Search in This Blog

Showing posts with label SKENDO. Show all posts
Showing posts with label SKENDO. Show all posts

"ISABELA" AMROPOKEA SINTAH KWA KUPENDA KUFATILIA NA KUCHUNGUZA MAISHA YA WATU

ISABELA Mpanda ambaye ni mwanamuziki na muigizaji wa filamu nchini ameonekana kuwa katika beef na Sintah kwa kumchana live kupitia mtandao mmoja wa kijamii. Hata hivyo sababu ya Bella kumtolea uvivu Sintah ambaye ni muigizaji wa filamu pia na blogger haijajulikana. Bella aliandika na kuweka picha ya Sintah kama inavyoonekana hapo chini.........

Isabela
Wewe sinta kwa nini unapenda kufwatilia maisha ya watu. Jione apo miwan na ilo pua lako na miziwa na viguu kama chelewa na mkorogo wa mia 2 . Nimekuchoka why wewe unapenda kufwatilia mambo ya watu. Nafikir umenielewa nini namaanisha. Na chokoza hao wapole mimi nitakufuraisha
 

DOKTA MAARUFU WA KUTOA MIMBA ANASWA, SOMA HABARI KAMILI HAPA


Stori: Waandishi Wetu
MWAKA umeanza, mambo mapya pia yapo! Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers imeingia kazini kwa kasi zaidi. Safari hii imemnasa daktari anayejulikana kwa jina moja la Mambo maarufu sana kwa jina la Dokta Mambo katika jaribio linalodaiwa kuwa ni la utoaji mimba.

Tukio hilo lilitokea katika zahanati yake (jina lipo) iliyopo Kawe jijini Dar es Salaam ambapo daktari huyo anayejulikana sana na wateja wake, hasa akina mama alipoingiliwa na OFM wakishirikiana na polisi baada ya kumuwekea mtego wa mbinu za kishushushu.
MALALAMIKO YA AWALI
Mwishoni mwa Desemba, mwaka jana, mtu mmoja (jina lipo) alituma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda OFM akimlalamikia dokta huyo kwamba amekuwa na mchezo wa kutoa mimba wanawake wakiwemo mabinti wa shule, kitendo alichodai haoni kama ni sawa.

“Naitwa….(jina lipo), nilikuwa naishi Kawe lakini kwa sasa nimehamia Mbezi (hakusema Mbezi gani). Kama hapo ni OFM (Oparesheni Fichua Maovu) naomba mumshughulikie daktari mmoja anaitwa Dokta Mambo wa Kawe. Huyu daktari jamani amekuwa na tabia ya kutoa mimba wanawake hata wasio na matatizo.
“Ninavyojua mimi hakuna hospitali inayoruhusiwa kutoa mimba Tanzania, labda pale ambapo itathibitika kwamba mjamzito ana kifafa, kwa hiyo hatari inakuwepo ya kumpoteza mama au mtoto tumboni ndiyo mimba hutolewa. Wananchi wa Kawe wamekilalamikia kitendo hicho hadi wamechoka. Polisi Kawe wamemshindwa,” alisema raia mwema huyo.
OFM YAANZA KAZI
Baada ya kupokea tuhuma hizo, OFM ilijipanga na kuingia kazini. Ilimwandaa paparazi wa kike na kumtengenezea ujauzito wa bandia na paparazi wa kiume ambaye ni mchumba wake (wa bandia) ili kwenda naye kwa Dokta Mambo kuona kama kweli anajihusisha na kazi hiyo au la!

JUMANNE, DESEMBA 31, 2013
Ilikuwa Jumanne ya Desemba 31, 2013, OFM na paparazi huyo walitia timu kwenye zahanati hiyo na kukutana na dokta huyo ambaye alikubali kumtoa ujauzito paparazi huyo.
‘Mchumba’ wa paparazi huyo alimwambia dokta kwamba wamekubaliana kuitoa mimba hiyo kwa sababu ya hali ya uchumba, daktari akasema haina shida.

AWEKA MASHARTI MAGUMU   
Katika hali ambayo OFM hawakuitarajia, daktari huyo alisema kwa kawaida kabla hajamchoropoa mimba mteja wake lazima aipime kwanza ili kujua ina muda gani.
Zoezi hilo lilikuwa gumu kwa OFM kwa sababu paparazi huyo hakuwa na ujauzito. Ilibidi ‘wateja’ hao waondoke kwa kisingizio kwamba wanakwenda kujipanga kwa fedha aliyoitaka ambayo ni shilingi laki moja na kwamba wangerudi siku iliyofuata (Jumatano).

OFM WAJIPANGA UPYA
‘Wachumba’ hao waliondoka na kuungana na Timu ya OFM ambayo ilikuwa mahali imekaa mkao wa mtego. Baada ya kupata simulizi za ndani ya zahanati hiyo, OFM ilirejea ofisini na kumweleza kamanda mkuu wake ambaye alikaa na timu hiyo na kupanga mpango mpya.

“Bosi, Dokta Mambo ameshakubali, lakini sera zake ni kwamba hawezi kumtoa mimba mjamzito hadi ampime kwanza na kujua ina miezi mingapi. Sasa huyu (paparazi) hana ujauzito, tungekubali ampime tungeumbuka, tukamwambia tunakwenda kusaka fedha kwanza,” OFM  mmoja alimwambia kamanda mkuu.
OFM YATUMWA MTAANI KUSAKA MWENYE MIMBA YA UKWELI
Kamanda Mkuu wa OFM (jina lipo) aliagiza timu yake kuingia mtaani ili kumsaka mwanamke mwenye mimba ya ukweli ambaye ndiye angekuwa na sifa za kutolewa ujauzito na daktari huyo.
Hayo yote yalifanyika baada ya pia uchunguzi wa kina kufanyika maeneo ya Kawe kuhusu tabia ya daktari huyo na kudaiwa kuwa, hawezi kuacha ‘kamchezo hako ka siku nyingi’.

Mjamzito wa kweli alipatikana (jina lipo), akiwa na mimba ya miezi mitatu.  Akashirikishwa katika zoezi hilo ambapo hata yeye aliumia kusikia kwamba kuna daktari anayetoa mimba wanawake hata wale ambao hawana sababu za kufanya hivyo kama sheria za utabibu zinavyotaka.
WATINGA POLISI KAWE
Baada ya kupatikana kwa mjamzito huyo, OFM ilimchukua hadi Kituo cha Polisi Kawe, Dar es Salaam na kuwaambia wahusika kuhusu tabia ya daktari huyo inayolalamikiwa na watu ili ikibidi watoe askari kwa kuungana na OFM kwenda kumtia nguvuni.

POLISI KAWE WAONESHA ‘MAAJABU’
Katika hali ya kushangaza, polisi wa kituo hicho, awali waliwataka OFM watoke nje ili wajadili wao. Baadaye waliwaita na kusema kwamba hawawezi kutoa polisi, kama ishu ni daktari huyo kulalamikiwa na watu, watamwita na kumkanya aache mchezo huo!

“Hatuwezi kushirikiana nanyi katika hilo zoezi, kama ni kweli kuna hayo maneno ya watu, sisi tutamwita tumuonye aache mara moja,” alisema mmoja wa askari wa Kituo cha Kawe.
Katika hali iliyoshangaza zaidi, polisi hao waliwataka waandishi wote walio kwenye msafara kuandika maelezo ya malalamiko kuhusu daktari huyo kwenye kitabu cha ripoti kituoni hapo (Report Book ‘RB’).
Maelezo yaliandikwa. Jina……, umri…., makazi…., kazi…., dini….. na aina ya malalamiko. Baada ya hapo wakatakiwa kuondoka zao.

OFM WARUDI KWA DOKTA MAMBO
Januari 3, 2014, OFM wakiwa na mjamzito wa kweli  walikwenda kwa dokta huyo ambapo kama ilivyo utaratibu wake, alimpima kwanza na kutoa majibu kwamba ana mimba ya miezi 3 na wiki mbili, akasema ni kubwa sana, hivyo zinatakiwa shilingi 160,000.

Hata hivyo, mchumba mtu alisema hana kiasi hicho cha pesa. Ikatokea vuta nikuvute hadi kufikia shilingi 100,000. Ikumbukwe kwamba, mpaka hapo Dokta Mambo hakuwa anajua kwamba mchezo wa pili ni uleule wa kwanza.
“Basi dokta tunaomba tuje kesho na hiyo laki moja,” mchumba mtu alimwambia daktari huyo ambaye alikubali huku na yeye akiomba kuwa, hiyo kesho iwe saa kumi na moja jioni.
OFM, POLISI, MJAMZITO NA MCHUMBA’KE
Kesho yake ilifika, OFM ikiwa na mjamzito huyo akiwa na mchumba’ake walikwenda maeneo ya Kawe jirani na zahanati ya Dokta Mambo kujaribu kupanga namna ya kufanikisha oparesheni hiyo.

Bado tatizo lilikuwa uwepo wa polisi baada ya kubaniwa na wale wa Kawe. Mungu si Athumani, wakiwa wanashangaashangaa eneo, ilipita pikipiki ya askari wa doria ‘Tigo’ na mara moja OFM ikawasimamisha.
Bila kupoteza muda, OFM waliwaeleza polisi wale mchezo mzima ulivyokuwa na kwamba walihitaji msaada wao ili kufanikisha zoezi hilo, walikubali bila kinyongo na mara moja wakaongozana hadi eneo la tukio.
OFM mmoja kati yao aliingia ndani ya zahanati hiyo akijifanya amekwenda kupima malaria, wale polisi wawili na OFM wengine walikaa mafichoni kutega mingo, wachumba nao waliingia mpaka kwa dokta wakiwa na kitita cha shilingi laki moja mkononi.
MJAMZITO APELEKWA CHUMBA CHA KAZI
Baada ya kuwapokea na kutoa kiasi hicho cha pesa, mjamzito huyo alipelekwa chumba kinachodaiwa ni cha kutolea mimba huku mchumba mtu akikaa kwenye fomu kusubiri matokeo.

UTAALAM WA OFM
Kilikuwa kipindi kinachotaka mawasiliano ya hali ya juu, OFM ikitambua kuwa kosa moja goli moja, walikuwa makini kwa mawasiliano. Mjamzito chumbani kumwambia mchumba wake kwenye fomu, naye kuwaambia OFM wa nje hatua kwa hatua.

Katika mazingira hayo, hakuna OFM aliyetakiwa kupokea simu wala kutuma meseji kwa mtu asiyehusiana na kazi hiyo.
TUKIO LANASWA
Ilikuwa wakati daktari huyo akiwa na glovsi mikononi, mjamzito wa kweli akiwa kitandani na nesi mmoja wa kumsaidia daktari wakiwa ndani ya chumba, ndipo OFM na polisi walipovamia na kunasa tukio ambalo lilionekana dhahiri kwamba lilikuwa jaribio la kutoa mimba.

Hapo ndipo Dokta Mambo alipogundua kuwa kumbe ‘kazi’ aliyopewa ilikuwa feki na wale walikuwa makamanda wa OFM wakishirikiana na polisi waaminifu, wazalendo na wanaopenda kazi yao sawasawa.
KWA NINI?
Lilikuwa jaribio la kutoa mimba kwa sababu, ndani ya chumba zilikutwa zana za shughuli hiyo huku mjamzito akiwa kitandani tayari kwa kufanyiwa mchakato.

Huku OFM wakimpiga picha (zipo za kumwaga kwenye maktaba yetu – ukitaka kuziona njoo Bamaga), askari nao wakichunguza mazingira zaidi na kukamata vifaa, daktari huyo alinywea huku msaidizi wake akitokwa machozi.
POLISI WAMWINGIZA NDANI YA GARI
Zoezi hilo lilikamilika kwa daktari huyo kuchukuliwa na askari hao ambao walikodi gari, mmoja akawa na dokta garini akiwa na vifaa vyake chini ya ulinzi, mwingine akiwafuata kwa nyuma na pikipiki.

Askari hao, waliwaeleza OFM kuwa wataitwa Kituo cha Polisi Oysterbay kwa ajili ya kuandika maelezo.
Risasi Mchanganyiko lilimtafuta kwa njia ya simu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camillius Wambura ili kujua kama suala hilo limefika mezani kwake, lakini simu yake haikupatikana muda wote ilipopigwa.

Hata lilipomtafuta Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova ili limsimulie mchezo mzima ulivyokuwa, naye hakupatikana hadi tulipokwenda mitamboni.
Bado tunaendelea kuwatafuta viongozi wa polisi na ukweli wa kina kuhusu namna ishu hiyo inavyoendelea, tunawajulisha katika matoleo yetu yanayofuata.
-GPL

MWANGA ANASWA NA POLISI USIKU WA MANANE


 Mtu mmoja asiyefahamika jina anayedaiwa kuwa ni mwanga amenaswa na polisi baada ya kudondoka katika eneo la Ilala Bungoni, jijini Dar  akiwa kama alivyozaliwa.

Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita kuamkia Jumapili  saa kumi usiku wakati mtu huyo alipodaiwa kudondoka akiwa na ungo, hirizi na kusabababisha watu waliokuwa eneo hilo kutahamaki.
Chanzo chetu kimesema kuwa, mara baada ya mtu huyo kudondoka watu waliitana na kukusanyika na wengine kutoa taarifa  jeshi la polisi kwa njia ya simu  ambao walifika haraka.
Watu waliokuwa katika eneo hilo walishangaa kuona mtu wa namna  hiyo ametokea kusikojulikana  na kuanguka na vitu ambavyo inadaiwa ni vya kiuchawi.
Askari polisi waliofika eneo la tukio walifanya kazi ya ziada kuzuia watu waliokuwa na lengo la kumpiga  mtu huyo aliyeonekana kutojitambua kwa madai kuwa ni kwa sababu ya kudondoka kutoka angani.
Polisi walipomhoji hakuweza kutaja jina lake wala kuongea lolote hali ambayo iliwalazimu askari hao kumpeleka katika Kituo cha Polisi Pangani, Ilala kwa uchunguzi zaidi.
“Hili ni tukio la kwanza kutokea hapa na limetushangaza sana, tunaamini kuwa alidondoka kwa sababu tulisikia kishindo na tulipokuja kuangalia ni nini tukamkuta mtu huyu akiwa na hirizi, ungo na tunguri, alitueleza  kwa tabu kuwa alikuwa na wenzake,” alisema shuhuda mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Juma Hussein.
Naye Asha Hamisi alisema mtu huyo wamaamini kuwa ni mwanga kwa kuwa alikuwa na vitu vinavyofanywa na wachawi au waganga.
“Hapa alipoangukia ndipo ninapofanyia biashara na tangu adondoke nakosa wateja kabisa tofauti na zamani,  hali hii naamini imetokana na kudondoka kwa mtu huyo,…serikali sasa ijue kuwa uchawi upo,” alisema Asha.

ANYOFOLEWA SIKIO KISA KUONGEA NA SIMU USIKU WA MANANE NA MUMEWE YUPO




Consolata Edward ni mke wa mtu, mkazi wa Igoma jijini hapa ambaye amebaki na kipisi cha sikio baada ya kunyofolewa kiungo hicho kisa kikidaiwa kuwa ni hawara yake.

Tukio hilo lilitokea Desemba 16, mwaka jana ambapo mwanamke huyo alidai kuwa alikuwa akizungumza kwa simu na mfanyakazi mwenzake ambaye anauza naye chakula maeneo ya Mlango Mmoja jijini hapa kabla ya mumewe kumvamia na kumpiga.
Kwa huzuni, Consolatha aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa baada ya mumewe kumpiga yeye aliamua kupigana naye kisha kumchania ‘boksa’ na kusababisha viungo vyake vya uzazi kubaki wazi.
Alisema wakati timbwili likiendelea, ghafla alitokea mama mwenye nyumba akifuatana na mwanamke aliyemtaja kwa jina moja la Hawa na kumg’ata sikio lake hadi akalinyofoa na kulitema.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mume wa Consolatha aliyejitambulisha kwa jina moja la Athuman alidai kuwa siku ya tukio alimuona mkewe akiongea na simu usiku jambo ambalo halikuwa kawaida yake na alipomuuliza alikata simu na kwenda kuongelea nje ya nyumba.
Aliongeza kuwa, alimfuata nyumanyuma na kupata wasiwasi kutokana na mada zilizokuwa zikiongelewa ndipo alipomnasa kofi mkewe aliyekimbilia kumchania boksa yake.
Athuman alisema kuwa mama mwenye nyumba alipoona ugomvi huo unazidi ndipo alipowaita majirani walioingia wakiwa na huyo Hawa aliyedaiwa kumg’ata mkewe.

“Wakati mimi natafuta khanga ili nijistiri ndipo nilipoona mke wangu ameloa damu huku kipande cha sikio lake kikiwa chini kabla ya kuliwa na mbwa, sijui kwa nini Hawa aliingilia ugomvi wetu,” alisema Athuman huku kukiwa na madai Consolatha alikuwa akizungumza na mume wa Hawa.
Baadaye sakata hilo lilipelekwa kwa mwenyekiti wa mtaa na watu hao kutakiwa kuripotiwa Kituo cha Polisi cha Nyakato (Mwatex) ambapo jalada la kesi lilifunguliwa kwa NY/RB/8709/2013 KUPIGANA HADHARANI wakisubiri sheria kuchukua mkondo wake.
HABARI NA MATUKIO BOFYA HAPA

GPL 

MCHUNGAJI AZIDIWA NA HAMU YA NGONO NA KUAMUA KUTAFUTA KAHABA MWENYE MIMBA, NA MWISHOWE KUFUMANIWA





According to reports, a husband who suspected his wife of infidelity has caught her red-handed in the arms of another man.
Sources revealed that the woman, who is already a few months pregnant, has been seeing her lover and having extra-marital affairs with him for a while now. The husband has reportedly been hearing the rumours of his wife’s affair and decided to take action.
On this fateful day, the wife and her lover, met at their usual location (a hotel) to have their lovemaking session. The husband, at this time, got a call from his informant. He then busted into the hotel room and caught his pregnant wife in the act.
The husband reportedly took photos and started distributing them on social media.

KIZAAZAA CHA MWAKA MPYA, MUME WA THEA AFUMWA NA MKE WA MTU


Stori: Shakoor Jongo
MWAKA ulianza vibaya kwa mke wa mtu ambaye jina lake halikupatikana mara moja kumkimbia mumewe na kumfuata mume wa msanii wa filamu, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ aitwaye Michael Sangu ‘Mike’ jambo lililosababisha ale kichapo cha nguvu na kuuanza mwaka mpya vibaya.

Tukio hilo lililovuta hisia za wengi, lilitokea siku ya mkesha wa mwaka mpya, usiku wa kuamkia Jumatano, katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar ambapo Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ ilikuwa ikikonga nyoyo za mashabiki wake.
KAMERA ZA IJUMAA
Paparazi wetu aliyekuwa ukumbini humo alimuona Mike akiwa upande mwingine na washikaji zake huku wakiendelea kula raha wakati wa shangwe za mwaka mpya wakati mdada huyo ‘kibonge’ akiwa na mumewe na watu wengine wakifanya yao.

Ijumaa lilipata shaka kidogo, baada ya kumuona dada huyo akimwacha mumewe kila wimbo unapokolea na kwenda alipokuwa Mike kisha kucheza naye.
Harufu ya ugomvi ilianza kunukia mapema, baada ya paparazi wetu kumshuhudia mume wa dada huyo akionekana kumkaripia japo kwa sauti ndogo mkewe kila aporudi akitokea kucheza na Mike.
ONYO HALIKUZAA MATUNDA
Pamoja na onyo alilokuwa akitoa mume huyo kwa mkewe mara kwa mara, bado dada huyo alionekana kumfuata Mike na kucheza naye tena kwa ukaribu kama vile wanajuana.
Baadaye jamaa huyo aliamua kuwashirikisha marafiki aliokuwa amekaa nao meza moja kuhusu tabia ya mkewe, wakamsihi asiende tena kucheza lakini bado hakusikia.

“Sisi tulimwambia, mwenzako hataki uende kucheza na yule msanii, anahisi labda kuna kitu kinaendelea lakini hakusikia, sijui ni pombe zilimzidi au vipi,” alisema mmoja wa watu waliokuwa wameketi meza moja na wanandoa hao muda mfupi baada ya tukio la kichapo kutokea.
Akaongeza: “Kuna wakati alikuwa akijifanya ameelewa, lakini sasa alikuwa akiaga na kujifanya anakwenda msalani halafu mumewe akifuatilia anagundua kumbe amemfuata Mike ili wacheze, jamaa akachukia sana.”
KICHAPO
Baada ya mume kuona dharau za waziwazi zikifanywa na mkewe mbele ya watu aliokuwa amekaa nao, aliamua kusimama na kumfuata alipokuwa akicheza na Mike.
Hakuwa na haja ya kuuliza chochote, alimkamata mkewe na kuanza kumshushia kichapo cha nguvu huku wengi wakiendelea kuponda raha kama vile hakuna kilichotokea.

“Ni mke wake? Hizo ni dharau, acha apigwe. Hawa wanawake wa Dar ni wajinga sana. Utamwachaje mumeo uende kushobokea wasanii? Huu ni upuuzi. Ni haki ale kichapo,” alisikika akisema jamaa mmoja aliyekuwa jirani na paparazi wetu.
DAMU CHAPACHAPA
Hasira zilipompanda yule jamaa, hakuchagua mahali pa kupiga, alimvuta nywele na kumpiga makonde kila sehemu ya mwili wake hali iliyosababisha damu imwagike chapachapa (angalia picha ukurasa wa mbele).
Mashuhuda walipoona damu imemwagika ndipo wakaingiwa na huruma na kuamulia ugomvi huo.

UTETEZI WA MKE
Katika kujitetea, mwanamke yule alimlaumu mumewe kwa kumpiga hadi kufikia kutoa damu kwa kosa la kucheza na Mike akisema kwamba, haoni kosa lake.
“Mume wangu unanionea tu bure, huyu sina uhusiano naye wowote ule... nacheza naye tu kama marafiki. Simfahamu na wala sijawahi kumuona zaidi ya kwenye filamu,” alisema mwanamke huyo.

MIKE HUYU HAPA
Kwa upande wa Mike, alipoulizwa na mwandishi wetu kuhusu kisanga hicho alisema, anamshangaa jamaa mwenye mke kwa sababu amemuonea mkewe bila sababu ya msingi.

“Kuna kosa gani watu kucheza muziki? Hapa ni ukumbi wa muziki, tena usiku. Hakuna mipaka, yeyote anaweza kucheza na yeyote. Ule mimi naweza kusema ni ulimbukeni wa kutojua mambo.
“Amemuonea... yule dada alikuwa anafurahi tu sherehe za mwaka mpya ambapo staili yake ya kucheza labda imemkera mumewe lakini kama alikuwa hataki mkewe acheze na mtu mwingine, si wangekaa tu chumbani kwao wawashe redio wacheze wawili tu kuliko kuja kuleta kero kwenye kumbi za burudani?” alisema Mike.
Alipoulizwa hajisikii vibaya kucheza na mke wa mtu alijibu kwa kifupi sana: “Kwanza ningejuaje?”

MADAI MENGINE
Ndoa ya Mike na Thea kwa sasa ipo kwenye mgogoro mzito ambapo wawili hao wametengana huku sababu kubwa ikitajwa na vyanzo vyetu kuwa ni Thea kumtuhumu mumewe kuwa hajatulia.
Bado tunafuatilia sakata hili, likikamilika tutawaletea.

USISAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA HARAKA NA UHAKIKA, BOFYA HAPA<<<< MDADISI MAMBO PAGE

FUMANIZI LA KWANZA 2014: AVUA NGUO KWA FURAHA BAADA YA SHEMEJI YAKE KUFUMANIWA

AMA kweli dunia uwanja wa fujo! Mrembo aliyetajwa kwa jina la Baby amefanya kituko cha aina yake kwa kusaula nguo mbele ya hadhara baada ya shemeji yake maarufu kwa jina la Baba K kufumaniwa. FUMANIZI LAIVU
Tukio hilo la aina yake lililovuta wengi lilijiri kwenye gesti moja (jina tunalo), maeneo ya Temeke jijini Dar hivi karibuni baada ya jamaa mmoja kumwekea mtego rafiki yake aliyekuwa akimtongoza mkewe na kumfumania laivu.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mara baada ya fumanizi hilo, mrembo huyo ambaye ni shemeji wa mwanaume aliyefumaniwa alionesha maajabu alipoamua kuvua nguo bila kusitasita.
“Alianza kuvua kidogokidogo, baadaye akaamua kuvua zote na kubakia na nguo ya ndani tu. Kwa kweli iliwashangaza wengi pale kwenye eneo la fumanizi. Halafu unajua fumanizi lenyewe lilikuwa ndani ya chumba, dada yake alikuwa huko, yeye nje,” alisema mmoja wa mashuhuda.
Imeelezwa kuwa, baada ya mwanamke huyo kuvua nguo  alianza kushangilia kwa nguvu huku akirukaruka kwa furaha na kusema:
“Heee! Mwanaume kapatikana leo, kwa furaha namwaga lazi, eti shemeji. Shemeji gani unamwacha mkeo unakwenda kwa vidampa?”

AKATA MAUNO
Ilielezwa kuwa furaha ya mwanadada huyo haikuishia katika kuvua nguo na kusema hivyo tu, kwani aliendelea kusheherekea kwa kukata mauno huku na kule kama anayetamba.
Ilisemekana kwamba wakati ‘akifanya yake’ midume na watoto walikuwa wakifaidi sinema ya bure huku wengine wakiona aibu na kujichomoa zao eneo la tukio.

“Labda anamshukuru Mungu kwa kufanikisha fumanizi la shemeji yake kwa kuwa alihusika kwenye kusuka mchezo mzima,” alisema shuhuda mwingine.
MSHANGAO
Kitendo hicho cha kusaula nguo zote na kushangilia kiliwashangaza baadhi ya watu ambao walikuwepo eneo hilo la tukio na wengi wao wakajiuliza kulikoni shemeji mtu apitilize furaha kiasi hicho kisa tu mume wa dada yake kafumaniwa?
Wakizungumza na Amani, mashuhuda hao walisema kwa vyovyote kuna la ziada nyuma ya pazia ndiyo maana mwanadada huyo alifurahi kupita kiasi.

“Kwa vyovyote kuna kitu, si bure. Mbona huyu dada kapagawa kuliko hata aliyefumania? Mh! Yetu macho,” alisema mmoja wao huku mwingine akidakia:
“Hapa dada mtu anatakiwa kuwa makini sana na huyu dada si ajabu anachochea ili ndoa ivunjike achukue nafasi. Hawa ndiyo akina dada wa mjini bwana.”

BOFYA HAPA KUMSIKIA
Amani lilipomvaa mrembo huyo na kumuuliza kwa nini alikuwa amepagawa na kusaula nguo, mwanadada huyo alijibu kwa mkato kuwa alifurahishwa mno na fumanizi hilo ingawa alikiri aliyefumaniwa anaumia huko alipo.

“Hahahahaaa…Huyu shemeji yangu amezidi, afadhali leo amefumaniwa nimefurahi sana,” alisema dada huyo huku akikatiza mtaani akiwa na kufuli pekee.
TURUDI KWENYE FUMANIZI
Katika fumanizi hilo ambalo lilikuwa la aina yake ilielezwa kuwa shemeji mtu alikuwa akimsumbua mke wa rafiki yake ndipo mke huyo akaamua kumweleza mumewe ambaye walimwekea mtego na kufanikisha kumnasa laivu.

Hata hivyo, mfumaniaji na mfumaniwa, wote walikubaliana ambapo jamaa aliyefumaniwa alipewa kibano na onyo kali iwe mwanzo na mwisho kusarandia wake za watu.
Ilidaiwa kuwa, baada ya makubaliano hayo, mambo yote yaliishia hapo bila kufika kituo chochote cha polisi.

MAFUMANIZI YA SIKU HIZI
Uchunguzi wa Amani umebaini kuwa, miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mafumanizi ya makusudi. Katika kila wafumaniwa kumi, saba ni mitego tofauti na zamani ambapo ilikuwa ya kushtukiza.

Hata hivyo, uchunguzi inaonesha kuwa, wengi wanaofumaniwa ni wanaume wenye tabia ya kutongoza wake za watu au wake za marafiki zao wa karibu.

HIVI NDIVYO JACK PATRICK ALIVYONASWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA


Jack akiwa chini ya ulinzi.
Stori: Stori: waandishi Wetu
MADAI ya kukamatwa kwa tuhuma za kumeza madawa ya kulevya aina ya Heroin nchini China kwa msanii, Video Queen na mwanamitindo maarufu Bongo, Jacqueline Patrick, kumeibua maswali ya kila aina,  mengi yamesemwa, uvumi umeenea, lakini Ijumaa Wikienda linadondosha hatua kwa hatua.

Baada ya kuinyaka taarifa hiyo ya aibu kwa staa huyo na taifa kwa jumla, kwa uchungu mkubwa timu yetu imara ilijipanga na kuingia mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba, mtu kwa mtu kuchimbua, kudadavua na kufukunyua kwa undani zaidi juu ya tuhuma hizo. Aya zinazofuata zitakupa mwanga.
ALIVYONASWA HATUA KWA HATUA
Wikienda lilichorewa mchoro kwamba, Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Macau nchini humo akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.

NINI KILISABABISHA?
Inadaiwa kuwa miongoni mwa mambo yaliyochangia kunaswa kwake ni uso wa uchovu, kuanza kuwa na hali mbaya ya mwili, kushindwa kujibu maswali vizuri na hati yake ya kusafiria (passport) yake kuonesha kugongwa mihuri ya kuingia nchini humo kila mara.

Habari zinasema ndipo maafisa wa uwanja huo walipomweka pembeni na baadaye kumpeleka kwenye chombo cha kukagua kwa undani mwili wa binadamu, walipojiridhisha ana ‘mzigo’ wakampa polisi mwanamke (WP) kwa ajili ya kwenda kusimamia utoaji wa kete hizo chooni kwa njia ya haja kubwa.
AVALISHWA MASKI, AWEKWA MBELE YA MAPAPARAZI
Baada ya kutoka chooni, ikafuata hatua nyingine. Jack aliwekwa mbele ya mapaparazi akiwa amevalishwa maski nyeusi usoni ili asionekane sura kisha akapigwa picha za kumwaga.
Sheria za Macau, mtuhumiwa huvalishwa maski usoni ili watu wasiione sura yake. Kete alizozitoa ziliwekwa juu ya meza, pia simu zake mbili, Iphone na Samsung nyeupe zilikuwa pembeni. Baadhi ya watu Bongo walizitambua simu hizo kwamba ni zake.

AINA YA MADAWA
Jack ambaye ni Miss Ilala Namba 3, 2005, alikamatwa na madawa aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 yakiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 223 kwa kuhifadhiwa ndani ya kete 57.

ATANYONGWA?
Kwa sheria za Beijing, China mtu akithibitika kubeba unga hukumu yake ni kunyongwa tu lakini waandishi wetu walipozungumza na wataalam mbalimbali wa sheria za kimataifa ili kujua ni adhabu gani inaweza kutolewa kwa mrembo huyo endapo atakutwa na hatia, walisema Beijing si Macau, ni vigumu kula kitanzi lakini kwenda jela miaka mitatu, minne au nane inaweza ikamhusu. Majimbo mengi ya China yanaongozwa kwa sheria zake badala ya sheria mama moja kwa nchi nzima.

Hata hivyo, sheria za eneo alilokamatiwa zinasema kuwa uwezekano wa ndugu, jamaa na marafiki kumuona kwa sasa haupo mpaka Machi, 2014 uchunguzi utakapokuwa umekamilika.
WATU WA KARIBU WALIVYOPOKEA TAARIFA
Awali, baadhi ya watu wa karibu na modo huyo waligoma kuweka bayana kuhusu yaliyompata Jack huko ughaibuni wakidai si wasemaje wake na kuwataka mapaparazi kwenda kuchimba kwenye Ubalozi wa China nchini Tanzania.

Kwa sharti la kutotajwa jina mahali popote kwenye ukurasa huu, mmoja wa marafiki wa karibu wa Jack aliyeko China kwa masomo, alisema amethibitisha ukweli kupitia balozi ndogo ya Tanzania nchini humo.
“Nilishituka sana niliposikia habari hizo, ikabidi nijiridhishe kwa kwenda kwenye ubalozi mdogo wa Tanzania nchini hapa na kupewa maelezo kamili juu ya sakata hilo.

“Nikaulizia uwezekano wa kuonana na Jack, nikaambiwa ni ngumu kutokana na utata mkubwa juu ya ishu yenyewe,” alisema rafiki huyo na kuongeza:
“Hata jana (Jumatano ya wiki iliyopita) gazeti moja liitwalo Daily China la huku lilitoa habari hiyo ndipo nikathibitisha baada ya kuona sura gazetini. Kweli ni Jack Patrick, najisikia uchungu na huruma juu yake, inauma lakini hatuna jinsi,” alisema rafiki huyo.

NYUMBANI KWAKE KAMA MSIBA
Kazi ni kazi tu. Timu yetu ikiwa na kiu, hamu na shauku kubwa ya kuujua ukweli, ‘ilisaga lami’ mguu kwa mguu hadi kwenye nyumba aliyokuwa anaishi Jack iliyopo Mikocheni B jijini Dar ili kuona hali ikoje na kujiridhisha zaidi ambapo iliashiria kila dalili ya kuwepo kwa habari mbaya.

Ukimya, utulivu na hali ya kupoa viliitawala nyumba hiyo baada ya waandishi wetu kuwasili na kukuta hakuna chochote zaidi ya milio ya ndege iliyokuwa ikisikika.
Mmoja wa waandishi wetu alipanda ukuta na kuchungulia ndani ambapo hakuona binadamu isipokuwa gari lake lile Benz jeusi likionekana liliegeshwa siku nyingi.

MAJIRANI HAWA HAPA
Roho za kutoridhika ziliwasukuma mapaparazi wetu kuwatafuta majirani wa msanii huyo ili kusikia walau chochote kipya kuhusiana na taarifa za Jack kunaswa na unga.
“Mh! Hata sisi hatujui maana hatujamuona siku mbili hizi, lakini kama ni kusikia hata sisi tumesikia juu ya uvumi huo, lakini hatuna uhakika,” alisema mama mmoja (jina linavunda kwenye droo zetu).

NANI YUKO NYUMA YA JACK?
Watu wengi (tukiwemo sisi) wana hamu kubwa ya kujua ni nani hasa anahusika na mzigo ambao msanii huyo anatuhumiwa kukamatwa nao. Katika pitapita ya waandishi wetu kupeleleza kwa undani suala hili, lilibahatika kuzungumza na baadhi ya watu ambao walihoji na kutaka kujua ni kigogo yupi yuko nyuma ya ishu nzima.

“Lazima kutakuwa na mtu nyuma yake, si bure nyie fuatilieni sana,” alisema mdau mmoja ambaye hakupenda jina lake litajwe mahali popote.
Aliongeza kuwa, mtu anayekutwa na kete za unga tumboni maana yake katumwa (punda) na bosi wake, kwa hiyo suala kubwa kwa sasa ni kumsaka bosi huyo ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

UWANJA WA NDEGE DAR MATUMBO JOTO
Hakuna ubishi kwamba hali ni mbaya kwa wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage jijini Dar, kwa madai kuwa piga, ua, galagaza mzigo huo, Jack alikatiza nao pale.
“Jack alitokea Dar kwenda Thailand kupitia Nairobi, lazima mzigo alitoka nao Bongo, tena jijini Dar. Sasa pale eapoti alipitaje? Serikali iwachunguze wafanyakazi wa pale,” alisema nguli mmoja wa filamu za Bongo (jina lake lipo).

NI ZAIDI YA MASOGANGE
Hii imekaa vibaya! Wataalam mbalimbali wa masuala ya kisheria walizungumza na gazeti hili juzi na kusema kuwa sakata la Jack ni kubwa zaidi ya lile la Agnes Gerald ‘Masongange’ na nduguye, Melisa Edward  waliokamatwa nchini Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu.

NI AIBU KWA TAIFA
Wakizungumza na Wikienda kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi walisema tukio la Jack limezidi kuchagiza aibu kubwa kwa taifa katika medani za kimataifa kufuatia matukio mengi ya Watanzania kukamatwa na madawa ya kulevya nje ya nchi.

MSIKIE NZOWA
Akizungumzia suala hilo, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alisema taarifa hizo zilimfikia kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, hivyo anaendelea kufuatilia suala hilo kwa ukaribu zaidi ili kupata taarifa sahihi.

Aidha, Kamanda Nzowa alisema kuna wakati aliyekuwa mume wa mwanamitindo huyo, Abdulatif Fundikira aliwahi kukamatwa na madawa za kulevya nchini na kuachiwa kwa dhamana, ina maana kesi bado ipo mahakamani.

MWANADADA MAUNDA ZOLLO APIGWA PICHA ZA UTUPU AKIWA GEST..ZIANGALIA PICHA HAPA

Noma kweli kweli..!
Ni mara nyingine tena star mwingine tokea bongo picha zake chafu zimevuja katika mtandao mara hii ni kutoka kwenye Industry ya musc bongo






MANENO HAYA HAPA CHINI YAMEANDIKWA MOJA KWA MOJA KWENYE PICHA HAYAJAANDIKWA NA MWANDISHI WA WEBSITE HII.

TETESI: PICHA HII NDIO CHANZO KWA OBAMA KUTENGANA NA MKEWE

RAIS wa Marekani, Barack Obama na mkewe Michelle wanadaiwa kutengana. Habari zinadai kuwa wawili hao wanalala katika vyumba tofauti kwa sasa ndani ya Ikulu ya Marekani 'White House'.
 


 Mgogoro baina ya wawili hao ulianza zamani na wameweza kuendelea kuishi pamoja kwa sababu ya watoto wao wawili wa kike Sasha na Malia na kulinda heshima ya urais.
Michelle anadai amechoka na atakutana na mwanasheria wa masuala ya talaka ili aweze kuachana na rais huyo wa 44 nchini Marekani. Michelle ataendela kuishi Ikulu 'White House' kwa muda wote uliobaki katika kipindi cha utawala wa Obama, ila ameweka wazi kuwa watakuwa wakiishi vyumba tofauti.

Anataka kuishi katika chumba kimojawapo cha familia kilichowazi na anajiandaa kuhamisha nguo zake na kila kilicho chake kutoka kwenye jumba lao la kifahari la mamilioni ya dola lililopo Chicago.

Michelle alichanganyikiwa zaidi baada ya Obama kupiga picha za kimahaba akiwa na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt, wakati wa mazishi ya marehemu Nelson Mandela nchini Afrika Kusini.

Obama mwenye miaka 52, alikuwa akifurahi, kunong'enezana na kumshika begani mrembo huyo mwenye umri wa miaka 46 ambaye amekuwa Waziri Mkuu wa Denmark tangu Oktoba 3, 2011.

OBAMA NA MKEWE MICHELLE WADAIWA KUTENGANA

Barack Obama na mkewe Michelle kila mmoja akionekana kuwa kivyake.
Obama akimshika begani Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt, wakati wa mazishi ya Mandela nchini Afrika Kusini. Kulia ni Michelle Obama akiwa amenuna.
RAIS wa Marekani, Barack Obama na mkewe Michelle wanadaiwa kutengana. Habari zinadai kuwa wawili hao wanalala katika vyumba tofauti kwa sasa ndani ya Ikulu ya Marekani 'White House'.
Mgogoro baina ya wawili hao ulianza zamani na wameweza kuendelea kuishi pamoja kwa sababu ya watoto wao wawili wa kike Sasha na Malia na kulinda heshima ya urais.
Michelle anadai amechoka na atakutana na mwanasheria wa masuala ya talaka ili aweze kuachana na rais huyo wa 44 nchini Marekani. Michelle ataendela kuishi Ikulu 'White House' kwa muda wote uliobaki katika kipindi cha utawala wa Obama, ila ameweka wazi kuwa watakuwa wakiishi vyumba tofauti.
Anataka kuishi katika chumba kimojawapo cha familia kilichowazi na anajiandaa kuhamisha nguo zake na kila kilicho chake kutoka kwenye jumba lao la kifahari la mamilioni ya dola lililopo Chicago.
Michelle alichanganyikiwa zaidi baada ya Obama kupiga picha za kimahaba akiwa na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt, wakati wa mazishi ya marehemu Nelson Mandela nchini Afrika Kusini.
Obama mwenye miaka 52, alikuwa akifurahi, kunong'enezana na kumshika begani mrembo huyo mwenye umri wa miaka 46 ambaye amekuwa Waziri Mkuu wa Denmark tangu Oktoba 3, 2011.

MAKAMBA AMPIGA ZINGA LA DONGO JACK BAADA YA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

Hayo ndio maneni ya Mwamvita baada ya habari kuwa Jack Amekamatwa china na Madawa ya Kulevya

BAADA YA KUZIDIWA NA MATAMANIO YA NGONO, MNENGUAJI WA TWANGWA PEPETA AKUTWA LAIVU AKILILIA PENZI HADHARANI, MUONE HAPA

Ufuska mtupu! Mnenguaji wa kiume wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Bakari Kisongo ‘Mandela’ ametoa kali ya kufungia mwaka baada ya kunaswa ‘laivu’ akililia penzi kutoka kwa dada aliyetajwa kwa jina moja la Zainab.

 Bakari Kisongo ‘Mandela’ (kushoto) ametoa kali ya kufungia mwaka baada ya kunaswa ‘laivu’ akililia penzi kutoka kwa dada Zainab.
Tukio hilo la aina yake lililoshuhudiwa na ‘fotografa’ wetu lilitokea juzi nje ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar ambapo Twanga ilikuwa ikivurumisha burudani ya Sikukuu ya Krismasi.

Bakari Kisongo ‘Mandela’ (kushoto) akilazimisha penzi.
Mara baada ya bendi hiyo kumaliza kufanya onesho lake majira ya saa 9:30 usiku, mnenguaji huyo alionekana akizama kwenye Baa ya Uhuru Peak inayotazamana na Mango kisha akamwita msichana huyo ili waondoke.

Bakari Kisongo ‘Mandela’ (kushoto) kanaswa ‘laivu’ akililia penzi kutoka kwa dada Zainab.
Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa karibu, kulitokea kama mtafaruku kwani msichana huyo alikataa katakata kuondoka na mnenguaji huyo.
Baada ya kuona hivyo, Mandela alitumia mbinu mbadala (nguvu) ambapo alimvutia mrembo huyo ndani ya Bajaj iliyokuwa imepaki eneo hilo ndipo mtafakuru ukazuka.
Huku na huku, dada huyo alipata upenyo ambapo alichoropoka na kutoka nje ambapo Mandela naye alimrukia na kuanza kumlilia huku akilazimisha mambo ya kikubwa hadharani ikiwepo ‘kudendeka’.
Hata hivyo, Mungu mkubwa kwa sababu mrembo huyo alifanikiwa kumtoka Mandela kisha akadandia Bajaj nyingine na kuondoka kwa kasi huku akimwacha jamaa na mfadhaiko.
Mashuhuda wa tukio hilo walimponda Mandela wakidai kuwa huo ni ufuska kwani kitendo alichotaka kufanya si cha kuigwa katika jamii.
Gazeti hili lilipomtaiti Mandela kutaka kujua kulikoni kuomba mambo ya kikubwa hadharani hakuwa na la kusema zaidi ya kusikitika kumkosakosa mrembo huyo.

ARARURIWA NA MAPANGA, HAWARA ETI NDIO CHANZO, SOMA ZAIDI

MAMA mmoja mkazi wa Ronsoti, Kata ya Nyamisangura, wilayani hapa, Eliza Marwa,28, hivi karibuni amenusurika kuuawa na mumewe, baada ya majirani kufika kumuokoa kutokana na kukatwakatwa mapanga.

Mariamu akiugulia maumivu.
Mama huyo aliliambia gazeti hili akiwa katika Hospitali ya Wilaya Bomani, Tarime kuwa mume wake Marwa Ogora alimkatakata mapanga baada ya kumtuhumu kuwa akikwenda kwa hawara yake badala ya kwenda kwenye mazishi ya mjomba wake huko Bunchari.
Akifafanua zaidi, Eliza alikuwa na haya ya kusema: ‘’Mjomba alifariki na mazishi yake yalifanyika Desemba, kumi na sita mwaka huu ambapo nilihudhuria baada ya kumwarifu mume wangu kuwa nitahudhuria lakini alinijibu kuwa hakuwa na fedha za kunipa ili niende kwenye mazishi.
“Nilichukua jukumu la kwenda kwa kutumia nauli yangu kwa kuwa muda huo mume wangu alikuwa kazini na baada ya mazishi kesho yake asubuhi Desemba kumi na saba mwaka huu nilirudi nyumbani na kumkuta mume wangu ambaye alianza kunipiga kwa mpini wa jembe kisha panga akidai kuwa sikuwa nimeenda kwenye mazishi badala yake nilikuwa nimeenda kwa mpenzi wangu.
“Alinishambulia sehemu mbalimbali za mwili hususani kichwani, kidogo anitoe ubongo, wasingekuwa majirani kuniokoa baada ya kupiga yowe naamini angeniua kwani hivi sasa siwezi hata kuamka na masikio yameziba, miguu ina ganzi, siwezi kutembea.
“Mume wangu Ogora amekuwa akinipiga mara kwa mara lakini kutokana na watoto tuliozaa naye nimekuwa nikivumilia mateso, naogopa kuondoka na kuacha watoto walelewa na mama wa kambo,”alidai mama huyo.
Ogora hakupatikana kuzungumzia tukio hilo kwani anasakwa na dola na afisa mmoja wa polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema  wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa. Naye daktari wa hospitali aliyolazwa mama huyo, Nega Malico alikiri kumpokea mgonjwa huyo. JIUNGE NA PAGE YETU YA FACEBOOK  HAPA >> MDADISI MAMBO

MUME AFUMANIWA AKIDO NDANI YA GARI KWENYE MKESHA WA KRISMAS

KRISMASI noma sana! Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Baba Pendo ameiona chungu Sikukuu ya Krismasi 2013 kufuatia tukio la kufumaniwa na mkewe, Mama Pendo au Mama P ‘akibanjuka’ na mwanamke ndani ya gari.
NI MKESHA WA KRISMASI
Tukio hilo la aina yake lilijiri eneo maarufu Kijitonyama jijini Dar linalojulikana kwa jina la Miti Mirefu, usiku wa Mkesha wa Krismasi, majira ya saa 8:00 usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita.
Ina maana kwamba Baba Pendo aliamua ‘kumalizia shida’ zake ndani ya gari hilo ambalo namba zake za usajili tunaziweka kapuni.

OFM YAJUZWA
Kabla ya tukio hilo, mara kadhaa Mama P aliwasiliana na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers na kulalamika juu ya mumewe kutoka nje ya ndoa na mwanamke mmoja wa mjini.
Mama P: Haloo…naongea na OFM? Jamani naombeni mnisaidie kuna mwanamke anamzuzua sana mke wangu.
OFM: Una uhakika mama?

Mama P: Nina uhakika wa asilimia mia moja. Hapa nimeona meseji wamepanga kukutana leo na ndiyo maana nikawatafuta. Ninyi mpo wapi?
OFM: Sawa, sisi tupo kikazi Mango Garden (Kinondoni, Dar) wewe upo wapi?
Mama P: Nipo Sinza A (Dar) nitawashtua mambo yakiiva maana najua lazima mume wangu atatoka muda si mrefu, nimemuona anajiandaa.

OFM: Oke lakini uwe makini sana.
Mama P: Sawa, nitawashtua.
Hiyo ilikuwa saa 5:12 usiku, hivyo OFM iliendelea na majukumu mengine ya kufichua uovu katika jamii.

BABA PENDO AAGA ANAKWENDA MKESHA
Kwa mujibu wa Mama P, majira ya saa 5:20 usiku, mumewe alimuaga anakwenda kwenye mkesha wa kumpokea mwana wa Mungu (Yesu) aliyezaliwa ambapo kwa mujibu wa mume huyo, alikuwa anakwenda kusali Kanisa la Mtakatifu Maximilian Kolbe lililopo Mwenge, Dar.

MAMA P MZIGONI
Baada ya mumewe kuondoka, mwanamke huyo aliwasiliana na OFM na kuwapa ishu nzima ambapo walimpa mbinu ya kumfuatilia mumewe ikiwa ni pamoja na kubadili aina ya usafiri ili asishtuke.

Mama P alichukua Bajaj na kumfuatilia mumewe hadi maeneo ya Sinza-Kijiweni ambapo alimuona akipaki gari lake na kuingia kwenye ‘pabu’ moja kisha akaagiza ‘ngumu kumeza’ (mzinga wa konya) ambayo aliipiga taratibu hadi mishale ya saa 8: 05 usiku huku akipiga stori na washkaji.
Baada ya hapo, Baba Pendo aliingia garini kuondoka. Mama P naye akachukua bodaboda kumfuatilia kwa nyuma.
Alipofika maeneo ya Kijitonyama  alimuona akisimamisha gari na kuingia kwenye ‘kamtaa’ f’lani, akatoka na mwanamke kisha akaingia naye kwenye gari.
Alisema yeye akiwa bado nyuma, walipofika Miti Mirefu  mumewe alipaki gari lakini hakuna aliyeshuka.

Aliendelea kusimulia kisa mkasa mbele ya ‘kachero’ wa OFM kuwa uvumilivu ulimshinda, alihisi kuna linaloendelea ndani ya gari,  akaamua kulisogelea na ndipo hamadi! Akamkuta mumewe ‘laivu akiduu’ na mwanamke huyo na ndipo OFM walipochomoza baada ya kujulishwa kuwa ishu imetiki.
“Uzuri ni kwamba walisahau ‘kuloki’ milango ya gari ‘so’ nilipoushika ukafunguka,” alisema Mama P baada ya OFM kupiga picha za kutosha.
TIMBWILI
Katika tukio hilo kulitokea timbwili ambapo askari waliokuwa doria walitonywa na kufika eneo la tukio na kuamulia damu isimwagike.
Mwanamke aliyenaswa na mume wa mtu alikula mbata za kufa mtu huku mwanaume akitoka nduki kukwepa aibu ya kamera za OFM.

MAMA P HASIRA
OFM ilimsikia Mama P akisema: “Kumbe ndiyo wewe…nilikuwa nakufuatilia muda mrefu, badala ya kwenda kanisani unahangaika na waume za watu hata humuogopi Mungu.”

Hadi gazeti hili linaondoka eneo la tukio, wanawake hao walikuwa mikononi mwa polisi wakitakiwa kuacha ugomvi na kama kuna malalamiko wayafikishe kituoni.

KIDUME CHAOA WANAFUNZI WAWILI, MTU NA DADA YAKE

unnamed_4_1e2fa.jpg
Mkuu wa Dawati la Jinsia Nkasi, CPL-Anna Kisimba (kushoto) akipitia kitabu cha orodha ya matukio ya dawati hilo. Kulia ni msaidizi wake.
unnamed_5_5bb88.jpg
Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri wa Wilaya ya Nkasi, Oscar Mdenye
JESHI la Polisi Wilaya ya Nkasi kupitia dawati la Jinsia na Watoto, linamshikilia Pius Jacob Mkazi wa Kijiji cha Chala kwa kosa la kuoa mtu na dada yake, ambapo mdogo mtu alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kabwe wilayani Nkasi.
Jacob alikamatwa na Polisi wa Dawati la Jinsia na watoto Kituo cha Nkasi ikiwa ni wiki moja tangu amchukue kwa nguvu binti huyo wa darasa la tano (umri miaka 12) na kuja kuishi naye kama mke na mume huku akiwa tayari amemuoa binti mwingine wa kwanza mwenye umri wa miaka 16 ambaye pia ni dada wa binti wa pili.
Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Dawati la Jinsia Nkasi, CPL-Anna Kisimba alisema walimfuatilia Jacob na kumkamata baada ya wao kupewa taarifa na mmoja wa majirani wa mtuhumiwa kuwa alikuwa akiishi kinyumba na wanafunzi hao.(P.T)
"...Tulikuwa katika ziara zetu za kawaida zilizoambatana na siku 16 za kupinga ukatili tukizunguka baadhi ya vijiji vya wilaya yetu, ndipo raia wema walituarifu kuwepo kwa tukio hilo na kuanza kufuatilia hatimaye kumkamata mtuhumiwa," alisema Kisimba.
Tayari mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Desenba 10, 2013 kwa kosa la kumuoa mwanafunzi na kubaka katika Mahakama ya Wilaya ya Nkasi, Mkoa wa Rukwa kujibu mashtaka ya tuhuma zake.
Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri wa Wilaya ya Nkasi, Oscar Mdenye alisema baada ya kufuatilia zaidi wamebaini hata binti (16) aliyemuoa wa kwanza alikuwa ni mwanafunzi haijulikani alitumia mbinu gani za kumpata na kuanza kuishi naye kama mke na mume.
Aidha ameongeza kuwa kwa mujibu wa tarifa ambazo walizipata kutoka kwa majirani inadaiwa binti wa pili alimpata kwa kutumia nguvu na vitisho, kwani alimfuata nyumbani kwao na kudai anakuja kuwasalimia lakini baada ya kufika kwake alimjulisha binti huyo kuanzia sasa wewe ni mke wangu na kuanza kuishi naye.
"...Hadi Polisi na Ofisi ya Ustawi wa Jamii tunafikiwa na taarifa hizo inadaiwa mtuhumiwa huyu alikuwa tayari ameishi na binti huyu wa pili kwa wiki nzima nyumbani kwake, na majirani walijua baada ya binti wa pili (12) kuanza kulalamika kwao kuwa alikuwa amechukuliwa kwa nguvu na kulazimishwa kuolewa," alisema Mdenye.
Juhudi za kumpata mtuhumiwa kuzungumzia tuhuma zake hazikuweza kuzaa matunda baada ya kuwa mahabusu akisubiri mwenendo wa kesi yake inayomkabili.
Hata hivyo matukio ya ukatili yanayoripotiwa polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Nkasi yamekuwa yakipungua kutoka mwaka hadi mwaka, kwani kwa mujibu wa takwimu za dawati hilo kwa mwaka 2012 kulikuwa na kesi 224 za ukatili zilizoripotiwa, ilhali kwa mwaka 2013 jumla ya kesi 143 zimeripotiwa wilayani hapo.

PADRI MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUTOMTUNZA MTOTO ALIYEZAA NA MHUDUMU WA KANISA

Catholic-Church 75136
PADRE wa Kanisa Katoliki Singida mjini Deogratus Makuri amefikishwa mbele ya mahakama ya mwanzo Utemini mjini hapa akituhumiwa kushindwa kutunza mtoto wake wa kike.
Ilidaiwa mahakani hapo, kuwa Padre Makuri alikuwa na uhusiano wa kimapenzi wa muda mrefu na Maria Boniphance (26) mkazi wa Mitunduruni mjini hapa na mhudumu katika parokia ya Singida mjini.(HD)
Ilidaiwa mbele ya hakimu wa mahakama hiyo,Ferdnand Njau kuwa katika muda huo wa mahusiano ya kimapenzi ndipo mdaiwa Makuri alipompa ujauzito Maria.
Maria aliiambia mahakama hiyo kuwa mara tu alipopata ujauzito huo alilifikisha tukio hilo kwa wazazi wake.
Amesema wazazi wake walimwendea na bila kuuma ulimi alikubali kumpa uja uzito Maria na kuahidi kwa maandishi kuwa atamtunza mtoto wake (jina tunalo) hadi hapo atakapokuwa na uwezo wa kujitegemea.
Maria amesema Padre ambaye inadaiwa kwa sasa amesimamishwa wadhifa wake huo kutokana na tuhuma hiyo, alitekeleza ahadi yake hiyo kwa miezi michache na kisha kugoma kuendelea kutoa matunzo.
"Baada ya hapo nilimfikisha mbele ya ofisi ya ustawi wa jamii ambapo katika hati ya mkataba, aliahidi kuwa atakuwa anatoa kila mwezi shilingi 80,000/= na endapo atashindwa kutekeleza ahadi hiyo,aliomba afikishwe mahakamani mara moja",amesema.
Ilidaiwa kuwa pamoja na ahadi hiyo nzito,Padre Makuri alianza kudai kwamba mtoto huyo sio mtoto wake wa kuzaa na kisha kuacha kutoa matunzo kama alivyoahidi.
Katika hatua nyingine,Maria amesema walianza mapenzi siku Padre huyo kumpa kazi ya kufanya usafi kwenye kabati la vitabu chumbani kwakewakati akiendelea kufanya usafi alifungiwa kwa nje hadi hapo usiku aliporejea Padre akiwa na chakula cha jioni cha mhudumu Maria.
Amesema Padre alimwambia kwa vile umekuwa ni usiku alale humo ndani na Padre na kitendo hicho ndicho kilichoanzisha safari ya mahusiano yao ya kimapenzi na kupelekea wapate matunda ya kuwa na mtoto.
Habari zaidi kutoka kwenye parokia hiyo zinadai kuwa Padre Makuri alikuwa kwenye maandalizi ya kwenda kuongeza elimu nje ya nchi.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger