MTANGAZAJI wa Channel O mwenye mvuto wa aina yake, Jokate Mwegelo
‘Kidoti’ amefunguka na Weekly Star Exclusive na kuanika kuwa tangu
amwagane na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ hajawahi kuanguka
dhambini na mwanaume mwingine.
Penzi la Jokate na Diamond lilichanua kwa takriban miezi miwili mwaka
jana wakati Kidoti alipomwagana na aliyekuwa mpenzi wake, mcheza kikapu
wa Ligi ya NBA ya Marekani, Hasheem Thabit.
Akizidi ‘kutema madini’ mbele ya kinasa sauti cha Weekly Star
Exclusive, Jokate alisema kwa kuwa alikuwa na mapenzi ya dhati na
Hasheem, ndiyo maana alimwagana na Diamond ndani ya muda mfupi na tokea
hapo amekuwa bize na kazi zake.
“Daah! Nipo bize sana na kazi zangu, ninaimba, ninaigiza, nina
kampuni yangu ya urembo ya Kidoti huku bado natakiwa kutangaza Channel O
basi kazi kwelikweli hata muda wa huyo mwanaume nakosa,” alisema
Jokate.
Alipoulizwa anamudu vipi hisia za matamanio ya kibaiolojia, Jokate
alisisitiza kuwa kazi pekee ndiyo silaha kubwa ya kumuepusha na
vishawishi ingawa anatambua upo umuhimu wa kuwa na mpenzi.
“Akitokea mkweli, nipo tayari ingawa hadi sasa hata sijajua nani
anaweza kuwa kama alivyokuwa Hasheem, nilimpenda sana,” alisema.