Search in This Blog

Showing posts with label AUNT EZEKIEL. Show all posts
Showing posts with label AUNT EZEKIEL. Show all posts

"MUME WANGU NI KWELI KAKAMATWA DUBAI" HAYA NI MANENO YA ANTI EZEKIEL

STAA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amekiri mumewe kukamatwa na kupata misukosuko lakini si kufungwa kama baadhi ya watu wanavyoeneza uzushi.
Aunt Ezekiel.
Akipiga stori na mwandishi wetu hivi karibuni, Aunt alisema mumewe, Sunday Demonte alikamatwa kutokana na viza yake kuisha ambapo alishikiliwa kwa muda na alipokamilisha taratibu za ‘kurinyuu’, aliachiwa.
“Nashangaa sana mambo haya yamevuma kuwa mimi nimemuacha mume wangu amefungwa, ukweli ni kwamba mume wangu yuko huru na hata sasa ukitaka ongea naye, ni mwanamke gani atakuwa na furaha hivi wakati mumewe ana matatizo?” alihoji Aunt.
http://api.ning.com/files/MN6ZNqVOIKOj4UGweglrZ7yo2eHgFV0ZU-eQnP5tErLW4PbZZ9Zb84QoA41aCDvL26jOJJb5G7i9cBqgodCdlcfPSY-h3SI8/AUNTNADEMONTE.jpg?width=650
Aunt akiwa na mumewe.
Katika mistari mingine, Aunt alisema watu wengi wanatamani kuona ameachika au kujua mwenendo wa maisha yake na mumewe lakini wanajidanganya kwani yeye ni mwanamke aliyeamua kuolewa na amefundwa hivyo wataambulia patupu.
“Siyo  rahisi mimi kutoa siri ya maisha ninayoishi na mume wangu, ni makubaliano yetu. Kimsingi ndoa yetu iko imara, watasubiri sana na watachoka wenyewe,” alisema Aunt

"TUNAFANYA MASKENDO ILI TUZIDI KUWA MAARUFU, SASA KAMA WEWE HUNA SKENDO BASI WEWE SIO STAA" HAYA NI MANENO YA ANTI EZEKIEL

  AUNT Ezekiel ni muigizaji wa filamu mwenye jina kubwa, linaloenda sambamba na muonekano wake wenye mvuto, hasa anapovaa mavazi yake yanayoonyesha baadhi ya sehemu muhimu za mwili wake.
Kwa wasiomfahamu vizuri, Aunt ni mtoto wa mwanasoka mahiri wa zamani wa Simba na Taifa Stars, marehemu Ezekiel Greyson, maarufu zaidi kwa mashabiki wa kabumbu kama Jujuman. Alitamba katika miaka ya sabini na mwanzoni mwa themanini.
Ni mmoja wa wasichana waliofanikiwa kupata majina makubwa, ingawa uwezo wake kama muigizaji, bado haujakidhi viwango!
Hivi karibuni Aunt, mke wa mfanyabiashara Sunday Demonte, kijana wa Kitanzania anayefanyia shughuli zake Ughaibuni, alinukuliwa na chombo kimoja cha habari akisema kuwa haogopi kukutwa na skendo, kwani hilo ni jambo la kawaida.
Mimi sijali, ninachoangalia ni kuingiza kipato, mambo mengine shauri yao, kuna watu wananichukia na kunitungia uongo, huwezi kupendwa na kila mtu, msanii ni kioo cha jamii, lazima upate skendo ili uweze kujirekebisha,” Aunt alinukuliwa na paparazi wetu.

Ninazifahamu kidogo kazi alizoshirikishwa, nyingi kati ya hizo akicheza na marehemu Steven Kanumba. Aina ya uigizaji wake haubadiliki, ni Aunt yule yule anayependa kuvaa nguo zenye kuonyesha nje sehemu kubwa ya matiti yake, maungo yake na hata mavazi yake mara zote ni yenye utata mkubwa.
Muigizaji mzuri ni yule mwenye kubadilika. Leo anaweza kucheza vizuri kama changudoa, kesho yake akafiti kiufasaha kabisa kama mtoto yatima anayeishi katika umaskini mkubwa, kabla ya keshokutwa kumkuta akiigiza vyema akiwa ni msomi mwenye mafanikio makubwa kimaisha!
Sifa hizo Aunt Ezekiel, kama walivyo mastaa wengi wa Tanzania katika filamu, hana. Ni muigizaji wa kuigiza matanuzi, demu bomba mwenye mitoko mingi, mikogo na mambo kama hayo, ndiyo maana hata mavazi yake, uigizaji wake ni wa aina ileile katika filamu zote alizocheza!
Anasema haogopi skendo, anajali kuingiza kipato. Anahitimisha kwa kukiri kwamba skendo ni jambo la kawaida kwa mastaa, kwani kwa kutokea hivyo, ndipo wao hupata nafasi ya kujirekebisha! Hawa ndiyo aina ya wasanii tulio nao, wenye wafuasi lukuki mtaani, wanaosimama na kusema wazi kuwa hawaogopi skendo. Mtu makini na hasa anayetakiwa kuwa mfano, hawezi kuwa haogopi skendo!
Ndiyo maana kumbe kila siku tunasikia, mara kapiga picha za nusu utupu na kuzitupia katika mitandao ya kijamii ili watu waone ‘figa’. Mara amepigana na mwenzake club (bila chanzo hasa cha ugomvi kuelezwa, ingawa ni rahisi kuamini walikuwa wakigombea bwana).
Ninaheshimu maoni yake ya kutoogopa skendo, lakini napingana naye kwa kauli kuwa ni kawaida kwa mastaa kupata skendo. Siyo kweli. Wapo mastaa wakubwa, tena wale wanaojua kazi, lakini hawajawahi kuwa mabingwa wa skendo.
Riyama Ally ni mmoja ya waigizaji ‘wanaojua’ kwa levo za Bongo, lakini siwezi kumuweka katika orodha ya wauza sura wanaotumia tasnia kwa malengo yao binafsi.
Wasanii wetu wanaponzwa na uwezo wao mdogo wa ubunifu, ndiyo maana bado wanaamini katika skendo ili kuwaweka juu. Mtu anajisikia vizuri akiandikwa gazetini, bila kujali anaharibu vipi ‘image’ yake kwa jamii. Eti wanasingiziwa, hivi kuna mtu gani makini anaweza kukubali kunyamaza gazeti linapoandika uongo dhidi yake?
Kuna namna moja tu unayoweza kuwazungumzia hawa mastaa wetu wa aina hii, kwamba wanatengeneza skendo makusudi ili wavutie macho na masikio ya wahanga wa ngono!

ALIYEMPIKA CHUPA AUNT EZEKIEL APELEKWA PUTA NA POLISI


'Yvonne Maximilian (22) amenaswa na kuhenyeshwa kortini kisa kikiwa ni kumpiga chupa Aunt Ezekiel.'

Hatimaye yule mbaya wa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel aitwaye Yvonne Maximilian (22) amenaswa na kuhenyeshwa kortini kisa kikiwa ni kumpiga chupa mwigizaji huyo.
Yvonne aliburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar baada ya kukamatwa maeneo ya nyumbani kwake Kinondoni-Manyanya.
Habari za ndani kutoka kortini zilieleza kuwa awali kesi hiyo ilikuwa isikilizwe na hakimu Agustino Mbando lakini baadaye kulitokea mabadiliko ambapo ilisomwa na Fundi Fimbo.
Akiwa mahakamani hapo huku Aunt naye akihudhuria kama mlalamikaji, Yvonne alishuhudiwa akipelekwa puta na polisi.
Hata hivyo, baada ya kesi hiyo kusomwa iliahirishwa hadi Oktoba 17, mwaka huu, itakaposikilizwa tena.
Agosti 26, mwaka huu, Yvonne anadaiwa kumjeruhi Aunt kwa chupa tupu ya bia na kumpasua mkono wa kushoto wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bilicanas, Posta jijini Dar.

CREDIT GPL

AUNT EZEKIEL AMTOSA MUMEWE

Wengi  walitegemea  kuwa  Aunt  Ezekiel ataungana  na  mumewe Sunday  katika  kipindi  hiki  cha  mwezi  mtukufu wa Ramadhani  lakini  hali  imekuwa  ni  tofauti....

Aunt  anayetumia  jina  la  Rahma  baada  ya  kubadili  dini  ili  aolewe  na  mwanaume  huyo,   amemtosa  mkaka  huyo  na  kuendelea  kula  bata  nchini  huku  akidai  kuwa  mumewe  hana  mengi.

"Sina  mpango  wowote  wa  kuondoka  nchini  kumfuata  mwanaume.Yeye  ni  mume  wangu, ntamkuta  tu  hata  nikienda  mwakani.

"Kwanza  mume  wangu  hana  mengi  na  si  mkorofi  na  anajua  wazi  kwamba  sipendi  kubanwa.Kwa  sasa  nina  mambo  mengi  likiwemo  hili  la  kuisambaza  filamu  yangu  mpya  ya  Scola  mwezi  ujao"...Alisema  aunt  Ezekiel

" NATARAJIA KUBEBA MIMBA SIKU ZA HIVI KARIBUNI" AUNT EZEKIEL

STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel juzikati alifunguka na kuweka wazi juu ya mipangilio yake ya ndoa kuwa anatarajia kubeba ujauzito siku chache zijazo kwani ana kiu kubwa ya kuitwa mama.  Akichonga na paparazi wetu Julai 9, mwaka huu nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar, Aunt alisema kuwa anajutia sana kukaa kwa muda wote bila kuiruhusu mimba iingie ila siku si nyingi mambo yatakuwa yametiki.
Nina mpango wa kubeba mimba na nizae siku chache zijazo kwani sina sababu tena ya kunifanya nisipate mtoto kwa wakati huu ambao niko ndani ya ndoa na naamini itaimarika zaidi nikiitwa mama huku pembeni akiwepo baba wa mtoto wangu,” alisema Aunt Ezekiel

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger