KLABU ya Arsenal baada ya kumalizana kwa dau la Pauni Milioni 22 na
Gonzalo Higuain kutoka Real Madrid, sasa inahamishia nguvu zake kwa
mshambuliaji wa Manchester United, anayeuzwa Pauni Milioni 20, Wayne
Rooney - huku kocha Arsene Wenger akiwa amedhamiria kuendelea kumtumia
katika nafasi ya kiungo mshambuliaji nyuma ya Muargentina huyo.
Higuain ni mchezaji ambaye Arsenal sasa wana uhakika wa kumnasa, huku
Carlo Ancelotti kocha mpya wa vigogo hao wa Hispania, akitarajiwa kutua
leo kuthibitisha kuondoka kwa mchezaji huyo Bernabeu.
Matawi ya juu: Lakini mustakabali wa Wayne Rooney bado haueleweki
Lakini katika uhamisho huo wa Rooney, Arsenal italazimika kumlipa
mshahara wake wa Pauni 220,000 kwa wiki, ambao ni mkubwa mno kulingana
na tamaduni za Arsenal, imekuwa klabu 'bakhili'.
Wenger haoni kama Rooney ni mshambuliaji wa kati, lakini kama
kiunganishi, baina ya kiungo na Higuain nafasi ambayo mchezaji mwenyewe
amesema inamfaa.
Lakini Chelsea pia inamtaka Rooney na kocha mpya wa United, David Moyes
anatarajiwa kukutana na Rooney wiki mbili zijazo, hivyo uwezekano wa
yeye kujiunga na klabu hiyo ya London bado mdogo.
United haitataka kumuuza Rooney kwa Chelsea, ambao wanatarajiwa kuwa
washindani wao wakuu katika mbio za ubingwa na matumaini ya mchezaji
huyo yanabakia katika kikao chake na Moyes kwamba anaweza kupata mwanzo
mpya mzuri Old Trafford, hususan baada ya klabu kusema hajawahi kuomba
kuondoka United.
Hilo ni suala lililotokana na wasiwasi wa Rooney juu ya uhusiano wake na
mashabiki wa United. Rooney anatarajia kikao kama alichowahi kufanya na
kocha aliyetangulia, Sir Alex Ferguson mwishoni mwa msimu uliopita, cha
binafasi kujadili mustakabali wake katika klabu.
Arsenal imetenga bajeti ya kutosha kupambana katoka soko la usajili,
lakini tatizo ni kwamba wataweza kuwashawishi wachezaji wanaowataka, kwa
sababu ni wenye kiu ya mataji, vitu ambavyo kwa sasa klabu hiyo
vimekuwa adimu.