Zaidi ya
hapo Berlusconi ambaye amewahi kuiongoza Italia kama waziri mkuu kwa
vipindi vitatu tofauti amefungiwa kutojihusisha na siasa kwa maisha yake
yote kufuatia kashfa hiyo .
Hukumu
hii ni ya tatu kwa Silvio ndani ya kipindi cha miezi tisa iliyopita
ambapo mwezi oktoba mwaka 2012 alihukumiwa miaka minne gerezani kwa
kukutwa na hatia ya ukwepaji wa kodi na miezi miwili baada ya hapo
alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kutumia ushahidi wa
kunasa mazungumzo ya simu kinyume cha sheria .
Berlusconi
anatarajiwa kukata rufaa juu ya hukumu ambayo hata hivyo haina nafasi
kubwa ya kufanikiwa kutokana na kashfa zinazomzunguka ambazo zinafanya
iwe vigumu kwake kusafishika