Mara nyingi linapotokea jambo kwa msanii mkubwa katika kipindi
ambacho anatarajia kutoa album au kufanya show huwa linaleta hisia za
stunt ya kuvuta attention ya watu, kitu ambacho kimejitokeza kwa
mwimbaji wa R&B Ne-Yo aliyetangaza kuachana na mchumba wake Monyetta
mama wa watoto wake wawili kipindi ambacho anajiandaa kutoa album yake
mpya.
Jumamosi iliyopita (June 29) Ne-Yo alipost picha (hapo juu) yenye
ujumbe kuwa yeye na mchumba wake Monyetta Shaw wameachana kwa amani na
kusema kuwa ataendelea kumpenda siku zote.
“The fate has decided to split our romantic paths, know that I will
ALWAYS LOVE YOU. Forever your partner…Forever your friend.Forever my
MIRACLE”. Huo ndio ujumbe ulioko katika picha aliyopost mkali huyo wa
R&B ukimwendea mchumba wake.
Wakati Ne-yo anapost picha hiyo mchumba wake aliyekuwa Los Angeles,
Marekani muda huo huo naye alipost picha akiwa na marafiki zake na
wenye furaha (akiwa bado na pete ya uchumba ya Ne-Yo kidoleni) na
akasindikiza picha hizo na tweet inayoonekana ni jibu ya ujumbe wa Ne-Yo
“No worries! Got a gang of bad chick!!!! #girlpower #betweekend
#letsgo #goodtimes”.