Bila shaka umeshajiuliza sana kwanini wabunifu wengi wa nguo wa kiume duniani ni mashoga. Haya ndio majibu:
Kwanza,
tasnia ya mitindo (fashion industry) kiutamaduni imekuwa ikiwakubali
zaidi mashoga wanaojulikana wazi (openly gay men) tofauti na fani
zingine. Hata leo, ni changamoto kubwa kwa shoga kufikia level ya kuwa
CEO ama Mkurugenzi kuliko wanaume wa kawaida.
Tofauti ni kwamba shoga kwenye fashion anaweza kuheshimika na kuenziwa kwenye fani hiyo na kufanikiwa binafsi na kifedha bila kudhihakiwa kama ambavyo anaweza kujikuta akifanyiwa kwenye fani zingine kama upolisi, jeshi na kwenye michezo.
Marc Jacobs

Mifano
mizuri inaweza kuwa kwa manguli wa fashion duniani kama Valentino
Garavani, Yves Saint Laurent, Perry Ellis, Karl Lagerfeld, Alexander
McQueen, Gianni Versace, Alexander Wang, Giorgio Armani, Marc Jacobs
(Louis Vuitton) Domenico Dolce na Stefano Gabbana, Tom Ford na wengine. Na hata kwa Tanzania wapo wengi wanaofahamika wazi.
Karl Lagerfeld
Japokuwa
mambo yanabadilika na hasa kwa nchi za wenzetu na kukubalika kwa watu
wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, kumefanya mashoga nao
wafanikiwe kwenye fani zinazotawaliwa na wanaume wa kawaida, lakini
mifano ya dunia halisi inabaki michache na hasa tu kwenye majiji ama
nchi ambazo mashoga na wasagaji wanapewa heshima sawa na wengine.
Pia kihistoria mashoga kwenye fashion walikuwa wakipewa kipaumbele zaidi kuliko wanawake. Ni Coco Chanel pekee ndio alikuwa miongoni mwa wanawake wachache waliofanikiwa kwenye kiwanda hicho kilichokuwa kikitawaliwa zaidi na mashoga Christian Dior na Cristobal Balenciaga.

Dolce & Gabbana
Pili,
inasemekana kuwa utamaduni wa ushoga huwapa nafasi watu hao uwezo wa
ubunifu. Mashujaa kwenye jumuiya ya mashoga sio wachezaji wa soka ama
wanajeshi- japo wapo. Lakini zaidi wapo kwenye muziki, uigizaji,
utengezaji wa filamu, uandishi na sanaa zingine.
Hii ni kwasababu ya ukweli kwamba hizi ndio zilikuwa kazi ambazo mashoga waliweza kufanikiwa na kuendelea kuwa walivyo na kujivunia wanachokifanya. Uwezo wao wa ubinifu huongezeka na ile sense ya upekee ambayo mashoga huikuza ndani ya ulimwengu wa mapenzi ya jinsia mbili (heterosexual world).

Tom Ford
Pointi
ya msingi: Upenzi wa mashoga katika urembo, utanashati hauwezi
kuelezeka. Inasemekana kuwa mwanaume anayebuni nguo nzuri kwa mwanamke
aidha hutaka kuwa na mwanamke ama hutaka kuwa mwanamke’