BEAUTIFUL Onyinye, Wema Isaac Sepetu ametengeneza habari mpya
kama kawaida yake. Safari hii amemuanzishia timbwili zito fundi wake
aliyefahamika kwa jina moja la James.
Akizungumza kupitia kipindi chake cha In My Shoes mapema wiki hii,
Wema ambaye hachukii ukimuita Madam, aliweka bayana kuwa tukio hilo
ambalo lilitokea siku za nyuma lilimkera kwa sababu fundi huyo
alimuamini kuwa atamfanyia ukarabati mzuri wa nyumba yake, badala yake
akamharibia.
Siku ya tukio, Wema aliyekuwa amehama kwa muda kupisha
ukarabati wa nyumba hiyo, baada ya fundi kujiridhisha kuwa amekamilisha
ujenzi, alimuita Wema akakague ndipo mtiti ulipoanza. Alimtukana fundi
huyo, akamfokea vya kutosha akidai hajaridhishwa na ukarabati
alioufanya.
“This is my house, kwa nini umefanya vibaya? Sijapenda,
sasa hivi ndiyo nini? Rangi gani hii umepaka? Yaani umeniharibia kila
kitu, sipendi kuharibiwa kabisa nyumba yangu…” alifoka Wema.
Licha ya
Meneja wa Wema, Martin Kadinda kuwepo nyumbani hapo na kumsihi wampe
siku mbili fundi huyo ili arudie ukarabati, Madam aliendelea kuvurumisha
‘mitusi’ kama aliyechanganyikiwa.
Sini hiyo ya varangati ilioneshwa
‘live’ kupitia kipindi chake hicho kinachorushwa na Runinga ya East
Africa ambapo fundi huyo alionekana akimwaga machozi kisha kuondoka
nyumbani hapo kwa unyonge baada ya kukosa muafaka.