Showing posts with label NAY WA MITEGO. Show all posts
Showing posts with label NAY WA MITEGO. Show all posts
NEY WA MITEGO APATA PIGO LA MWAKA MPYA, ATEMWA NA MPENZI WAKE
UCHUMBA wa staa wa wimbo wa Muziki Gani, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mpenzi wake anayefahamika kwa jina moja la Siwema umedaiwa kuvunjika.
Kwa mujibu wa chanzo makini, chanzo cha kumwagana ni baada ya Siwema kukuta meseji za watoto wa kike tofauti katika simu ya Nay wa Mitego katika nyakati tofauti.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa, wawili hao walimwagana tangu Januari 2, mwaka huu, nyumbani kwa Nay wa Mitego, Manzese jijini Dar es Salaam baada ya Siwema kujiridhisha kuwa mpenzi wake huyo anamsaliti kutokana na ushahidi wa meseji alizozifuma.
Hata hivyo, chanzo kilizidi kumwaga ‘ubuyu’ kuwa, wapendanao hao wamekuwa wakizinguana mara kwa mara na kilichomuuma zaidi Siwema ni baada ya mkali huyo kuachia video yake mpya ya Nakula Ujana ambayo ameonekana katika pozi za kimahaba na warembo kibao.
“Imemuuma sana video ya Nakula Ujana, warembo wale inasemekana hakuishia katika video, sasa aliendelea kuwasiliana nao na Siwema akagundua ndipo mtiti ulipoibuka, Siwema akarudi kwao Mwanza,” kilisema chanzo.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Siwema ambaye alikiri kugombana na Nay na kusema ameshindwa kuvumilia na ameona ili kujiepusha na presha zisizo za lazima arudi kwao Mwanza.
“Kweli tuna ugomvi na Nay na haswa kuna mambo yananikera sana ila kubwa zaidi kwa sasa ni ile video yake mpya kuna parties mle sijazipenda...mchumba wa mtu ufanye video ujiachie vile, unashikwa shikwa ovyo,” alisema Siwema.
Alipotafutwa Nay, alikiri kutokea kwa ugomvi huo na kudai yupo katika jitihada ya kumaliza tofauti hizo kwa kuzungumza na Siwema.
NEY WA MITEGO AFANYIKA KITU MBAYA NA WAJANJA WA MJINI
Msanii wa Hip Hop, Nay Wa Mitego usiku
wa kuamkia leo ameibiwa vifaa vya gari lake aina ya Toyota Verossa lenye
namba T 418 CGK vyenye thamani ya shilingi milioni 4 lililokuwa
limeegeshwa nyumbani kwake.
Nay ameiambia alifunguka kuwa jana
aliliacha salama wakati anaenda kulala lakini alivyoamka leo
asubuhi,akakuta limenyofolewa baadhi ya vifaa. Hizi ni picha za gari la
Nay baada ya kuporwa baadhi ya vifaa vyake.
NAY WA MITEGO ARUDI BONGO KWA NAULI YAKE, HII NI TUZO ZA NZUMARI ZA KENYA ZASHINDWA KUFANYIKA DAKIKA YA MWISHO,
Mwandaaji wa tuzo za Nzumari za Mombasa, Eve ‘Queen’ Adhiambo amelazimika kuziahirisha tuzo za mwaka huu katika dakika za mwisho kutokana na mahudhurio hafifu na maandalizi ya zimamoto.
Eve
Hadi saa nne usiku, sound system na jukwaa vilikuwa havijawekwa na watu wachache waliokuwa wamehudhuria walilazimika kurudi makwao baada ya kuzuiwa kuingia ndani ya ukumbi sababu mambo yalikuwa hayajakaa sawa. Eve ambaye alionekana kupagawa wazi alisema kuwa watu waliokuwa wameenda walidanganya na watu wachache getini kwamba show hiyo ilikuwa imeahirishwa.
“Unajua kulikuwa na watu kwenye geti waliokuwa wakiwahadaa watu waliokuwa wamekuja kwa kuwaambia kuwa tukio lilikuwa limeahirishwa, hizi ni tetesi kubwa na nahisi iliwafikia hata wale waliokuwa wamepanga kuja,” Eve aliiambia website ya ommydallah.com.
“Ntalazimika sasa kusitisha tukio hili mpaka ntakapotangaza tena kwakuwa bado nahitaji kuwatuza washindi,” aliongeza.
Eve aliwalaumu pia wafundi wa sauti aliowapa kazi kuishughulikia na kusema kuwa walichelewa kwenda.Hata hivyo mmoja wa mafundi hao aliiambia tovuti ya . Ommydallah kuwa ni Eve ndiye alichelewa kuwataarifu.
“Huyu demu sisi mwanzo alitufuata jana (Friday) akitaka sound then sasa leo ndio akaja vizuri tena saa tisa na sisi mdosi akatutuma kazi na tukaja, lakini nadhani shida ilikuwa ni mambo na pesa maana watu wengi hapa wanaogopa kufanya kazi na huyu dem,” alisema.
Eve alikanusha madai hayo na kusema kuwa kilichotokea ni hujuma. “Unajua sipendi kumtukuza shetani na nikisema kuwa kuna mkono wa mtu nitakuwa namtukuza ila ningependa kusema kuwa usishangilie wakati mwenzako amepatakina na shida kama hii maana kesho inaweza kuwa wewe,” alisema..(usisahau kulike page yetu ya mdadisi mambo blog, bofya hapa) Rapper Nay wa Mitego aliyekuwa ameenda Mombasa kuhudhuria show hiyo alilazimika kulipia mwenyewe gharama za malazi na tiketi ya ndege kurejea Dar kwakuwa mwandaaji hakuweza kuingiza fedha za kuweza kulipa gharama hizo.
“Unajua kaka me nimetoka Nairobi kushoot clip na nikaunganisha direct na hapa but mambo ni kama unavyoyaona, cha msingi nilichokua nataka kutoka kwao ni wanipe ticket yangu ya ndege tu ya kurudi bongo asubuhi maana nina show na Diamond kesho,” ameiambia tovuti hiyo. “Kama bahati mimi hutembea na hela zangu mfukoni maana nayajua mambo haya sasa itabidi nijilipie tu kila kitu na hela yangu.”
Hata hivyo Nay aliyekuwa ametajwa kuwania tuzo hizo amesema amemsamehe Eve.
“Yani kulingana na heshima na ukubwa wangu unadhania mimi nastahili kuhangaika hivi?!! inakera sana ila huyu dada mimi nishamsamehea.”
Drama nyingine iliyotokea ni baada ya Eve na timu yake kuamua kuondoka ukumbini ambapo watu waliokuwa wamelipa kiingilio walimfuata kudai warudishiwe chao. Watu hao walirushiana maneno na timu ya Eve japo hawakuambulia chochote.
Rich Mavoko alikuwa ahudhurie show hiyo pia lakini machale yalimcheza.
Pamoja na Nay Wa Mitego wasanii wengine waliokuwa wametajwa kuwania tuzo hizo ni pamoja na Ommy Dimpoz, Lady JayDee na Rich Mavoko.

“UKISEMA MADEE NI MIONGONI MWA WASANII AMBAO WANAINGIZA FEDHA NYINGI SANA, HICHO KITU NI UONGO".....NEY WA MITEGO
Wiki hii Nay wa Mitego alifanya
mahojiano marefu na mtangazaji wa kipindi cha Mambo Mseto (Radio
Citizen, Kenya) Willy M Tuva kuhusiana na mambo mengi kuanzia tofauti
zake na Chidi Benz, Madee na Kimbunga.
Nay wa Mitego akiwa na mtangazaji wa Radio Citizen, Willy M Tuva
Akijibu madai ya rapper Kimbunga kuwa alikuwa amepanga kumshirikisha kwenye hit yake Salam Zao lakini baadaye akamtosa, Nay alisema hakuwahi kumwambia kuwa angemshirikisha.
“Kimbunga ni mshkaji wangu, ni mtu ambaye hajielewi,” alisema Nay.
“Mimi sikuwahi kumwambia kwamba ‘nataka kufanya collabo na wewe’ hata siku moja. Lakini sijui alikaa na akina nani wakashikana masikio wakamwambia ‘bwana ukitaka kutoka pitia hapa’ akafanya hivyo. Mi sikuwa na time ya kujibizana naye, mimi niliendelea kufanya yangu. Siwezi kufanya competition na mtu ambaye hayupo level yangu.”
Akimuongelea Madee, Nay amesema kwanza hakubaliani na taarifa kuwa hitmaker huyo wa ‘Sio Mimi’ ni miongoni mwa wasanii wenye fedha nyingi.
“Ukisema Madee ni miongoni mwa wasanii ambao wanaingiza fedha nyingi sana hicho kitu hakina uhakika. Madee labda wimbo uliomuingizia hela ni ‘Nani Kamwaga Pombe Yangu’. Lakini ukitaja wasanii ambao wana hela Bongo, ukimweka Madee umekosea sana.” Hata hivyo Nay amesema ugomvi wake na Madee ni wa kibiashara na sio wa kupigana.
Akiongelea ugomvi wake na Chidi Benz, Nay alisema kwa sasa tofauti zao hazipo tena.
“Ziliisha tofauti zetu kama miezi mitatu hivi minne tulikuwa kwenye tour, tofauti ziliisha, yeye ndio alikuwa ana tofauti na mimi lakini mimi always sipendagi kuwa na tofauti na mtu ila nikiongea huwa naongea kitu cha ukweli. So this time tunaongea, tunapigiana simu kila kitu kiko sawa.”

"BASATAACHENI KUNITAFUTA MIMI SIWEZI KUACHA KUVAA MLEGEZO"...... NEY WA MITEGO
Siku chache zilizopita mwana Hip Hop kutoka pande za Manzese Nay Wa
Mitego alipokea barua kutoka BASATA inayomtaka kubadili aina ya mavazi
anayovaa katika show zake (mlegezo/mtepesho) ambayo hayaendani na
Tamaduni za kitanzania.
Akizungumza na Bongo5 leo kwa njia ya simu Nay amesema amekuwa akivaa
mlegezo kwa kipindi cha miaka ishirini hali ambayo itamwia vigumu
kubadilika kutokana ni mtindo ambao hata mashabiki wake wengi wameuzoea.
“Nahisi kuna kitu kingine wanakitaka toka kwangu kuhusu muziki
wangu ndiyo maana wananitishia kunifungia wakati mimi nafanya muziki
kama ndiyo maisha yangu, kwahiyo kubadilika kwa haraka kuvaa mlegezo
siwezi labda baada ya miaka 3 ila inategemea” Alisema Nay.
Aidha katika mahojiano mengine na kipindi cha Showtime kupitia kituo
cha RFA ya Mwanza Nay amesema kuwa Baraza hilo lina majukumu mengi ya
kufanya kwaajili ya kuboresha maslahi ya wasanii badala ya kuhangaika
na kumzuia kuvaa mlege ili hali wanaovaa hivyo ni wengi.
“Sasa hata baraza la sanaa Tanzania wana shughuli nyingi sana za
kufanya nyingi sana ili sanaa yetu isonge mbele mambo yetu yaani
wasanii tuishi maisha mazuri lakini si swala la kufuatilia mlege wa Nay,
hapana kuna kitu behind ambacho kinaendelea sijui ni nini maybe
wameamua waanzie hapo ili wastopishe kile ambacho nakifanya.”
Source: Bongo5
NAY WA MITEGO ASWEKWA SERO BAADA YA KUTUMIA SARE ZA POLISI KUFANYIA VIDEO.

Rapper
Ney Wa Mitego ameniambia kuwa hii picha hapo juu tukio hilo limetokea
Jana wakati wana shoot video ya wimbo wake Unaofanya vizuri kwa sasa
kwenye radio stations ' Salam Zao'.
Ney
Wa Mitego Amesema ' Nikweli nilitupwa sero jana baada ya raia wasio
julikana kuleta fujo eneo la kazi yangu kwasababu kulikuwa na waigizaji
waliokuwa na sare za polisi. Watu hao sijuani nao na walijitambulisha
kama askari na kutaka kujua kwanini natumia sare za polisi kwenye video
yangu bila kibali. hicho ndio kitu kilichopelekea nikapelekwa polisi.
Mitego
ameendela kusema kuwa baada ya kuka sero kwa dakika kama 15 mkuu wa
kituo alikuja na kusikiliza tatizo hilo na ndio aliachiwa huru baada ya
kutoa maelezo kuhusu tukio hilo na sare hizo kuonekana uraiani.
Ney
aliwekwa sero Kwenye kituo cha polisi Urafiki kilichopo Manzese na wiki
ijayo video hii itaonekana kwenye vituo vya televison Tanzania.
NAY WA MITEGO AONJA JEURI YA TRAFFIK BAADA YA KUKAIDI KUTII AMRI YA KUJISALIMISHA.
JESHI la Polisi mkoani Morogoro limemkamata msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa kosa la kuendesha gari kwa mwendo wa kasi wakati alipokuwa akiwahi shoo ya Fiesta iliyofanyika mjini hapa Jumapili iliyopita.Kwa mujibu wa askari mmoja wa kikosi cha usalama wa barabarani aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa si msemaji wa jeshi hilo, walimkamata msanii huyo eneo la Msamvu baada ya kugoma kutii amri ya kusimama kama alivyotakiwa na askari wa barabarani ‘trafiki’ eneo la Nanenane nje kidogo ya mji.
“ Msanii huyo akiwa na gari lake aina ya Alteza alitumia vibaya barabara na kuendesha gari kwa mwendo kasi kiasi cha kupiga ovateki eneo lisiloruhusiwa na askari alipomsimamisha akagoma kutii amri hiyo.
“Askari huyo aliwajulisha wenzake kwa njia ya simu ya upepo na Nay alipofika Msamvu alikamatwa na kupigwa faini papohapo,” alisema askari huyo.
Baada ya kulimwa faini ya shilingi 30,000 msanii huyo aliachiwa na kuwahi shoo ya Fiesta iliyokuwa ikifanyika ndani ya Uwanja wa Jamhuri ambapo wasanii mbalimbali walitoa burudani ya kiwango cha juu
Subscribe to:
Posts (Atom)