Search in This Blog

BANZA: MWAKA HUU AFYA YANGU NI NZURI SASA NAFUNGA MWEZI MZIMA

TOFAUTI na mwaka jana ambapo msanii wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ hakuweza kufunga, mwaka huu amesema anafunga mwanzo mwisho mpaka mwezi mtukufu uishe.
Msanii wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’.
Akistorisha na Ijumaa, Banza alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa mwaka huu ameweza kufunga kwani mwaka jana alishindwa kufunga hata siku moja kutokana na afya yake kutokuwa vizuri.
“Nashukuru mwaka huu naweza kufunga kwani mwaka jana nilishindwa, na hivi niko nyumbani tu najipanga sijajua baada ya mfungo nitaenda kwenye bendi au laa ila nataka nipumzike kwanza muziki,” alisema Banza.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger