Search in This Blog

KOCHA MPYA WA AZAM AMETUA LEO NA KUTAMBULISHWA

Mtoto wa Omog Henry (wa kwanza kutoka kushoto) akisikiliza utambulisho wa baba yake, wa kwanza kulia ni Jafar Idd Msemaji wa Azam FC.
Kocha mpya wa Azam FC Joseph Omog (kushoto) akishika jezi ya timu hiyo mbele ya mwenyekiti wa klabu hiyo Said Mohamed.
KOCHA mpya wa Azam FC Joseph Omog hatimaye leo ametua rasmi jijini Dar tayari kwa kuanza kazi ya kukinoa kikosi hicho.
Omog raia wa Cameroon ametua leo saa 3:00 asubuhi na Ndege ya Shirika la Kenya ambapo mara baada ya kuwasili alipelekwa moja kwa moja katika ofisi kuu za timu hiyo zilizopo Mzizima na kusaini mkataba wa miaka miwili.
Mara baada ya kusaini mkataba huo Omog anayechukua nafasi ya Muingereza Stewart Hall alitambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari na mwenyekiti wa timu hiyo Said Mohamed ambaye alimtaja kocha huyo kuwa ni kati ya makocha bora sita wanaopatikana Bara la Afrika.
Mohamed maarufu kama Mzee Said amesema Azam inafuraha kubwa kumpata Omog ambaye uongozi wa timu hiyo umeona ndiye anayestahili kuchukua nafasi ya Stewart aliyesitisha mkataba mwezi uliopita.
Omog kwa upande wake kocha wa zamani wa kikosi cha A.C Leopards ya Congo Brazaville alionyesha kushangazwa na mapokezi aliyoyapata ambapo amesema mara baad ya kusaini mkataba huo sasa kazi yake kubwa ni kuhakikisha timu hiyo inaoata mafanikio ndani ya uwanja
Kivutio kikubwa katika ujio wa kocha huyo ni kuja na mwanaye Henry Omog ambaye ni beki wa zamani wa  Canon de Yaunde huku akiwa ndiye meneja wa baba yake huyo.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger