Search in This Blog

Showing posts with label MADAHA. Show all posts
Showing posts with label MADAHA. Show all posts

CHOKOCHOKO ZA MADAHA KWA DIAMONDA SASA KWISHA, HII NI BAADA YA KUPATA SHAVU LA MILLION 200


Ile record label maarufu ya muziki afrika mashariki - candy n candy imechapa fimbo nyingine baada ya kufanya deal ya mtonyo mrefuu na kampuni maarufu ya  kusambaza filamu afrika mashariki na kati, (Jina kapuni ) kwa ajili ya kusambaza filamu ya “The gal bladder”  ambayo imechezwa na mwigizaji baby madaha akishirikiana na waigizaji wengine toka kenya.

Kama alivyonukuliwa toka mtandao mmoja maarufu wa habari Afrika Mashariki, msemaji wa kampuni hiyo amesema imekua neema kwao kufanya kazi na kampuni kubwa kama candy n candy films ya nchini kenya, na hiyo itapanua wigo wa ukuaji wa tasnia ya filamu afrika mashariki hususani kenya na tanzania..deal hiyo yenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni mia mbili ( mil.200 )inakua moja ya mikataba minono zaidi kufanywa east africa kutoka kwa  kampuni kwenda kwa kampuni kwenye upande wa filamu.
Hiyo inachukukuliwa kuwa moja la pigo la kukata na shoka kwa  kampuni pinzani grandpa records nayo ya nchini kenya ambayo kwa muda mrefu imekuwa ndani ya tasnia ya burudani kwa takribani zaidi ya miaka kumi  bila kuleta mabadiliko yoyote katika tasnia nzima ya burudani,jambo ambalo  candy n candy imeweza kufanya ndani ya miezi mitano tu,katika kutengeneza muziki wa kimataifa bila kusahau project yao ya sasa “highly budget movie   the gal bladder”….ni mfano wa kuigwa kutoka kwa candy n candy records label kuzalisha kampuni tanzu ndani yake ya candy n candy films ambayo itakuwa ikidili na filamu.
Mbali na hayo kampuni hii ina plans za kuanzisha kipindi matata cha runinga ambacho kitakua kikirushwa  Afrika Mashariki yote ,ambapo kama kawaida huwa hawachezi mbali host wake atakua first lady wa candy n candy mwanamuziki,mwigizaji,mwanamitindo na mtangazaji baby madaha”the queen of swaggz”,ikumbukwe hivi karibuni alilamba mamilioni ya shilingi kupitia mkataba wake na kampuni hiyo.
kaaazi kweli kweli…….yetu macho wabongo mpoooo????

BABY MADAHA AMROPOKEA TENA DIAMOND SAFARI HII ASEMA "DIAMOND ANATUMIA WANAWAKE MASTAA ILI KUPATA UMAARUFU".




WIKI kadhaa zilizopita tulisikia msanii wa filamu na muziki Baby Madaha akifunguka na kusema kuwa Diamond siyo msanii bali ni malaya na anatumia wasichana maarufu ili apate kiki katika muziki anaoufanya. Baby Madaha alizidi kufunguka na kusema endapo wasanii maarufu wa kike wakipata uelewa na wakamgundua Diamond basi ndiyo mwisho wa msanii huyo kusikika hewani. 

Madai hayo ya Baby Madaha yanaweza yakawa na ukweli ndani yake kwa hiki ambacho kinaendelea kwa sasa kati ya msanii Diamond na Wema Sepetu. 
Diamond hivi karibuni  atatambulisha wimbo wake mpya wa Number 1 remix aliyoufanya nchini Nigeria na msanii Davido wa nchini humo, Kulingana na madai ya Baby Madaha yaonekana Diamond anatafuta Kick kwa kutoka na mwanadada Wema Sepetu na mpaka kutambulisha anataka kuoa.

BIFU LAENDELEA:BABY MADAHA AMCHANA TENA DIAMOND BAADA YA DIAMOND KUMDISS


Baada ya mwanamuziki wa kizazi kipya kufunguka na  kuamua kumdiss mwanadada baby Madaha a.k.a The Bad Gul kuwa hawalingani hivyo hana muda muda wa kuwa na beef na mrembo huyu wa filamu na muziki bongo, hatimaye tumeweza kumpata baby Madaha na kufanya naye EXCLUSIVE interview na mwanadada huyu kuhusu hayo mazito aliyoyasema bwana platnumz. Na kwakuwa mwaka huu ni mwaka wa kufunguka bila kuficha chochote binti huyu aliamua kuanika yake ya moyoni kama yanavyosomeka hapo chini….
Baby alianza kwa kusema
“….Kwanza nitafute keeck kwa diamond kwa lipi,wakati anakuja kuniomba kuperfome 2010  akiwa ana single moja ya mbagala pale maisha plus mimi nikiwa judge na kina masoud,tayari nishafanya album ya amore india na nishapiga show kibao,wakati yeye akifikiria amkamate demu gani ili a hit kimuziki mimi tayari nishafanya  movie tatu na moja imeshinda ziff tz na ziff berlin,akiendelea kuwapanda kama farasi hao wajinga wajinga wenzie mie tayari nina tuzo tatu ziff ambazo hata marehemu kanumba angefurahi kupata japo moja(rip)….”
“…..Wakati sasa anaongea blah blah akiwa na single yake moja mpya akihangaika kwenda nigeria kuonyesha skin tight yake ya mistari na kuomba omba collarbo, mi tayari nina single tatu hit na najiandaa kushusha movie kali mpya,tatizo ni kutotaka kukosolewa na kujiona mungu mtu kwenye muziki lakini ukweli anaujua na hata yeye anauogopa kama anabisha afanye nao collarbo anahangaika nini na wote wanaimba bongo flava??upuuzi na ujanja ujanja tu wa mjini unafanyika huku wale punda wake wakikubali kumbeba kwa malipo gani umaarufu???mi sijautafuta kwa nguvu hiyo, nimepikwa bss na watu wakaniona na wakanitambua.kama ni suala la pesa hata asiongee launching yangu ya (kempinsky)hyatt regency 2010 hakuna msanii yeyote wa bongo flava including na yeye ameweza kufanya jeuri hiyo,aliyejaribun labda yule demu wake wa zamani aliyemshit pia kwa vihela vyake mbuzi…”
“….Akiwa bado anastruggle kupata mkwanja awatishe tishe watoto wenzake wa tandale..mimi nishazindua brandy yangu ya manukato na gift bagz zangu ambazo zinaingia sokoni rasmi 31 december…bado anachanja na prado old model,asogee kwenye audi tt yangu apunge upepo yani ye anatafutaa..mi nishapata so wa nini???wanaompapatikia ni wale drama queens wenzie, mi ama bad gul sijali kama kumchana namchana tu so wat??,scandal kitu gani?ye sukari guru ata survive si tandale bwana eeh, vipi wale kwenye list za kubadilishwa kama nguo za ndani je watapata wa kuwaoa???/… wakija forbes hapa watu wataumbuka ooh na hekalu langu kuubwa unakaaje kwenye nyumba ya kupanga?haliishi??hahahaha na kuhusu ati mimi nimesema ana paja la mtoto wapi na wapi he is not ma type at all si hook na little mama’s boy na hook up na big boys tu…”
“…. Mi sio wale farasi zake wanaopokezana kupandwa na yeye after role kuambiwa ukweli sio bif kweli mzinzi na hajui kuimba kama sio kweli atulie tu asipande pande hapo tutamwona mfalme kweli kama mzee yussuf,mimi naimba aina yangu ya muziki tanzania nzima nipo peke yangu hakuna demu anapiga riddim,ragga sasa natafutaje keeck kwa bongo flava????anaeimba nyimbo zake za kipuuzi kutaja taja farasi wake ana (tusi kali sana) angekuwa ameni***** sawa but mpaka anakufa i think atakuwa ananiota mimi na lulu……….kama mbwai mbwai  mjini hapa kila nyumba ina namba..adios…”
Hatuna la kuongezea hapo, kazi yetu ni kuwajulisha kinachotokea tu mjini hapa.
Source:Bongomovies

"NARUDIA KUSEMA TENA DIAMNOND NI FUSKA TENA JIFUSKA KWELIKWELI" BABY MADAHA ASEMA TENA MANENO HAYA, SOMA KUJUA KWA NINI KASEMA HIVYO

ACHANA na mabifu yaliyotangulia, hili ni jipya kabisaa! Msanii wa sinema na Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ameingia kwenye bifu zito na Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ na kudai staa huyo wa Wimbo wa Number One ni mzinzi ‘fuska’, Amani lina mkanda mzima.
Baby Madaha akiwa na Diamond.
Bila kumung’unya maneno, mapema wiki hii, Baby Madaha alimvaa Diamond ambaye ni Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB) akimtuhumu kuwa na tabia za kifuska.
Baby Madaha alidai hata muziki anaoufanya Diamond kamwe hauwezi kulingana na mafanikio makubwa ya jina lake zaidi ya kubebwa na skendo tu.

Diamond na Wema.
CHOKOCHOKO ZILIVYOANZA
Kupitia mitandao ya kijamii, ilivuja posti ambayo ilidaiwa kutoka kwa Baby Madaha ikimpaka Diamond kuwa siyo mwanamuziki kama ilivyo kwa wasanii wengine wenye uwezo mkubwa, akitolea mfano Elias Barnaba wa THT.
Sehemu ya posti hiyo ilionesha kuwa, Diamond si msanii wa muziki bali ni mzinzi f’lani hivi anayefanya biashara ya muziki kupitia mapenzi.

“Siku wanawake maarufu nchini Tanzania watakapojitambua na kuacha kulewa penzi la Diamond, huo ndiyo utakuwa mwisho wa maisha yake kimuziki kwa sababu hatakuwa na jipya na hivyo soko lake litaporomoka,” ilisomeka posti hiyo.
Diamond na Penny.
UKWELI NI UPI?
Baada ya ishu hiyo kugeuka habari ya mjini na kuibuka kwa makundi mawili yanayokinzana, Amani lilimtafuta Baby Madaha ili kujua ukweli wa posti hiyo ndipo akatiririka aya za kuthibitisha kuwa picha haziivi, hamkubali Diamond na kudai hata kimuziki hamkubali kwani anaamini wapo wanamuziki wanaofanya vema katika gemu kuliko yeye.

“…tuseme ukweli, Diamond ni mfanyabiashara siyo mwanamuziki. Kuhusu hiyo posti iwe ni mimi nimeandika au si mimi lakini kimsingi hayo maneno yanamstahili kabisa. Mzinzi tu.
“Diamond anabebwa na media (vyombo vya habari). Kuna wanamuziki wengi wazuri sembuse yeye? Ana nini haswa?” alihoji Baby.

Diamond na Jokate.
AMANI LAMGEUKIA DIAMOND
Baada ya kusikia maelezo ya Baby kwa kifupi, Amani lilimuweka ‘pending’ kwa muda na kumwendea hewani Diamond ili liweze kujua upande wake analizungumziaje bifu hilo ambalo lilikuwa likienea mitandaoni kama moto wa kifuu.
Tofauti na matarajio ya mapaparazi wetu kwamba huenda angejibu mashambulizi makali kwa Madaha, Diamond au ‘Sukari ya Warembo’ aling’aka huku akimponda mwanadada huyo na kumshangaa:

BOFYA HAPA KUMSIKIA
“Daaah! Huko ni kunishusha…mimi na huyo (Baby) wapi kwa wapi kamwe huwezi kunilinganisha na mtu ambaye yupo chini yangu sana, nikijibizana naye nitajishusha tu. Ingekuwa ni mtu mkubwa mwenye levo yangu hapo ningesema natakiwa kusema neno.
“Hana lolote huyo anatafuta ‘kiki’ tu kupitia mimi, nipo na dili zangu za maana nipoteze muda kwake? Atafute wa levo yake na wala si mimi.”

UZINZI VIPI?
Alipoulizwa kuhusu suala la uzinzi ambalo Baby Madaha aliumaanisha katika posti yake, Diamond aliendelea kukazia kuwa hana muda wa kupoteza kwa mtu kama Baby Madaha ambaye kimsingi ni kama ardhi na mbingu.
“Huyo anatafuta kiki tu, aachane na mimi…mbona hatufanani kabisa mimi na yeye wapi kwa wapi?” alikazia Diamond a.k.a Weka Mbali na Watoto Wazuri wa Kike.

BABY AREJEA HEWANI
Wakati mapaparazi wetu wakimalizana na Diamond, kilongalonga kimoja cha paparazi wetu kilikuwa kikionesha kinaita, ilivyokatika ya Diamond, Baby akapanda hewani kwa mara nyingine.

Safari hii alimchana laivu: “Nimeisoma upya posti yenyewe, kilichopo humu ni ukweli mtupu. Hakuna hata tone la uongo, wewe utamlinganisha Diamond na mtu kama Barnaba? Huyu ni mfanyabiashara tu, hajui kuimba kwa kutumia vyombo kama mimi.
“Diamond hawezi kupiga chombo hata kimoja cha muziki atajiitaje mwanamuziki? Anastahili kabisa ujumbe huu.”

UFUSKA
Mapaparazi wetu walilazimika kumtwanga swali Baby Madaha kuhusiana na ufuska ambao ulikuwa umetajwa katika maelezo ya awali, kama endapo Diamond ni mzinzi au yeye ndiyo mzinzi.
Katika maelezo yake, Baby Madaha aliwashangaza mapaparazi wetu kwa kutaja namna gani anaweza kumuita Diamond mzinzi. Sikia:

Amani: “Umesema Diamond si mwanamuziki, je, suala la uzinzi ni nani analo kati yako na yeye?”
Baby: “Mimi si mzinzi. Diamond ndiyo mzinzi tena sana tu.”
Amani: “Uzinzi wake upo wapi?”
Baby: “Kitendo cha kubadilisha wanawake, kufumaniwa na Wema Sepetu akiwa na Jokate Mwegelo ndiyo uzinzi wenyewe huo.”

Amani: “Kwani wewe hujawahi kuwa na wanaume tofauti? Hujawahi kufumaniwa?”
Baby: “Mimi sijawahi, yeye amewahi na hakuwahi kukanusha hivyo inadhihirisha kuwa ni kweli. Kwangu mimi kila aliyetajwa kutoka na mimi kama haikuwa kweli, nilikanusha mara moja yeye mbona hakanushi?”
Amani: “Kwani Diamond alifumaniwa na nani?”
Baby: “Acha hizo, kwani hukumbuki kipindi cha Wema? Mara alinaswa na Aunt mara na… yule ndiyo mzinzi sasa.”

KWANI WALITONGOZANA?
Kuhusu suala la kutongozwa, Baby alisema Diamond hajawahi. Cha kushangaza zaidi, alisema hata kama ikitokea siku staa huyo akamtongoza kamwe hawezi kumkubalia kwani hawaendani hata kidogo.
Alisema yeye ni mtu wa kutembea na vigogo na si vitoto kama Diamond.

“Hana hela, kamwe siwezi kumkubalia. Ni mtu ambaye ana vihela mbuzi sasa mtu kama yeye mimi wa nini? Ndiyo maana aliwahi kukimbiwa na mwanamke kwa kuwa hana hela.
“Tena yule mwanamke akaenda kwa kigogo mwenye hela, mimi na yeye ni mbalimbali kabisa. Hata muziki ninaofanya hauwezi, mimi ninaimba RnB yeye anafanya Pop, tuko tofauti kabisa,” alisema Baby pasipo kumtaja mwanamke aliyemkimbia Diamond.

TUJIKUMBUSHE PANDE ZOTE
Diamond aliwahi kuripotiwa kutoka kimapenzi na ‘totoz’ kibao wakiwemo yule wa mwanzo aliyemzingua aitwaye Sarah, Rehema Fabian, Jacqueline Wolper, Upendo Mushi ‘Pendo wa Maisha Plus’, Wema Sepetu, Natasha (Video Queen wa Wimbo wa Moyo Wangu), Najma (aliwahi kuwa mpenzi wa Mr. Blue), Jokate Mwegelo, yule demu wa Kenya na aliyekuwa mwigizaji aliyefulia ambaye ni mke wa mtu.

Kwa upande wake Baby Madaha anayekimbiza na ngoma yake ya Summer Holiday naye si haba kwani aliwahi kuripotiwa kuminya kimapenzi na yule mtoto wa mwanasiasa maarufu Bongo (jina lipo), Mwisho Mwampamba, Dokta Pakir, Juma Nature na Joe Kairuki aliye naye sasa ambaye ni mume wa mtu.

BABY MADAHA AHAMIA KWA LULU, AMPAKA MATOPE VIBAYA MNOO, SOMA KUJUA SABABU

WAKATI Lulu Semagongo maarufu kwa jina la (Anti Lulu), akiendelea kumchafua msanii wa filamu nchini Wastara Sajuki, kwamba anafanyishwa mapenzi kinyume na maumbile kutokana na hatua yake ya kuamua kuishi kimapenzi na msanii mwenzake wa filamu Bond Bin Suleiman, ambaye anadaiwa kuwa na tabia ya kuwaingilia wanawake kinyume na maumbile.Msanii wa Muziki wa Bongo Flever na filamu nchini Tanzania, Baby Madaha amevunja ukimwa na kumtaka Anti Lulu kuacha tabia ya kumharibia Wastara.(Anti Lulu:Wastara,anafanyishwa mapenzi kinyume.......)

Baby Joseph Madaha akiwa katika pozi
Baby Madaha anakuwa mtu wa kwanza kujitokeza hadharani kumlaani Anti Lulu kwa madai kwamba alishindwa kuishi Bond Bin Suleiman, kutokana na tabia yake kupenda kuingiliwa kinyume na maumbile na si kwamba jamaa alikuwa na tabi hiyo.
Akizungumza na mdadisi mambo blog hivi punde Baby Madaha alisema kwamba, "Mimi binafsi nimeshangazwa sana na kauli ya Anti Lulu,nikiwa nchini Kenya nimekuwa kisoma kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, kwamba Bond Bin Suleiman anatabia ya kuwaingilia wana wakwe kinyume na maumbilie, huo ni uongo na uzushi mkubwa" alisema Baby Madaha na kuongeza;
'Mimi jamaa ninamfahamu nani mtu wangu wakaribu, tumetokanaye Mwanza,ni mtu mweye hekma sana ila walishindwana na Lulu kwa sababu za tabia kwani Lulu alikuwa na tabia za kufanyishwa mapenzi kinyume na maumbile, tangu siku nyingi na kuna wakati aliwahi hata kujitangaza kwamba anapenda sana mchezo huo, sasa iweje leo aseme kwamba jamaa ndiyo anapenda mchezo huo?"alisema Baby Madaha na kuhoji.
Katika kuonyesha kwamba amekerwa na tabia hiyo chafu inayoenezwa na Anti Lulu, Baby Madaha aliongeza kwamba, Kwanza Lulu alishatangaza kwamba amebadilika na kwamba hivi sasa amekuwa mtu mwenye tabia nzuri, kwanini arudie tabia yake hiyo chafu? kwanza hana lolote huyo ama analingia hayo makalio yake ambayo wanaume wajanja siku hizi hawababaiki nayo, ama alitaka Wastara aendelee kumkumbika Sajuki? amwache Wastara atulie kama amempata mtu wakumtulizia mawazo, amwache kwani walisha anchana na Bond Bin Suleiman kitambo".
Kuhusu Wastara alisema kwamba, "kwanza mimi nafurahi sana kusikia Wastara ameamua kuwa na Bond Bin Suleiman, kwani jamaa anatabia nzuri ni mtu mwenye hekma anayejuwa nini maana ya utu, tofauti na jinsi ambayo Anti Lulu anamsemea, Wastara amejitahidi sana kuwa mwaminifu mbele ya Mungu wake tangu Mumewe alipofariki Dunai, tena wote ni waislamu hivyo wakipenda kiukweli na wakaamua kuishi pamoja hata thawabu watapa kwa Mungu".

"DIAMOND SI MSANII BALI NI MPENDA NGONO TU" BABY MADAHA

MSANII filamu na muziki wa kizazi kipya wa Tanzania Baby Joseph Madaha maarufu kwa jina la (Baby Madaha) amesema kwamba msanii mwenzake wa muziki nchini,Naseeb Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platinumz si msanii bali ni mfanyabiashara.
Madaha amesema kwamba Diamond si mwanamuziki na kwamwe huwezi kumlinganisha na msanii kama Barnaba Boy, anayefanya muziki kama sanaa na kazi kulingana na kipaji chake na kwamba Diamond si msanii wa muziki bali ni msanii ngono anayefanya biashara ya muziki kupitia mapenzi.

Baby madaha ambaye hivi sasa yuko nchini Kenya kwa shuguli za muziki amesema kwamba, Diamond hajui kuimba na ndiyo maana amekuwa msanii wa matukio huku nyota yake ikiegemea kwenye mapenzi na wasichana wenye majina makubwa hususn wasanii.
Akizungumza na Mdadisi Mambo katika mahojiano maalum leo baby Madaha alisema kwamba, "Binafsi niliposikia kwamba Diamond anaumiza kichwa kunasa penzi la msanii Elizabeth Michael maarufu kwa jina la (Lulu) sikushangaa hata kidogo. kwa sababu nilitambua kwamba soko lake la muziki limeanza kushuka hivyo lazima atafute eneo lingine la kujiimarisha kibiashara, ili jina lake liendelee kuwika".
"Siku wanawake maarufu nchini Tanzania watakapo jitambua na kuacha kulewa penzi la Diamond ndiyo itakayokuwa mwisho wa maisha yake kimuziki,kwa sababu hatakuwa na jipya na hivyo soko lake litaanza kuporomoka"alifafanua Baby Madaha.

"NIPO TAYARI KUPIGANA NA JACK WOLPER ENDAPO ATAENDELEA KULITUMIA JINA LANGU KUJIPATIA UMAARUFU"...BABY MADAHA


Staa  wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph ‘Baby Madaha’ ameomba pambano la ngumi dhidi ya Jacqueline Wolper ili waweze kumaliza ubishi wa bifu lao.


Akipiongea na  mwandishi wetu, Baby alisema amechoshwa kusikia tambo za mpinzani wake huyo hivyo kama kweli ni mwanamke, wakutane kwa  ngumi  ili amuoneshe cha mtema kuni.

 “Asiniambie mimi natafuta kiki, mimi ni msomi kuliko yeye, arudi shule au akauze vipodozi. Najua kuimba, kuigiza na ni msomi yeye anaweza hayo? 


"Kimsingi naomba pambano nimtoe  manundu.Nipo  tayari  kupigana  naye  ili  nimshikishe  adabu,” alisema Baby Madaha.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger