Search in This Blog

Showing posts with label AMANDA. Show all posts
Showing posts with label AMANDA. Show all posts

AMANDA WA BONGO MOVIE AFUNGUKA NA KUSEMA " HAJAMUONA MWANAUME SAHIHI WA KUZAA NAE

Staa wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’
STAA wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa mpaka sasa hajazaa kwa sababu bado alikuwa hajamuona mwanaume wa kuwa baba watoto wake.
 
Akichonga na gazeti hili, Amanda alisema katika maisha yake anapenda sana mtoto lakini bado hajatokea mwanaume sahihi wa kuzaa naye ila anashukuru kwa sasa amempata. 
“Miaka yote sijazaa kwa sababu nilikuwa sijamuona mwanaume sahihi wa kuzaa naye, lakini kwa sasa nimemuona japokuwa siwezi kumtaja kwa sababu bado naye nipo katika hatua za mwisho za kumpitisha kama anafaa,” alisema Amanda.

AMANDA AANIKA CHANZO CHA TABIA CHAFU YA USAGAJI KWA MASTAA!

MSANII wa filamu, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefungukia sababu za baadhi ya mastaa kujiingiza kwenye tabia chafu ya usagaji akidai kuwa, kutendwa na wanaume ndiyo chanzo cha yote.
Tamrina Poshi ‘Amanda’.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Amanda alisema maudhi ambayo baadhi ya mastaa wamekuwa wakiyapata kutoka kwa wapenzi wao waliotokea kuwapenda ndiyo husababisha baadhi yao kuona suluhisho ni kuhamia kwenye usagaji.
“Wasanii wanajiingiza huko sababu wanaumizwa na wanaume, wanadhani usagaji ni raha, wanaona hii ni njia sahii ya kujituliza,” alidai Amanda huku akikwepa kujibu swali la kama naye yumo kwenye kundi la wasagaji ama laa.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger