Search in This Blog

Showing posts with label MAHUSIANO. Show all posts
Showing posts with label MAHUSIANO. Show all posts

NJIA ZA KUMTONGOZA MWANAMKE NA AKAKUPENDA DAIMA

Kuna baadhi ya wanaume hawajui jinsi ya kuzungumza na mwanamke au msichana. Kwa njia hii wanaume wengi wanaishi maisha ya bila kumvutia mwanamke yeyote.

Hapa kunanjia 10 utakazozitumia wewe mwanaume ili kuhakikisha humkwazi mwanamke unayempenda mnapokuwa katika mazungumzo ;

1. Wakati ukizungumza nae, jaribu kuzungumzia "hisia" kama vile kumbu kumbu yako ya utotoni, matarajio ya baadae au matamanio yake. Mada hii ya mazungumzo yenu yatafungua milango ya hisia zake ghafla.

2. Wanawake huhitaji mwanaume asiyekuwa na uoga wa kuwamiriki na kuwaongoza. Wakati unazungumza na mwanamke tawala mazungumzo yenu na kamwe usimpe nafasi ya yeye kuanza kufikiri kuwa nini ulichokuwa ukizungumzia.

3. Kuwa makini wakati unapokuwa ukizungumza nae huku akikupatia majibu yasiyo na hisia zozote za mapenzi. Hapo utajua kunakitu, hivyo kama kwa bahati mbaya uko nae karibu kiasi cha kugusana, basi jisogeze pembeni wakati ukiwa unaendelea kuongea ili asishtukie au unaweza kumuona hayuko sawa katika utoaji majibu.. kwa kawaida atakuonyesha ishara, hivyo kuwa nazo makini.

4. Kumbuka hii kauli mbiu "Ucheshi/vituko si mapenzi". Wanawake huvutiwa sana na wanaume wanaoweza kuwafanya wawe na furaha muda wote. Usijikite zaidi katika kufanya utani unaopita kiasi na kusahau ulichokuwa unaongea. Bali jikite zaidi katika mambo yanayomfanya ajisikie kuwa na msisimko na starehe wakati ukonae.

5. Zama katika undani wa mazungumzo baina yako na yeye. Mwanamke huendana na mwanaume asiyekuwa muoga wa kuzungumzia mambo binafsi kwa ukaribu.

6. Wanawake wengi hupenda kujua maoni yako kuhusiana na jinsi unavyomuona. Mwambie vitu unavyoviona kutoka kwake, lakini jaribu kuwa makini ili usitamke vitu vingine vitakavyo msababishia apoteze furaha.

7. Epuka kumpa ofa nyingi mwanamke, mwanamke huwa na mashaka na mwanaume anayempatia vitu vingi kwa wakati mmoja ama kila mara. Kwasababu atafikiri vitu unavyompatia ni kutaka kumvutia tu ili umpate kiurahisi. Kitu ambacho baadae kitaleta madhara makubwa.

8. Kama unahitaji kujua njia nzuri ya kuweza kuongea na mwanamke au msichana bila kumfanya asikudharau au kuboreka, basi usitumie njia ya kumuuliza  maswali mengi katika mazungumzo yenu. Bali jaribu kueleza mawazo yako kuhusu vitu flani.

9. Kumbuka kauli juu ya kuuliza maswali: Badala ya kumuuliza "wewe umekulia wapi?", uliza "unaonekana kama hujakulia maeneo haya!" Hii itakusaidia wewe kufanya uchunguzi juu yake bila yeye kujua.

10. Usifiche utambulisho wako - zungumza vitu kutoka katika hisia zako, onyesha uhalisia wako katika kuzungumza na usitumie mikogo ya mtu yeyote.

Njia bora ya kufikiria jinsi ya kuzungumza na mwanamke, ni kutambua njia sahihi ya mazungumzo ya furaha na yakimahaba utakayopenda kuitumia, isipokuwa usimuige mtu. Kuzungumza na mwanamke sii vigumu bali nikujua ni vitu gani hasa mwanamke hapendi kuvizungumzia na vitu gani anapenda kuvisikia. Fuata maelekezo hapo juu utaona matunda yake...kisha rudi toa maoni yako hapa.

MUHIMU: Maelekezo haya yote yatafanikiwa kwa mwanamke mwenye kuhitaji mapenzi ya kweli - yani sio kwa wanawake wanaolenga kuchota pesa kwako na kutokomea. Hivyo kuwa makini sana.

UKIFANYA MAMBO HAYA HAUTOUMIZA/HUTOUMIZWA NA MPENZI WAKO KAMWE KATIKA MAPENZI YENU, YASOME HAPA


1. Wivu Wa Kupindukia

Ni Jambo Jema Kwa Mwanamume Kumtakia Heri Mpenzi Wake Na Kufanya Kila Awezalo Kuhakikisha Kuwa Hapati Madhara, Lakini Iwapo Utakuwa Mtu Wa Wasiwasi Na Mashaka Pale Unapomwona Mpenzi Wako Akizungumza Na Mwanamume Mwingine, Au Anapotoka Na Marafiki Zake Wa Kike, Au Anapovaa Nguo Inayomfanya Atamanishe, Basi Fahamu Kuwa Tayari Umekunywa Sumu Ya Mapenzi.

Katika Uhusiano Wa Kimapenzi, Kuaminiana Ni Jambo Muhimu Sana. Kama Kweli Unataka Mpenzi Wako Akupende Kwa Dhati, Mwoneshe Kuwa Unamwamini Na Unaheshimu Maamuzi Yake, Ikiwa Ni Pamoja Na Maamuzi Ya Kutoka Na Marafiki Zake Wa Kike Na Kuwa Na Marafiki Wa Kawaida Wa Kiume. Ondoa Hofu Na Acha Kabisa Kumpeleleza, Maana Wapo Wanaume Ambao Hutumia Muda Wao Mwingi Kuwapeleleza Wapenzi Wao Ikiwa Ni Pamoja Na Kuwategeshea Kamera Na Rekoda Za Simu.

2. Kutomwachia Nafasi Mpenzi

Kama Huishi Na Mpenzi Wako Ni Jambo La Kawaida Kuwa Na Hamu Ya Kumwona Mara Kwa Mara, Lakini Kumbuka Kuwa Mpenzi Wako Naye Ana Maisha Yake Na Anahitaji Nafasi Ya Kuwa Peke Yake Kwa Ajili Ya Mambo Yake Binafsi.

Hisia Za Kutaka Kuwa Na Mpenzi Wako Muda Wote Zinaweza Kudhaniwa Kuwa Ni Za Mapenzi Ya Dhati, Lakini Kwa Hakika Hiyo Si Ishara Njema Ya Mapenzi Ya Kudumu. Hebu Jiulize Kama Unaweza Kuendeleza Hali Hiyo Maisha Yako Yote. Ni Wazi Kuwa Utachoka. Kwa Hiyo, Mpe Mpenzi Wako Fursa Ya Kupumua. Namna Hii Mpenzi Wako Atajenga Hamu Ya Kutaka Kukutana Nawe Lakini Ukiwa Naye Muda Wote Hamu Hiyo Itaisha.

3. Kumwamulia Mpenzi Mambo Yake

Unaweza Kujikuta Ukisukumwa Kumwambia Mpenzi Wako Awe Anavaa Nini Wakati Gani, Akutane Na Nani Na Kwa Wakati Gani Au Ale Nini. Ukiona Hivyo, Fahamu Kuwa Hayo Si Mapenzi, Bali Umepitiliza Na Pengine Mwisho Wa Uhusiano Wenu Unanukia.

Hata Ukiachilia Mbali Suala Zima La Usawa Wa Jinsia, Hakuna Mwanamke Ambaye Angependa Apangiwe Kila Kitu Kuhusiana Na Maisha Yake. Kama Ilivyodokezwa Hapo Juu, Kila Mtu Ana Maisha Yake Na Kilichowaunganisha Ni Mapenzi Tu. Kama Utataka Kumpangia Kila Kitu Ni Wazi Kuwa Utaishia Kuishi Peke Yako.

4. Kumuuliza Mpenzi Maswali

Iwapo Utajikuta Ukimuuliza Mpenzi Wako Maswali Mengi Yanayoonesha Wasiwasi Wako Kuhusiana Na Mwenendo Wake, Fahamu Kuwa Kuna Tatizo Na Tatizo Hilo Lisipopatiwa Ufumbuzi Utakuwa Mwanzo Wa Mwisho Wa Uhusiano Wenu.

Mwanamke Angependa Umuulize Maswali Ya Kawaida Kuhusiana Na Jinsi Siku Yake Ilivyokuwa Na Kama Marafiki Zake Hawajambo Au La, Lakini Kila Jambo Lina Mpaka Wake. Mwanamke Hatarajii Kuwa Kila Mnapokutana Atakuwa Kama Ameingia Kwenye Chumba Cha Mtihani Au Usaili Wa Kazi.

5. Kutoamini Anachokweleza Mpenzi

Wakati Mwingine Watu Hushindwa Kuwaamini Wenzao, Lakini Kwa Sababu Ambazo Ni Za Msingi, Lakini Kuna Wakati Ambapo Mtu Hushindwa Kumwamini Mwenzake Bila Sababu Yoyote Ya Msingi, Au Kwa Sababu Zisizo Sahihi, Kisingizio Kikiwa Ni Mapenzi.

Kuna Tatizo La Kisaikolojia La Kujishuku Au Kuwashuku Wenzako. Hili Ni Jambo Ambalo Linaweza Kukuharibia Mustakabali Wako Katika Mapenzi, Maana Husababisha Kujengeka Kwa Mazingira Ya Kutokuaminiana. Ili Uweze Kwenda Sanjari Na Mpenzi Wako, Amini Kila Anachokweleza Hadi Pale Utakapokuwa Na Sababu Za Msingi Za Kutokumwamini. Na Hata Unapokuwa Umelithibitisha Jambo, Endelea Kuwa Katika Uhalisia Wako.

6. Kuacha Hobi, Marafiki

Mahusiano Ya Kimapenzi Mara Nyingi Huhusisha Kila Mmoja Kuacha Baadhi Ya Mambo Yake Kwa Ajili Ya Mwenzake. Hata Hivyo, Lengo Ni Kuweka Tu Uwiano Wa Mahitaji, Si Kuacha Kila Kitu Ulichokuwa Nacho Kwa Ajili Ya Mwenzako, Ama Kwa Shinikizo, Au Kwa Kulewa Penzi.

Iwapo Utabaini Kuwa Marafiki Zako Sasa Wamekuwa Ni Marafiki Zako Wa Zamani Na Hobi Zako Zimebaki Tu Katika Kumbukumbu Japo Kwa Hakika Bado Unahisi Mapenzi Katika Hobi Hizo, Basi Tambua Kuwa Huyo Mrembo Wako Amekunywesha Sumu Ya Penzi Na Sasa Huwezi Hata Kuitumia Vema Mantiki Yako.

Mbaya Zaidi, Iwapo Utabaini Kuwa Marafiki Zako Wapya Ni Marafiki Wa Siku Zote Wa Mpenzi Wako Na Hobi Zako Ni Zile Za Mpenzi Wako, Basi Tambua Kuwa Huna Tena Nafsi Yako, Bali Umejisalimisha Mzima Mzima Kwa Mpenzi Wako. Lakini Msemo Mmoja Wa Hekima Unatwambia Usiweke Mayai Yako Yote Kwenye Kikapu Kimoja. Yamkini Unaelewa.

7. Kukubali Kupelekeshwa

Pengine Unakumbuka Kuwa Kuna Nyakati Ambapo Ulikuwa Na Uwezo Wa Kujikita Katika Jambo Moja Na Kulifanya Kwa Umakini, Huku Ukiwa Pia Mwerevu, Mjanja Na Unayejisimamia, Lakini Leo Unayeyuka Kirahisi Tu Kama Barafu Iliyowekwa Juani! Hii Ni Hatari Kwa Mustakabali Wa Maisha Yako.

Mbaya Zaidi Ni Pale Utakapoiacha Kazi Yako Inayokulipa Vizuri Na Kufanya Kazi Nyingine Kwa Ajili Ya Kumfurahisha Mpenzi Wako. Ukifika Hali Hii Ujue Wewe Mwenyewe Kuwa Hapo Hakuna Mwanamume.

8. Utayari Wa Kufa Kwa Ajili Yake

Umewahi Kujisikia Kuwa Na Utayari Wa Kufa Kwa Ajili Ya Mpenzi Wako? Kama Jibu Ni “Ndiyo”, Basi Fahamu Kwa Hakika Kuwa Hayo Uliyo Nayo Si Mapenzi Bali Ni Upumbavu. Pengine Huku Ndiko Kunywesha Sumu Ya Mapenzi. Kwa Hakika, Hakuna Mwanamke Ambaye Anastahili Kumfanya Mwanamume Yeyote Kufa Kwa Ajili Yake.

Yamkini Wanaume Wanaolengwa Katika Makala Haya Si Wavulana Wanaosoma Sekondari, Waliobalehe Majuzi, Ambao Wakipenda Au Kupendwa Hujiona Kama Wako Katika Sayari Yao. Mwanamume Aliyepevuka Hujiamini Na Hayaweki Maisha Yake Yote Mikononi Mwa Mwanamke, Hata Kama Mwanamke Huyo Angekuwa Ndiye Mrembo Wa Dunia.

Iwapo, Ama Kwa Ujinga Au Kwa Kufahamu Umewahi Kumwambia Mpenzi Wako: “Ukiniacha Nitajiua,” Na Ukawa Unaamini Hivyo Kabisa, Basi Yamkini Unahitaji Kutafuta Msaada Wa Ushauri Nasaha, Maana Kwa Hakika Umepotoka.

9. Muda Wote Unawasiliana Naye

Vijana Wa Siku Hizi Ni Watumiaji Wazuri Sana Wa Simu, Lakini Iwapo Utabaini Kuwa Asilimia Kubwa Ya Muda Wako Unautumia Ama Kwa Kuongea Au Kuwasiliana Kwa Ujumbe Mfupi Na Mpenzi Wako, Basi Fahamu Kuwa Kuna Tatizo Ambalo Linahitaji Ufumbuzi Wa Haraka.

Kumbuka Kuwa Mapenzi Hayachukui Nafasi Ya Kila Kitu. Yamkini Huyo Mpenzi Wako Amekukuta Unaishi Na Kuna Mambo Ya Muhimu Ya Kufanya. Hebu Achana Na Simu Kwanza Ufanye Mambo Ya Muhimu Kuhusiana Na Maisha Yako. Kama Mpenzi Wako Hakwelewi Katika Hili Basi Hakufai.

10. Ndugu Zake Wanakufuatilia

Iwapo Utabaini Kuwa Marafiki, Ndugu Na Jamaa Za Mpenzi Wako Wanamtonya Mpenzi Wako Kuhusiana Na Kile Wanachokiita Mwenendo Wako Mbaya, Usipuuze Hali Hii. Kuna Uwezekano Mkubwa Kuwa Watu Hawa Wanayo Sababu Ya Kuwa Na Wasiwasi Na Mwenendo Wako, Kwa Hiyo Jichunguze Na Kuangalia Jinsi Unavyoenenda.

Hata Hivyo, Jambo Hili Si Ishara Njema Ya Mustakabali Mwema Wa Uhusiano Wenu. Iwapo Mpenzi Wako Ataweka Watu Wake Wakufuatilie, Maana Yake Halisi Ni Kwamba Hakuamini. Katika Hali Kama Hii, Haitarajiwi Kuwa Mustakabali Wa Uhusiano Wenu Utakuwa Mzuri, Kwani Kutakuwa Na Uingilizi Mwingi Wa Ndugu, Jamaa Na Marafiki Zake. Unaweza Kukubali Kuendelea Kuishi Katika Hali Hii Kwa Kisingizio Cha Mapenzi, Lakini Ukweli Ni Kwamba Hayatakuwa Mapenzi Bali Karaha.

KUWA MAKINI

Kama Unavyoona, Hizi Ni Baadhi Tu Ya Dalili Kuwa Mapenzi Yako Kwa Mwanamke Sasa Yanaelekea Katika Ulevi, Mithili Ya Ule Wa Dawa Za Kulevya. Jambo Moja La Kukumbuka Ni Kwamba Kweli Mapenzi Ni Kitu Kizuri, Lakini Pia Mapenzi Yanahitaji Kuwa Jambo Linaloashiria Mustakabali Mwema Kwa Wahusika Wawili. Yakiwapo Mambo Haya Kumi Hauwezi Kuwapo Mustakabali Mwema Katika Mapenzi

WANAUME HUFANYA MAKOSA HAYA WAWAPO KITANDANI NA MPENZI MPYA.



Linapokuja swala la kujamiiana kwa wapenzi wapya ambao hawajawahi kukutana kimwili tangu kujuana kwao ni mtihani mkubwa. Kwani kila mmoja anakuwa na matarajio tofauti na mwenzake. Yaani hakuna anayejua kwa usahihi kwamba mwenzake anapenda afanyiwe nini ili kupata ashki ya kushiriki jambo hilo, lakini wanawake wengi ndio ambao hulichukulia jambo hilo kwa uzito mkubwa kiasi kwamba, kama mwanaume asipomudu kuwa mtundu kitandani, nafasi yake kwa mwanamke huyo inaweza kuwa finyu sana labda tu kama atakuwa amempendea pesa…

Hapa chini nitaeleza makosa yanayoonekana madogo yanayofanywa na wanaume kitandani
wakutanapo na wapenzi wapya ambayo wanawake huyapa uzito mkubwa:



1. Kumuandaa

Kumuandaa mwananamke sio pale muwapo kitandani tu, la hasha, maandalizi huanzia katika mazungumzo ili kumuweka katika mood. Hapa mwanaume anatakiwa aongee na mpenzi wake kwa lugha nzuri, kwa maneno matamu na yenye mahaba. Atumie muda mwingi kuzungumza naye, asiwe na haraka kuanza kufanya tendo. Mazungumzo yahusu masuala ya uhusiano ukiwemo upendo. Busu lililotulia na sio la papara linatajwa kuamsha hisia za mwanamke kushiriki tendo, lakini pia mwanaume anashauriwa kuwa msomaji mzuri wa hisia za mwanamke ili kujua ni eneo gani akimgusa kwa kumpapasa mwili wake unasisimka. Kwa mwanamke kufanya mapenzi sio kile kitendo cha kuingiliwa, bali ni kitendo cha kumuandaa kiakili na kimwili ili awe kwenye mood ya kushiriki jambo hilo. iwapo mwanaume akili yake itakuwa inalenga tu kile kilichopo katikati ya mapaja ya mwanamke na labda matiti yake, basi hapo mwanamke atamuona sio kabisa, yaani hatoweza kumfikisha kileleni.



2. Unadhifu

Hakuna kitu kinachowakera na kuwakwaza wanawake kama mwanaume mchafu hususan wakati wa kujamiiana. Hilo linaweza kumfanya mwanamke asifikirie tena kufanya tendo na mwanaume huyo. Unakuta mwanaume ananuka kikwapa au amevaa chupi wiki nzima bila kuifua na akiivua eneo la chini ya kitovu lote linanuka au ana kucha ndefu tena chafu na zina ncha kali kwenye kona (sharp edge) kiasi kwamba akimpapasa mwanamke zinamkera badala ya kumpa ashki. Akipumua mdomo unanuka, yaani akimpiga busu mwanamke anamkata stimu yote ya kufanya tendo hata kama alikuwa tayari. Inashauriwa mwanaume kuoga na kupiga mswaki kama hana uhakika na harufu ya kinywa chake, la sivyo anaweza kutumia chewing gum za kuondoa harufu mbaya mdomoni kabla ya kukutana na mwanamke na pia kukata kucha na kuondoa ncha kali zile zinazojitokeza pembeni ya ukucha ili zisimkere mwanamke wakati wa kumuandaa……



3. Mapenzi ya vurugu na yenye kuumiza

Tukiacha tatizo la kukerwa na harufu na kucha, lakini pia wanawake hawapendi mwanaume anayetwanga nje ndani wakati wa kufanya mapenzi kama vile anachimba dhahabu. Wanawake wanapenda mitwango yenye staha. halafu itokee mwanaume huyo awe ana kucha ndefu zenye ncha zilizojitokeza pembeni, kisha awe anautumia mkono wake kumpapasa mwanamke sehemu mbalimbali za mwili wake huku akiendelea kutwanga kwa fujo……..Aaaaaaagh!!

Asije akatarajia mwanamke huyo akatamani tena kujaamiana naye, labda kuwe na kitu kingine anachokitafuta kwa mwanaume huyo na siyo mapenzi. Kuna baadhi ya wanaume hupenda kuchezea chuchu za maziwa wakati wa kufanya mapenzi kwa kuziminya kwa nguvu au kung’ata maeneo mbalimbali ya mwili wa mwanamke kwa nguvu. Mwili wa mwanamke uko laini laini na unatakiwa ashikweshikwe kwa makini na kwa staha. Hakuna ubaya kumng’ata ng’ata mwanamke kimapenzi (love bite) hapa na pale lakini inashauriwa kuchunguza kama anafurahia kitendo hicho kwa kumwagalia usoni, akiona anaonyesha sura ya kukereka kwa maumivu, basi inashauriwa kuacha na kubadilisha kwa kujaribu kitu kingine kwani wanawake wana maeneo mengi sana ya kuamsha ashki, na akimpatia atamsikia mwenyewe akiweka msisitizo kwamba aendelee……



4. Kimya mno ….. Au kupiga makelele

Wanaume wengi hupenda sana mwanamke anapopiga makelele pale wafanyapo mapenzi lakini pia wanawake hupenda kuona kama mwanaume naye anafurahia tendo kama anavyofurahia yeye anavyofurahia. kama mwanaume ni mkimya anapofanya mapenzi yaani haongei chochote yeye anatwanga tu, mwanamke anaweza kujiuliza kama mwanaume huyo anafurahia tendo au la. Wakati mwingine ile sauti ya kupumua kwa sauti itolewayo na mwanaume wakati wa kufanya mapenzi inaweza kuwaridhisha baadhi ya wanawake, lakini wengine wanapenda kusikia mazungumzo kutoka kwa mwanaume. Iwapo mwanaume atapotelewa na maneno kutokana na kusikilizia utamu wa tendo inashauriwa japo ataje jina la mwanamke hata mara chache ili kumfanya mwanamke ajue kuwa akili na mawazo ya mwanaume huyo yapo kwake.

Hapa naomba kuweka angalizo…. kama mwanaume ni mtu wa kuongea sana wakati wa kufanya mapenzi anaweza kumpotezea mwanamke umakini wa kuvuta hisia ili kufika kileleni. Kwani kuna baadhi ya wanaume huwauliza wanawake wanaofanya nao mapenzi maswali mengi yasiyo na maana.. “Unauonaje huu mtindo.” “Unajisikiaje nikikushika hapa.” “Je ninafanya vizuri na huumii.” Lo lo lo lo loooooo….Huna haja ya kuuliza maswali yote hayo, kwani mwili wake unakupa ushirikiano sasa maswali yote hayo ya nini….! Najua hakuna ubaya kumuuliza mwanamke kama anajisikiaje au kama unavyofanya ni sahihi kwa maana kama mtindo unaotumia haumuumizi, lakini hilo hufanyika katika hatua ya mwanzo, sio pale mchezo umekolea unaanza kuuliza maswali, unakuwa unamkera tu…… Funga mdomo wako na uendelee na shughuli.



5. Kulazimisha Oral Sex

Nikisema orol sex, nadhani mnaelewa. Kuna baadhi ya wanaume hupenda kuchezewa sehemu za siri au kunyonywa. Si vyema kumlazimisha mwanamke kunyonya bila ridhaa yake. Kama anapenda kufanya hivyo mwache aamue mwenyewe na sio umshike tu kichwani na kumuelekeza yalipo maumbile yako. Kama mwanamke anapenda kufanya hicho kitendo mwache afanye mwenyewe na hahitaji kuelekezwa..



6. Kumaliza haraka au kuchelewa kumaliza

Najua wanaume watasema “hii ni ‘too much.’ Kumaliza haraka ni shida na kuchelewa kumaliza pia ni shida, sasa tushike lipi…..!”Nataka muelewe, kama inakuchukua dakika mbili kumaliza, hilo ni tatizo kaka yangu, katafute msaada wa kitabibu uondokane na fedheha kabla ya kuparamia mwanamke. Kwa wanawake wengine inaweza isiwe ni tatizo iwapo utamuandaa vizuri kabla ya kumuingilia ili kama ni kumaliza mmalize pamoja hivyo kutogundua tatizo lako labda..! lakini kama sio mzuri katika kumuandaa mwanamke, linaweza kuwa tatizo na ukajikuta anakudharau baada ya kumaliza tendo… (Najua kwamba siku ya kwanza kukutana na mpenzi mpya inaweza kukufanya ukamaliza haraka kutokana na kuhemkwa, lakini basi jitahidi mara ya pili uende sawa usije ukamaliza haraka tena…..).

Lakini pia wanawake hawakuumbwa kwa ajili ya mashindano ya mbio za kufanya mapenzi. Nakubali kwamba wapo baadhi ya wanawake wanahitaji muda zaidi ili kufika kileleni. Lakini kama itachukua dakika 45 mpaka saa moja bado unatwanga tu, angalia usije msababishia mwenzio michubuko katika sehemu zake za siri. Inatakiwa kuonyesha ushirikiano katika jambo hilo zaidi ya kujipendelea mwenyewe……!



7. Hutupi kifanyio baada ya kumaliza…!

Kutupa kondom uliyotumia wakati wa kufanya mapenzi ni kazi yako na si kazi yake. Sio uungwana umemaliza kufanya naye mapenzi kisha unamwagiza akatupe kondom uliyotumia. Lakini pia sio busara kuiweka chini na kuiacha ikichafua sakafu. Haijalishi mko guest house, nyumbani kwako au kwa mpenzi wako, kinachotakiwa ni kuonyesha ustaarabu. Ni nyema ukaivua na kuiviringisha kwenye toilet paper, karatasi au kipande cha gazeti na kuiweka mahali pazuri kabla ya kwenda kuitupa mahali panapostahili………. Vinginevyo mpenzi wako atakuona wewe sio msafi na siyo mstaarabu…

MDADA ALIYEFANYA NGONO NA WANAUME WENGI KWA MUDA MFUPI



Tracy Lawrence raia wa ghana mwenye umri wa miaka 28 alijitoa muhanga kwa kufanya mapenzi na wanaume 1,000 tofautitofauti, Siku alipofanya mapenzi na mwanaume wa 738 akachangamka ndani ya mwaka mmoja na miezi 4 akahakikisha ametimiza hesabu ya
wanaume 1,000, Ameahidi kwamba mpaka tarehe 24th mwezi wa kwanza 2014 atahakikisha ametimiza hesabu yake anayoitarajia kuvunja nayo rekodi.

Balaa........ soma maneno yake hapa chini.



"I am me, take me for who I am. It's my life and life is short so I'm going to live it to the fullest and have fun. #Getting-to-a-thousand-baby Mmmuaaah"

KAMA MPENZI WAKO ANAKUPIGA BUSU KAMA HILI, BASI KAZI UNAYO


HILI inaelekea ni busu la kufungia mwaka maana muda si mrefu mmoja kati yao atamjeruhi mwenzie.

FANYA MAMBO HAYA KUZUIA UGOMVI ILI MAHUSIANO YENU YAENDELEE KUDUMU MILELE, YASOME HAPA

LEO usiku wa saa sita, tutakuwa tumekaa pamoja na familia zetu na wapendwa wetu, tukiisubiri kwa hamu dakika ya kwanza ya mwaka mpya, 2014. Kama inavyotokea mara zote, tutashangilia kwa furaha sana tukio hili, maana jambo lenyewe hutokea mara moja tu kila mwaka.
Ni siku ambayo kila mtu anayebahatika kuifikia, huifurahia sana, maana Mwenyezi Mungu anakuwa amekuchagua kuwa miongoni mwa binadamu waliopendelewa, hasa ukitilia maanani kwamba wenzetu wengi, wanaofikia mamilioni, wameshindwa kuufikia mwaka huu!
Kwa kutambua kwamba tunaanza mwaka mpya 2014, nimeona ni jambo la busara kuja na mada hii kwa sababu wote tunafahamu kuwa katika uhusiano wetu wa kimapenzi na hata ndoa, mara nyingi matatizo yanayojitokeza, huonyesha dalili tokea mapema.
Wewe unamfahamu vizuri mwenza wako, mambo gani huyapenda, yapi huyachukia, chakula anachokula (kama mnaishi pamoja), aina ya mazungumzo anayopenda na kuchukia na hata aina ya mavazi yanayomsisimua. Kama hivyo ndivyo, ni rahisi kujua kitu kinachoenda kutokea.
Kwa mfano, kama mumeo amekuja nyumbani akitokea kazini akiwa amechoka, sura yake haina furaha hata kidogo, anakuja moja kwa moja na hasira zake anakaa kwenye kochi akiwa amenuna. Kwa vile unatambua tabia zake anaporudi kutoka kazini, ni wazi utaona mabadiliko makubwa.
Utatambua kwamba mwenzio amekerwa na kitu, kama siyo na wewe, basi huko kazini kwake au popote pengine. Katika nyakati kama hizi, kuwa mpole, vuta subira na anza naye mazungumzo taratibu, tena ukiwa na staha. Siyo umemuona mwenzio katika hali kama hiyo, wewe unakurupuka, ‘Nini tena? Umeshaharibu huko eeeh, au umefumaniwa?’
Kauli kama hizi zitazidisha tatizo, kwa sababu hata kama amepata matatizo kazini, njiani au popote pale, kauli hizi zitamfanya azidi kukasirika na wengine wanaweza hata kuibua jambo jipya.
Tunasema tunaweza kuzuia ugomvi baina yetu kabla haujaanza. Tunasema hivi tukimaanisha nini? Ni kwamba mume anaweza kuwa amekosea, tuseme jambo dogo tu, kama kugeuka nyuma kuangalia makalio ya mwanamke mwingine, wakati anajua ameongozana na mkewe.
Wako wanawake ambao lazima waseme jambo kwa kitendo hicho cha mumewe, tena wakati mwingine kwa hasira na sauti kubwa. Lakini wapo ambao wanaweza kuchagua kukaa kimya. Ingawa lile ni kosa kwa mume, lakini kukaripiwa kwa ukali na wakati mwingine hata mbele za watu, kunaweza kumfanya akakosa uvumilivu, akajikuta naye anakuja juu na matokeo yake kusababisha ugomvi.
Ni lazima kila mmoja awe wa kwanza kukubali makosa, hata kama siyo kweli.
Hapa nazungumzia matatizo tunayosababisha sisi wenyewe, achana na yale ya kibaolojia. Kama mwenza wako amekuja akiwa na hasira kubwa, hakuna sababu ya upande wa pili nao kulipuka. Kaa kimya, mwenza wako akishamaliza kutoa yake kwa hasira, waweza kuwa wakati wako wa kujieleza, lakini kwa sauti ya chini.

Vipo baadhi ya vitu ambavyo tukivifanya, vinaweza kutusaidia kuzuia ugomvi wa ndoa au uhusiano wetu kabla haujatokea. Vitu hivi ni pamoja na uvumilivu, utayari wa kusamehe, kukubali kukosolewa na busara katika majadiliano.

NJIA SAHIHI YA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, SOMA KUJUAZAIDI


Wanaume wengi hapa duniani
huamini kuwa, mwanaume hasa ni
yule anayeweza kufanya tendo
hilo kwa muda mrefu na mara
nyingi ndio maana vijana wengi
utawasikia wakijisifu kuwa,
mpenzi wake hakulala usiku
mzima kutokana na dozi ya maana
aliyompa na ukimuuliza mtu wa
namna hii atakwambia kuwa
alikwenda mizunguko sita usiku
mzima.


Hata hivyo, ukweli ni kuwa, watu
wengi hufikia hatua ya kusema
uongo ili waonekana kuwa ni
wanaume hasa mbele ya wenzao
huku wangine wakigubikwa na
nadharia kuwa ukubwa wa uume
unaashiria jinsi gani walivyo
wanaume kitu ambacho si kweli.

Ni mtazamo huu ndio
unaowafanya wanaume
wakitaniwa au kuambiwa kuwa
wako kama wanawake wanaweza
waue mtu. Tunaamini kuwa
uanamke ni udhaifu na uanaume
ni ushujaa fulani hivi.
Wakati hali ikiwa hivyo, hivi sasa
wanaume wengi wamekuwa
wakihangaika na jambo moja
kubwa, kutafuta dawa za
kuongeza nguvu za kiume ili
kujiongezea heshima faragha!
Ukitaka kuthibitisha hili jaribu
kuangalia karibu katika kila gazeti
utakalo soma, ni nadra sana
kukosa tangazo dogo la biashara
lililotolewa na mganga wa kienyeji
anayejigamba kuwa anazo dawa
za kuongeza nguvu za kiume, na
matangazo hayo hayaishii
magazetini tu, bali hata redioni pia
yapo.

Mbaya zaidi dawa zinazoongelewa
hupewa majina mengi ya
`kusisimua` kama kombora, simba
na nyati siushasikia mziki wa nyati
akikasirika sasa jenga picha nuvu
ya hiyo dawa, hata hivyo, dawa
nyingi ni uzushi tu na hupewa
majina hayo ili kuwavuta wateja
na kuwashawishi kuzijaribu,
enewei ndivyo biashara zilivyo.

Wingi huu wa matangazo
umeanza kuonekana katika miaka
ya hivi karibuni, na kadiri siku
zinavyozidi ndivyo idadi ya
waganga wanaojigamba kuwa na
dawa hizo inavyozidi kushamiri,
kuna waganga wenye dawa za
Kiswahili, Kiarabu na za Kichina
ndio usiseme!

Binafsi utitili wa matangazo haya
umenifanya niamini kuwa, kuna
tatizo kubwa la wanaume
kupungukiwa nguvu hizo, na
ingawa hakuna utafiti wa
kitaalamu uliofanywa rasmi, lakini
inaonyesha kuwa tatizo hilo kwa
sasa ni kubwa sana na si Tanzania
tu, bali ni dunia nzima.

Kutokana na hali hiyo ndipo
waganga wa kienyeji pamoja na
makampuni mengi makubwa
duniani hujaribu kuelekeza nguvu
zao katika kufanya utafiti wa
kutengeneza dawa za kusaidia
watu wenye tatizo hilo, na bahati
nzuri kwa makampuni na
waganga hao ni kwamba
inaonekana kama biashara
inawaendea vizuri.

Kwa mujibu wa utafiti wa taasisi
moja ya biashara ya dawa za aina
hiyo nchini Uingereza, imebainika
kuwa asilimia 46 ya wanaume
nchini humo hutumia dawa hizo,
hata hivyo wengi wao huzitumia
bila ya kupata ushauri wa daktari
na maduka mengi ya dawa
yametozwa faini kwa kuwauzia
dawa hizo bila ya kuwa na vyeti
vya daktari.
Kupungua kwa nguvu miongoni
mwa wanaume wengi
kumesababisha wengi wao waishi
katika maisha na hali ya
usononekaji na wengine
wamekumbwa na umauti
kutokana na hali hiyo ya kuishi na
sononi kwa muda mrefu.

Kuna mambo mengi
yanayosababisha wanaume wengi
wajikute wakipungukiwa nguvu za
kiume, wataalamu wa masuala ya
saikolojia wanaamini kuwa mara
nyingi suala hilo, hasa kwa watu
wenye umri wa chini ya miaka 45,
husababishwa na msongo wa akili
kuliko ufanyaji kazi wa misuli ya
mwili.

``Watu wengi wanaofikiri kuwa
wamepungukiwa na nguvu hizo
huwa hawako hivyo,`` inasema
sehemu moja ya utafiti uliofanywa
na wataalamu wa Chuo Kikuu cha
Havard, nchini Marekani na
kufafanua kuwa:
``Tatizo la watu hao huwa ni
kushiriki tendo hilo kwa wakati
usio muafaka kwao, wanashiriki
wakati bado hawajajitayarisha
kiakili au wanapokuwa
wamejitayarisha, basi `njiani`
hukutana na wenzi ambao
hawaafiki mwelekeo wa `safari`
yao``.

Wataalamu wa masuala ya
vyakula nao wanaeleza kuwa
tatizo hilo huwapata wanaume
wengi kwa sababu ya utumiaji wa
vyakula vyenye kuongeza kiwango
kikubwa cha mafuta mwilini
ambao hawashiriki katika mazoezi
ya viungo ambayo huifanya misuli
ya damu mwilini kutokufanya kazi
vizuri na hivyo kusababisha
matatizo mengi ya mwili
kushindwa kufanya kazi zake
vizuri.

Kumbukumbu yangu inaonesha
kuwa, Mheshimiwa Mbunge wa Viti
maalumu kuputua tiketi ya Chama
Cha Mapinduzi, Janet Bina Kahama,
10 Aprili 2007 katika kikao cha
saba cha bunge aliulizwa swali
ambalo lilikuwa namba 8 lenye
kipengele a, b, na c ambapo
kwenye kipengele b aliuliza: Je,
serikali inafahamu ni sababu gani
zinasababisha kupungua kwa
nguvu za kiume kunakotangazwa
sana na waganga wa jadi?

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, wakatik huo
Prof. David Homeli Mwakyusa
alijibu kuwa, Upungufu wa nguvu
za kiume unasababishwa na
mambo mengi, baadhi yao ni lishe
duni hasa mboga za majani,
kutokula aina mbalimbali za jamii
ya karanga (nuts), matumizi
yasiyofaa ya ulevi kama pombe,
sigara na dawa za kulevya, dawa
zinazotibu baadhi ya magonjwa
kama kisukari, shinikizo la damu,
magonjwa ya akili na vilevile
kutopumzika kunakosababishwa
na shughuli nyingi za kijamii hivyo
kusababisha uchovu.

Lakini ni kweli dawa hizi za asili
zinauwezo wa kutatua tatizo la
upungufu wa nguvu za kiume?
Pro. Mwakyusa anathibitisha kwa
kusema kuwa, dawa nyingi za tiba
asili ni virutubisho ambavyo
muhitaji angeweza kuvipata
endapo angekula vyakula vyenye
virutubisho hivyo.

Pamoja na kuwa dawa hizo
hazijafanyiwa utafiti wa sayansi ya
leo na kutokana na unyeti wa usiri
wa watumiaji wa dawa hizo
zingekuwa na madhara
zisingetumiwa na wananchi hata
huko zinakotoka yaani maeneo
yake ya asili.
Na kusisitiza kuwa, Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii haijapokea
taarifa ya tukio kutoka kwa
walalamikaji wanaotumia dawa
hizo za kuongeza nguvu za kiume.
Hata hivyo, hali ni tofauti kidogo
katika nchi zilizoendelea kama
Marekani na baadhi ya nchi za
Ulaya, matumizi ya dawa hizi
hutolewa kwa watu baada ya
kuandikiwa cheti na daktari, na
watu wenye matatizo ya
msukumo wa ndamu (BP), mara
nyingi wamekuwa wakishauriwa
kutotumia dawa hizo kwa sababu
ni hatari kwa maisha yao.

Hii ni kwa sababu dawa nyingi,
kama Viagra, Ciallis, Levitra,
Yohimbine na nyingine mbali ya
kuwa na nafasi ya kusababisha
magonjwa ya moyo, kwa watu
wasiokuwa nayo, pia yana
madhara mengine kama vile
kusababisha upofu na kuleta hali
ya mwili kuwa na kitetemeshi.
Madhara mengine ya dawa hizo ni
pamoja na kumsababishia
mtumiaji hali ya kuumwa na
kichwa mara kwa mara, macho
kuwa mekundu, kuziba kwa hewa
puani na maumivu ya tumbo
pamoja na kuharisha.

Haya ni aina ya madhara
yanayotokana na dawa za kizungu,
ambazo kabla ya kuingia
madukani kufanyiwa utafiti wa
kina kuangalia madhara yake kwa
watumiaji, na ingawa hayo yote
yanafanyika lakini bado athari
zake kwa watumiaji zinaonekana.
Mwandishi na muandaaji
mkongwe wa filamu nchini
ambaye kwa sasa anaishi
Marekani, Chemi Che-Mponda
alishawahi kuandika makala
isemayo ‘kukosa nguvu za kiume si
mwisho wa dunia!’ na katika
makala hiyo kulikuwa na hadithi
hii isome ili ujue kinachoweza
kukutokea kwa kujifanya mjuaji na
kuagiza dawa za kuoneza nguvu
kwenye mtandao.

Chemi alianza hivi: “Jamani,
jamani, jamani, kuna jirani yangu
kafa hivi majuzi. Alikuwa ni baba
wa makamu, mmarekani mweusi.
Alikuwa mcheshi na ilikuwa kila
tukionana lazima tusalimiane.
“Mara ananinunulia kahawa halafu
tunakaa namsimulia kuhusu Afrika.
Yule baba, alionekana mzima na
mwenye afya fiti kabisa. Nilibakia
kushangaa kusikia kafa na si kwa
ajali. Mke wake alifariki mwaka
juzi, lakini miezi ya karibuni
alikuwa anaonekana mwenye
furaha kwa vile alipata mpenzi,
dada mwenye miaka 25 hivi.

”Story niliyosikia ni hivi: Kumbe
jamaa alikuwa na matatizo ya
moyo. Alifia kitandani akiwa
kwenye shughuli ya kufanya tendo
la ndoa na mpenzi wake. Tena
wanasema alifariki mara alipofikia
kilele cha tendo.“Navyosikia
ilikuwa ni ‘massive heart attack’.
Kama ni massive bila shaka na
utamu wa shughuli hakujua kuwa
yuko hatarini. Mpenzi wake alipiga
sana kelele, majirani walipigiga
simu 911 (polisi) kwa vile
walidhania wameingiliwa na
majambazi.

“Kumbe jamaa alikuwa mtumizi
wa Viagra, yaani vile vidonge vya
kuongeza uume, na kumpa
mwanaume uweza wa kufanya
tendo la ndoa. Ndugu zake
wanalamika kweli, maana
hakuzipata kwa prescription
(maelezo) ya daktari, alizaiagiza
kwenye mtandao (internet).
Hiyo ni baadhi ya mifano hai
inayoonesha wazi madhara
unayoweza kupata kwa kuamua
kutumia tu dawa bila maelekezo
kutoka kwa daktari!

Binafsi nina hofu juu ya dawa ‘za
kienyeji’ zinazotengenezwa na
waganga na kuuzwa kama
karanga kila kona ya miji
mbalimbali ya Tanzania bila ya
kufanyiwa utafiti wa kina, ni wazi
kama kanuni za kiafya
zinavyosema, kuwa kila dawa ina
madhara yake, lakini je, ni nani
anapima madhara mabaya
yatokanayo na dawa hizi za
kienyeji zinazouzwa kama njugu?
Ukiacha madhara yatokanayo na
dawa hizo, pia wanaume wengi
hukumbwa na tatizo hili la
kupungukiwa nguvu kwa sababu
ya uvutaji wa sigara kwa wingi,
utafiti mbalimbali wa kitabibu
duniani unaonyesha kuwa
matumizi ya bidhaa zitokanazo na
tumbaku huwasababishia
wanaume upungufu wa nguvu
hizo.

Ni kweli ulio wazi kwamba tatizo
la wanaume wengi kupungukiwa
nguvu za kiume nchini kwetu na
duniani kote linazidi kushika kasi
na tiba mbadara zinahitajika ili
kurudisha heshima na furaha
miongoni mwa wanaume wengi
duniani, lakini utumiaji wa dawa
za kuongeza nguvu haupaswi
kufanyika kiholela kwa kuzingatia
kuwa matatizo yake kiafya ni
makubwa kuliko faraja ya muda
mfupi anayopata mtumiaji!

Siku moja nilikuwa nimekaa
kwenye kijiwe cha kahawa
Kariakoo jijini Dar es Salaam
nikachokonoa wazee kwa
kuchomekea mada hii, mambo
mengi walinieleza lakini kubwa
zaidi ni kuwa, vijana wa siku hizi
wanakubwa zaidi na tatizo hili
kutokana na kufakamia vyakula
visivyo vya asili na kusahau kuwa,
miogo, asali, karanga na pweza
huweza kukusaidia ukawa na
nguvu kama nyati. Vyakula vingi
vinavyoingizwa nchini vikiwa
vimesindikwa ambavyo vijana
wengi hukimbilia na kujiona kuwa,
babu kubwa wakivila hivyo na
kumcheka mzalendo anayepata
muogo wa kuchoma na chachandu
huku akishushia na juisi ya mua
pale Kariakoo bila kujua kuwa
sehemu kubwa ya aina nyingi ya
vyakula wanavyokula ni sumu
yenye ladha nzuri
inayonenepesha!

Madhara yake ni
mengi na miongoni mwake ni
kuwasababishia watumiaji kukosa
nguvu za kurudia tendo.
Hata hivyo, kuna wakati pia
upendo unapopungua na mvuto
unapungua baina ya wanandoa,
mwanaume anaweza kujikuta kila
akiwa faragha anashindwa
kuendesha gari kwa muda mrefu
na anaweza kudhani kuwa ana
matatizo kumbe hali hiyo
inamkumbwa kutokana na
kutokuvutiwa na mwenzi wake.

Tatizo kama hili linaweza
kutatuliwa kwa kumueleza wazi
mkeo ama mpenzi wako jinsi gani
anaweza kujipanga na kuonekana
na mvuto wa hatari utakaokufanya
uchanganyikiwe kila umuonapo na
hata mkiingia kwenye mambo
fulani basi kwa hakika
utahamasika na kutoa dozi ya
maana.

Uchovu wa kazi za ajira
Mkufunzi wangu wa saikolojia
katika Chuo Kikuu cha Tumaini
Iringa ambaye ameshatanulia
mbele za haki, Pro. Samuel Mshana
(Mungu amlaze mahali pema
peponi) aliwahi niambia kuwa
wanawake wanataka security
kutoka kwa mwanaume nami
nikamtania Pro. Sasa mbona mimi
na mwili mdogo nitampa ulinzi
gani mwanamke akacheka kisha
akaniambia ulinzi naouzungumzia
ni wa jumla ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha mambo yanakwenda
sana ndani ya nyumba yani watoto
wanakwenda shule na mambo ya
mlo wa uhakika.

Hivyo ni wazi kuwa wanaume
huhangaika kwa kiasi kikubwa
kuhakikisha wanamudu majukumu
yao ya kila siku na huko makazini
kuna mauzauza mengi na usiombe
ufanye kazi kwenye kampuni
binafsi kila kukicha wewe upo
roho juu sasa katika hali kama hiyo
ukikutana na mwenzi wako
kunako majambozi utahisi una
upungufu wa nguvu za kiume
kwani mara tu baada ya kumaliza
mshindo wa kwanza hutoweza
kurudia tena! Hali ni hivyo hivyo
kwa watu wanaofanya kazi nzito
zinazosababisha wajikute
wanarudi majumbani wakiwa
wamechoka.

Hivyo basi, endapo nawe ni
miongoni mwa watu
wanaokumbana na tatizo la
kushindwa kurudia majambozi
kwa sababu ya uchovu na msongo
wa mawazo kutoka kazini
hakikisha unapanga muda
muafaka na mwenzi wako
kupeana raha.

Mfano kama Jumamosi unafanya
kazi nusu siku ukitoka usiende
kulewa kama ni mtu wa kinywaji
bali nenda kapumzike kisha kesho
yake waweza kumtoa out mama
na kwenda mazingira tofauti
kupeana kitu roho inapenda
hakika utajishangaa jinsi
utakavyomudu majambozi.
Kuchacha
Nakumbuka vema miaka ya 1990
enzi hizo Redio Tanzania pekee
ndio ilikuwa ikitupa burudani na
moja kati ya nyimbo ambazo
ilikuwa ikinikuna ni ‘kuchacha
usiombee’ iliyoimbwa na Juwata
Jazz na hichi ni kibwagizo chake
‘Maradhi yote ugua lakini kuchacha
usiombe…’ ebwana usije ukawa
katika hali mbaya kifedha na kila
jambo unalolipanga linakwenda
ndivyo sivyo hali
inayokusababishia uchache kisha
mwenzi wako akakuomba
unyumba hapa kuna mawili ama
kuchelewa sana kufika safari yenu
ama kumaliza halaka kisha jamaa
analala chapchap na hataki tena
kuonesha ushirikioano hata
mamaa akimbembeleza vipi!

Hivyo basi, si vema kukutana
kimwili na mwenza wako kipindi
ukiwa umechacha kwani wanaume
wengi pindi wanapokuwa na
msongo wa mawazo hukimbilia
kuomba unyumba kwa wenzi wao
wakiamini kuwa, wao ndio
watawasaidia kuwapunguzia
mawazo badala ya kutafuta njia
mbadara ya kumaliza tatizo.

Kuishiwa hamu ya nyama na
mapishi yale yale kila siku
Uzoefu wangu unanionesha kuwa
wanaume wengi hujikuta
wakikosa hamu ya kurudia tendo
la ndoa mara bada ya kumnaliza
mzunguko wa kwanza kutokana
na wake zao kutowaonesha
ubunifu yaani kila siku ni kifo cha
mende tu hakuna jipya
linaloongezwa hata nakshi za
miguno ni ile ile hali
inayosababisha wanaume wakose
hamy ya kuendelea mara baada ya
kumaliza mzunguko wa kwanza.

Wanaume wengi hujikuta
wanalazimika kutafuta kimada ili
kupata radha mpya na huko
mambo huwa mulua kwani
hufanikiwa kwenda raundi hadi
tatu na bado akawa na hamu kwa
vile tu amekutana na vitu adimu
hivyo basi, mwanaume anapaswa
kumueleza wazi mkewe kuwa
anahitaji wakutane faragha
ambapo anataka vutu hadimu vya
kabatini na si kumsaliti mwenza
wako kwani uwezo wa kumfanya
awe bora kunako majambozi unao
wewe mnwenyewe mwanamme.

Mfano siku akikwambia
anakwenda kwenye kitchen party
mruhusu kisha akiwa huko
mtumie meseji kuwa, “mpenzi
najiandaa kumalizia sehemu ya pili
ya soma ulilojifunza yaani la
vitendo, hakika leo nitafaidi”
asikdanganye mtu hapo hata kama
bi. Harusi mtarajiwa
hakufundishwa mambo fulani ya
kumpagawisha mumewe
atahakikisha hakuangushi atakuja
na mambo mapya na hapo ndipo
mwanaume hujikuta akiganda
kifuani.

Nimalize kwa kusema kuwa,
hakuna haja ya kukurupuka na
kukimbilia kununua dawa za
kuongeza nguvu ya kiume bila
kutafakari kwa kina chanzo cha
tatizo lako kwani yawezekana
tatizo ulilonalo linaweza kutatulika
kwa njia nyingine ambazo
hazitakufanya uwe hatarini.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger