Search in This Blog

Showing posts with label DIAMOND. Show all posts
Showing posts with label DIAMOND. Show all posts

LAANA HIYOO YAMNYEMELEA DIAMOND

Oooh! Nooh! Wakati akimpa mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ gari la Sh. milioni 38 huku akitawanya mamilioni ya fedha kwenye matukio mbalimbali, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anadaiwa kunyemelewa na laana kufuatia baba yake, Abdul Jumaa kuugua na kuvimba miguu bila msaada wowote.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akila ujana na mpenzi wake Wema Sepetu.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa, baba wa staa huyo anayeishi Magomeni-Kagera jijini Dar, amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu na hakuna msaada wowote anaoupata kwani chanzo cha mapato anachokitegemea ni kodi tu ya nyumba ambayo anaipata kutoka kwa wapangaji wachache alionao.
BOFYA HAPA KUKISIKIA CHANZO
“Yaani tunashangaa kusikia Diamond ana fedha nyingi, juzikati tuliona katika gazeti kamnunulia mama yake gari la milioni 38 (Toyota Lexus-Harrier) sasa kwa nini asimthamini baba yake hata kidogo?
“Ukweli ni kwamba baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba.

“Amekuwa akilalamika mara kwa mara lakini Diamond hatujawahi kumuona,” kilinyetisha chanzo hicho na kuongeza:“Juzikati hapa baba Diamond alishikika kwelikweli miguu, akaugulia mwenyewe ndani pasipo kuwa na msaada wowote tena nasikia mzee huyo hataki hata kuongelea lolote kuhusu Diamond maana haoni umuhimu wa kufanya hivyo wakati amemsusa muda mrefu sana.”
MATIBABU HAYAZIDI MILIONI
Katika aya nyingine, chanzo hicho kilidai kwamba ugonjwa wa miguu ambao unamsumbua mzazi huyo, gharama za matibabu haziwezi kufikia hata shilingi milioni moja za madafu achilia mbali mamilioni anayoyatapanya staa huyo.

Mama yake Diamond,Sanura Kassim ‘Sandra’ akilitesti gari alilokabiziwa na Mwanaye kama zawadi.
“Ingekuwa tatizo kubwa sana, hapo sawa, kwa sababu miguu huwa inamvimba lakini akipata dawa za kutumia huwa inarudi katika hali ya kawaida, kwa nini lakini anamfanyia hivyo baba yake? Amemkosea nini?” Kilihoji chanzo hicho.
UTAJIRI WAKE WAANIKWA
Wakati chanzo hicho kikiweka nukta hapo kwa muda, mapaparazi wetu walipewa malalamiko mengine kutoka kwa jirani mmoja wa baba Diamond ambaye alimsihi amsaidie mzazi wake kwani anaamini uwezo anao kupitia kumbukumbu ambazo Diamond mwenyewe alizithibitisha kupitia vipindi mbalimbali vya runingani kama Take One na Spora Show vya CloudsTV.

Pia kwenye vyombo vingine vya habari zikiwemo redio na magazeti pendwa ya Global Publishers.
Jirani huyo alidai kwamba mwaka jana Diamond alitangaza kuwa ana utajiri wa Sh. bilioni moja ikiaminika kwamba mwaka huu umeongezeka mara dufu.

“Nakumbuka mwaka jana kupitia Kipindi cha Spora Show na kile cha Take One, Diamond alikiri kuwa ana mkwanja usiopungua bilioni moja, hiyo ilikuwa kwa mwaka jana, sasa mwaka huu unadhani atakuwa na shilingi ngapi? Aache hizo bwana, amsaidie baba yake hata kwa kumpa mtaji mdogo wa biashara ambao unaweza kumsaidia,” alisema jirani huyo.
MATANUZI  YA DIAMOND, WEMA
Katika kuendelea kuichimba habari hiyo, mapaparazi wetu walinasa malalamiko kutoka kwa jirani mwingine wa mzazi huyo ambaye alieleza masikitiko yake kwa kulinganisha starehe ambazo staa huyo anazifanya na asali wake wa moyo, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na maisha halisi ya baba yake.

“Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa habari za mastaa, naona kila siku kwenye vyombo vya habari jinsi gani Wema na Diamond wanavyotumia fedha nyingi katika masuala ambayo hayana ulazima kiivyo.
“Sisi kama majirani hatupendezwi na hali hii, angekuwa anakuja angalau siku mojamoja kumuona baba yake kuliko kila siku kumhudumia mama yake pekee,” alisema jirani huyo.

Baba yake Diamond, Abdul Jumaa akitafakari jambo.
TATIZO NI NINI?
Mapaparazi wetu waliingia mzigoni kusaka kiini halisi kwa nini Diamond amwage fedha nyingi kwa mama yake pasipo kumkumbuka japo kiduchu baba yake ambapo ilielezwa kuwa staa huyo wa Mdogomdogo hakuwa na ugomvi wowote na mzazi wake huyo.

“Kama ni ugomvi ulikuwepo kati ya mama na baba lakini Diamond hahusiki, tunashangaa kuona kama staa huyo naye anaweza kumsusia baba yake,” kilieleza chanzo na kuongeza:
“Mbaya zaidi nasikia Diamond amekuwa mzito kupokea simu za baba yake, sasa huoni kama siyo jambo la busara, mzazi ni mzazi tu hata iweje. Kwa mtazamo wangu kinachofuata ni laana.
“Kuna mifano ya watu wengi ambao waliingia kwenye laana za wazazi wao na wakajikuta kama siyo kufulia kama (wanatajwa mastaa waliofulia wa muziki Bongo) au hata kukutwa na umauti.
“Jambo hili si la kibinadamu tu, kwa wale wanaosoma vitabu vitakatifu watakuwa na mifano mingi ya watu waliowakosea wazazi wao wakalaaniwa.”

BABA DIAMOND ANASIKITISHA
Ijumaa lilipomtafuta baba Diamond kwa njia ya simu aliongea maneno ya kusikitisha huku akikataa katakata kumzungumzia kijana wake huyo.

“Jamani naomba mumuache Diamond na maisha yake, sitaki kabisa kusikia habari zake maana hata nikiongea naonekana najipendekeza kwake.
“Namshukuru Mungu, kama ni kuumwa kwa sasa naendelea vizuri na maisha yangu, niacheni nipumzike,” alisema mzee huyo kwa unyonge.
DIAMOND ANASEMAJE?
Alipotafutwa Diamond ili kumsikia anazungumziaje madai hayo, simu yake iliita bila kupokelewa. Tunaamini atasoma habari hii hivyo si vibaya akatutafuta ili afunguke kwa upande wake.

MAONI YA MHARIRI
Diamond ni staa mkubwa kwa sasa ndani na nje ya Bongo, uwezo alionao kifedha unapaswa kuendana na baraka za wazazi wa pande zote mbili. Vitabu vya Mungu vinatufundisha kwamba wazazi ndiyo Miungu wetu hapa duniani hivyo hata kama kuna kosa amefanya, mzazi atabaki kuwa mzazi tu. Hatutakiwi kumkosoa!

HIVI NDIVYO WEMA NA DIAMOND WALIVYOKUTANA SIKU YA KWANZA

Screen Shot 2014-03-28 at 1.52.37 AM

Screen Shot 2014-03-28 at 4.07.47 AMInaaminika katika mapenzi au uhusiano wa kimapenzi uliowahi kuandikwa sana kwenye mitandao na magazeti Tanzania, huu wa mwigizaji Wema Sepetu na Diamond Platnumz umevunja rekodi, mastaa ambao walifikia mpaka kuvalishana pete ya uchumba.

Pamoja na yote waliyopitia bado kalamu za Waandishi mbalimbali zilihusika kuwaandika.
Ommy Dimpoz ambae ni rafiki wa Diamond kitambo hata kabla hatawa staa (Ommy) ameshea hii picha inayowaonyesha Wema na Diamond walipokutana kwa mara ya kwanza na kuiambatanisha na hii caption hapa chini.
Screen Shot 2014-03-28 at 1.52.48 AM

HII NDIO HEKAHEKA INAYOMHUSU MAMA WA DIAMOND PLATNUMZ

mama diamondMama yake Diamond Platnumz leo July 11 alikua kwenye kipindi cha Leo Tena kutoka Clouds Fm na alipata nafasi ya kutoa Hekaheka yake ambayo inahusu maisha yake pamoja na Diamond Platnumz kwenye malezi yake mpaka hapo alipo Diamond kwa sasa. dmn

DIAMOND NI MWIZI, KANIIBIA WIMBO WANGU, HAYA NI MAENO YA WABABA

 Malalamiko ya wasanii kuibiana au kupigana kanzu kwenye kazi zao yaliripotiwa sana mwaka jana na mwaka huu mambo yalikuwa shwari, lakini baada ya kuvuka nusu ya mwaka yameibuka tena.
Mshiriki wa shindano la kuimba la Bongo Star Search (BSS) , Wababa amewatuhumu maswaiba wa ‘Muziki Gani’ Nay wa Mitego na Diamond Platinumz kwa kumuibia kazi zake kwa wakati tofauti. 

Akiongea kupitia Friday Night Live ya East Africa TV, Wababa amesema Diamond amemuibia wimbo wake ambao alikua anaiita ‘Kitorondo’ na kwamba aliibadilisha jina baadae.
Kiukweli kuhusu Diamond, mimi mwenyewe nimetumiwa hiyo ngoma ambayo ameitoa, nimeiskiliza jinsi ilivyo kuanzia idea, mwendo, style ambazo anafanya. Ambayo ameibadilisha jina tu baada ya ya kwamba ilikuwa mitandaoni nilikuwa nimemfatilia ilikuwa inaitwa Kitorondo mwezi mmoja kama uliopita. Kwa hiyo nilishindwa kulalamika kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa analalamika kuwa imevuja. Kwa hiyo sikuona sababu ya kuongea kitu kwa sababu haikuwa official. Kwa hiyo sikuwa na sababu ya kucomplaini kwa sababu haikuwa official, lakini mpaka jana ina maana ilikuwa serious kama biashara.” Ameeleza Wababa.
                                                                        Wababa 
 Alipoulizwa ni wapi ambapo Diamond aliusikia wimbo huo, amesema huo ni wimbo wake alioutoa miaka minne iliyopita akiwa na Dogo Asley na aliuweka kwenye mtandao wakati anatumia jina la Nurdi, kabla hajaanza kutumia jina la Wababa aliposhiriki BSS. “Ni nyimbo ambayo iko mtaani na watu wengi wanaielewa. Kwa hiyo sijaelewa..” Kwa upande mwingine, Wababa amedai kuwa alifanya kazi na Nay wa Mitego katika studio za Mazoo lakini baaadae Nay alirudi studio na kuongea na Mazoo kutaka kuunua wimbo huo kwa shilingi milioni  moja bila kumshirikisha Wababa.
Hivi karibuni nimefanya ngoma mpya na Nay wa Mitego, ni ngoma ambayo ilikuwa iko paid kwake pamoja na studio. Lakini kitu cha kushangaza ni kwamba siku mbili baada ya kufanya kazi nikapigiwa simu na producer akaniambia kwamba jamaa amerudi tena kwa ajili ya kutaka kununua wimbo kwa milioni moja, auchukue wimbo aende akaufanye sehemu nyingine. Baada ya hapo hata mahusiano yangu na mshikaji yamekuwa sio mazuri. Ukimpigia simu anakwambia yuko busy kuna kazi anafanya atanicheki, hadi kufikia leo sielewi.”
Nay alipigiwa simu lakini hakuwa anapatikana kwa muda huo.

SIRI YAFICHUKA, WEMA NA DIAMONDA SASA NI ......

http://photos-g.ak.instagram.com/hphotos-ak-xpa1/927739_312353152262798_239351557_n.jpg

IN THE NAME OF #INSTAGRAM
 ONE OF WEMA'S FAN COME WITH A DOUBT CONCERNING A RING WHICH SEEMED ON THE WEMA'S COURT FINGER SO THE QUESTION COMES DOES WEMA SEPETU TAKE IT FOR DECORATION OR NEAR TO MARRIAGE??

POWER TO YOU!!

ONE OF WEMA'S FAN COME WITH A DOUBT CONCERNING A RING WHICH SEEMED ON THE WEMA'S COURT FINGER SO THE QUESTION COMES DOES WEMA SEPETU TAKE IT FOR DECORATION OR NEAR TO MARRIAGE?? POWER TO YOU!!

POMBE YATIBUA FUTARI NYUMBANI KWA DIAMOND

NIkama jina la wimbo wake mpya wa Mdogo Mdogo ambao ndani yake kuna kikorombwezo ‘mwendawazimu kaingiaje’, ndiyo hali iliyotokea kwenye futari ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alipofuturisha nyumbani kwake ambapo pombe zilitibua shughuli nzima.
Wema akifungua shampeini.
Pamoja na kufuturisha, pia Diamond alimwandalia pati mama yake mzazi, Sanura Kassim a.k.a Sandra aliyekuwa akisheherekea siku yake ya kuzaliwa.
WAALIKWA WATAZAMANA
Katika tukio hilo lililojiri nyumbani kwa staa huyo maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar mapema wiki hii, wageni waalikwa walijikuta wakitazamana na kuhoji uhalali wa chupa za pombe kuwepo ndani katika sehemu ambayo walitakiwa kufanyia dua.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mbele ya wanahabari wetu, baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo maustadhi walioshangazwa na jambo hilo, walihoji kuwa kulikuwa na ulazima gani au kilishindikana nini wahusika kuziondoa pombe hizo halafu wazirudishe baadaye.
Pombe zilizonaswa.
“Unajua huu ni mwezi wa imani zaidi, sasa linapotokea suala la ibada kama hili la kufuturisha basi kuna vitu vingine unatakiwa uvifiche ikiwezekana uachane navyo kabisa.
“Sioni sababu ya zile pombe kuachwa pale sebuleni kila aliyeingia ndani kula keki anakutana nazo uso kwa uso,” alisikika akilalama mmoja wa waumini wa Dini ya Kiislamu walioalikwa.

POMBE ZAONDOLEWA
Hata hivyo, pombe hizo kali ziliondolewa mahali hapo mara moja kisha shughuli ikaendelea.

SHAMPEINI YA WEMA YATILIWA SHAKA
Katika kuendelea kuweka walakini, muumini mwingine alikwenda mbali zaidi na kuitilia shaka shampeini iliyofunguliwa kuwa ni nani aliichunguza kama ilikuwa na kilevi au la!.

Maustadhi wakielekea kwenye futari.
“Wakati shampeini inaletwa niliona, aliileta kijana mmoja namjua kwa jina la James ambaye ndiye aliyempatia Babu Tale (meneja wa Diamond), naye akampatia Wema Sepetu (laazizi wa Diamond).
“Sidhani kama walikuwa na muda wa kusoma kama ina kilevi au la ndiyo maana baada ya Wema kuifungua watu waliikataa wakidhani ina kilevi hivyo ikamdodea mrembo huyo kwani ilidaiwa kama ilikuwa na kilevi ni jambo baya kwa mwezi mtukufu.
WAINYWA WATATU
“Walioinywa ni watatu tu, Wema, mama Diamond na dada yake Diamond, Esma Platnumz,” alisema mmoja wa waumini hao akitoa hoja juu ya kuitilia shaka shampeini hiyo ambayo waandishi wetu hawakupata nafasi ya kusoma maelezo yake.

Wageni waalikwa wakipata futari.
MSIKIE BABU TALE
Baada ya kupata maelezo hayo, Ijumaa lilijaribu kuhoji kwa wahusika ambapo Meneja wa Diamond, Babu Tale alisema kuwa licha ya kutokaguliwa kwa Shampeini lakini haikuwa na kilevi.
“Shampeini haikuwa na kilevi, lakini kuhusu suala la chupa za pombe pale sebuleni, ule ulikuwa ni urembo tu ambao upo siku zote.

“Hata mama Diamond akitaka kuswali huwa anasogeza meza na kufanya ibada yake ya swala, zile chupa zinakuwa zipo palepale ila kwa Wabongo siku zote wapo kwa ajili ya kuwakatisha watu tamaa tu.“Zile chupa huwa zipo kila siku zimekaa tu kama nilivyosema kuwa ni urembo,” alisema Babu Tale.Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
DIAMOND HAKUWEPO
Katika shughuli hiyo, pamoja na kwamba alikuwa nchini Marekani, Diamond alimzawadia mama yake gari aina ya Toyota Lexus Harrier lililogharimu Sh. milioni 38.1 alilokabidhiwa na Babu Tale.

HIZI NDIO PICHA ZAIDI YA 40 ZINZOONYESHA JINSI DIAMOND PLATINUM ALIPOPOKELEWA UWANJA WA TAIFA, NI SHIDAA

57mond Diamond Platnumz ameingia Dar es salaam usiku wa July 10 mashabiki wengi wakiongozwa na mama yake,dada yake pamoja na mpenzi wake Wema Sepetu ni miongoni mwa watu waliojitokeza kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere Internation Airpot.

Hizi ni baadhi ya picha za mapokezi ya Diamond Platnumz.
68mond
67mond
66mond
65mond
64mond
63mond
53mond
54mond
55mond
62mond
50mond
49mond
41mond
42mond



43mond
44mond
45mond
40mond
39mond
37mond
36mond
34mond
28mond
29mond
30mond
31mond
32mond
27mond
26mond
24mond
21mond
20mond
14mond
15mond
16mond
17mond
18mond
19mond
6mond
7mond
11mond
13mond
5mond
2mond
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger