Search in This Blog

MPENZI WAKE JACKIE CLIFF AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA BAADA YA MPENZI WAKE KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI CHINA


Muimbaji wa kundi la Wakacha, Jux amefunguka kwa mara ya kwanza tangu mpenzi wake Jackie Cliff akamatwe na madawa ya kulevya aina ya heroin huko Macau, China, December mwaka jana.



Jackie alikamatwa na madawa hayo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 220 akitokea Thailand.

Jux ambaye hajawahi kuuweka wazi uhusiano wake na Jackie jana alipost picha akiwa amekaa nje ya gari lililo mlango wazi huku akiwa amejiinamia na kuandika: Kila kitu kinatokea kwa sababu kwenye maisha.”

Hadi sasa hatma ya Jackie nchini China haijulikani na bado anashikiliwa napolisi. Kuna uwezekano mkubwa akafungwa jela huko huko.

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger