HII NDIO PATASHIKA KATI YA MACHINGA NA MGAMBO ILIYOTOKEA HAPO JANA HUKO MWENGE
Leo jioni wakati natoka katika shughuli zangu nilipita maeneo ya Mwenge
pale stand ya mabasi nimekuta kweupe wale vijana wanao uza nguo kwa
kupanga chini na kuzishika sikuwaona ...nikauliza nikaambiwa wamefukuzwa
kwa ajili Oboma Anakuja...Mmhhh
Kazi kweli kweli ...
Wakati bado
nashangaa shangaa Mara likaja gari la Polisi na Wale mgambo
wa jiji...Mara nikaona watu wanakimbia huku na kule ...Kushangaa kumbe
wale wamachinga bado wapo ila wanauza kwa kujificha ficha kwenye
vichochoro vya maduka..Sasa Kimbembe kikaanza wale wanamgambo
wakawafuata huko huko na kuanza kuwapiga na kuwavunjia meza na viti
vyao...Kwa kweli iliniuma sana kuona watanzania wenzetu wakifanyiwa
hivyo ....Bado sijapata jibu ...siko zote mbona hawakufukuzwa ?? Huu
Ugeni ndio imekuwa Nogwaaaaa....Na uhakika kuna ambao wanalisha na
kutunza familia kwa kazi hizi za umachinga sasa watakula wapi kama hali
ndio hiyo