MeTL Group watangaza zawadi nono kwa atakayefanikishwa kukamatwa kwake
Kibali cha kazi cha Meneja huyo.
KAMPUNI YA MOHAMMED ENTERPRISES TANZANIA LIMITED (MeTL) Makao Makuu
inatangaza kwa umma wa watanzania kwamba Meneja wa MeTL tawi la Iringa
Mr Aamir Iqbal anatafutwa na mwajiri wake kwa kosa la wizi wa mamilioni.Mr Iqbal (pichani juu) aliyekuwa Meneja wa tawi la MeTL Iringa anatuhumiwa kwa kosa la kumwibia mwajiri wake mamilioni ya pesa yeyote atakayewezesha kukamatwa au kutoa taarifa zake katika kituo chochote cha Polisi zawadi nono itatolewa.
Tukio hilo lililotokea jana mchana Iringa limeripotiwa Kituo Kikuu cha Polisi Iringa na RB ya Polisi ni ref no. IR/RB/7229/2013.
Kampuni ya MeTL Group itatoa zawadi nono kwa yeyote atayefanikisha kukamatwa kwake.
Au piga simu namba: 0755 030 014 , 2118930/1, 0713 324 332, 0715 030 024