Search in This Blog

Showing posts with label WEMA. Show all posts
Showing posts with label WEMA. Show all posts

HIVI NDIVYO WEMA NA DIAMOND WALIVYOKUTANA SIKU YA KWANZA

Screen Shot 2014-03-28 at 1.52.37 AM

Screen Shot 2014-03-28 at 4.07.47 AMInaaminika katika mapenzi au uhusiano wa kimapenzi uliowahi kuandikwa sana kwenye mitandao na magazeti Tanzania, huu wa mwigizaji Wema Sepetu na Diamond Platnumz umevunja rekodi, mastaa ambao walifikia mpaka kuvalishana pete ya uchumba.

Pamoja na yote waliyopitia bado kalamu za Waandishi mbalimbali zilihusika kuwaandika.
Ommy Dimpoz ambae ni rafiki wa Diamond kitambo hata kabla hatawa staa (Ommy) ameshea hii picha inayowaonyesha Wema na Diamond walipokutana kwa mara ya kwanza na kuiambatanisha na hii caption hapa chini.
Screen Shot 2014-03-28 at 1.52.48 AM

JAMAA ANAVYOMFAIDI WEMA, LAITI KAMA DIAMOND ANGEMFUMA... MMMH SIJUI INGEKUWAJE



 Wema Sepetu na Kajala wakibadilishana mawazo huku burudani ya Skylight Band ikiendelea.
 Benny Kinyaiya, William Malecela na Wema Sepetu.
 Pichani juu na chini ni Wema Sepetu akimpagawisha Sam Mapenzi wa Skylight Band 
 Sam Mapenzi akimwimbia Wema Sepetu ndani kiota cha Thai Village kilichopo Masaki jijini Dar Juma lililopita.
Maimatha wa Jesse akishow love na marafiki alipotinga kwenye kiota cha Thai Village kuanza week end yake na burudani za Skylight Band
Aneth Kushaba AK47 na Mary Lucos wakitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band.

KAJALA: WEMA NI MNAFIKI NA PIA NI KIGEUGEU


Musa Mateja na Shakoor Jongo STAA wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja ameibuka na kusema kuwa ushosti wake na Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu, uliorudishwa hivi karibuni baada ya kuwekana sawa ni wa kinafiki huku akidai Wema ni kigeugeu.
Staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja
Akizungumza kwa kujiamini mbele ya waandishi wetu, juzi Jumatano pande wa Mikocheni jijini Dar es Salaam, Kajala alisema: “Wema ni mnafiki kabisa. Upatanisho wetu ni wa uongo. Mimi moyoni nimeondoa kinyongo lakini mwenzangu naona kama bado ana donge moyoni.”
Kajala alisema hayo alipoulizwa na Risasi Jumamosi, sababu ya kutoonekana kwenye tukio la futari lililofanyika nyumbani kwa mama mzazi wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ambaye ni mkwe wa shosti wake huyo.
Katika tukio hilo, mama Diamond alifanyiwa sapraizi ya nguvu alipokabidhiwa gari kali aina ya Toyota Lexus Harrier kama zawadi ya bethidei yake, ambayo ilitolewa na meneja wa Diamond, Babu Tale kwa niaba ya mwanamuziki huyo ambaye alikuwa safarini nchini Marekani.
Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu,
“Tunakubaliana kuwa kitu kimoja lakini mwenzangu anaonekana ana kinyongo. Hebu angalia, anawezaje kuacha kunialika kwenye shughuli muhimu kama ile kama kweli tumepatana? Mbona amealika watu wengi lakini mimi ameniacha? Wema aache unafiki bwana.
“Mbaya zaidi, hivi juzi tu ameweka picha ya msichana mmoja anayekaa China, huyu mdada anaitwa Sabrina, niliwahi kugomabana naye, lakini yeye amemuweka Instagram na kumwandikia maneno kibao ya kumsifia akim-wish happy birthday, hapo si kama ananisimanga? Wema si mkweli,” alisema Kajala.
Akizungumzia ishu hiyo, siku ya tukio Wema alisema: “Ukiniuliza kuhusu Kajala kutokuwepo hapa, kwa kweli utakuwa kama unanichanganya tu maana leo sijashika simu muda mrefu sana.
“Hata ujio wangu hapa nilikurupushwa, ndiyo maana sijakumbuka kumuita Kajala, lakini tuko vizuri na mara ya mwisho tumeongea jana (Jumapili) usiku tu,” alisema Wema.

SIRI YAFICHUKA, WEMA NA DIAMONDA SASA NI ......

http://photos-g.ak.instagram.com/hphotos-ak-xpa1/927739_312353152262798_239351557_n.jpg

IN THE NAME OF #INSTAGRAM
 ONE OF WEMA'S FAN COME WITH A DOUBT CONCERNING A RING WHICH SEEMED ON THE WEMA'S COURT FINGER SO THE QUESTION COMES DOES WEMA SEPETU TAKE IT FOR DECORATION OR NEAR TO MARRIAGE??

POWER TO YOU!!

ONE OF WEMA'S FAN COME WITH A DOUBT CONCERNING A RING WHICH SEEMED ON THE WEMA'S COURT FINGER SO THE QUESTION COMES DOES WEMA SEPETU TAKE IT FOR DECORATION OR NEAR TO MARRIAGE?? POWER TO YOU!!

DIAMOND KAOZA KWA MADAM WEMA, SASA KUMNUNULIA NYUMBA YA SHILLING MILLION 125


STAA wa Bongo Fleva mwenye mbwembwe kibao, pia anasifika kwa kuwa msafi na anasemekana ndiye mwenye mkwanja wa nguvu Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ anadaiwa yuko kwenye mchakato wa kumnunulia jumba la kifahari mpenzi wake wa ‘nenda rudi’, Wema Sepetu, Amani limeinyaka hii.

KUNA SABABU?
Kwa mujibu wa chanzo, Diamond ameamua kuingia kwenye kujikamua huko kufuatia taarifa kwamba, mmiliki wa nyumba anayoishi Wema kwa sasa (jina lipo), Kijitonyama, Dar es Salaam amemwamuru mlimbwende huyo kuhama kwenye mjengo wake mara baada ya kumaliza mkataba mwezi Juni, mwaka huu. Awali mjengo huo aliutangaza ni wake.

HEBU SIKIA
“Mwenye nyumba anayoishi Wema kwa sasa amekataa mrembo huyo kuendelea kuishi pale, akimaliza mkataba wake Juni, mwaka huu basi, hataki tena.

“Sasa Diamond aliposikia hilo akamwambia Wema isiwe tabu, akamuahidi kumnunulia nyumba ya kifahari yenye thamani ya shilingi milioni mia moja na ishirini na tano.
“Nadhani hiyo nyumba ipo tayari, ndiyo maana amemtajia na bei. Lakini ninavyojua mimi ipo Mwananyamala,” kilisema chanzo.

KUHUSU NYUMBA YA SASA
Kuhusu nyumba ya sasa, ni kweli ‘kifo cha nyani miti yote huteleza’ kwani Wema anatakiwa kutoendelea na mkataba mpya ikiwa ni siku chache tu baada ya Mahakama ya Ilala, Dar es Salaam kuamuru anyang’anywe lile gari lake la kifahari aina ya Audi Q7 lenye usajili wa T 973 BUJ na kukabidhiwa mmiliki wake halali, Shadrack Tweve.

Wema alipewa gari hilo na mwanaume anayedaiwa ni mpenzi wake anayejulikana kwa jina la Clement ambaye alilikopa kwa mmiliki huyo lakini alikuwa akikwepa kulipa deni la shilingi milioni 90.
Akizungumza na mwandishi wetu katika mahojiano maalum yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar, mmoja wa ‘kruu’ ya Wema ambaye hakutaka jina lake lionekane gazetini alisema kwa sasa Wema yuko katika kipindi kigumu baada ya kumwagana na kigogo huyo aliyekuwa akidaiwa kumpa jeuri na kufuatia kuamriwa kuhama kwenye nyumba hiyo.
Chanzo chetu kikazidi kumwaga data kuwa mbali na Wema kuachana na Clement, bado mrembo huyo amekuwa katika kipindi kibaya zaidi baada ya kunyang’anywa gari hilo ambalo ndilo alilokuwa akilitumia.
MKATABA WA NYUMBA ULIVYOKUWA
Mpashaji wetu aliendelea kujuza kuwa mmiliki wa nyumba anayoishi Wema ameamua kusitisha mkataba wa kumuongezea Wema muda wa kuendelea kuishi hapo baada ya kusikia madai ya msanii huyo akitamba kwenye magazeti kuwa mjengo huo ni mali yake na aliununua kwa shilingi milioni 400.

“Mkataba wa awali unaisha Juni, mwaka huu, hivyo hataweza kuendelea kuishi hapo lakini pia hana pesa za kuweza kulipa gharama ya nyumba kama ile, kwa sasa hana jeuri tena,” kilisema chanzo hicho.
Kikaongeza: “Unajua mara baada ya Wema kuingia kwenye nyumba ile na magazeti kuandika kwamba ameinunua, mmiliki wake alimfuata Clement kwa sababu ndiye aliyeingia naye mkataba.

“Akamuuliza inakuaje Wema anatangaza nyumba ni yake? Clement akampoza mwenye nyumba kwa kumwambia kwamba, asiwe na wasiwasi, Wema ni staa, mastaa wa Bongo wanapenda kujisifu, yeye adili na yeye aliyeingia naye mkataba.”
AANZA KUSAKA CHUMBA KIMOJA:
Habari zinadai kuwa mtazamo wa Wema (kama nyumba ya kununuliwa na Diamond itachelewa) ni kutafuta chumba kimoja na kupanga ili maisha yaendelee.

MAMA WEMA ASHAURIWA JAMBO:
Wadau hawakuishia hapo, walifika mbali zaidi kwa kumshauri mama mzazi wa staa huyo, Bi. Mariam Sepetu amchukue Wema na kuishi naye nyumbani kwake, Sinza-Mori, Dar ili kuficha aibu hiyo nzito na kubwa ya binti yake.

“Hata kama kuna tofauti baina yao, namshauri mama Wema amchukue mwanaye waishi pamoja, hii ni aibu ya familia kwa jumla,” alisema mdau mmoja kwa sharti la kutotajwa jina lake.
DIAMOND SASA:
Amani lilimsaka Diamond ili kuzungumza kuhusu madai ya kumnunulia Wema nyumba ambapo alisema:
“Mimi sipendi Wema apate tabu, naweza kumgharamia chochote kile ilimradi atulie tu.”

WEMA ATAFUTWA:
Mwandishi wetu alipomtafuta Wema kwa njia ya simu, iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa, hata mwandishi wetu alipomtumia ujumbe mfupi wa maneno (SMS), bado hakujibu.

CLEMENT NAYE:
Katika harakati zetu za kutetea ukweli, mwandishi wetu alimtafuta kigogo huyo kwa ajili ya kupata ukweli halisi ambapo baada ya mwandishi kujitambulisha, Clement alitoa udhuru wa kwenda kikaoni na kutaka apigiwe baada ya dakika tano.

Baada ya dakika 20, mwandishi alimpigia simu Clement lakini kila ilipoita kwa muda aliikata.

HII NDIO EPISODE YA TISA YA WEMA IN MY SHOES

 
Angalia sehemu ya tisa ya kipindi cha TV cha muigizaji wa kike wa Filamu nchini, Wema Sepetu 'In My Shoes'

DIAMOND NA WEMA KUJA NA ZINA LA MUVI, MSIKILIZE DIAMOND HAPA

Diamond alidondoka kwenye Exclusive interview ya XXL ya Clouds FM na kuyajibu maswali ya Raymond Mshana ambae ndio alikua anaifanya XXL kwa siku hii ya January 6 2014.
Kwenye show ya Xmas Diamond alifanya show yake kwa ajili ya watoto Leaders Dar es salaam ambapo baadae vyombo vya habari vilimkariri akitangaza kwamba Wema Sepetu ndio mpenzi wake wa sasa.
Kwenye XXL Diamond amekwepa kulijibu hilo swali ila akamzungumzia Wema na uwepo wake pamoja na movie yake ambayo wamecheza pamoja na inatarajiwa kutoka mwaka huuhuu wa 2014.

WEMA AUANZA MWAKA KWA MKOSI, NI BAADA YA MAHAKAMA KUTAKA KUMFILISI, SOMA MKASA MZIMA HAPA


Gari aina ya Audi Q-7 lenye namba za usajili T 973 BUJ alilokuwa akiendesha Wema.
Kwa mujibu wa vyanzo vilivyoenda shule vya Ijumaa Wikienda, gari hilo lilikamatwa Januari 2, mwaka huu Namanga, Oysterbay jijini Dar likiwa mikononi mwa kijana wa kiume aliyedaiwa kuwa ni mdogo wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’.
“Alikuwa nalo yule dogo ‘waiti’, mdogo wake huyu msanii Diamond. Alikuwa na wenzake pale Namanga kuna kibarabara cha vumbi, walikuwa wanarekodi video. Jamaa walikuwa wanalifuatilia so lilipopaki ndipo wakalipiga ‘tanchi’ (kulikamata),” kilisema chanzo chetu cha kuaminika.
Ilifahamika kuwa gari hilo lilikamatwa na kampuni kiboko ya madalali wa mahakama nchini (court brokers) ya jijini Dar iitwayo Unyangala Auction Mart Ltd & Court Brokers yenye ofisi zake kwenye Jengo la Harbour View Tower ‘JM-Mall’, Dar.
WEMA ACHANGANYIKIWA
Habari za uhakika zilidai kuwa kabla ya kulipeleka ‘yadi’ dogo huyo aliyekamatwa na gari hilo aliwasiliana na Wema na kumjulisha ambapo ilisemekana kwamba bidada huyo alichanganyikiwa.
Baada ya pale walilipeleka gari hilo kwenye yadi yao hiyo kisha kuwasiliana na mmiliki halali tayari kwa kumkabidhi.

KWA NINI?
Habari za uhakika ziko hivi; Januari 17, 2013, mwanaume aitwaye Clement  (yule kigogo mume wa mtu aliyekuwa mpenzi wa Wema) aliingia kwenye makubaliano ya kulinunua gari hilo kutoka kwa jamaa aliyetajwa kwa jina la George Tesha.

ILIKUWAJE?
Habari zilizochimbuliwa zilieleza kuwa, Clement ana rafiki yake ambaye ana kidosho anayesukuma gari la aina hiyo jijini Dar es Salaam na ‘kuwatesa’ wanawake wenzake.

ETI WEMA AWE NG’ARING’ARI
“Clement naye akasema anataka baby wake (Wema) naye awe anawasumbua na ‘mkoko’ kama huo.
“Tatizo wakati ule magari ya aina ile yalikuwa yanahesabika mjini. Huku na huku Clement akaliona lile gari, akamfuata Tesha na kumbembeleza amuuzie ili akampe Wema naye awe ng’aring’ari mjini.

MAKUBALIANO YANAFANYWA, SHILINGI MILIONI 90
“Jamaa walikubaliana ‘dheni’ Clement akalichukua lile gari kwa makubaliano ya kulipa Sh. milioni 90 za Kibongo.

“Kuna ‘misteki’ aliifanya Tesha kwa kukubali kumpatia gari jamaa bila ‘keshi’ kwa sababu alimwambia amwachie ‘dheni’ akachukue cheki ya mkwanja kesho yake ofisini kwake maeneo ya Magogoni, Dar.
“Kilichotokea ni kwamba kila Tesha alipomfuata ofisini aliambiwa na walinzi kuwa hawezi kuonana na Clement na wakati mwingine aliambiwa hayupo.

NYUMBANI
“Tesha alifanya hivyo mara kwa mara huku miezi ikikatika. Ilifika wakati akaenda hadi nyumbani kwa Clement kule Masaki (Dar) lakini nako aliambiwa hayupo na kama vipi amfuate nyumbani kwa Wema, Kijitonyama.

“Tesha alikuwa hapajui kwa Wema hivyo alianza kupatafuta hadi akapapata nako aliambiwa jamaa huwa anafika na kuondoka zake.
KUMBE SIYO LA TESHA
“Wakati hayo yakiendelea, kumbe lile gari nalo halikuwa la Tesha. Lilikuwa la jamaa mmoja mfanyabiashara (haijulikani ni biashara gani) mwenye mkwanja wake aliyetajwa kwa jina la Shadrack Tweve.

MAHAKAMANI
“Tweve alipoona hivyo vihela (ilisemekana Sh. milioni 90 kwake haimnyimi usingizi) havipati ndipo alipoamua kwenda kufungua kesi ya madai katika Mahakama ya Ilala.

“Mahakama ikaendesha kesi Tweve akimdai Tesha gari lake huku Clement akitafutwa, maana alikuwa hapokei simu wala hajibu meseji zaidi ya kusikika tu mara leo kamfanyia Wema hiki, mara kesho kile.
“Kuna purukushani nyingi zilipita. Hatimaye mahakama ikaamua gari likamatwe akabidhiwe Tweve mzigo wake.

GARI LASAKWA
“Hata kabla ya hukumu ya kesi hiyo, jamaa walikuwa wakilisaka kwa udi na uvumba bila mafanikio.

LAONEKANA MEEDA
“Kuna siku lilionekana maeneo ya Meeda Bar (Sinza-Mori) lakini aliyekuwa nalo akalikimbiza kulificha nyumbani kwa mama Wema, Mariam Sepetu maeneo yaleyale.

LAFICHWA KWA MAMA DIAMOND
“Pia kuna siku nyingine lilionekana Kijitonyama lakini likakimbizwa kwenda kufichwa kwa mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ pale Sinza-Mori.
“Lakini sasa Wema hana tena lile gari na mmiliki halali ni Tweve,” kilitiririka chanzo chetu.

WIKIENDA MZIGONI
Baada ya kujikusanyia data hizo za kiuchunguzi, Ijumaa Wikienda lilifika kwenye ofisi za madalali hao lakini kabla ya kuonana na wahusika lilikutana na gari hilo likiwa ‘yadi’.

Mwanzoni makachero wetu walisita kwa kuwa namba na aina ya gari ni kweli ni lile la Wema lakini rangi ni ‘silva’ badala ya ‘dakibluu’.
KWA NINI ALILIBADILISHA RANGI?
Kuna madai kuwa, Wema alilibadilisha rangi ili lisikamatwe kirahisi kwa kuwa Clement alishaambiwa kuwa linasakwa.

Hata hivyo, walijiridhisha kuwa ni la Wema na kwamba alishalibadili rangi kwa ushahidi wa siku aliyofika nalo Mahakama ya Mwanzo, Kawe wakati wa msala wa Wema kumtandika makofi yule meneja wa hoteli.
Ijumaa Wikienda lilimvaa mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Patrick Sanga ambapo alikiri kupewa kazi ya kulikamata gari hilo na kulikabidhi kwa Tweve.
KUMBE CLEMENT  ALIKIUKA MAKUBALIANO
“Huyo Clement alikiuka makubaliano hivyo mahakama iliamuru tulikamate hili gari na kulikabidhi kwa Tweve kwani ndiye mmiliki halali,” alisema Sanga.

Haukupita muda mrefu, Tweve na Tesha walifika ambapo walionesha kadi ‘orijino’ ya gari hilo (Global ina nakala) kisha gari hilo likakabidhiwa kwa Tweve.
AKABIDHIWA
Huku Ijumaa Wikienda likishuhudia, Tweve aliingia kwenye gari hilo, akaliwasha huku akilalamika kuwa limetumika mwaka mzima hivyo halifanani na lilivyokuwa awali.
“Anyway, bora nimelipata, tayari limetumika mwaka mzima so halipo kama mwanzo,” alisema Tweve.

UTEKAJI?
Wakati Tweve akitabasamu kwa kupata chake ndipo madai mengine mazito yakashushwa kuwa baada ya gari hilo kukamatwa Namanga likiwa na ndugu wa Diamond, Wema alikwenda Kituo cha Polisi Kijitonyama  ‘Mabatini’ kuripoti kuwa eti ametekwa na kuporwa gari hilo.

Ijumaa Wikienda lilichoma mafuta hadi Polisi Mabatini na kunusa dodoso zozote juu ya kuwepo kwa shitaka hilo ambapo ilibainika kuwa halipo na badala yake ikaelezwa kuwa inawezekana alikimbilia Kituo cha Polisi Oysterbay lakini huko nako halikuonekana shitaka hilo.
Baada ya kupata ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta Wema ambaye anadaiwa kumpiga kibuti Clement lakini akawa hapokei simu.
Hata alipofuatwa nyumbani kwake, Kijitonyama (Makumbusho) ilielezwa kuwa, Madam ambaye kwa sasa anaminya kimalavu na Diamond hayupo. Ijumaa Wikienda lilikwenda hadi ofisini kwake, Mwananyamala ambako palikuwa pamefungwa.

DIAMOND AINGIA KWENYE BIFU NA KIGOGO WA WEMA SEPETU, KISA KIZIMA HIKI HAPA

Yule kigogo au taita aliyekuwa akimpa jeuri ya fedha Wema Isaac Sepetu ajulikanaye kwa jina moja la Clement anadaiwa kutangaza vita na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.
Habari ‘hoti’ zinadai kuwa Clement anataka Diamond arudishe gharama alizomgharamia Wema ndipo waendeleze mapenzi yao.

Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ na Wema Isaac Sepetu katika pozi.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa kigogo huo, Clement anadai kwamba gharama alizotumia kwa Wema ni kubwa mno lakini bidada hakujali chochote na kuukabidhi moyo wake kwa ‘Mtoto wa Tandale’ ambaye ndiye barafu wa moyo wake.
Wema Isaac Sepetu.
“CK (Clement) anaumia sana kuona kuwa ameteketeza fedha nyingi kwa Wema lakini bila hiyana, mrembo huyo akabwaga manyanga kisha akarudisha mpira kwa kipa na kuanza moja huku kaka mkubwa akiachwa kwenye mataa,” alitonya mnyetishaji huyo bila kufafanua kama Clement aliachwa mataa ya eneo gani.
Akiendelea kutiririka bila kuweka nukta au ya mkato, mtu huyo alisema kuwa kiasi ambacho kinadaiwa kuteketea kwa Wema kinakaribia Sh. milioni 279.6 ambazo gharama hizo zinahusisha vitu kadhaa alivyowekeza kwa Wema.
“Kuna gharama za utengenezaji wa Filamu ya The Super Star ambayo haijulikani kilichotokea kwani hadi leo haionekani sokoni.

“Kama hiyo haitoshi kwenye uzinduzi wa filamu hiyo akamleta staa wa filamu wa Nollywood, Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde na sherehe mbili za uzinduzi zilifanyika katika hoteli kubwa mbili tofauti, ikasemekana milioni arobaini na nane ziliteketea.
Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.
“Kuna kodi ya pango la ofisi ya Wema ya Endless Fame iliyopo Mwananyamala Koma-koma, Dar, jamaa alilipa milioni nane na laki nne kodi ya miaka miwili ambayo kwa mwezi ni laki tatu na nusu.
“Ukiachana na gharama za nyumba na ofisi, kuna gari aina ya Audi Q7, inadaiwa kanunua Clement kwa Sh. milioni 98, Toyota  Harrier Lexusya Sh. milioni 48 na Toyota Mark X iliyomtoa Sh. milioni 25.
“Usisahau hata lile Toyota Noah ‘kitimoto’ la ofisi alinunua Clement kwa Sh. milioni 10, faini aliyolipiwa

Kajala Masanja mahakamani Sh. milioni 13, gharama za kuirekebisha ngozi yake alipoenda nchini China iligharimu Sh. milioni 14, yaani jumla ni kama Sh. milioni 279 na ushee. Na hiyo ni kwa vitu vinavyojulikana ukiachia mbali shopping za Dubai,” alitiririka kikulacho huyo.
Baada ya kujazwa data, Risasi Jumamosi lilijaribu kumtafuta kigogo huyo lakini licha ya juhudi zote hizo hakuweza kupatikana ndipo alipogeukiwa Diamond:
 “Sitishiki kwa lolote lile kwani huko nyuma kabla sijawa maarufu kivile enzi ya Nenda Kamwambie (wimbo) niliwahi kukaa mahabusu kwa siku kadhaa na sababu ilikuwa mapenzi kwa hiyo kwa hili siogopi kitu kwanza mimi ndiyo alinichukulia na mwana mpotevu amerudi kundini,” alisema Diamond anayekimbiza na Ngoma ya Number One.

"JAMANI NGOZI YA WEMA WA SEPETU NI LAINI VIBAYA MNO" HAYA NI MANENO YA DIAMOND

"Umemwona Wema, kwa sasa ana ngozi nzuri yenye afya na iliyo na mng’aro kama alivyokuwa awali,ni nzuri sana yani,  ameacha kabisa kutumia dawa za kung’arisha ngozi hilo ndilo lililonivutia zaidi kwani alisikiliza ushauri niliompa kabla.”
Hiyo ni kauli ya staa aliyetikisa mwaka 2013 bwana Diamond Platnumz aliyoitoa hivi karibuni alipokuwa akizungumza na gazeti maarufu la michezo nchini hivi karibuni.

 Diamond amesema Wema ndiye mwanamke anayetamani kuwa naye katika maisha yake, hivyo kauli yake aliyoitoa mwanzo kuhusu kuzaa na Wema ipo mbioni kutimia.

“Miezi kadhaa nyuma niliongea kuhusu nia yangu ya kuzaa na Wema, wakati huo nilikuwa bado na Penny, siwezi kukimbia kivuli changu kwani ukweli unabaki palepale nampenda yule binti, japokuwa wapo wanaosema kwamba sijatulia au natafuta ‘kiki’ kupitia warembo hawa, si kweli, Wema nilikuwa naye kabla ya Penny na vigezo vyangu ni mchumba anayejali kazi yangu na kujua kwamba mimi ni staa nahitajika sehemu yoyote, muda wowote, Wema ni mwelewa.” Alisisitiza Diamond

WEMA ASEMA MARTINI KADINDA NDIO MWENYE SIRI YA KILA MAFANIKIO ANAYOYAPATA, SOMA ZAIDI WEMA ALICHOKISEMA


MSANII nyota wa filamu Bongo Wema Isack Sepetu amefunguka kwa kudai kuwa hawezi kuvunja urafiki na meneja wake Martin Kadinda kwa sababu kama kuna kitu chochote cha mafanikio nyuma yake yupo Kadinda.

Wema Sepetu ameuambia mtandao wa FilamCentral  kuwa hana rafiki anayejua siri zake zaidi ya meneja huyo ambaye amekuwa akimuongoza vema.

“Kadinda ndo kila kitu kwangu, hata akiondoka na kukaa mbali na mimi kwa muda mrefu ninapokutana naye tu, nitamweleza kila kitu toka siku ya mwisho tuliyoachana, hivyo inakuwa kama sijapoteana naye,yaani ni kama vile nipo naye kila siku iendayo kwa Mungu,”anasema Wema.
 
Msanii huyu ameendelea kusema kwamba hata kampuni yake ya Endless Fame film aliifungua kwa msaada wa Kadinda baada ya kumshauri  kuwa kwa hadhi yake anastahili kuwa na kampuni na aache kuigiza filamu za watu wengine.

MPANGO WA WEMA WATIMIA, DIAMOND ATANGAZA NDOA NA WEMA

HUKU mchumba’ke, Penniel Mungilwa ‘Penny’ akifungasha virago kurejea kwao, mzee mzima Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametangaza kumuoa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’(kushoto) na Penniel Mungilwa ‘Penny’ wakiongea jambo enzi za mapenzi yao.
Ishu hiyo ilijiri ndani ya Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar ambapo mkali huyo wa Bongo Fleva alikuwa akikamua kwenye sherehe ya Krismasi aliyoiandaa mwenyewe. Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ baada ya kupanda jukwaani katika viwanja vya leaders.
TANGAZO LA AWALI
Awali kabla ya kufikia eneo la kutangaza kuoana, Diamond aliweka wazi jukwaani kwamba yeye na Wema wamerudiana.
Diamond Platnumz akiongea jambo baada ya Wema Isaac Sepetu ‘Madam’  kupanda jukwaani.
MTIRIRIKO ULIVYOKUWA
Diamond, akiwa ameshika kipaza sauti alikatisha kuimba na kuwauliza mashabiki wake, hasa watoto waliohudhuria kwa wingi tamasha hilo, je, wanataka kumuona shemeji yao?
“Itakuwa si vizuri mkaondoka bila kumuona shemeji yenu, nikuleteeni mumuone?” aliuliza  Diamond. Swali hilohilo akalirudia tena ambapo lilipokelewa kwa shangwe huku mashabiki wakilitaja jina la Wema.
                                        Diamond Platnumz na Wema Isaac Sepetu wakijiachia.
WEMA APANDISHWA JUKWAANI
Kufuatia kelele za mashabiki, Diamond alimuomba Disco Joker (DJ) wake amuwekee Wimbo wa Ukimwona ambao ulisindikiza ujio wa Wema jukwaani akifuatana na wapambe wa Diamond.
“DJ acha huo, nipigie Wimbo wa Ukimwona watu wangu wa nguvu wamwone shemeji yao kwani tangu nilivyokwenda naye China walikuwa wakisumbuliwa na maneno tofautitofauti kutoka kwenye mitandao ya kijamii,” alisikika Diamond.
Diamond, akiwa ameshika kipaza sauti akiima Wimbo wa Ukimwona na Wema akiwa amemkumatia.
JUKWAA SASA
Hali haikuwa ya kawaida jukwaani kwani kilichofuata hapo ni Wema kuonesha kwa vitendo mambo yaliyoashiria kuwa, wawili hao sasa ni mwendo mdundo.
Wema alishuhudiwa akimzungushia mikono Diamond kwenye kiuno jambo ambalo liliwafanya baadhi ya mashabiki wa mastaa hao kutoa machozi ya furaha kuona penzi la wawili hao limerudi upya, wengine walimwambia Diamond amuoe Wema.
“Diamond muoe Wema, mnapendezana sana,” walisikika mashabiki.

Wema Isaac Sepetu ‘Madam’akimuaga Diamond Platnumz kwa kumkumatia.
MAWIFI WADAI KUHARIBIWA SIKU NA KAKA YAO
Hata hivyo, kitendo cha Diamond kumwita Wema jukwaani kilionekana kuharibu furaha ya sikukuu kwa ndugu zake kwani bila ya kuuma midomo dada zake staa huyo wakiongozwa na Esma Khan walinuna na kuanza kuondoka.
“Yaani siku yangu imeshaharibika, nilikuja nina furaha sasa imepotea, tuondokeni ndugu zanguni,” alisema Esma akiwaambia Mwanaisha Abdul ‘Queen Darleen’ na Halima Haroun ‘Kimwana’.

Diamond Platnumz na Penny wakiwa pamoja enzi za mapenzi yao.
MAMA DIAMOND ASHANGAA
Kitendo cha ndugu hao kukasirika hakikupokelewa vizuri na bi mkubwa wao yaani mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambaye aliwajia juu akiwashangaa.
“Wajinga nini? Sasa walitaka Diamond… (tusi) wao, mtu ameshaamua kupenda wamwache, mi’ mwenyewe nimeshajifunza, sitaki kuingilia penzi lake,” alisema mwanamke huyo ambaye mjini anazungukia usafiri aina ya Altezza.

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’  na Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Baada ya shoo hiyo iliyomalizika saa moja usiku, paparazi wetu alimfuata Diamond akiwa amesimama na Wema na kuwauliza kama kweli wana nia ya kufunga ndoa.
“Hilo mwana mbona lipo wazi, nataka kumuoa staa na nataka kuzaa na staa,” alisema Diamond huku Wema akiwa hapingi.

MAMA WEMA ATANGAZA VITA  NA DIAMOND
Wakati Dimaond akitambia ndoa na Wema, siku hiyohiyo ya Krismasi, mama wa Wema, Mariam Sepetu alidaiwa kutangaza vita na mwanamuziki huyo baada ya kusikia tetesi kuwa amerudiana na mwanaye.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa mama Wema (jina tunalo) mama wa staa huyo alichukizwa na kitendo cha Diamond kurudiana na mwanaye kwani anaamini anamchezea tu.

Mama wa Wema, Mariam Sepetu.
Rafiki huyo alizidi kudai kuwa, taarifa hizo zimemuweka  mama huyo kwenye wakati mgumu na kudai kuwa popote atakapokutana na mwanamziki huyo atampopoa mawe au machungwa hata ikiwa siku ya ndoa yao.
“Mama Wema amesema hampendi Diamond, popote atakapomuona itakuwa vita ya wawili, kama kuna jiwe atamrushia, hata machungwa kama yapo yatakuwa halali yake,” alisema rafiki huyo.

WOSIA WA MZEE SEPETU
Mpashaji huyo wetu alizidi kufunguka kuwa, mama Wema ana wosia mkononi ambao aliuacha marehemu mumewe, mzee Isaac Abraham Sepetu.
Alisema katika wosia huo, mzee huyo alisema hataki Diamond amuoe Wema na kama mrembo huyo atakiuka  wosia huo atapatwa na laana mbaya katika maisha yake.
“Kinachomuumiza zaidi mama Wema ni huo wosia, mzee Sepetu alisema hataki mtoto wake aolewe na Diamond, kama atakataa kuna kitu kibaya kitamkuta katika maisha yake,” alisema rafiki huyo.

MAMA WEMA ASAKWA
Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili lilimvutia waya mama Wema ili kuweza kuthibitisha madai hayo ambapo alisema kuwa, hayuko tayari kuzungumzia jambo hilo kwa wakati huo mpaka atapoamua akisisitiza muda si mrefu.
“Jamani nina mambo mengi sana ya kufanya na sijatulia kabisa siko tayari kuzungumza chochote kwa sasa nikiwa tayari nitawaambia kila kitu,” alisema mama Wema.JIUNGE NA PAGE YETU YA FACEBOOK  HAPA >> Mdadisi MAMBO

 

"WEMA KANIFUKUZA KWA SABABU ALIKUWA HANIPI MSHAHARA NA SI KWAKMBA KANIFUMA NIKIZINI" HAYA NI MANENO YA CHID

BAADA  ya kudaiwa kufanya ngono katika magari ya Kampuni ya Endless Fame inayoongozwa na Wema Issac Sepetu, Prodyuza, Rashid Mohammed ‘Chid Classic’ amefunguka na kusema chanzo cha yote ni mshahara  na ukuwadi ndani ya kampuni hiyo wala siyo uzinzi, Amani linakujuza.
Prodyuza Rashid Mohammed ‘Chid Classic’.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili, Chid amesema hajafukuzwa katika kampuni hiyo kama alivyodai mratibu wa kampuni hiyo, Petit Man bali ameondoka baada ya kuchoka  kufanya kazi bila ya kulipwa mshahara.
“Ni uongo kusema kwamba nimenaswa nikifanya uzinzi Coco Beach nikiwa ndani ya magari ya Wema, sijawahi hata siku moja kufanya hivyo kwani nina kwangu ambako nina uwezo wa kumwingiza mwanamke wakati wowote,” alisema.
Wema Isaac Sepetu.
“Tangu kampuni ianzishwe haijawahi kulipa mishahara unadhani nitakuwa na moyo wa kufanya kazi, sikwenda pale kufanya ukuwadi kama wengine, tena nawaomba wasiendelee kusema uongo kwani nina mengi nayajua ya Endless Fame,” aliongeza Chid.
Baada ya kusikia maelezo hayo, Amani lilimtafuta Wema bila ya mafanikio ndipo likaongea na meneja wake, Martin Kadinda.
“Nina wasiwasi na kauli za Chid kwanza tatizo siyo mshahara na hayo masuala ya ukuwadi ni uongo na uzushi, kama ni kweli kwa nini asiongee siku zote hadi lilipoibuka hili la kunaswa akifanya uzinzi kwenye gari?” alihoji Kadinda.

"MIMI MSANII WA FILAMU NA DIAMOND NI MUIMBAJI, SO SIWEZI KUSHINDANA NAE" HAYA NI MANENO YA WEMA SEPETU


Je wewe ni kati ya wanaoamini kuwa wapenzi ‘wa zamani’ Wema Sepetu na Diamond Platnumz wanashindana kwa namna yoyote? Star wa kipindi cha ‘In My Shoes’ Wema Sepetu ameshare ujumbe kwa wote wanaofikiria hivyo.

Kupitia Instagram ameandika kuwa kitu pekee kinachosababisha watu wahisi hivyo ni kutokana na wote wawili kuwa na mafanikio katika fani zao (muziki na movie), na kuongeza kuwa hawezi kushindana na Diamond sababu yeye sio muimbaji

WEMA AWEKA PICHA YA DIAMOND KWENYE AKAUNTI YAKE YA INSTAGRAM NA KUANDIKA MANENO MAZURI, YASOME HAPA

 
Mcheza filamu za kibongo Wema Sepetu ametuma picha ya mpenzi wake wa zaman mwanamuziki Diamond Platnamu kwenye akaunti.yake ya instagram na kuandiki
“ i jus happen to love dis picture“
baada ya kuweka picha hiyo mashabiki wameanza kumsifia uku wakimponda mpenzi Penny ambae anaaminika ndio mpenzi wa Diamond kwa sasa
Website hii imepitia akaunti ya Diamond na kukuta picha ile ile aliyoweka Wema ikiwa na maneno kuonesha kua usiku wa jana masanii huyu alikua kwenye sherehe ya kuzaliwa mrembo wa zamani wa Tanzania Jackline Ntuyabaliwe.

YALE YA KWENYE KESI YA KAJALA YAMKUTA NA WEMA , SOMA KUJUA NI NINI KIMEMKUTA

KICHEKO! Ile kesi ya kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni Meneja wa Hoteli ya Mediteranian iliyopo Kawe Beach, Dar, Godlucky Kayombo iliyokuwa ikimkabili Wema Isaac Sepetu imetolewa hukumu yake kama ilivyokuwa ile ya shosti’ake, Kajala Masanja.
Wema Sepetu akitinga Mahakama ya Mwanzo ya Kawe, Dar.
Habari kutoka kwa chanzo makini cha gazeti hili kilieleza kuwa Wema alihukumiwa kifungo cha miezi mitatu au faini ya shilingi laki moja kwa maana ya elfu hamsini kwa kila kosa baada ya kukutwa na hatia ya kutenda makosa hayo mawili ya kupiga na kutukana.
WEMA AOMBA IHARAKISHWE
Habari za ndani kutoka kwa mtu wa karibu wa Wema au Madam zilieleza kuwa hukumu ya kesi hiyo ilikuwa iahirishwe lakini staa huyo akaomba itolewe kwa kuwa alitaka kusafiri.
Ilisemekana kuwa mbali na kuwa na safari pia aliomba itolewe kwa sababu yupo ‘bize’ na maandalizi ya arobaini ya baba yake, Isaac Sepetu aliyeaga dunia hivi karibuni.

Hukumu hiyo ilitolewa katika Mahakama ya Mwanzo ya Kawe, Dar ambako ndiko kesi hiyo ilipokuwa ikirindima tangu mwezi Agosti, mwaka huu.

Wema Sepetu na rafiki zake wakijadiliana jambo eneo la Mahakama ya Mwanzo ya Kawe, Dar.
ASUBIRIWA KUPELEKWA GEREZANI, ACHOMOA ‘MADOLARI’
Ilielezwa kuwa katika hukumu hiyo iliyosomwa kwa takriban saa mbili, Wema alikuwa akisubiriwa nje tayari kupelekwa gerezani lakini kama kawaida yake fedha iliongea ambapo alizamisha mkono laini kwenye ule mkoba wake na kuchomoa ‘madolari’.
Chanzo kilidai kuwa zilihitajika fedha za Kibongo hivyo Wema alichambua mkoba wake na kutoa ‘wekundu’ kumi huku akirejesha zile dola za Kimarekani.

“Wema alifanya kama alivyomfanyia Kajala siku ile pale Kisutu. Kwa Wema ishu ya fedha siyo tatizo sana. Kuliko kumpotezea muda, Wema yupo tayari kutoa kiasi chochote cha fedha.
“Kwa Wema muda ni kitu cha muhimu zaidi kuliko hata hiyo fedha ndiyo maana alitoa tu hiyo faini mara moja,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kupokea maelezo hayo, gazeti hili lilimsaka Wema ili kupata mzani wa habari hiyo lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
Wema na shosti wake Kajala wakitoka mahakamani hapo.
Hata hivyo, alipotafutwa meneja wake, Martin Kadinda na kuulizwa juu ya suala hilo alifunguka:
“Ile kesi iliisha tangu Ijumaa iliyopita, watu hawakujua tu. Wema alihukumiwa kifungo cha miezi mitatu au faini ya shilingi laki moja.

“Alichokifanya Wema alilipa faini hiyo na sasa yupo freshi na mishe zinaendelea. Unajua haruhusiwi kufanya mahojiano hadi amalize arobaini ya baba yake.”
Chanzo kilisema kuwa kabla ya hukumu hiyo, Wema alikuwa katika hali kama ile iliyomkuta Kajala wakati wa hukumu yake miezi kadhaa iliyopita kwani alikuwa akilia, kujuta na kumuomba Mola amuepushe na balaa hilo lililosababishwa na kuwa ‘tilalila’.

Hata hivyo, hukumu hiyo iliwashangaza watu kwani iliendeshwa kwa muda mrefu na kwa mbwembwe nyingi lakini hokumu yake ikawa ya kawaida tofauti na matarajio ya wengi.
Wema Sepetu na kampani yake wakiondoka eneo la mahakama.
KAJALA NAYE KICHEKO TENA
Wakati Wema akikenua, wiki hii Kajala naye ilikuwa chereko chereko baada ya  Mahakama ya Rufaa Kanda ya Dar kuridhika na hukumu yake iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema mwaka huu kufuatia rufaa iliyokatwa na mume wa staa huyo Faraji Chambo.

Katika kesi ya awali, Kajala alihukumiwa kifungo cha miaka mitano au faini ya Sh. milioni 13 baada ya kupatikana na hatia ya kushirikiana na mumewe kwenye msala wa kutakatisha fedha haramu wakati mwanaume huyo akifanya kazi Benki ya NBC, Dar.
Hata hivyo, Wema alimlipia faini hiyo kama alivyofanya kwenye kesi yake.

Katika hukumu ya rufaa hiyo, majaji walijiridhisha kwamba kesi hiyo iliendeshwa ipasavyo na Kajala alitimiza taratibu za kuwa huru kwa kulipa faini lakini mumewe aliyehukumiwa miaka saba alishindwa kulipa faini ya Sh. milioni 213.
MAOMBI YAO YASIKIKA
Wema na Kajala wamekuwa kwenye maombi ya kufunga wakisali na kufanya dua ili kuwaepusha na kifungo hivyo kwa sasa wote ni vicheko.

-GPL
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger