Search in This Blog

Showing posts with label MONALISA. Show all posts
Showing posts with label MONALISA. Show all posts

MONALISA ADAI KUPORWA BWANA


MSANII mkongwe kunako gemu la filamu Bongo, Yvonne Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’ amedaiwa kunyang’anywa bwana na shosti wake aliyejulikana kwa jina moja la Doro.


Yvonne Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Monalisa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume anayefahamika kwa jina la Yusuph ambapo miezi kadhaa iliyopita alifanya sherehe ya kuzindua nyumba yake, Kimara jijini Dar lakini Monalisa hakuhudhuria kutokana na mgogoro uliokuwepo kati yao.
Inadaiwa kuwa katika sherehe hiyo, Doro ndiye aliyefungua shampeni. Ikazidi kudaiwa kuwa kuanzia siku hiyo, wawili hao wakawa wapenzi huku Yusuph akionesha mabadiliko makubwa kwa Monalisa. Baadaye aliupata ukweli kwamba wawili hao ni wapenzi.
Chanzo hicho kilisema, Monalisa baada ya kuupata ukweli, aliamua kuachana na Yusuph ili aendelee na Doro.
Waandishi wetu walipomtafuta Monalisa, alikuwa na haya ya kusema: “Wale ni rafiki zangu kama wanapendana sijui, kwanza sipendi kuwaongelea.”
Naye Yusuph alipotafutwa  alisema: “Kweli Monalisa ni mtu wangu wa muda mrefu lakini tuligombana kidogo baada ya kupewa maneno ya uongo.” Akafafanua kuwa chanzo cha madai hayo ni baada ya watu kumuona Doro akifungua shampeni kwenye uzinduzi wa nyumba yake.
Doro alipopatikana alisema kuwa Monalisa ni rafiki yake wa muda mrefu na hawezi kugombana naye kwa sababu ya mwanaume.

"SIPO TAYARI KUOLEWA TENA NA KUACHIKA" MONALISA

Msanii mkongwe  kwenye  soko  la  filamu  Tanzania,Yvonne Cherry "Monalisa"  amesema  hatarajii  kuolewa  tena  baada  ya  kuvunjika  kwa  ndoa  zake  kadhaa  ikiwemo  ile  ya  producer  Tyson....

Akisimulia  mikasa  ya  maisha  yake  mbele  ya   mwandishi  wetu,Monalisa  aliema  kuna  siku  walipokuwa  kwenye  kikao  cha  sendoff  ya  mama  yake, alitania  na  kusema  ataolewa  disemba  lakini  hakuwa  serious....

"Sina  mpango  wa  kuolewa  kabisa,kwanza  sina  mchumba, ntaolewaje?

"Siku  ile  nilikuwa  natania  tu kwa  sababu  sipo  tayari  kuolewa  na  kuachika  tena"..Alisema  Monalisa
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger