Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka hivi karibuni aliamua
kumkimbia mumewe Malick Bandawe, kisa mfungo wa Ramadhani ambapo sasa
anaishi Kigogo na mama yake mzazi.
Akipiga stori na Ijumaa, Rose alisema amelazimika kwenda nyumbani
kwao ili kumpisha mumewe atimize nguzo hiyo ya Uislam bila kipingamizi
kutokana na kutokufunga ndoa.
“Mimi sifungi hivyo nimeona pia ni jambo la busara kumpa nafasi
mwenzangu kwa ajili ya kufanya ibada hiyo, mwezi ukiisha nitarudi na
maisha yetu yataendelea kama kawaida,” alisema Rose ambaye awali alikuwa
akiishi na mumewe huyo Tandale jijini Dar.