raha wamekuwa vinara hivyo wameshindikana.
Akipiga stori na Ijumaa ndani ya viwanja vya TCC Club Chang’ombe jijini Dar huku akimuegemea msanii mwenzake, Shamsa Ford mwishoni mwa wiki iliyopita, Mayasa alisema starehe imechukua sehemu kubwa ya maisha ya wasanii wengi na kwamba hakuna anayeweza kubadili staili hiyo ya maisha.
“Ila sisi wasanii tumeshindikana kwa starehe jamani, lakini hata hivyo kutokana na ugumu wa kazi zetu tuna haki ya kupumzisha akili kama hivi, acha tule raha bwana,” alisema Maya huku akigonganisha ‘chiaz’ na wasanii wenzake.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger