Search in This Blog

HUU NDIO MKWANJA ULIOMTOKA DIAMOND KUNUNUA GARI LA ZAWADI YA MAMA YAKE

Habari zinazo-make headlines hivi sasa kila kona ya media hapa town ni tukio la mkali wa AfroPop Diamond Platnumz kumzawadia mama yake zawadi ya gari aina ya Toyota Lexus, huku mama yake akiwa anatimiza miaka 55 ya kuzaliwa kwake, Diamond Platnumz inasemekana ilimtoka kitita cha shilingi milioni 38(38,100,000/-) kuweza kununua usafiri huo kama zawadi kwa mama yake mzazi, ambapo mil.35 imetumika kulinunulia gari hilo mpaka kuingia Tanzania na Milion 3.1 imetumika kulipamba na kuweka Music System pamoja na seat Cover. .90bdy
Diamond Platnumz kwa bahati mbaya hakuwa katika eneo la tukio kutokana na kuwa safarini huko marekani, ila mama yake alionekana kufrahi sana hadi kutokwa na machozi kwa surprize hiyo, jambo lililomfanya Diamond mwenyewe kufunguka na kusema kuwa chozi lilimtoka alipomuona mama yake akiwa analia kwa furaha namna hiyo.Siku hiyo hiyo iliambatana na suprize kwa fans wake kwa kudondosha pia video zake mpya mbili.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger