WATOTO wawili wa familia moja wameteketea kwa moto wakati wakiwa wamelala mjini Nansio.
Dolphin Dikson (5) na mdogo wake Drofina Dikson (3) walikutwa na
mauti jana saa 7 usiku katika eneo la National Housing, mjini hapa.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Dk Sundi Kabuli alisema
uchunguzi kuhusu kadhia hiyo bado unaendelea. Wakati huo huo watu wawili
wamekufa baada ya kugongwa na gari lenye namba T. 771 AKN aina ya
Toyota Corola mali ya Datus Evalist (63) lililokuwa likiendeshwa na
Peter Malisel (37).
Abiria wa gari hilo waliojeruhiwa wametajwa kuwa Makoye Ludovic (46),
Jastine Kitende (18), William Richard (39),Olva Mtebe (33) na Radislaus
Amos (32).
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mery Tesha ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo amekiri kuwepo matukio hayo.
Alisema ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike.
Mwandishi ni Jovither Kaijage , Ukerewe