Search in This Blog

Showing posts with label UKATILI. Show all posts
Showing posts with label UKATILI. Show all posts

UKIO LA JAMAA ALIYEMPASUA KICHWA MTOTO KISHA KULA UBONGO WAKE.

HKHKAsubuhi ya July 18 kutoka Moshi zilitoka taarifa za mfanyakazi wa ndani wa kiume [Houseboy] kumpasua kichwa mtoto mdogo wa darasa la 3 kisha ubongo wake kuamua kuutafuna.
Baada ya kumaliza tukio hilo kilichofuata ni yeye kujikata sehemu zake za siri,Hapa utawasikiliza mashuhuda wa tukio hili pamoja na kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro.

Bonyeza play kusikiliza.

PICHA ZAIDI 10 ZA KUTISHA: SAKATA LA BABA ALIYEMUUA MWANAE JIJINI MBEYA KWA KUMZIKA AKIWA HAI

Marehemu Debora Riziki miaka 3 enzi za uhai wake

Riziki Mwangoka kulia anaetuhumiwa kumzika mtoto wake akiwa hai



Hapa maiti ya mtoto Debora ikiwa imetolewa nnje mara baada ya kufukuliwa ndani ya nyumba ya baba yake mzazi 

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI TUNAZOZIONYESHA



Mwili wa marehemu Debora ukionyeshwa kwa mzazi na kudhibitisha kuwa ndiye mwenyewe aliyemfukia 

Mwili wa mtoto Debora ukiandaliwa kwa kuzikwa kwa heshima zote


Mwili wa Debora tayari kwa kuzikwa

Hatimae sasa Debora anazikwa


Mara tu baada ya mazishi baba mzazi wa Debora anapelewa kituo cha polisi Tukuyu




Mama mzazi wa marehemu Debora asimulia kisa chote

Mama mzazi wa Marehemu, Esther Mwambenja, alisema kabla ya tukio hilo kutokea kulikuwa na viashiria vingi vya mumewe kufanya ukatili

Bibi wa marehemu Debora 


Tukiwa na baadhi ya waandishi wenzangu tukiendelea kupata historia fupi ya marehemu Debora toka kwa mama yake mzazi

Novemba 15 mwaka 2012 serikali ya kijiji chini ya Mwenyekiti, Lutengano Mwakyoma na mashahidi watano wakiwemo wazazi na ndugu zake, walinikabidhi barua ya kuridhia kuondoka na mwanangu, huku ikimuonya mume wangu kutorudia kosa hili la kumuiba mtoto hadi hapo atakafikisha miaka saba.


Dada wa marehemu Debora, Neema Stevini(5) kulia ambaye ni mtoto wa kufikia wa baba mzazi wa marehemu, akisimulia jinsi mdogo wake alivyoibwa , alisema kuwa anakumbuka mara ya mwisho ilikuwa jioni majira ya saa 12 jioni. 

“Nilitaka kwenda nao, lakini baba Debora akaniambia nirudi kuchochea moto ndani na niliporudi nikakuta wameondoka na nilipokimbilia sana siku waona” alisema kwa masikitiko Neema. 

MKASA wa baba kumuua mwanae kwa kumzika akiwa hai kutokana na mgogoro wa ndoa, umezidi kuibua mapya, baada ya mama mzazi wa marehemu ,Debora Riziki (3), kusimulia mkasa mzima . 

Akizungumza kwa hisia kali, katika mahojiano maalumu na Mbeya yetu kijijini kwake Ibula, katika kata ya Kiwira, wilayani Rungwe, Mama mzazi wa Marehemu, Esther Mwambenja, alisema kabla ya tukio hilo kutokea kulikuwa na viashiria vingi vya mumewe kufanya ukatili. 

Alisema tukio la mzazi mwenza huyo kumwiba mtoto na kwenda kumfanyia ukatili huo wa kinyama lilikuwa la pili, baada ya awali kumuiba akiwa na miaka miwili na miezi mine na alimrudisha kwa maandishi ya serikali ya kijiji. 

Alisema katika tukio la kwanza la mtalaka wake huyo kumuiba mtoto wao huyo, lilitokea Septemba mwaka 2012, baada ya wiki chache za kumfukuza katika nyumba waliyokuwa wakiishi katika kitongoji cha Iponjola, kijiji cha Asenga, nyumba iliyotumika kuzikwa mtoto huyo. 

Alitaja sababu za yeye kufukuzwa ni ugomvi uliotokana na yeye kuhoji sababu za kuficha fedha kiasi cha sh. 120,000 zilizotokana na wao kwa pamoja kufanya kazi ya kibarua katika mashamba kijijini hapo na baada ya malipo kutolewa mtalaka wake huyo alionesha kiasi kidogo cha sh.80,000. 

Alisema ugomvi huo ndio ulisababisha yeye arudishwe kwa wazazi wake, lakini baada ya muda mfupi mwanaume huyo alimfuata na kumbembeleza ili warudiane na alipogoma aling’ang’ania aondoke na mtoto . 

“Nakumbuka ilikuwa Novemba mwaka jana baada ya mimi kuondoka nyumbani kwake na kurudi kuishi hapa nyumbani, siku hiyo tukiwa shambani huyo bwana alikuja hapa nyumbani na kumkuta mwanangu wa kwanza (Neema Steven ) niliyezaa na mwanaume mwingine” alisema Mwambenja. 

Alisema baada ya kufika eneo hilo majira ya saa mbili asubuhi alitumia ujanja na kufanikiwa kumuiba mtoto na kisha kutokomea naye kijijini kwao Asenga, hali ambayo ilisababisha kutoa taarifa kituo cha polisi Kiwira. 

“Unajua kuwa baada ya kwenda kutoa taarifa polisi walitusaidia kufika kijijini kwao ambapo serikali ya kijiji ilikubali nimchukue mwanangu kwa kuwekeana mkataba wa kisheria kwa mujibu wa sheria, kwani alikuwa chini ya miaka saba”. 

Aliongeza kuwa Novemba 15 mwaka 2012 serikali ya kijiji chini ya Mwenyekiti, Lutengano Mwakyoma na mashahidi watano wakiwemo wazazi na ndugu zake, walinikabidhi barua ya kuridhia kuondoka na mwanangu, huku ikimuonya mume wangu kutorudia kosa hili la kumuiba mtoto hadi hapo atakafikisha miaka saba. 

Tukio la pili la kuiba mtoto. 

Alisema tukio hilo lilitokea Novemba 29 mwaka jana 2012, ambapo alifika nyumbani kwao majira ya saa 12 :00 na kumkuta dada wa marehemu kumchukua mtoto akimdanga kuwa anaenda kusenya kuni eneo la jirani. 

Aliongeza kuwa baada ya kuona dada wa marehemu anang’ang’ania kwenda wote alimuamuru arudi nyumbani kuchochea moto kwa kuwa kulikuwa kumeinjikwa mboga na kukubali kurudi. 

“kwa mujibu wa maelezo ya mwanangu huyu wa kwanza alisema baada kurudi toka ndani, alikuta baba yake huyo ameondoka na mtoto na tuliporudi na kupokea taarifa hizo tulichanganyikiwa na kuanza kuhangaika hovyo” alisema mama wa marehemu. 

Mwambenja alisema kuwa baada ya kucha siku ya pili asubuhi yake walienda kutoa taarifa kituo cha polisi cha Kiwira ili waweze kupata msaada wa kumtafuta, huku wakionesha barua ya makubaliano ya awali ya yeye kuwa na haki ya kisheria ya kusimamia malezi ya mwanao hadi afikishe miaka saba. 

Alisema baada ya kutoa taarifa hizo kituoni hapo, askari aliyekuwa zamu siku hiyo alimtaka kutoa kiasi cha shilingi 50,000 ili fedha hizo wapewe askari mgambo wa kwenda kijijini kwa mzazi mwenzake huyo, kwani tayari walikuwa na taarifa kuwa alikuwa amekimbilia huko. 

“Kutokana na hali ngumu ya maisha tulikosa kiasi hicho cha fedha hivyo suala hilo kubaki bila msaada wa polisi na pia hatukuweza kwenda kwa kijijini kwao”. 

Aliongeza “sababu ya mimi kuwa mzito kuendelea kumfuatilia kijijini kwao kwa mara ya pili ili kujua kama yupo huko na mtoto ilitokana na hofu niliyoijenga, kwani awali tukiwa kwenye ugomvi alitamka maneno ya vitisho kuwa endapo nitaendelea kung’ang’ania kumchukua mtoto pale anapomchukua atakuja kumuua ili tukose wote”. 

Hata hivyo mama huyo mzazi wa Debora, alisema kuwa baada ya kuona hali hiyo, aliendelea kuwasiliana na wifi yake , Bupe Mwangoka,ambaye ni dada mkubwa wa mume wake anayeishi eneo la Isanga Jijini mbeya, ambaye ndiye alisaidia kwa kiasi kikubwa kubainika kwa unyama aliofanya. 

Maisha kabla ya tukio. 

Akielezea maisha yao kabla ya kutengana na baadae kuamua kufanya ukatili huo, alisema aliwahi kumtamkia maneno makali wakati akiwa na ujauzito wa miezi nane . 

Alisema baada ya kuibuka ugomvi katika kipindi hicho, mwanaume huyo alimtaka kwenda kuiuza mimba ile kwa mwanaume mwingine yeyote atakayempenda ili asije akazaa mtoto ambaye atachanganya damu ya koo hizo mbili. 

“Maneno yale katika kipindi hicho sikuyatilia maanani kwani nilifikiri zilikuwa ni hasira, lakini leo hii ndio najua maana ya ile kauli ” alisisitiza Mwambenja. 

Hata hivyo alisema inashangaza kwani kuna wakati tukiwa katika maisha ya kawaida kabla ya yeye kufanya tukio hilo, mara kadhaa alijutia na kuonya juu ya matukio machafu yaliyojitokeza na kusikika ya watu kuuawa au kuondolewa baadhi ya viungo vya miili yao. 

Aidha, alieleza mkasa mwingine wa mume wake huyo ni ule wa wao kufukuzwa katika mji wa Kiwira walikokuwa wakiishi awali kwa kufanya shughuli za umachinga. 

Alisema walitimuliwa na serikali ya mtaa katika mji huo kutokana na mumewe huyo kutuhumiwa kuiba simu ya mkononi ambapo alipokea kipigo kikali na baadae kufukuzwa. 

Kutokana na hali hiyo, mama wa marehemu Debora alisema yote yaliyotokea amemwachia mungu na kwamba kama ingekuwa uwezo wake angeamuru naye anyongwe, hivyo mamlaka husika zitajua cha kufanya. 

Kwa upande wake dada wa marehemu Debora, Neema Stevini(5) ambaye ni mtoto wa kufikia wa baba mzazi wa marehemu, akisimulia jinsi mdogo wake alivyoibwa , alisema kuwa anakumbaka mara ya mwisho ilikuwa jioni majira ya saa 12 jioni. 

“Nilitaka kwenda nao, lakini baba Debora akaniambia nirudi kuchochea moto ndani na niliporudi nikakuta wameondoka na nilipokimbilia sana siku waona” alisema kwa masikitiko Neema. 

Hata hivyo uchunguzi wa Mbeya yetu umebaini kuwa marehemu Debora alifariki dunia siku hiyo ya Novemba 29 mwaka jana, majira ya saa nne usiku baada ya baba yake kufanikiwa kumuiba kutoka nyumbani kwa mama yake. 

Inadaiwa kuwa baada ya kufanikiwa kumtorosha baba huyo wa marehemu alitembea kwa mguu umbali wa kilomita 50 kutoka kijiji cha Ibula alikomuiba hadi nyumbani kwake kijiji cha Isange katika kata ya Isange. 

Imeelezwa kuwa baada ya kufika nyumbani kwake, baba huyo mzazi wa marehemu alichimba shimo katikati ya sebule na kumchukua mtoto wake huyo akiwa usingizini na kisha kumfukia akiwa hai. 

“Mwanaume Yule alikuwa katili sana, kwani baada ya kumfukia alichukua meza ya chakula na kuiweka juu yake huku akiipamba kwa magazeti jambo ambalo lilifanya ndugu zake wasigundue kirahisi” alisema mpasha habari. 

Chanzo hicho kilisema baada ya kufanya hivyo aliishi kwa wiki moja na baadae kukimbilia Jijini Mbeya ili watu wasibaini juu kitendo alichofanya na kwamba kila alipohojiwa na ndugu zake alisema mwanae huyo alimuweka kwa rafiki yake Jijini Mbeya. 

Hata hivyo baada ya danadana za muda mrefu ndipo dada wa mtuhumiwa huyo aliamua kutoa taarifa jeshi la polisi na kufanikiwa kumkamata akiwa katika harakati za kutorokea wilayani Chunya na alipobanwa alifichua siri ya alipo mwanae kwa kueleza kuwa alimuua na kumfukia ndani kwake.

MUME KUMCHINJA MKEWE ARUSHA, HABARI KAMILI IPO HAPA

Dada wa Lucas Lomayany Molel (37) anayesakwa kwa kumuua mkewe wa ndoa, Agnes Lucas (24), akiwa katika chumba kilichotumika kwa mauaji hayo.
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linamsaka kwa udi na uvumba, muuza nyama jijini hapa, Lucas Lomayany Molel (37) mkazi wa Ilboru kwa madai ya kumuua mkewe wa ndoa, Agnes Lucas (24) kwa kumcharanga na sime kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.
Chanzo cha habari kimeliambia Amani kuwa, tukio hilo la kutisha lilitokea usiku wa kuamkia Julai 7, mwaka huu, nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo baada ya kutekeleza mauaji hayo aliufunika mwili wa marehemu kwa shuka na kuendelea kulala nao kitandani hadi alfajiri alipotoroka. 
Akisimulia kuhusu mauaji hayo, ndugu wa marehemu aitwaye William Lomayany alisema usiku wa tukio, saa 4, mtuhumiwa alirejea nyumbani kwake na kutomkuta mkewe, akamsubiri hadi saa 6 usiku, mke akarejea.
Godoro la kitanda alipokuwa analala marehemu, Agnes likiwa limechafuka kwa damu.
Alisema marehemu baada ya kufunguliwa mlango na kuingia, alivua nguo zote na kubaki na ‘kufuli’ ambapo alijifunga kanga na kupanda kitandani kulala. Mtuhumiwa alimfuata chumbani na kumhoji kuhusu kuchelewa nyumbani hadi muda huo na ndipo mzozo ulipoanza. 
William alizidi kusema kuwa, wawili hao walianza kugombana kwa maneno lakini baada ya muda hali ya utulivu ilirejea, ndipo asubuhi ilipopatikana taarifa za kuuawa kwa Agnes jambo lililotafsiriwa kuwa huenda utulivu huo tayari Agnes alishauawa.
Ndoo ikiwa na damu ya Marehemu Agnes Lucas.
Inadaiwa kuwa, mtoto wa kwanza wa mtuhumiwa, Jessica Lucas (11) ndiye aliyekuwa wa kwanza kufungua mlango wa  chumbani kwa wazazi wake na kumkuta mama yake amelala na damu chapachapa, akaenda kutoa taarifa kwa majirani.
 Ilidaiwa kuwa, baada ya taarifa hiyo, majirani waliingia ndani ya chumba hicho na kuukuta mwili wa marehemu ukiwa umelala kwenye dimbwi la damu huku akiwa mtupu.
Agnes Lucas, enzi za uhai wake, akiwa kwenye picha ya pamoja na mumewe, Bw. Lucas Lomayany Molel.
Akizungumza mbele ya askari polisi waliofika kushuhudia tukio hilo, Jessica alisema baba yake alimwamsha usiku akimtaka atoke kufunga mlango baada ya kutoka ndani. Akajua baba yake anakwenda kazini kama ada.


“Nilikwenda kufunga mlango, baba aliondoka bila kusema chochote. Lakini jana usiku (Julai 6) baba alimpiga sana mama na alinipiga na mimi wakati namwambia amsamehe,” alisema Jessica.
Majirani wa wanandoa hao, wamelaani mauaji hayo na kusema Lucas hakupaswa kumuua mkewe badala yake angewashirikisha watu wengine wakiwemo wazazi wamkanye kama alikuwa akimsaliti.
“Kwa jinsi Lucas alivyokuwa mpole sikutegemea kama angemuua mkewe kikatili, kama  alikuwa akimsaliti angewaeleza wazazi wake ili wamkanye,” alisema jirani yao ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, uchunguzi  unaendelea na jeshi lake linamsaka mtuhumiwa huyo.

HUU NDIO MKASA KAMILI WA KUTEKWA KWA MWENYEKITI WA CHADEMA


MWENYEKITI wa Chadema wilayani Temeke, jijini Dar Joseph Yona,33, ameeleza A-Z sakata la kutekwa, kuteswa kwake na vijana sita wakati akienda nyumbani kwake Mtoni kwa Azizi Ally.

Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Temeke na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Joseph Yona akipelekwa Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) kutoka wodini.
Akisimulia mkasa huo kwa mwandishi wa gazeti hili juzi Jumanne akiwa Hospitali ya Taifa, Muhimbili, Yona ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu, Taifa Chadema alikuwa na haya ya kusema: “ Majira ya usiku nikiwa na baadhi ya vijana wa Chadema Tawi la Ukombozi lililopo karibu na kwangu maeneo ya Benki Klabu, Mtoni kwa Azizi Ally tulikuwa tukiongea.
“Ilipofika saa sita tukatawanjika mimi nikawa naelekea nyumbani, kabla sijafika mbali nikashitukia vijana sita wakinivamia na kunikaba kisha kunivua tisheti na kunifunga usoni,  wakaniingiza katika gari ambalo walikuwa wamepaki pembeni.
“Nilipowauliza mnanipeleka wapi? Wakawa wanajifanya ni askari kwani walikuwa wanasema, ‘tumeshamkamata, tunamleta huko kituoni afande’, tukiwa njiani waliniambia niseme Zitto ni msaliti badala yake nikawaambia kuwa hilo waulizeni viongozi wa juu.
“Baada ya kuona tumesafiri kwa muda mrefu niliwauliza mbona hatufiki kituoni? Wakasema wewe ndiye tulikuwa tunakutafuta, utakiona cha moto, usipokufa utawasimulia wenzako. Walinipeleka mpaka kwenye msitu, baadaye ikafahamika kuwa ni Ununio, Tegeta wilayani Kinondoni. Huko walinipiga sana kisha kunitelekeza katika pori hilo nikiwa nimezimia.
“Baadaye  nilipata fahamu nikajikokota kwa taabu hadi kwenye nyumba moja, nikagonga lakini hawakunifungulia. Nikaenda nyumba ya pili kugonga napo hawakunifungulia. Nyumba ya tatu nilipoigonga wakanifungulia. Walinishangaa na kuniuliza kulikoni umelowa damu? Nikawaeleza kilichonipata.
“Watu hao waliwasiliana na polisi ambao walikuja na kunichukua mpaka hapa Muhimbili nilipofanyiwa uchunguzi nikahamishiwa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi). Lakini kule porini wale watekaji walichukua vitu vyangu kama vile simu mbili na pochi yenye fedha na waliondoka nazo.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, SACP Engelbert Kiondo akiongea na mwandishi wetu ofisini kwake alikiri kutokea kwa tukio hilo. “Msako mkali unaendelea ili kuwabaini na kuwakamata wale waliohusika na unyama huo ili wafikishwe mahakamani,” alisema Kiondo.

MISS AFANYIWA KITU MBAYA NA VIBAKA, SOMA HAPA KUJUA ZAIDI


Ama kweli dunia haina huruma! Dada Happy amejikuta akiishiwa nguvu na kuanguka mbele ya kadamnasi na kuzimia pasipo msaada wowote ambapo badala yake watu waliodaiwa kuwa ni vibaka walimuibia vitu vyake vyote.

Kwa mujibu wa mashuhuda, mrembo huyo ambaye alikuwa katika mishemishe za kawaida alidondoka ghafla akiwa Mitaa ya Nyakato jijini hapa mbele ya kituo cha polisi, Januari 4, mwaka huu.
Ilidaiwa  kuwa baada ya kupoteza fahamu, wahuni walimliza simu pamoja na fedha zote kisha kumwacha akiwa hana msaada wowote.

Hata hivyo, dada huyo alisaidiwa na wasamaria wema ambao walimpeleka Hospitali ya Buzuruga ambapo alipatiwa matibabu na baadaye ndugu zake walipata taarifa kutoka kwa mashuhuda wanaomjua Happy kisha wakaenda kumchukua.
Gazeti hili lilitaka kujua kilichompata mrembo huyo lakini madaktari hospitalini hapo walidai hawawezi kutoa siri ya mgonjwa huku ndugu nao wakiweka ngumu kusema kilichosababisha Happy kudondoka ghafla na kupoteza fahamu.
“Mimi sijui kilichompata lakini sasa hivi hali ni mbaya. Unaweza ukashangaa mtu kasimama halafu akadondoka ghafla na kupoteza maisha. Cha msingi tucheki afya zetu mara kwa mara,” alisema mmoja wa ndugu hao ambaye hakutaka kutajwa gazetini.

AULIWA WENYE MKESHA WA MWAKA MPYA KISA IMANI ZA KISHIRIKINA, TIRIRIKA HAPA



MWILI wa Marehemu Milembe Jengamalulu ukiwa eneo la tukio

Mwanamke mmoja Alifahamika kwa jina la Milembe Jengamalulu anayekadiriwa kuwa na

umri wa miaka 50-55, mkazi wa Ulowa no 4 wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga umri wa miaka 50-55, amefariki dunia baada ya kuchinjwa na watu ambao mpaka sasa hawajajulikana.

Kwa mujibu wa majirani tukio hilo limetokea katika mkesha wa mwaka mpya majira ya saa moja usiku, nyumbani kwake maeneo ya Ulowa no 4 ambapo kikongwe huyo alikuwa anaishi na mtoto wake wa kiume.

Wameeleza kuwa Wakati tukio hilo likitokea, mtoto wake wa kiume ambaye hakutajwa jina lake (miaka 34-40) alikuwa ameenda kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya akiwa na mkewe maeneo ya Ulowa no 5, na wote walirudi nyumbani majira ya saa 10 na usiku ndipo walikuta mwili wa marehemu Milembe Jengamalulu.

Baada ya kuukuta mwili huo ukiwa nje ya nyumba huku ukiwa umetapakaa damu nyingi, huku ukionesha kuwa amechijwa kwa kutumia panga na shoka, walitoa taarifa kwa majirani ambao walisaidia kutoa taarifa kwa uongozi.

Kuuawa kwa kikongwe huyo kunafuatia mfululizo wa matukio mengi ya kuuwawa kwa vikongwe mkoani Shinyanga ambayo yanasadikiwa kuwa yanatokana na Imani za Kishirikina

DOKTA MAARUFU WA KUTOA MIMBA ANASWA, SOMA HABARI KAMILI HAPA


Stori: Waandishi Wetu
MWAKA umeanza, mambo mapya pia yapo! Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers imeingia kazini kwa kasi zaidi. Safari hii imemnasa daktari anayejulikana kwa jina moja la Mambo maarufu sana kwa jina la Dokta Mambo katika jaribio linalodaiwa kuwa ni la utoaji mimba.

Tukio hilo lilitokea katika zahanati yake (jina lipo) iliyopo Kawe jijini Dar es Salaam ambapo daktari huyo anayejulikana sana na wateja wake, hasa akina mama alipoingiliwa na OFM wakishirikiana na polisi baada ya kumuwekea mtego wa mbinu za kishushushu.
MALALAMIKO YA AWALI
Mwishoni mwa Desemba, mwaka jana, mtu mmoja (jina lipo) alituma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda OFM akimlalamikia dokta huyo kwamba amekuwa na mchezo wa kutoa mimba wanawake wakiwemo mabinti wa shule, kitendo alichodai haoni kama ni sawa.

“Naitwa….(jina lipo), nilikuwa naishi Kawe lakini kwa sasa nimehamia Mbezi (hakusema Mbezi gani). Kama hapo ni OFM (Oparesheni Fichua Maovu) naomba mumshughulikie daktari mmoja anaitwa Dokta Mambo wa Kawe. Huyu daktari jamani amekuwa na tabia ya kutoa mimba wanawake hata wasio na matatizo.
“Ninavyojua mimi hakuna hospitali inayoruhusiwa kutoa mimba Tanzania, labda pale ambapo itathibitika kwamba mjamzito ana kifafa, kwa hiyo hatari inakuwepo ya kumpoteza mama au mtoto tumboni ndiyo mimba hutolewa. Wananchi wa Kawe wamekilalamikia kitendo hicho hadi wamechoka. Polisi Kawe wamemshindwa,” alisema raia mwema huyo.
OFM YAANZA KAZI
Baada ya kupokea tuhuma hizo, OFM ilijipanga na kuingia kazini. Ilimwandaa paparazi wa kike na kumtengenezea ujauzito wa bandia na paparazi wa kiume ambaye ni mchumba wake (wa bandia) ili kwenda naye kwa Dokta Mambo kuona kama kweli anajihusisha na kazi hiyo au la!

JUMANNE, DESEMBA 31, 2013
Ilikuwa Jumanne ya Desemba 31, 2013, OFM na paparazi huyo walitia timu kwenye zahanati hiyo na kukutana na dokta huyo ambaye alikubali kumtoa ujauzito paparazi huyo.
‘Mchumba’ wa paparazi huyo alimwambia dokta kwamba wamekubaliana kuitoa mimba hiyo kwa sababu ya hali ya uchumba, daktari akasema haina shida.

AWEKA MASHARTI MAGUMU   
Katika hali ambayo OFM hawakuitarajia, daktari huyo alisema kwa kawaida kabla hajamchoropoa mimba mteja wake lazima aipime kwanza ili kujua ina muda gani.
Zoezi hilo lilikuwa gumu kwa OFM kwa sababu paparazi huyo hakuwa na ujauzito. Ilibidi ‘wateja’ hao waondoke kwa kisingizio kwamba wanakwenda kujipanga kwa fedha aliyoitaka ambayo ni shilingi laki moja na kwamba wangerudi siku iliyofuata (Jumatano).

OFM WAJIPANGA UPYA
‘Wachumba’ hao waliondoka na kuungana na Timu ya OFM ambayo ilikuwa mahali imekaa mkao wa mtego. Baada ya kupata simulizi za ndani ya zahanati hiyo, OFM ilirejea ofisini na kumweleza kamanda mkuu wake ambaye alikaa na timu hiyo na kupanga mpango mpya.

“Bosi, Dokta Mambo ameshakubali, lakini sera zake ni kwamba hawezi kumtoa mimba mjamzito hadi ampime kwanza na kujua ina miezi mingapi. Sasa huyu (paparazi) hana ujauzito, tungekubali ampime tungeumbuka, tukamwambia tunakwenda kusaka fedha kwanza,” OFM  mmoja alimwambia kamanda mkuu.
OFM YATUMWA MTAANI KUSAKA MWENYE MIMBA YA UKWELI
Kamanda Mkuu wa OFM (jina lipo) aliagiza timu yake kuingia mtaani ili kumsaka mwanamke mwenye mimba ya ukweli ambaye ndiye angekuwa na sifa za kutolewa ujauzito na daktari huyo.
Hayo yote yalifanyika baada ya pia uchunguzi wa kina kufanyika maeneo ya Kawe kuhusu tabia ya daktari huyo na kudaiwa kuwa, hawezi kuacha ‘kamchezo hako ka siku nyingi’.

Mjamzito wa kweli alipatikana (jina lipo), akiwa na mimba ya miezi mitatu.  Akashirikishwa katika zoezi hilo ambapo hata yeye aliumia kusikia kwamba kuna daktari anayetoa mimba wanawake hata wale ambao hawana sababu za kufanya hivyo kama sheria za utabibu zinavyotaka.
WATINGA POLISI KAWE
Baada ya kupatikana kwa mjamzito huyo, OFM ilimchukua hadi Kituo cha Polisi Kawe, Dar es Salaam na kuwaambia wahusika kuhusu tabia ya daktari huyo inayolalamikiwa na watu ili ikibidi watoe askari kwa kuungana na OFM kwenda kumtia nguvuni.

POLISI KAWE WAONESHA ‘MAAJABU’
Katika hali ya kushangaza, polisi wa kituo hicho, awali waliwataka OFM watoke nje ili wajadili wao. Baadaye waliwaita na kusema kwamba hawawezi kutoa polisi, kama ishu ni daktari huyo kulalamikiwa na watu, watamwita na kumkanya aache mchezo huo!

“Hatuwezi kushirikiana nanyi katika hilo zoezi, kama ni kweli kuna hayo maneno ya watu, sisi tutamwita tumuonye aache mara moja,” alisema mmoja wa askari wa Kituo cha Kawe.
Katika hali iliyoshangaza zaidi, polisi hao waliwataka waandishi wote walio kwenye msafara kuandika maelezo ya malalamiko kuhusu daktari huyo kwenye kitabu cha ripoti kituoni hapo (Report Book ‘RB’).
Maelezo yaliandikwa. Jina……, umri…., makazi…., kazi…., dini….. na aina ya malalamiko. Baada ya hapo wakatakiwa kuondoka zao.

OFM WARUDI KWA DOKTA MAMBO
Januari 3, 2014, OFM wakiwa na mjamzito wa kweli  walikwenda kwa dokta huyo ambapo kama ilivyo utaratibu wake, alimpima kwanza na kutoa majibu kwamba ana mimba ya miezi 3 na wiki mbili, akasema ni kubwa sana, hivyo zinatakiwa shilingi 160,000.

Hata hivyo, mchumba mtu alisema hana kiasi hicho cha pesa. Ikatokea vuta nikuvute hadi kufikia shilingi 100,000. Ikumbukwe kwamba, mpaka hapo Dokta Mambo hakuwa anajua kwamba mchezo wa pili ni uleule wa kwanza.
“Basi dokta tunaomba tuje kesho na hiyo laki moja,” mchumba mtu alimwambia daktari huyo ambaye alikubali huku na yeye akiomba kuwa, hiyo kesho iwe saa kumi na moja jioni.
OFM, POLISI, MJAMZITO NA MCHUMBA’KE
Kesho yake ilifika, OFM ikiwa na mjamzito huyo akiwa na mchumba’ake walikwenda maeneo ya Kawe jirani na zahanati ya Dokta Mambo kujaribu kupanga namna ya kufanikisha oparesheni hiyo.

Bado tatizo lilikuwa uwepo wa polisi baada ya kubaniwa na wale wa Kawe. Mungu si Athumani, wakiwa wanashangaashangaa eneo, ilipita pikipiki ya askari wa doria ‘Tigo’ na mara moja OFM ikawasimamisha.
Bila kupoteza muda, OFM waliwaeleza polisi wale mchezo mzima ulivyokuwa na kwamba walihitaji msaada wao ili kufanikisha zoezi hilo, walikubali bila kinyongo na mara moja wakaongozana hadi eneo la tukio.
OFM mmoja kati yao aliingia ndani ya zahanati hiyo akijifanya amekwenda kupima malaria, wale polisi wawili na OFM wengine walikaa mafichoni kutega mingo, wachumba nao waliingia mpaka kwa dokta wakiwa na kitita cha shilingi laki moja mkononi.
MJAMZITO APELEKWA CHUMBA CHA KAZI
Baada ya kuwapokea na kutoa kiasi hicho cha pesa, mjamzito huyo alipelekwa chumba kinachodaiwa ni cha kutolea mimba huku mchumba mtu akikaa kwenye fomu kusubiri matokeo.

UTAALAM WA OFM
Kilikuwa kipindi kinachotaka mawasiliano ya hali ya juu, OFM ikitambua kuwa kosa moja goli moja, walikuwa makini kwa mawasiliano. Mjamzito chumbani kumwambia mchumba wake kwenye fomu, naye kuwaambia OFM wa nje hatua kwa hatua.

Katika mazingira hayo, hakuna OFM aliyetakiwa kupokea simu wala kutuma meseji kwa mtu asiyehusiana na kazi hiyo.
TUKIO LANASWA
Ilikuwa wakati daktari huyo akiwa na glovsi mikononi, mjamzito wa kweli akiwa kitandani na nesi mmoja wa kumsaidia daktari wakiwa ndani ya chumba, ndipo OFM na polisi walipovamia na kunasa tukio ambalo lilionekana dhahiri kwamba lilikuwa jaribio la kutoa mimba.

Hapo ndipo Dokta Mambo alipogundua kuwa kumbe ‘kazi’ aliyopewa ilikuwa feki na wale walikuwa makamanda wa OFM wakishirikiana na polisi waaminifu, wazalendo na wanaopenda kazi yao sawasawa.
KWA NINI?
Lilikuwa jaribio la kutoa mimba kwa sababu, ndani ya chumba zilikutwa zana za shughuli hiyo huku mjamzito akiwa kitandani tayari kwa kufanyiwa mchakato.

Huku OFM wakimpiga picha (zipo za kumwaga kwenye maktaba yetu – ukitaka kuziona njoo Bamaga), askari nao wakichunguza mazingira zaidi na kukamata vifaa, daktari huyo alinywea huku msaidizi wake akitokwa machozi.
POLISI WAMWINGIZA NDANI YA GARI
Zoezi hilo lilikamilika kwa daktari huyo kuchukuliwa na askari hao ambao walikodi gari, mmoja akawa na dokta garini akiwa na vifaa vyake chini ya ulinzi, mwingine akiwafuata kwa nyuma na pikipiki.

Askari hao, waliwaeleza OFM kuwa wataitwa Kituo cha Polisi Oysterbay kwa ajili ya kuandika maelezo.
Risasi Mchanganyiko lilimtafuta kwa njia ya simu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camillius Wambura ili kujua kama suala hilo limefika mezani kwake, lakini simu yake haikupatikana muda wote ilipopigwa.

Hata lilipomtafuta Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova ili limsimulie mchezo mzima ulivyokuwa, naye hakupatikana hadi tulipokwenda mitamboni.
Bado tunaendelea kuwatafuta viongozi wa polisi na ukweli wa kina kuhusu namna ishu hiyo inavyoendelea, tunawajulisha katika matoleo yetu yanayofuata.
-GPL

MAMA MJAMZITO WA MIEZI NANE AUINGIA MWAKA MPYA KWA MKOSI, APIGWA RUNGU KICHWANI


Martha Laurent akiwa hospitali baada ya kupigwa rungu kichwani na mumewe Jumanne Suyi.
Stori: Makongoro Oging’
“ILIKUWA siku ya mkesha wa mwaka mpya nikiwa nyumbani Mwembe Yanga, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, mume wangu alifika huku akiwa anapiga kelele na nilipomuuliza akanieleza kuwa leo ndiyo mwisho wangu kwani mimi ni mbwa.

Majeraha aliyoyapata kichwani.
“Nilimweleza kuwa sitaki fujo pia sikupenda tuukaribishe mwaka mpya kwa ugomvi bali kama kuna ugomvi, ulikuwa muda mwafaka kuumaliza.”
Maneno hayo alikuwa akiyasema Martha Laurent ambaye ni mjamzito wiki iliyopita akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wodi ya Mwaisela namba mbili anakojiuguza alipozungumza na gazeti hili.
Aliendelea kusema: “Sikuamini kama mume wangu Jumanne Suyi angeweza kunitia ulemavu kiasi hiki kwani tangu nianze kuishi naye ndani ya mwaka mmoja hatukuwahi kugombana, tumekuwa tukiishi kwa mapenzi ya hali ya juu na tulikula kiapo kuwa hatutapigana na linapotokea kosa tumekuwa tukilitatua sisi wenyewe.
“Asubuhi siku hiyo tuliamka salama huku nikiwa nimemwandalia chakula ili akija kutoka safari zake aje ale kwani aliniahidi kuwa tungeweza kutoka, tukatembee, cha ajabu hata kabla hajala chakula, alichukia akaanza kunipiga.
“Alinipiga na rungu kichwani, nimepata majeraha makubwa sana hadi nikashonwa, sikio langu la kushoto halifanyi kazi, tumbo langu linaniuma sana, sijui kama kiumbe tumboni kimedhurika kwani nina ujauzito wa miezi minne.
“Nilifikishwa hapa hospitali na majirani nikiwa sijitambui, kwa sasa naongea kwa shida nasikia kizunguzungu, sijui kama nitapona, mume wangu atafutwe aulizwe sababu ya kunipiga kiasi hiki, naomba taarifa hizi ziwafikie familia yetu huko Dodoma,” alisema Martha.
Naye Afisa Ustawi wa Jamii Kitengo cha Mifupa MOI, Muhimbili, Mary Ochieng’ alisema kwamba mgonjwa huyo alifikishwa hapo hospitalini akiwa hajitambui na kwa sasa ana mabadiliko na wanatarajia kumfanyia vipimo vingine wakati wowote.

MUME AMKATA MKEWE PANGA MGUUNI KISA KUMZUIA MTOTO KUKEKETWA


MKAZI wa Kitongoji cha Songa Mbele wilayani Tarime mkoani Mara, Modester Mwita,33, amepigwa panga na mumewe kwa madai kuwa hataki mtoto wake wa kike wa umri wa miaka 14 (jina linahifadhiwa) kwenda kukeketwa.

Modester Mwita.
Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita akiwa Hospitali ya Bomani mjini hapa, Modester alisema kuwa tukio hilo lilitokea  asubuhi saa mbili Desemba,13, mwaka jana baada ya kukataa mtoto wake huyo asikeketwe.
“Nilimwambia mume wangu Mwita Daudi kwamba haiwezekani mtoto wetu kwenda kukeketwa kwa kuwa mila hiyo imepitwa na wakati jambo ambalo lilimfanya kupatwa na hasira na kunikatakata kwa panga mguu,” alisema.
Modester aliongeza kuwa alikuwa ameenda mnadani Nyamwigura kupeleka biashara siku ya Desemba 12, aliporudi jioni nyumbani alikuta binti yake na mumewe hawapo ndipo mdogo wake akamwambia mwanaye alipelekwa kukeketwa.
‘’Mume wangu aliporudi nyumbani asubuhi nilimuuliza alikokuwa mwanangu hakunijibu, nilipomueleza kuwa sitaki akeketwe akaanza kunipiga na kunikimbiza kwa panga,” alisema mama huyo na kuongeza:
“Aliponikamata alinikatakata mguuni, wasamaria wema wakanileta hapa Hospitali ya Bomani, yeye ametoroka na sijui hali ya binti yangu huko aliko ikoje,” alisema.

Afisa mmoja wa polisi ambaye hakupenda jila lake liandikwe kwa kuwa siyo msemaji wa jeshi la polisi mkoani humo, amethibitisha kutokea kwa tukio na kuongeza kuwa mtuhumiwa anasakwa ili aweze kufikishwa mahakamani kwa tuhuma zinazomkabili.

INASADIKIWA MEJA WA JWTZ KUUA MADENT

Stori: Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
MKESHA wa Mwaka Mpya (2014) ulikuwa ni kilio, huzuni na majonzi kwa wakazi wa Pugu Kwamustafa, Ilala jijini Dar es Salaam kufuatia Meja wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Rashid Musa (43) kudaiwa kuwaua kwa kuwapiga risasi hadi kufa madenti wawili na wengine watatu kujeruhiwa wakati wakisherehekea mwaka.

Madenti waliouawa ni Ibrahim Mohamed (16), wa kidato cha tatu na Abubakar Hassan (14), wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari ya Kinyamwezi.
Kwa mujibu wa mashuhuda, siku ya tukio, Meja Rashid wa Kikosi cha Jeshi Land Force Kibaha, alidaiwa kuwamiminia risasi vijana hao waliokuwa wakishangilia kuuona mwaka mpya wakati walipokuwa wakivuka barabara.

SHUHUDA NZITO
Kufuatia tukio hilo la kuhuzunisha,  mwishoni mwa wiki iliyopita, Uwazi liliwatafuta mashuhuda wa tukio hilo na kuzungumza nao wanachokijua.

“Kwa jina naitwa Rashid Juma  nina miaka kumi na tatu, nakumbuka siku hiyo tulikuwa watoto wa kike na wa kiume, wengi wenye umri kati ya miaka nane hadi kumi na saba, tulikuwa kama themanini hivi, ilipofika saa sita kamili usiku tuliingia mitaani kushangilia kwa kuuona mwaka mpya.
“Si mara ya kwanza sisi watoto wa mtaa huu kusherehekea mwaka mpya, kila mara tunafanyaga hivyo na kurudi majumbani salama, lakini nashangaa safari hii kipindi hiki hili balaa limetoka wapi?
“Ilipofika saa sita na dakika tano tukiwa tunaendelea kusherehekea huku tukivuka barabara, tulipishana na gari la mwanajeshi huyo, hatukumtukana wala, ghafla tulisikia mlio wa risasi, paa! Paa! Papapa!
“Kabla hatujakaa sawa tulimwona mwenzetu (Abubakar) yupo chini huku akilia kwa uchungu akihitaji msaada, kabla hatujakaa sawa tena risasi ziliendelea kusikika, wengine wakiwa wamedondoka chini.

Mimi na wenzangu wengine tulikimbia, tulijua ni majambazi,” alisema shuhuda huyo, akaendelea:
“Baada ya kutawanyika, tuliliona gari likiondoka katika eneo la tukio, tukapiga kelele, ndipo wazazi wetu wakatoka nje na kuliona lile gari. Wengine walilitambua kwa vile yule mwanajeshi anaishi karibu na maeneo haya, amekuwa akipita na gari lake hilo mara kwa mara.

“Hata hivyo, yule mwanajeshi  hakusimama, nasikia alikwenda hadi kwake, tulirudi na kuwaangalia waliopigwa risasi ndipo tuligundua kuwa wenzetu wawili walikufa na wengine walijeruhiwa.
MAJERUHI AZUNGUMZA
Naye mmoja wa majeruhi aliyejitambulisha kwa jina la Agustina Pius alipohojiwa na Uwazi alisema siku ya tukio alikuwa nje ya nyumba yake akiongea kwa simu na ndugu zake wa mikoani akiwapongeza kwa kuuona mwaka mpya.

“Ghafla nikasikia  milio ya risasi barabarani huku watoto waliokuwa wakisherehekea wakipiga kelele za kusema tunakufa…tunakufa,” alisema majeruhi huyo.
Aliendelea kusema kwamba kufuatia hali hiyo, aliweka simu kwenye mfuko wa suruali na kuingia ndani, lakini ghafla alisikia kitu kimepiga simu yake na kulipuka.

Aliitoa  mfukoni ikiwa inawaka moto na kuitupa chini, alipojikagua ndipo aligundua anatokwa na damu nyingi kwenye paja, alipoangalia chini aliona risasi.
“Niliwaambia watu wa jirani yangu ambapo walinikimbiza Hospitali ya Amana kwa matibabu,” alisema.

BABA MZAZI WA MAREHEMU
Naye baba mzazi wa marehemu Abubakar, mzee Hassan alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo alisema ni tukio la ajabu sana kwake kwani watoto hao kila mwaka katika kuukaribisha mwaka mpya hutoka nje kuushangilia, anashangaa kusikia wameuawa kwa risasi.

KAMANDA MINANGI
Jumamosi iliyopita, Uwazi lilimfuata Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Afande Marietha Minangi Komba na kumuuliza kuhusu tukio hilo ambapo alikiri kulipokea, akasema:

“Uchunguzi wa awali unaonesha kwamba meja huyo alifyatua risasi hewani kwa kudhani kuwa wale  vijana walikuwa wahalifu, hivyo alikuwa akijihami.
“Kwa sasa tunamshikilia (meja). Wakati wa kukamatwa kwake bastola yake ilikuwa na risasi kumi, tano zilitumika katika eneo la tukio. Jeshi langu linaendelea na uchunguzi na sheria itachukua mkondo wake,” alisema kamanda huyo.
WALIOJERUHIWA
Waliojeruhiwa katika sakata hilo ni  Lugano Wanga (17), Kasim Abdul (16) na Agustina Pius (28) ambao walikimbizwa katika Hospitali ya Amana kwa matibabu na kuruhusiwa.

MFANYABIASHARA WA KIKE APORWA MABEGI MAWILI YA HELA BAADA YA KUPIGWA RISASI HUKO KARIAKOO


Damu ya Mfanyabiashara huyo ikiwa imetapakaa katika gari lake baada ya kupigwa risasi na majambazi waliompora kiasi kikubwa cha fedha na kutoweka.


Mfanyabiashara mmoja (Jina Halikufahamika) Mwenye asili ya Asia ameshambuliwa na majabazi (majira ya saa 12 Kasoro jioni )kwa kupigwa risasi katika paji la uso wake na kisha majambazi hao kutoweka na mabegi mawili yaliyoojaa fedha.
Hata hivyo haikujulikana kwa haraka ni kiasi gani cha fedha ambacho kilikuwemo katika mabegi hayo. Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya mashuhuda wa tukio walidai kuwa majambazi hao walikuwa  watatu na mmoja alikuwa na bunduki aina ya SMG. 
Raia wakishangaa mwili wa mfayabiashara huo ukiondolowa na polisi
          
  Wakielezea tukio hilo baadhi ya wafanyabiashara wengine katika maeneo hayo ya mtaa wa Lindi na Kongo (Kariakoo) walidai kwamba Mfanyabiashara huyo alitoka na kufunga duka lake huku akiwa na mabegi mawili na Mashine ya kutolea Risiti ya EFD na kuelekea katika gari lake dogo aina ya Suzuki Carry na Ghafla walitokea watu wawili waliokuwa katika pikipiki na mmoja wa tatu alikuwa amesimama pembeni kidogo na gari hiyo na kisha kuelekea moja kwa moja katika gari hiyo na kumpiga risasi mfanya biashara huyo aliyekuwa akijiandaa kuondosha gari lake.


         
Mfanya biashara apigwa risasi Kariakoo
Askari wakiliondoa gari la mfanya biashara huyo katika eneo la tukio
''Niliona watu kama wanagombania begi hivi ghafla nikasikia mlio wa risasi  na kisha nikaona pikipiki mbili aina ya boxer zikija kwa kasi kutokea upande wa mtaa wa gerezani na kisha  mlio wa pili wa risasi ulikika tena, nahisi ndio uliokuwa umemlenga yule "muhindi" na baada ya hapo kitendo kama cha dakika mbili hivi wale jamaa wakapokezana lile begi na kisha kupiga risasi nyingine juu basi hapo wote tukaanza kufunga maduka yetu na wale majambazi wakatoweka kirahisiii"
EFD machine ikiwa katika gari la mfanyabiashara aliyepigwa risasi leo jijini Dar es Salaam


Sehemu  ya fremu inayosemekana kuwa ni Duka la
 Mfanyabiashara aliyepigwa Risasi Leo majira ya saa 12 jioni
  Hata hivyo baadhi ya watu wamelaumu utaratibu wa wafanya biashara wengi wa kariakoo kuhifadhi fedha nyingi katika maduka na badala yake wamewataka wafanya biashara hao kutafuta mbinu mbadala itakayowaezesha kuweka fedha na mali zao salama kabisa ikiwa ni pamoja na kutumia huduma za kuhamisha fedha kwa kutumia mitandao, cheque, na hata credit card kuliko Cash kwani imekuwa kawaida kwa mtukio haya kujirudia eleo hili la Kariakoo.

BOMU LIMERIPUKA KANISANI HUKO ARUSHA

 
Taarifa ambazo zimetufikia kupitia kituo cha WAPO Radio FM zinaeleza kwamba kuna bomu limelipuliwa kwenye kanisa katoliki la Mtakatifu Karoli, Ruanga huko USA River jijini Arusha, ambapo wanakwaya takriban 6 wamejeruhiwa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo zimetufikia, zinaeleza kwamba watuhumiwa ni jeshi la Polisi, na kwamba walirusha kitu kinachosadikiwa kuwa bomu - lililojeruhi 6, ambapo 4 kati yao wameruhusiwa baada ya matibabu kwenye hospitali ya Mission na ya Wilaya ya Arumeru.

Majira ya saa sita na nusu, waumini walidai kuona gari la polisi likipita kwa kasi, na lilipowakaribia walistuka mlipuko ukiwarusha pembeni, ambapo walijikuta na majeraha na usoni, mapajani na maeneo mbalimbali ya mwili. Kisha baada ya hapo gari ilisogea mbele na kuanza kurusha mabomu kwa watu wowote iliokutana nao.

Hadi sasa inaelezwa kuwa uchunguzi umeshaanza kufanyika, huku Kamanda Liberatus Sabas akikataa kuzungumzia zaidi suala hilo. Alipotafutwa na WAPO Radio FM, hakueleza kwa kina, lakini akasema kuwa sio suala la kwaya kama ambavyo imeelezwa, bali ni wakinadada wawili na kwamba hawezi kuzungumza zaidi, bali kesho (Ijumaa) atatoa taarifa rasmi na iliyo kamili kwa vyombo vya habari.

Alipoulizwa kuwa kama ni kweli jeshi la Polisi linatuhumiwa kuhusika, alisema kuwa atazungumza kesho kuhusiana na tukio hilo. Tukio hili limetokea ikiwa ni siku mbili zimepita tokea kuapishwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi mpya, Ernest Mangu ambaye amechukua nafasi ya IJP Said Mwema aliyestaafu.

MWANAMKE AUWAWA KWA KUCHOMWACHOMWA VISU TUMBONI, SOMA MKASA HUU WA KUSIKITISHA

Waombolezaji  wakiwa  katika msiba  huo  eneo la Mtwivila  Mume wa marehemu Bw Hamza Kidava na mtoto wake  wakitoa heshima  za mwisho  kabla ya mazishi  mwili  wa marehemu Doris Lyandala Kaburi la marehemu Doris Aliyekuwa  mume wa marehemu Doris Lyandala Bw Hamza Kidava kushoto akiwa na rafiki  zake nyumbani kwao Mtwivila leo Bw Hamza Kidava  akiwa katika majonzi mazito Bw Hamza Kidava  akionyesha  eneo  ambalo mke  wake kipenzi alipouwawa kwa  kuchomwa visu na mtu anayesadikika kuwa ni kichaa Bw Hamaza kushoto akimwonyesha mwandishi wa mtandao huu mzee wa matukio  daima hayupo pichani na Bw Brown eneo ambalo mke  wake aliuwawa
Dereva  Taxi  aliyekuwa akimwendesha  Mzee wa matukio  daima  Bw Brown akiwa nje ya nyumba aliyekuwa akiishi mtuhumiwa wa mauwaji  ya Bi Doris Lyandala
HAKUNA Kati  yetu  ajuaye siku yake na  kufa na kifo  chake kitakuwaje na kama ungelijua lijalo mbele  yako hakuna ambaye angejaribu kutoka ndani ya nyumba yake kwenda  kukutwa na mauti.

Ni kauli  za  majirani  na marafiki wa karibu wa mrembo Doris  Lyandala  ambae kwa sasa kwa wakazi wa mji wa Iringa jina lake  ndilo limeendelea kutesa mawazo ya  wengi.

Doris ambae enzi za uhai  wake alipata  kuwa mmiliki wa Saloon yake ya kutengeneza  nywele  warembo wenzake na alipata kuwa mcheshi asiyependa makuu tulitamani tungekula na  kusherekea nae pamoja  Krismas  ambapo ilibaki siku moja pekee kula Krismas na rafiki ,familia yake na  zilibaki  siku takribani  7  kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 ila yote hayakuwezekana na badala  yake rafiki na ndugu walijikuta  katika simanzi ya kifo chake .

Mmoja kati ya marafiki zake wa karibu  Salima Alli alisema  kuwa alikuwa ni mteja  wake mkubwa katika  saloon na kabla ya  kukutwa na umauti  siku moja kabla alipata  kumseti nywele  zake.

Bw Hamaza Kidava  ndie mume wa marehemu  huyo anasema kuwa alipata  taarifa  kutoka kwa majirani  kuwa kipenzi chake mke wa mtoto mmoja amepatwa na tatizo na amekimbizwa katika  Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.

Alisema kuwa baada ya  kufika Hospital hapo hakuamini  kuona mke aliyempenda kuliko akitokwa na damu huku akieleza kwa  shida  kilichomkuta .

Akizungumza kwa uchungu mwigi huku akilengwa na machozi Hamza ambae ni mmoja  kati ya vijana watanashati na wenye ajira zao akiwa katika  sekta ya kutengeneza simu alisema  kuwa alichoelezwa  kuwa amechomwa visu na kichaa.

"Ina  niuma  sana  kumpoteza mke  wangu na ina niuma sana kuona  leo  nimebaki mpweke nikilea mtoto mmoja ambae nimezaa nae mke  wangu Doris ....kaka nashukuru kwa  kuja  kunifariji na  nawashukuru wote  walioshiriki kuuguza hadi mazishi  yake "alisema Hamaza  kumaliza kwa kusema twende nikakuonyeshe alipokutwa na mkasa huo  wakati akitoka dukani kutafuta mahitaji.

Ndudu wa karibu na mtuhumiwa wa mauaji  hayo ambae hakupenda  jina lake  kuandikwa hapa kwa kuwa si msemaji wa familia alisema  kuwa  mtuhumiwa  huyo wa mauwaji Bw Zakayo Lwambano (26) ni mkazi wa Mtwivila na alikuwa akiishi  mtaa mmoja na marehemu Doris .

Alisema  kuwa kijana  huyo Zakayo alianza kuugua ugonjwa  huo toka mwaka 2010 ambapo ndugu  walimpeleka Hospital ya vichaa Milembe Dodoma na kurejea akiwa mzima wa afya.

Hata  hivyo alisema  baada ya  kurejea  alikuwa ni mtu aliyetulia na kujipatia  kipato chake cha kila siku kwa  kufanya kazi ndogo ndogo za kusomba mchanga na nyingine kwa  wananchi wa eneo hilo .

Ndugu  huyo alisema wazazi wa mtuhumiwa huyo kwa  sasa  walisha fariki dunia na alikuwa akiishi peke yake katika getho ( nyumba yake ya chumba kimoja )  aliyojenga  mwenyewe
Alisema  kuwa  siku ya tukio Desemba 24 kabla ya kumshambulia Mrembo  huyo alianza kumchoma  kisu ndugu  yake James Moyo (28) ambae  alifika nyumbani hapo kwa  ajili ya kula sikukuu  akitokea Makambako Njombe.

Alisema kijana  huyo aliyejeruhiwa alikuwa akiishi nyumba nyingine tofauti na getho la mtuhumiwa na alichomwa  visu viwili kwapani na kukimbizwa Hospital ya rufaa ya mkoa wa Iringa na kwa sasa ameruhusiwa na kurejea Makambako kwao.

Pia  alisema mtuhumiwa  huyo baada ya mauwaji alijipeleka mwenyewe polisi na kutaka awekwe ndani kwa madai ameua
Jeshi  la  polisi  mkoa wa Iringa  limethibitisha  kutokea kwa mauwaji hayo na kuwa  mtuhumiwa huyo hadi sasa anashikiliwa na polisi .

Kamanda wa  polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi  alisema  kuwa mwanamke  huyo alichomwa visu sehemu mbali mbali ya mwili  wake na baada ya  kukimbizwa  Hospital akiendelea na matibabu alifariki dunia.

Alisema kuwa   mtuhumiwa   huyo amenashikiliwa kama  watuhumiwa wengine na kuwa mwenye mamlaka ya kumfunga ama kutomfunga ni mahakama na  wao kama polisi hawajui kama ni kichaa wanajua kama mtuhumiwa wa mauwaji.

Mtandao  huu na  wadau wake  unatoa pore  nyingi kwa familia ya Kidava na Lyandala pamoja na ndugu na jamaa wote ambao  wameondokewa na mpendwa  wao ambae sote  tulimpenda  sana ila Mungu kampenda zaidi yetu  hivyo hatunabudi kusema jina lake  lihimidiwe milele yote
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger