Search in This Blog

MZEE MAGALI ALIPIGIA MAHESABU JIMBO LA MBUNGE ABOOD WA MOROGORO, ANASWA BUNGENI NA WAHESHIMIWA

Mzee Charles Magali ambae hivi karibuni amekuwa akionekana Mjini Dodoma na Waheshimiwa na amekili kuwa na mpango wa kugombea ubunge Jimbo lolote la Morogoro.


Nguvu ya wasanii imeendelea kutikisa viongozi wa kisiasa na sasa kila chama kina mpango wa kuwashawishi wasanii hao kutangaza nia kwenye majimbo wanayokuwa wanakubarika,ambapo msanii nyota nchini na kipenzi cha watu Mzee Charles Magali amesema yuko tayari kugombea jimbo lolote endapo atatakiwa kufanya hivyo.

Akiongea na mwandishi wetu kwa njia ya simu toka mjini Dodoma msanii huyo alisema kuwa yuko kwenye mazungumzo mbalimbali na waheshimiwa Wabunge na Mawaziri na kuonekana kwake ndani ya bunge kuna mambo mengi ikiwemo alikuwa akifatilia kuwakilishwa kwa baje ya nchi.

Aidha msanii huyo aliongeza kusema " Mimi ni Chama tawala yani CCM hivyo nina maamuzi yangu binafsi ya kuamua kama nahitaji kugombea ubunge au laa hivyo kama chana kitahitaji nifanye hivyo nitafanya haraka sana na napenda kugombea Mkoani kwangu kwa vile bado nina kiu ya kuuletea mkoa wangu maendelea zaidi ya haya yaliyopo" Alisema Mzee Magali.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger