Search in This Blog

RAIA WA NIGERIA AKAMATWA UWANJA WA NDEGE AKIINGIZA MADAWA YA KULEVYA NCHNI


RAIA wa Nigeria, Okwubili Agu (40), amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) akiwa na pipi 71 za dawa za kulevya aina ya heroin, zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 54, alizokuwa amezimeza tumboni.
Kamanda wa Polisi wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Nzowa alisema jana kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi majira ya saa 4 usiku katika uwanja huo. Nzowa alisema kuwa mtuhumiwa huyo 
alikamatwa na Kikosi Kazi kinachofanya kazi katika Uwanja huo, akiwa katika harakati za kusafiri na ndege ya KLM kwenda Amsterdam, Uholanzi.
Credit:HabariLeo
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger