NEY WA MITEGO APATA PIGO LA MWAKA MPYA, ATEMWA NA MPENZI WAKE
UCHUMBA wa staa wa wimbo wa Muziki Gani, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mpenzi wake anayefahamika kwa jina moja la Siwema umedaiwa kuvunjika.
Kwa mujibu wa chanzo makini, chanzo cha kumwagana ni baada ya Siwema kukuta meseji za watoto wa kike tofauti katika simu ya Nay wa Mitego katika nyakati tofauti.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa, wawili hao walimwagana tangu Januari 2, mwaka huu, nyumbani kwa Nay wa Mitego, Manzese jijini Dar es Salaam baada ya Siwema kujiridhisha kuwa mpenzi wake huyo anamsaliti kutokana na ushahidi wa meseji alizozifuma.
Hata hivyo, chanzo kilizidi kumwaga ‘ubuyu’ kuwa, wapendanao hao wamekuwa wakizinguana mara kwa mara na kilichomuuma zaidi Siwema ni baada ya mkali huyo kuachia video yake mpya ya Nakula Ujana ambayo ameonekana katika pozi za kimahaba na warembo kibao.
“Imemuuma sana video ya Nakula Ujana, warembo wale inasemekana hakuishia katika video, sasa aliendelea kuwasiliana nao na Siwema akagundua ndipo mtiti ulipoibuka, Siwema akarudi kwao Mwanza,” kilisema chanzo.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Siwema ambaye alikiri kugombana na Nay na kusema ameshindwa kuvumilia na ameona ili kujiepusha na presha zisizo za lazima arudi kwao Mwanza.
“Kweli tuna ugomvi na Nay na haswa kuna mambo yananikera sana ila kubwa zaidi kwa sasa ni ile video yake mpya kuna parties mle sijazipenda...mchumba wa mtu ufanye video ujiachie vile, unashikwa shikwa ovyo,” alisema Siwema.
Alipotafutwa Nay, alikiri kutokea kwa ugomvi huo na kudai yupo katika jitihada ya kumaliza tofauti hizo kwa kuzungumza na Siwema.