Search in This Blog

HUU NDIO UHUSIANO WA JACKIE CLIFF NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA (UNGA)

Jackie Cliff… mrembo wa haja niliyeanza kumfahamu kwenye video ya She Got A Gwan ya Ngwair. Ni msichana aliyeenda hewani na Mungu kampelea haswaa. Ukikutana naye huwezi kumwangalia mara moja ukaridhika, lazima ugeukE kumwangalia tena.
85a7de969c6911e29c2822000a1fbe4c_7
Nilipata bahati ya kumhoji mwezi September mwaka jana kwenye fashion show ya Ally Rehmtullah iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam na katika maongezi yetu kuhusu Ngwair na kazi yake kama mrembo wa video nikagundua kuwa, Jackie ni msichana mpiganaji asiyejali kitu.
Jackie The Boss Lady, ni msichana anayejulikana kwa kuishi maisha ya kifahari yakiwemo kuendesha magari ya gharama ambayo wengi yaliwapa maswali mengi, ni wapi anapata fedha hizo? Ni kweli fani ya urembo inalipa hivyo? Sijasahau pia kuwa aliyekuwa mume wake, ni miongoni mwa madon wa Dar na ambaye alifungwa kwa miaka kadhaa kwa shutuma zile zile za sembe.
Huenda fedha alizokuwa akizitumia na kuziumiza roho za watu wengi zilikuwa za mume wake ama tayari alikuwa ameshaanza kufanya biashara hiyo haramu na ya hatari kabisa duniani.
Ni ngumu kujua nani aliyemuingiza Jackie kwenye biashara hiyo lakini uhakika mkubwa ni kuwa aliingizwa na mtu wake wa karibu, mume ama mpenzi wake. Kwa lugha nyingine ni kwamba, nyuma ya wasichana wengi wanaofanya biashara hii, wapo wanaume, madon wenye nguvu, madaraka, connection na fedha nyingi ambao si rahisi kuwafahamu. Hata wale wanaofahamika, ni nguvu kuthibitisha tuhuma hizo kwakuwa si wao wanaosafiri.
Kwa mtu kama Ray C, ambaye kukamatwa kwa Jackie hakumshtui hata kidogo kutokana na jinsi anavyowachukia wafanya biashara wa sembe, naamini anapata hasira kufahamu ukweli huu kwamba, wasichana hawa wanatumiwa tu.
Kuna watu wakubwa nyuma yao. Matajiri wakubwa katika nchi hii ambao ukitaka kuwajua, unaweza kujikuta pabaya hasa kama unaishi kwenye nchi kama Tanzania ambayo fedha inaongea kuliko haki na rushwa imetawala. Ni rahisi kudeal na majambazi kuliko kudeal na wazee wa unga. Wale waliojaribu wanajua vitisho walivyovipata. Biashara ya unga ni hatari kwa vijana wengi wa Tanzania na wauzaji wanajua hilo, lakini kamwe hawawezi kukubali kuona unawaharibia ugali wao.
Akina Jackie, Agnes na wengine, ni mfano tu wa wasichana wengi warembo na mastaa wa Tanzania wanaotumiwa kwenye biashara hii haramu. Wapo wengi, wanaume na wanawake, wenye majina na wanaofanya kazi hii. Naamini siku moja atakuja kukamatwa mtu asiyetegemewa kabisa na kila mmoja atabaki mdomo wazi.
2cf9b6de719811e3be8c12db5299872b_7
Pengine kinachowaponza wasichana wengi, ni kutaka kuishi maisha yasiyo yao. Hupenda kuishi maisha ya anasa na starehe. Kwa mji kama Dar es Salaam na maisha fake ya Instagram yanayooneshwa na wasichana wengi wa Kibongo, inahitaji moyo kwa msichana mrembo kuvumilia kuishi maisha ya kawaida.
Na ndio maana, wengi hujikuta kwenye himaya za wauza unga ambao pamoja na kuwageuza chombo cha starehe zao za kimwili, huwaingia kwenye biashara hizo hatari na hata kama uhusiano ukiisha, wengi hushindwa kujitoa.
Wakati ambapo kila mtu anamsema vibaya Jackie na kumkejeli kwa kila neno, tujikumbushe kuwa, nyuma yake wapo watu wazito na hatari zaidi. Jackie kafundishwa tu kuvua samaki na aliyemfundisha haoni shida kutafuta msichana mwingine wa kuziba pengo hilo na biashara itaendelea.
Kama ilivyo kwa Jackie na hata kwa Agnes Masongange, ukifanikiwa kuufuatilia mlolongo wa wahusika, ni lazima ukufikishe kwa mtu mzito anayewapa kazi hizo. Kwakuwa safari moja tu ya kupeleka ama kuleta madawa nchini na iliyofanikiwa inaweza kubadilisha maisha yao kabisa, wasichana wengi warembo wameshindwa kukataa ofa hizo.
Hujiulizi kwanini wanaotumiwa kwenye safari hizi karibu wote ni wasichana warembo?

Kwa muda mrefu, kumekuwepo uhusiano mkubwa kati ya urembo na biashara hiyo. Si Tanzania tu, bali ni duniani kote.
Hii ni kwasababu ni ngumu kuhisi ‘uharamu’ wowote kwenye sura nzuri ya msichana na tena anayejulikana kwa kazi nyingine tofauti. Kama ya ulimbwende.

Swali la kujiuliza, ni kwanini madon hawa huwatumia zaidi warembo wa video ama Mamiss? Hadi sasa watatu wanafahamika kunaswa na mtego. Binti Kiziwi ambaye amefungwa nchini China, Jackie Cliff ambaye naye kifungo kinamngojea na Agnes Masogange ambaye kesi yake iligeuka kuwa nyepesi na kuhukumiwa kulipa faini tu.
Hii ni mifano ya jinsi uhusiano kati ya urembo na usafirishaji wa madawa ya kulevya ulivyo.
Angie Sanclemente Valencia ni mfanyabiashara wa madawa ya kulevya nchini Colombia. Alianza kama mlimbwende na kushinda shindano la ‘Reinado Nacional del Cafe’ lakini alishika taji hilo kwa siku mbili tu na baadaye kupokonywa baada ya kubainika kuwa alikuwa ameolewa. Kuanzia hapo akaingia kwenye biashara hiyo.

Inaamina kuwa Valencia aliingia kwenye biashara hiyo baada ya kuwa na uhusiano na don mmoja wa madawa wa nchini Mexico. Walipoachana, alichukua ujuzi wote aliojifunza kwa mumewe na kuendelea na biashara mwenyewe.
Aliajiri mamodel na kuanza kuwatumia na kuwalipa $5,000 kwa kila safari ya kubeba cocaine kutoka Argentina kwenda Uingereza. Angie alikuwa akiwaita wasichana hao ‘malaika’ kwa kigezo kuwa ‘pretty girls pass easily through customs’ (wasichana warembo huvuka mipaka kiurahisi). madawa Angie baada ya kukamatwa
Baada ya msichana mmoja kati ya hawa kukamatwa, alikisanua na Valencia alikamatwa mwaka 2010 na kufungwa miaka 6.
Miss Sinaloa 2008 (eneo la Mexico maarufu kwa biashara ya unga) Laura Zuniga, alikamatwa mwaka 2010 akiwa na wanaume saba wakiwa na madawa ya kulevya.
gal-zuniga-6-jpg Laura Zuniga
Mrembo mwingine aitwaye Maria Susana Flores Gamez aliuwa mwaka juzi baada ya tukio la kurushiana risasi na wanajeshi nchini Mexico.
maría_susana_flores_gámez Maria Susana Flores Gamez
Mrembo huyo alikuwa akisafiri na kundi la wauza unga hatari nchini humo. February mwaka 2012, Flores Gamez alivishwa taji la Woman Of Sinaloa na pia alishiriki kwenye mashindano mengine saba makubwa. Kama angeendelea angekuja kugombea taji la Miss Mexico na kisha Miss Universe lakini badala yake Maria aliishia kujihusisha na biashara hiyo haramu.
“Kuna uhusiano kati ya biashara ya madawa ya kulevya na mashindano ya urembo,” aliandika Javier Valdez kwenye kitabu chake cha mwaka 2009 kiitacho ‘Miss Narco’ kilichoangalia uhusiano kati ya biashara hiyo na walimbwende.
“Ni suala la uhuru, nguvu, pesa lakini pia suala la mahitaji,” alisema Valdez.

“Kwa wasichana wengi ni rahisi kujiingiza kwenye matukio haya kwenye nchi ambayo inatoa fursa kwa vijana.”
Mtandao wa panoramas.pitt.edu uliandika makala iitwayo ‘Narcotrafficking and Beauty Queens’ kuangalia uhusiano huo pia.

Mfanyabiashara mmoja wa Colomboa aliliambia gazeti la ‘El Nuevo Herald’ sababu za wasichana warembo kujihusisha na biashara hiyo na kusema kuwa wengi huingia kupitia wapenzi wao, nguvu na status. Kingine wanawake wameonekana kumudu zaidi usafirishaji wa madawa ya kulevya na hivyo wafanyabiashara wengi hupenda kuwatumia.
Sababu ni kwamba, urembo hufukuza kushtukiwa na kwamba wanawake wanaweza kupitisha madawa kwa urahisi kuliko wanaume. Kwa sasa wanawake wameendelea kutokea kwenye orodha ya watu wanaotafutwa sana nchini Marekani, Mexico na Colombia.
Mtindo huu unaokua miongoni mwa wanawake na usafirishaji wa madawa ya kulevya, unachangia katika tatizo la kitamaduni lililopo la wanawake kuamini kuwa urembo na mvuto wa kimapenzi vinatakiwa kutumika kupata status na nguvu. “Stories, television shows and music exacerbate the normalization of women entering the world of illegal narcotics by the allure of lavish lifestyles,” uliandika mtandao huo.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger