Search in This Blog

Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

ZITTO AZIDI KUIPA TABU CHADEMA, SOMA HAPA KUJUA NI TABU GANI


HUKUMU iliyosomwa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, John Utumwa, Jumanne iliyopita (juzi), imemuongezea uzito Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, sasa amekuwa mzito zaidi ndani ya chama chake.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe akiwa ndani ya Mahakama Kuu wakati akisubiri hukumu ya kesi yake juzi.
Awali, ilionekana kama uamuzi wa Kamati Kuu (CC) ya Chadema ni msumari wa mwisho na kwamba Zitto hana uzito wowote wa kuutilia changamoto lakini kile kilichoamuliwa na mahakama ni wazi kimemuongezea nguvu mbunge huyo.
Wafuasi wa Zitto wakiwa na mabango wakati wa hukumu yake.
Hukumu ya Jaji Utumwa, ilimpa ushindi Zitto kuhusu pingamizi lake aliloweka mahakamani akitaka mahakama iweke zuio kwa CC ya chama chake kujadili uanachama wake mpaka atakapopewa fursa kukata rufaa katika Baraza Kuu la Chadema.
Kutokana na hukumu hiyo, baadhi ya wananchi walitoa maoni yao kwamba, Zitto anaweza kupumua sasa angalau kwa kiasi fulani kuweza kuuthibitishia umma kuwa, CC ilimuonea.
“Angeshindwa mahakamani, angekuwa na hatima mbaya kwenye chama chake, tena angefukuzwa uanachama mara moja lakini mahakama imempa nguvu, sasa uzito wake ni mkubwa na hata wanaomuunga mkono wanaweza kutembea kifua mbele,” alisema Shadrack Lyimo aliyekuwa mahakamani juzi.
Zitto, amefungua mashtaka mahakamani akimshitaki katibu mkuu wa chama chake na baraza la wadhamini  kwa kutompa fursa ya kuukatia rufaa uamuzi wa CC wa kumvua nyadhifa zake zote na sasa kesi ya msingi itasomwa kwa mara ya kwanza Februari 13, mwaka huu.
Katika madai ya msingi, Zitto anataka katibu mkuu na baraza la wadhamini wa Chadema kumpa fursa ya kukata rufaa Baraza Kuu kwa maelezo kwamba, CC ilikiuka taratibu ya kumvua nyadhifa zote za uongozi.
Jaji Utumwa akisoma hukumu yake alisema CC hairuhusiwi kujadili uanachama wa Zitto mpaka hukumu ya kesi ya msingi itakapotolewa au pale Baraza Kuu litakapoitishwa na kusikiliza rufaa ya mbunge huyo.

HUU NDIO MPANGO WA ZITTO KUTOTAKA KUJADILIWA UWANACHAMA WAKE


TABIA ya Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu, kumrushia madongo Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya chama hicho, Zitto Kabwe, imesababisha hasira kwa mlengwa na sasa ameamua kuchukua uamuzi mkali zaidi.

Zitto Kabwe pamoja na Mwanasheria wake,Albert Msando (kulia) wakiwasili katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam jana wakiongozana na wafuasi wanaopinga kuvuliwa uongozi wake, tayari kwa kwenda kusikiliza hukumu ya kesi yake.
Zitto, ameamua kumrudi Lissu kwa staili nyingine kwa kwenda moja kwa moja na kummaliza Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa sababu anayo makombora mengi makali ambayo hapo kabla aliyaficha ili kunusuru chama.
Chanzo chetu kimesema, Zitto amekasirishwa na mashambulizi kutoka kwa Lissu na kwamba baada ya kukaa kimya muda mrefu, sasa uzalendo umemshinda, kwa hiyo kinachofuata ni mashambulizi mwanzo mwisho dhidi ya Mbowe.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
“Huu ni mpango endelevu, Zitto anajua kwamba maneno ya Lissu ni ya kulishwa, mhusika ni Mbowe, ndiyo maana amesema hataki majibishano na kifaranga, anamtaka mama wa kifaranga ajitokeze,” alisema rafiki wa Zitto kwa sharti la kutotajwa jina na kuongeza:
“Mpango uliopo ni kukabiliana na mama wa vifaranga, yapo mabomu mengi ya maana ambayo Zitto anayo dhidi ya Mbowe, anachosubiri ni hukumu ya pingamizi lake mahakamani kuhusu Kamati Kuu ya Chadema kujadili uanachama mpaka itakampo fursa ya kukata rufaa Baraza Kuu.”
Hukumu hiyo, ilitarajiwa kusomwa jana Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam chini ya Jaji John Utamwa.

Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa Chadema, Tundu Lissu.
Jumapili iliyopita, Zitto alisema kuwa maneno yanayozungumzwa na viongozi wa Chadema, mengi yakipitia kwenye kinywa cha Lissu ni sawa na mipasho kwa sababu hayamo kwenye tuhuma 11 ambazo walimwandikia azijibu kwa maandishi.
Kwa upande wa Mbowe, alinukuliwa akisema kuwa Zitto hapaswi kuibua tuhuma mpya dhidi yake, isipokuwa anachopaswa kufanya ni kujibu yale ambayo anatuhumiwa, huku akiyaita maneno ya mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini ni ya kitoto.

ZITTO KABWE AIBUKA KIDEDEA KWENYE KESI YAKE

Mahakama kuu ya kanda ya dar es salaam imempa kinga ya muda mbunge wa kigoma
Kasikazini mh. Zito kabwe  kutojadiliwa uanachama wake na kamati kuu ya chadema

HUYU NDIO MWENYEKITI WA CHADEMA ALIYEPIGWA KIPONDO USIKU WA KUAMKIA LEO NA KUTUPWA

ununio1Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Temeke Joseph Yona amepigwa na watu wasiojulikana na kisha kutupwa kwenye eneo la Ununio kwenye Magorofa ya Wasomali Kawe Dar es salaam.
Shuhuda Abdul Ally ambae ni mkuu wa nyumba zilizokaribu na alikopigwa Mwenyekiti huyu, anasema walisikia kelele za huyu mtu kupigwa saa tisa usiku na walipomsogelea walimkuta peke yake.
‘Niliomba wasiniue, wamenipiga sana… wamenichukua saa tano nyumbani kwangu Kwa Aziz Ally, wao walikua na gari kama ya Polisi lakini inaonekana sio ya polisi wakasema tunakupeleka Central, tulikua wanne na hawakuhangaika na mtu wakanichukua mimi moja kwa moja.. tulipopanda kwenye gari wakachukua nguo yangu wakanifunga uso, wakaanza kunipiga wakisema nisiwajibu na hawakuniambia chochote’
Unaweza kusikiliza maelezo yake mengine akihojiwa kwa kubonyeza play hapa chini..

ununio8 ununio7 ununio6 ununio5 ununio4 ununio3 ununio1 DSC_0027 ununio2

HATMA YA ZITTO KABWE CHADEMA KUJULIKANA KESHO SAA NANE



Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeahirisha kutoa au kutotoa zuio la muda kwa Kamati Kuu ya Chadema kutojadili uanachama wa Zitto Kabwe mpaka kesho saa nane mchana!

ZITTO ASEMA YA MOYONI, NI KUHUSU UFISADI UNAOFANYWA NA FREEMAN MBOWE

Akizungumza katika press conference ya CHADEMA na waandishi wa habari iliyofanyika leo, Mwanasheria mkuu wa Chadema, Mh.Tundu Lisu alisema kuwa mkakati wa kuwachafua viongozi ni wa siku nyingi ambapo Chama kimefanikiwa kunasa mawasiliano ya Zitto tangu mwaka 2009 alipokuwa akiwasiliana  na  akina Denis Msack wa Mwananchi.

 Lissu alisema njama hizi ndio zilizopelekea mpaka mashtaka ya Ugaidi ambapo katika mahojiano yake ya Star Tv akiwa na akina Mwigulu Nchemba Zitto hakukanusha, pia aliandika kwenye mitandao kuwa Chadema imtose Wilfred Lwakatare 
 
Lissu aliongeza kuwa Zitto mpaka sasa ana magari mawili ya Nimrod Mkono na Mkono mwenyewe ndiye amewaambia taarifa hizo. Mkono amewaambia kuwa amempa Zitto hela nyingi sana na Zitto alishiriki moja kwa moja kumzuia mgombea wa Chadema katika Jimbo la Nimrod Mkono .
 
====Huu  ni  ujumbe  wa  Zitto Kabwe  kujibu  mapigo  ya  Tundu Lissu===
**
Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini. 

 Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa.

 Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa. Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka Conservative party?

Nimefanya internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda.

Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas.

They must know I am not a push over. Chacha died, I won't.

Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea mtu kidole kuhusu maadili.

YASOME HAPA MAAMUZI YA CHADEMA YA KAMATI KUU

Katibu Mkuu  anaanza kwa kuomba radhi kwa kuchelewa kuanza press akiungana na John Mnyika pia Katibu Mkuu anasema kuwa atasoma neno kwa neno kutokana na umuhimu wa hoja yenyewe! Ameanza kusoma na kusema kamati kuu ilikuwa ni ya dharura iliyokuwa na lengo la kuwajadili Wanachama watatu Dr. Kitila Mkumbo, Zitto Kabwe na Samsoni Mwigamba.
Dr Slaa anaonyesha kabrasha lenye nyaraka mbalimbali ikiwemo mkakati wa mabadiliko 2013, mashtka ya watuhumiwa na nyaraka nyingine muhimu. Sasa Dr. Slaa anasoma mashtaka yote 11 ya Watuhumiwa kama walivyokabidhiwa kwa maandishi

Katibu Mkuu anasema Watuhumiwa wawili yaani Dr. Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba waliitikia wito wa Kamati Kuu lakini aliyehojiwa na Kamati Kuu ni Dr. Kitila Mkumbo pekee ambaye katika utetezi wao walikana kuvunja katiba ya Chama na Kanuni zake.
Katibu Mkuu anasema Dr Kitila Mkumbo alikiri kumfahamu M2 na anamjua fika lakini hawezi kumtaja mpaka awasiliane nae kwanza. Pia Dr Kitila Mkumbo alisema yeye na Mwandishi wa waraka ule walimpa briefing Mh. Zitto Kabwe kwa hiyo alikuwa anaufahamu waraka huo.


Dr. Kitila Mkumbo alikataa kuzungumzia vifungu vya katiba walivyodai vimevunjwa kwa madai kuwa tayari wana malalamiko kwa msajili tayari. Aidha Dr. Kitila Mkumbo alishindwa kuithibitishia Kamati Kuu kwa ushahidi kuhusu madai ya taarifa ya fedha ambazo yeye na Zitto walishiriki, pia alishindwa kuonyesha ushiriki wa M/Kiti katika manunuzi ya vifaa mbalimbali vya Chama zikiwemo pikipiki za Chama.

MH. TUNDU LISSU ABWAGA CHOZI..CHEZEA SIASA WEWE.

Mbunge na mwanasheria wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA akilia machozi ya ajabu baaada ya purukushani yiliyosababishwa na makundi yaliyokuwa yakipingana...Wanaomuunga mkono na wasiomuunga mkono Mh Zitto Kabwe...!Anayebembeleza ni mbunge wa viti maalumu CHADEMA Mh. Jocya Mukya...HATARI SANA... IMEKAAJE HII...TOA MAONI YAKO HAPO CHINI

LOWASSA AKARIBISHA MWAKA 2014 KIAINA, CHECK HAPA

WAZIRI  Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Ngoyai Lowassa ameangusha bonge la pati la kuukaribisha mwaka 2014.

Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akizungumza katika sherehe ya mwaka mpya nyumbani kwake Ngarashi Monduli.Pembeni yake ni mkewe mama Regina Lowassa.
Tukio hilo lililojaa furaha ya aina yake lilifanyika Januari 1, mwaka huu nyumbani kwake Ngarashi- Monduli, mkoani hapa ambapo mamia ya watu walijumuika pamoja na mbunge huyo kuukaribisha mwaka.
Lowassa aliyeonekana na sura ya furaha, alishika kifaa chenye mkia wa ng’ombe ambacho ni cha asili na kuwasalimia waalikwa kwa kukichezesha kuashiria sherehe imeanza na watu waukaribishe mwaka mpya.
Mbali na wageni waalikwa, Lowasa alijumuika na familia yake akiwemo mkewe, Regina Lowassa ambaye pia alionekana akiambatana na mumewe kwa kuwasalimia ndugu wageni waalikwa.
Katika pati hiyo ya kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya, watu walikunywa, walikula hadi kusaza.
Waalikwa walimuomba Mh Lowassa kujenga utaratibu huo kila mwaka, ili kudumisha umoja na mshikamano.                   
Waalikwa katika shughuli hiyo, walikuwa ni pamoja na maaskofu na viongozi wengine wa dini wa ndani na nje ya nchi.
Waalikwa hao walimpongeza Mh Lowassa kwa kitendo cha kuamua kujumuika pamoja na ndugu zake na viongozi mbalimbali kwani kimeonesha ishara ya upendo.
“Ni jambo zuri sana Mh Lowassa amefanya kwa ndugu zake. Mwaka mpya ndiyo huu unaanza hivyo si vibaya akikutana na kufurahi pamoja na wadau mbalimbali,” alisema mmoja wa waalikwa.

PINDA BADO WAZIRI MKUU HADI 2015 NA BARAZA LA MAWAZIRI HALIVUNJWI


SIRI nzito imevuja! Ni dhahiri kwamba, Rais Jakaya Kikwete ‘JK’ hatavunja baraza la mawaziri kufuatia kusitisha kwake uteuzi wa mawaziri wanne na kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi,  Dk. William Augustao Mgimwa kama wengi wanavyoamini bali atabadilisha tu, Risasi Jumamosi lina cha kushika mkononi.
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda.
Mawaziri ambao uteuzi wao ulitenguliwa ni Emmanuel John Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Mathayo David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi) na Balozi Khamis Juma Kagasheki (Maliasili na Utalii) aliyejiuzulu kutokana na ukiukwaji wa maadili na haki za binadamu katika Oparesheni Tokomeza Ujangili.                                                                      Mhe.Nchimbi.
KWA NINI HAVUNJI BARAZA?
Kwa mujibu wa chanzo cha ndani serikalini, JK hana mpango huo kwa sababu kuu mbili. Kwanza kuvunja baraza la mawaziri ni kumuweka kando waziri mkuu wa sasa, Mizengo Kayanza Peter Pinda na kuteua waziri mkuu mwingine.
Pili, atakuwa  anaongeza mzigo kwa serikali kwa kuwa waziri mkuu akiondoka madarakani huendelea kulindwa na serikali na kupokea stahiki zake mbalimbali.

NI NYERERE
Tangu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ni Baba wa Taifa tu, hayati Mwalimu Julius Nyerere ndiye aliyewahi kuwa na mawaziri wakuu wanne.
Alianza na Rashid Mfaume Kawawa, akafuata Edward Moringe Sokoine, Salim Ahmed Salim (baada ya kifo cha Sokoine) na Cleopa David Msuya.

AWAMU YA MWINYI
Katika awamu ya pili, Rais Ally Hassan Mwinyi, mawaziri wakuu walikuwa Joseph Warioba, John Malecela na David Msuya.
Katika awamu ya tatu ya Rais Benjamin William Mkapa kulikuwa na waziri wakuu mmoja tu, Frederick Tuluwayi Sumaye.

WAZIRI MKUU HADI 2015
Kwa sababu hiyo, chanzo kikasema kuwa Pinda ataendelea ‘kuula’ kwenye nafasi yake ya kuwa waziri mkuu wa Tanzania hadi mwisho wa muhula wa awamu ya nne, mwaka 2015.

WATAENDELEA KUPANGUA
Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo hicho, JK na rais ajaye wataendelea kukumbwa na shinikizo la kupangua baraza la mawaziri kila wakati kutokana na mfumo wa madaraka uliopo sasa.
“Unajua mfumo wa sasa uko hivi; waziri anateuliwa na rais, katibu mkuu wa wizara pia anateuliwa na rais. Katibu mkuu wa wizara ana uwezo wa kumfukuza kazi mkurugenzi wa halmashauri bila waziri kujua, lakini waziri hana uwezo huo.
“Nguvu kubwa ya kazi ipo kwa makatibu wakuu ambao ndiyo watendaji wakubwa wa wizara. Kinachotokea ni kwamba kama wizara itampata waziri mwenye kusimamia sawa majukumu yake kiasi cha kutishia ulaji wa makatibu wakuu, atawekewa zengwe mpaka ang’oke.
“Ndiyo maana utakuta mawaziri kwenye wizara kila siku wanawajibika kisiasa lakini makatibu wakuu wapo tu. Ni mfumo mbaya wa kimadaraka hivyo JK atabadili kila siku, hata rais ajaye naye atakuwa katika harakati hizo,” kilisema chanzo hicho.

MAWAZIRI ZAIDI
Chanzo kikaenda mbele zaidi kwa kunyetisha kwamba, wapo mawaziri ambao wanakalia kuti kavu na huenda wakang’olewa kabisa kutokana na utendaji kazi wao usioridhisha.

SHUKURU KAWAMBWA
Huyu anadaiwa kung’oka wakati wowote kutokana na madai ya walimu.
Chanzo kilisema kuwa Kawambwa pia anaponzwa na mfumo kwani kwa kawaida mwalimu anaajiriwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi lakini usimamizi wake unakuwa chini ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Ikadaiwa kuwa mwalimu anapandishwa cheo na Wizara ya Utumishi, lakini mshahara analipwa na Wizara ya Fedha, Mipango na Uchumi (hazina).
“Sasa mwalimu akipandishwa cheo na utumishi, nyongeza ya mshahara inatakiwa itoke hazina. Hazina nao wanakuwa hawana habari kwa sababu ya mawasiliano duni, matokeo yake mwalimu analia na mwajiri wake ambaye ni Wizara ya Elimu. Hili la walimu litamng’oa Kawamba,” kilisema chanzo.
                       Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, mama Anne Kajumulo Tibaijuka.
ANNA TIBAIJUKA
Chanzo kilidai kwamba Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, mama Anne Kajumulo Tibaijuka naye yupo mguu pande, sawa kwa sababu ya migogoro ya wakulima na wafugaji.
Mfano: “Wakulima wanaopakana na Kiwanda cha Mbolea cha Minjingu, Manyara, wamekuwa wakilalamikia kitendo cha mazao yao kuunguzwa na mbolea hiyo, waziri ameshaambiwa akajibu atafuatilia, sasa atafuatilia mpaka lini?
“Kuna kamati iliundwa kufuatilia suala hili. Pia inadaiwa kuwa vigogo mbalimbali wa serikali wamejimegea maeneo makubwa ya ardhi mkoani Morogoro hivyo kusababisha migogoro isiyoisha kati ya wakulima na wafugaji wanaogombea ardhi kiduchu iliyobaki, huenda ikawa miongoni mwa mambo yatakayomng’oa madarakani Mheshimiwa Tibaijuka,” kilisema chanzo.

CHRISTOPHER CHIZA
Huyu ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika. Wizara yake inakabiliwa na tuhuma ya kuzembea kwenye eneo la mashamba ya mpunga katika Kijiji cha Kapunga, Mbarali, Mbeya.
“Kuna kaburu mwekezaji alinunua shamba hilo lililokuwa la Nafco, hajalilima matokeo yake  analikodisha kwa wanakijiji vipandevipande. Sasa mtu ataitwaje mwekezaji wakati ni mbangaizaji tu, hii ni kashfa, wizara ipo na haisemi lolote.
“Naamini ripoti ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyokuwa ikiongozwa na Profesa Peter Msolwa itaanika madudu yote haya,” kilisema chanzo.

WANAVYOTAKA WANANCHI
Risasi Jumamosi wiki iliyopita liliingia mitaani kusikiliza maoni ya wananchi juu ya watu wanaotakiwa kuwa mawaziri kushika nafasi zilizoachwa wazi.
Katika kila wananchi kumi, nane walitaka mawaziri na wizara zao wawe hivi:
Benard Membe, Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi. Asha-Rose Mtengeti Migiro (Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), Lazaro Samuel Nyalandu (Waziri wa Maliasili na Utalii) na Anne Kilango Malecela (Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi).
Wananchi hao walisema, Harrison George Mwakyembe na John Pombe Magufuli waendelee kwenye wizara zao  kwa vile utendaji kazi wao ni mzuri, hauna shaka huku wakitaka George Huruma Mkuchika awe Waziri wa Ulinzi.

“Ila Amos (Gabriel) Makalla awe waziri kamili wa habari, yule mama (Fenella Mukangala) apelekwe wizara nyingine. Waziri wa Mambo ya Ndani sisi wananchi tunamwona. Halafu yule mama anaitwa Joanista (Joackim) Mhagama aingizwe kwenye Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,” alisema mkazi wa Kijitonyama, Dar aliyejitambulisha kwa jina la Kadoda, fundi wa magari, Bamaga, Mwenge.

ANGALIA FUJO ZA CHADEMA MAHAKAMANI HAPO JANA

Ni January 3 2014 asubuhi ambapo watu mbalimbali wakiwemo Wafuasi na Wanachama wa Chadema walikua wamekusanyika Mahakama kuu kanda ya 88.5 Dar es salaam wakitaka kujua kitakachotokea manake kesi ya Mbunge Zitto Kabwe dhidi ya chama chake cha Chadema ilikua inaendelea.

Muda mfupi kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo, asubuhi kulitokea fujo baada ya jamaa mmoja alieshtukiwa kwamba anarekodi mazungumzo ya moja kati ya vikundi vilivyokua vimesimama kwenye kordo ya Mahakama kuanza kushambuliwa.
Yani ilikua hivi…….. wakati kesi inasubiriwa kuanza kusikilizwa kulikua na makundi mbalimbali ya hawa Wafuasi, wengine upande wa Chadema, wengine upande wa Mbunge Zitto Kabwe ambapo kwenye hivyo vikundi ndio kuna kimoja kikaanzisha vurumai baada kushtukia mchezo.
 Mpaka mwisho, hakikujulikana kilikua kikundi cha upande gani kati ya hizi pande mbili za hii kesi ambayo imeahirishwa mpaka Jumatatu January 6 2014

ZITTO AIBUKA KIDEDEADHIDI YA CHADEMA MAHAKAMANI LEO

 Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe (kulia) akitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam leo, ambapo aliwasilisha ombi la pingamizi la yeye kutojadiliwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinachotarajia kufanyika kesho, hadi rufaa yake ya kupinga kuenguliwa wadhifa huo kwenye Baraza Kuu la chama hicho. Kushoto ni Wakili wa Zitto, Albert Msando. Mahakama Kuu imekubaliana na Zitto Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kinachotarajiwa kufanyika kesho kutomjadili kwa namna yoyote.
Zitto Kabwe akiingia mahakama Kuu Dar es Salaam leo
Wanasheria wa Chadema, Tundu Lisu (kushoto) na Peter Kibatala waliofika kupinga hoja hiyo mahakamani.
Tundu Lisu na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakijadiliana jambo wakati wakisubiri uamuzi wa mahakama
Zitto ana wakili wake Msando wakiwasiliana na marafiki zao walipokuwa wakisubili uamuzi wa mahakama, ambapo Zitto aliibuka dedea kwa pingamizi lake kukubaliwa hivyo kikao cha Kamati Kuu kinachofanyika kesho kukatazwa kumjadili kwa namna yoyote Zitto.

MH ZITTO KABWE ATINGA MAHAKAMANI, ANGALIA HAPA

Mh. Zitto Kabwe atinga Mahakamani asubuhi hii ni Baada ya Jana Kuanza kwa Kuibwaga CHADEMA iliyowakilishwa na Wakili wake Tundu Lissu.Tofauti na Jana Mh.Zitto alifika mahakamani na Usafiri wake,HIi leo Zitto ametinga Mahakamani Kwa Miguu akitokea Kempisck Hotel akiongozana na Mwanasheria Wake Alberto Mhando,Hali ya Mahakama ni Tulivu Kabisa,Watu wamejitokeza kwa Uchache sana,Team Mbowe+Team Slaa na Team ZItto Kwa uchache wao wanabadilishana Mawazo,hakuna mkwaruzo wowote ule hapa Mahakamani.

Picha za ZItto akitinga Mahakamni Ingia hapa






KWA NINI KIPINDI CHOTE CHA UGONJWA WA MAREHEMU MGIMWA SERIKALI ILIFANYA SIRI?

WAKATI taifa likiwa katika msiba kufuatia kifo cha Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi, Dk. William Mgimwa, wananchi wameitaka serikali kueleza kwa nini kwa kipindi chote cha kuumwa kwake, ugonjwa uliomuua ulifanywa siri.
Marehemu Dk. William Mgimwa.
Waziri Mgimwa alifariki dunia Jumatano (juzi) saa 5:20 asubuhi kwa saa za Afrika Kusini (Tanzania saa 6:20) katika Hospitali ya Mediclinic Klooff jijini Johannesburg nchini humo.
Vyanzo mbalimbali kutoka wizara hiyo vinasema, waziri Mgimwa ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la  Kalenga, Iringa, kabla ya kuugua alikuwa na wakati mgumu kiutendaji kutokana na shinikizo mbalimbali alizokuwa akizipata.
“Kuna mambo sana pale wizarani, waziri alikuwa na wakati mgumu sana, haya mambo ndiyo yalimfanya hata akajikuta anapata matatizo na kuugua,” kilisema chanzo hicho ambacho kilikataa kutoa ufafanuzi zaidi wa mambo hayo yaliyomtokea kiongozi huyo.
Ijumaa liliwasiliana na daktari mmoja bingwa wa magonjwa ya binadamu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kuulizwa kama mtu ambaye ana matatizo ya mara kwa mara kazini kwake na kufokewa au kupewa amri anaweza kupata na tatizo gani, akafafanua.
Akifafanua zaidi, daktari huyo kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini alisema upo uwezekano wa marehemu Mgimwa kuwa alipata ugonjwa unaosababishwa na damu kuganda na kuziba kwenye njia ya mishipa.
“Kama mnasema alikuwa akipata shinikizo huko kazini kwake, basi huenda alitokewa na kitu kinachoitwa kitaalam Trans Ischaemic Attack (TIA). Hii ni hali ya damu au mafuta kuganda na kuziba kwenye mishipa, hivyo kusababisha damu kushindwa kutembea kuelekea sehemu mbalimbali kwenye mfumo wa ubongo,” alisema daktari huyo na kuongeza:
“Mara nyingi watu wanaopata tatizo hilo husababishwa na kupewa taarifa za kushtua kama kufokewa au kugombeshwa na kusababisha msongo wa mawazo.”
Akitoa ufafanuzi zaidi, daktari huyo alisema, TIA huweza kumtokea mtu yeyote na kwamba kwa kawaida, hudumu kati ya dakika moja hadi tano na anayekutwa na hali hiyo, kama asipopatiwa tiba mapema, huwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa kupooza (stroke).
“Lakini kama hali hiyo itaendelea kuwepo pasipo damu au mafuta yaliyoganda kuyeyuka, basi mishipa hushindwa kupitisha damu kuelekea sehemu za ubongo na hivyo kusababisha eneo hilo kufa. Kadiri TIA inavyokaa muda mrefu ndivyo madhara yanavyokuwa makubwa ya kuweza kusababisha kupooza au hata kifo,” alisema.
Hata hivyo, wananchi wameishauri serikali kuweka wazi taarifa za maradhi ya viongozi wa ngazi za kitaifa ili kuondoa sintofahamu mitaani.

MAJINA YA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA YAWASILISHWA NA MAKUNDI 50

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
WAKATI leo ndiyo siku ya mwisho Ikulu kupokea mapendekezo ya majina kutoka kwa makundi mbalimbali, tayari makundi yapatayo 50 yamewasilisha mapendekezo ya majina ya watu ambao wangependa wawe wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba.
Makundi hayo ni asasi za kiraia, mashirika yasiyo ya Serikali, vyama vya kitaaluma, madhehebu ya dini na vyama vya siasa ambayo jumla yanafanya idadi hiyo kuwa 50 na inatarajiwa kuongezeka leo kutokana na makundi mengine kuwasilisha majina leo.

Taarifa iliyotolewa juzi Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ilieleza kuwa taasisi hizo zimewasilisha majina yao kwa mujibu wa mwaliko uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete ili kukidhi Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Sheria hiyo sura ya 83 Kifungu cha 22(1) (c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kinataka makundi kupendekeza majina na kuyawasilisha kwa Rais ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kufanya uteuzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba.
Taarifa hiyo ilifafanua, kuwa makundi hayo 50 yaliyowasilisha majina yanayopendekezwa yanatokana na barua 169 zilizopokewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar.
Makundi ambayo yamewasilisha majina kwa mujibu wa taarifa hiyo ni Shirika la Wasaidizi wa Jamii Kabila la Wagogo, Tanzania Association of Social Workers (TASOWA), Jukwaa la Walimu na Wanafunzi Tanzania, Chama cha Walimu Wanawake Tanzania, Umoja wa Wanawake Wajane wa Wilaya ya Karagwe na Kyerwa (UWK).
Mengine ni Tanzania Peace and Development Society, Better World Organization (BWO), Youth Focus and Development, Association of Traditional Medicine Man, Registered Centre for Good Governance and Development in Tanzania, Chama Cha Kijamii (CCK), CHANETA na Muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania.
Makundi mengine ni Legal Aid Iringa Village, Tanzania Kilolo Orphans and Social Development Organization, Legal Aid and Social Welfare Association, Legal and Human Right Centre, Tanzania Lift Initiative NGO, Kilolo Paralegal Unit, Women Development and Social Activities Association, Defence of Human Right/Citizen Rights. Pia kuna makundi ya DAWSEN Trust Fund, Baruti Development Association (BADEA), Living Hope Ministries Trust, EFATHA Ministry, Bethel Assemblies of God Tanzania, Muslim and Christian Brotherhood Society, Baraza Kuu la Waislamu wa Kondoa – Tanzania na Jesus Temple Inner Transformation News.
Zingine ni Jumuiya ya Waithna Asharriyyah Tanzania, Rehmatfi Sabilillah Trust of Tanzania, Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), National Reconstruction Alliance (NRA), Sauti ya Umma (SAU), Chama cha Demokrasia Makini, African Progressive Part – APPT Maendeleo, National League for Democracy, Tanzania Film Federation, Taasisi ya Maendeleo ya Utamaduni, Al-Amoud General Enterprises.
Taarifa hiyo ilitaja makundi mengine kuwa ni Blue Belt and Water Sources Control, Community Development Training Institute – Tengeru, Tanzania Medical Student Association, Tanzania Sea Farmers Union, Medical Association of Tanzania, Chama cha Wastaafu wa Mbinga, Union of Tanzania Press Clubs, Umoja wa Wanawake Tanzania, Alliance for Tanzania Farmers Party na Tanzania Social Economic and Environment and Wellbeing.
Taarifa ya Ikulu ilisema kwa vile mwisho wa kupokea orodha ya majina hayo ni leo, Balozi Sefue alitoa mwito kwa makundi mengine ambayo hayajawasilisha orodha hiyo kufanya hivyo kabla muda uliowekwa kwisha.
Aidha, taarifa hiyo ilitaka makundi hayo kuwa wakati wa kuwasilisha majina hayo ni muhimu kuzingatia vigezo vilivyowekwa na sheria na kama vilivyofafanuliwa kwenye Tangazo la Serikali Namba 443 lililochapishwa Desemba 13, mwaka jana.
Wakati anatoa salamu zake za Mwaka Mpya kwa Taifa juzi, Rais Kikwete alisema mchakato wa kupata wajumbe 201 watakaoungana na wabunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuunda Bunge Maalumu la Katiba umeanza.
Alisema ni matarajio yake kuwa katika wiki ya tatu ya mwezi huu, uteuzi utakamilika. Siku 21 baada ya hapo Bunge la Katiba litaanza. Hii ni kwa nia ya kuwapa nafasi wajumbe hao kusoma Rasimu ya Katiba.
Chadema leo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kitawasilisha mapendekezo yao ya majina leo baada ya kupokea maombi mengi kutoka kanda zote 10 zinazohusisha mikoa, wilaya na majimbo.

Taarifa ya chama hicho iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano, John Mnyika ilieleza kuwa baada ya Ikulu kutoa tangazo la kutaka makundi kuwasilisha majina hayo, chama hicho kilitoa mwito kwa wanachama wake ambao wangependa kuteuliwa kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba kuwakilisha CHADEMA, watume maombi makao makuu ya chama na katika ngazi nyingine husika.

HABARI KUMI KALI ZA KISIASA ZILIZOBAMBA MWAKA 2013

Leo tunaanza mwaka mpya, huku tukiwa na kumbukumbu ya mambo yaliyotikisa anga za siasa hapa nchini katika mwaka 2013 kama yafuatayo:
1. Rasimu mbili za Katiba
Miongoni mwa matukio makubwa kwa mwaka uliopita ni kuzinduliwa kwa Rasimu mbili za Katiba. Ya kwanza ikiwekwa hadharani Juni 3, 2013 na ya pili juzi Desemba 30, 2013.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba alikabidhi rasimu hizo kwa Serikali kuamsha mjadala kuhusu mwelekeo wa nchi, baada ya rasimu hizo kubainisha uwezekano wa kutokea mabadiliko makubwa katika mfumo wa uongozi wa nchi.
Mambo makuu yaliyoibua mjadala mzito ni suala zima la kuwapo kwa serikali tatu – ya Muungano (shirikisho), Tanzania bara na Zanzibar.
2. Mawaziri wanne wang’olewa
Tukio kubwa la kufungia mwaka limetokea Desemba 20 baada ya mawaziri wanne kufutwa kazi baada ya ripoti ya madhila yaliyotokana na Operesheni Tokomeza Ujangili kuwasilishwa bungeni.
Mawaziri hao ni Balozi Khamis Kagasheki aliyekuwa Maliasili na Utalii, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo.
Kinachosubiriwa sasa ni Rais Kikwete kufanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri.

3. Kifo cha Nelson Mandela
Pengine tukio ambalo halijasahaulika vichwani ni kicho cha Nelson Mandela, aliyekuwa rais wa kwanza mzalengo wa Afrika Kusini hapo Desemba 5, 2013.
Kutokana na msiba huo wa dunia, viongozi zaidi ya 100 wakiwamo wakuu wa nchi na Serikali walishiriki hatua mbalimbali za safari ya mwisho ya mzee huyo maarufu kama Madiba.
Mandela alizikwa Jumapili, Desemba 15, 2013 katika Kijiji cha Qunu alikokulia, mazishi ambayo Rais Jakaya Kikwete alipata fursa ya kuhutubia na kueleza nafasi ya Tanzania ilivyoshiriki katika harakati za ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika.
4. Kikwete ahutubia Bunge
Mwezi Novemba Rais Jakaya Kikwete alihutubia Bunge lengo kubwa likiwa ni kufafanua kuhusu kuzorota kwa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC). Pia aligusia ushindi wa majeshi ya Umoja wa Mataifa yakijumuisha askari kutoka Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo), Katiba Mpya, na Operesheni Tokomeza Ujangili ambayo baadaye imekuja kusababisha mawaziri wake wane wafukuzwe kazi.
5. Chadema uamuzi mgumu
Vilevile Novemba 22, Chadema kilimvua madaraka yote Zitto Kabwe aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mjumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu kwa maelezo kuwa anakwenda kinyume na taratibu za chama hicho.
Pamoja na Zitto wengine waliovuliwa nyadhifa zao ni Samson Mwigamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu, Dk Kitila Mkumbo.
Viongozi hao wamepinga uamuzi huo wa Kamati Kuu na kukata rufaa kwenye vikao vya juu, uamuzi unayotarajiwa kutoka mapema mwezi huu.
6. Malumbano, matusi bungeni
Mwaka uliopita Bunge lilitawaliwa na matukio makubwa na mijadala mizito iliyoibua hisia kali, malumbano na wakati mwingine matusi yaliyowaacha wananchi midomo wazi.
Mojawapo ya mijadala hiyo ni ule wa Aprili 15, ambapo Ezekiel Wenje (Nyamagana) alitoa kauli za kukituhumu chama cha CUF kuwa na uhusiano na vyama vya kiliberali vinavyosapoti ushoga, hali iliyoibua majibu mazito kutoka kwa wabunge wa CUF kwamba Chadema “ni wehu, wahuni, wazushi na wameidhalilisha CUF”.
Katika hatua nyingine wabunge wakichangia hotuba ya Waziri Mkuu, Mbunge wa Kondoa Kusini (CCM), Juma Nkamia alijibizana na Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini-Chadema), alisema kuwa yeye “haongei na mbwa bali mwenye mbwa.” Naye Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde alitoa kauli ya iliyotafsiriwa kuwa ya kuudhi kuwa kuna “wabunge bungeni wenye mimba zisizitarajiwa.” Kauli nyingine iliyochoma masikio ya wabunge na wananchi ilikuwa ya Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini- Chadema) ya “akili ndogo kutawala akili kubwa” na wakati mwingine kutumia kifungu cha Biblia katika Kitabu cha Mithali 27:22, kinachosema kuwa; ‘Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu pamoja na ngano, upumbavu wake hautamtoka.
7. Makonde bungeni
Ukiacha zile kauli zilizolalamikiwa kuwa ni za kuudhi, mwaka 2013 ilifika wakati Bunge likawa kama sinema wakati maofisa usalama walipolazimika kumbeba mzobemzobe Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu).
Katika tukio hilo, ambalo maofisa usalama walitakiwa kumtoa nje Kiongozi wa Kambi Rasimu ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe huku wabunge wa kambi hiyo wakipinga kutolewa nje. Ilidaiwa kuwa Sugu alimrushia ngumi mmoja wa askari.
8. Lema ashinda rufaa ya ubunge
Mwezi Aprili 2013 Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema aliyekuwa nje ya Bunge baada ya ubunge wake kutenguliwa na Mahakama Kuu alishinda rufani baada ya Mahakama ya Rufaa kutupilia mbali maombi ya marejeo na kuamua arudi bungeni.
Maombi ya marejeo yalikuwa yamewasilishwa mahakamani hapo na makada watatu wa CCM mkoani Arusha, kupitia kwa mawakili wao Alute Mughway na Modest Akida wakiiomba Mahakama ya Rufani ifanye marejeo ya hukumu yake hiyo kwa madai kuwa hukumu ya Mahakama ya Rufaa iliyomrejeshea ubunge wake haikuwa sahihi.
9. Kicheko Aeshi Hilary
Furaha ya kurudi bungeni haikuishia kwa Lema, Mei 6, kicheko kilihamia kwa Aeshy Hilary baada ya Mahakama ya Rufani, kumthibitisha kuwa ni mbunge halali wa Sumbawanga Mjini baada ya kushinda rufaa aliyokata kupinga hukumu ya Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga, iliyomvua ubunge.
Hilaly alivuliwa ubunge na aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Bethuel Mmila Aprili 30, 2012, kutokana na kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 kupitia Chadema, Nobert Yamsebo.
10. Dk Kafumu kidedea Igunga
Ilipotimu Mei 9, msimu wa furaha ukahamia Igunga pale Dk Dalali Kafumu wa CCM, ambaye ushindi wake uliokuwa umebatilishwa na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, alirejeshewa ubunge wake na Mahakama ya Rufaa.
Dk Kafumu katika uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi iliyoachwa na Rostam Aziz aliyejiuzulu, alimshinda Joseph Kashindye wa Chadema. Kashindye alipinga ushindi huo kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi na ubunge huo kutenguliwa.
Sakata la gesi Mtwara
Ingawa suala hili lilianza katika mwaka uliotangulia wa 2012, mwaka 2013 umeshuhudia maandamano makubwa, hasira za baadhi ya wananchi waliojichukulia hatua mkononi na kuchoma majengo na magari, pia hatua za Serikali katika kutuliza vurugu hizo za kupinga gesi kusafirishwa kwa bomba kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Hali hiyo ilitulizwa na sasa ujenzi wa bomba unaendelea na hivyo kuweka matumaini kuwa ugunduzi wa gesi nyingi hapa nchini unaweza sasa kuwa wa manufaa badala ya kuwa mkosi kama ambavyo ilikuwa imeanza kuonekana.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger