Search in This Blog

Showing posts with label BATULI. Show all posts
Showing posts with label BATULI. Show all posts

ATULI AWACHANA LIVE MASTAA WANAOFUTURISHA MATAJIRI.

Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ ametamka kuwa hakubaliani kabisa na wale mastaa wenye tabia za kufuturisha watu wenye uwezo mkubwa kiuchumi.
Akizungumza na paparazi wetu, Batuli alisema anaamini kwamba twawabu nzuri zinapatikana kwa kufuturisha watu wenye mahitaji kama watoto yatima na ndiyo maana yeye amejiandaa kuwafuturisha. 

“Wasanii tubadilike, tuwafuturishe watu wenye mahitaji ili kuwafanya na wao wafurahi, banafsi nitafanya hivyo mwezi huu, nitafuturu na wasiojiweza,” alisema Batuli.

BATULI AWAPONDAWAIGIZAJI NA MASHABIKI WANAO POST MATUSI MITANDAONI

Mwigizaji Yobnesh Yussuph maarufu kama batuli ameamua kuwatolea uvivu waigizaji wanaoandika matusi kwenye mitandao na kuwaambia kuwa badala ya wao kupoteza muda huo kutukana matusi makali kwenye mtandao wangetumia muda huo kufanya Ibada ili wakifa waende peponi kwa Amani ambako wangeweza kupajaza mpaka wengine wakose viti.
“…Ule muda watu wanaoutumia kuandika naneno makali (MATUSI) kwenye instagram (Mtandao wa kijamii) wangekuwa wanautumia kwa ibada peponi kungejaa..” Alisema batuli.
Huku ikiwa bado haijajulikana anamlenga nani moja kwa moja na ujumbe huo baadhi ya wachunguzi wa mambo wamehusisha kauli hiyo na kitendo kilichotokea juzi cha mwanadada wa bongomovies kuporomosha matusi makali sana kwenye mtandao huo maarufu wa kijamii nchini.

BATULI ATUPA DONGO AKINA MASOGANGE NA WENZAKE


STAA mwenye sura ya mauzo kunako anga la Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amewatupia dongo wadada waliokuwa na mtindo wa kusafirisafiri nje ya nchi na kuwachana kuwa sasa hivi wamebuma kutokana na msako mkali wa serikali.
Yobnesh Yusuf ‘Batuli’.
Batuli alifunguka hayo mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter, ambapo alitumia lugha tata kuwatupia dongo wadada wa mjini ambao walikuwa hawashikiki kwa safari na kutanua kwenye kumbi mbalimbali za starehe.
“Eti wale wadada wanaojirusha kila siku, siku hizi mbona siwaoni? Na wale waliokuwa wanasafiri kila siku nao wamepotea, ha ha haaa Sembee lol,” aliandika Batuli.


CREDIT: GPL
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger