Staa wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’
STAA wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’
amefunguka kuwa mpaka sasa hajazaa kwa sababu bado alikuwa hajamuona
mwanaume wa kuwa baba watoto wake.
Akichonga na gazeti hili, Amanda alisema katika maisha yake anapenda
sana mtoto lakini bado hajatokea mwanaume sahihi wa kuzaa naye ila
anashukuru kwa sasa amempata.
“Miaka yote sijazaa kwa sababu nilikuwa sijamuona mwanaume sahihi wa kuzaa naye, lakini kwa sasa nimemuona japokuwa siwezi kumtaja kwa sababu bado naye nipo katika hatua za mwisho za kumpitisha kama anafaa,” alisema Amanda.