Stori: Makongoro Oging’
“ILIKUWA siku ya mkesha wa mwaka mpya nikiwa nyumbani Mwembe Yanga, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, mume wangu alifika huku akiwa anapiga kelele na nilipomuuliza akanieleza kuwa leo ndiyo mwisho wangu kwani mimi ni mbwa.
“Nilimweleza kuwa sitaki fujo pia sikupenda tuukaribishe mwaka mpya kwa ugomvi bali kama kuna ugomvi, ulikuwa muda mwafaka kuumaliza.”
Maneno hayo alikuwa akiyasema Martha Laurent ambaye ni mjamzito wiki iliyopita akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wodi ya Mwaisela namba mbili anakojiuguza alipozungumza na gazeti hili.
Aliendelea kusema: “Sikuamini kama mume wangu Jumanne Suyi angeweza kunitia ulemavu kiasi hiki kwani tangu nianze kuishi naye ndani ya mwaka mmoja hatukuwahi kugombana, tumekuwa tukiishi kwa mapenzi ya hali ya juu na tulikula kiapo kuwa hatutapigana na linapotokea kosa tumekuwa tukilitatua sisi wenyewe.
“Asubuhi siku hiyo tuliamka salama huku nikiwa nimemwandalia chakula ili akija kutoka safari zake aje ale kwani aliniahidi kuwa tungeweza kutoka, tukatembee, cha ajabu hata kabla hajala chakula, alichukia akaanza kunipiga.
“Alinipiga na rungu kichwani, nimepata majeraha makubwa sana hadi nikashonwa, sikio langu la kushoto halifanyi kazi, tumbo langu linaniuma sana, sijui kama kiumbe tumboni kimedhurika kwani nina ujauzito wa miezi minne.
“Nilifikishwa hapa hospitali na majirani nikiwa sijitambui, kwa sasa naongea kwa shida nasikia kizunguzungu, sijui kama nitapona, mume wangu atafutwe aulizwe sababu ya kunipiga kiasi hiki, naomba taarifa hizi ziwafikie familia yetu huko Dodoma,” alisema Martha.
Naye Afisa Ustawi wa Jamii Kitengo cha Mifupa MOI, Muhimbili, Mary Ochieng’ alisema kwamba mgonjwa huyo alifikishwa hapo hospitalini akiwa hajitambui na kwa sasa ana mabadiliko na wanatarajia kumfanyia vipimo vingine wakati wowote.