Baada
ya kufunguliwa shtaka hilo, Lissu ambaye alikuwa wakili wa Sugu
aliitaka mahakama ifutilie mbali shtaka hilo kwani halina msingi wowote
wa kisheria na baada ya mabishano ya kisheria baina ya Lissu na wanasheria wa serikali kushindwa kuthibitisha kuwa neno Mpumbavu ni lugha ya matusi, hakimu ameamua kufuta shtaka hilo na ametangaza kuwa Sugu yuko huru na hana kesi ya kujibu.
MAAHAKAMA YAMFUTIA SUGU MASHITAKA YA KUMTUKANA WAZIRI MKUU PINDA, YADAI KUWA HANA KESI YA KUJIBU.
Jana asubuhi Joseph Mbilinyi (Sugu) alipelekwa mahakamani kwa shitaka la
kutumia lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu, shtaka hili lilifunguliwa
kwenye mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Dodoma na mwendesha mashitaka
wa serikali.