Consolata Edward ni mke wa mtu, mkazi wa Igoma jijini hapa ambaye amebaki na kipisi cha sikio baada ya kunyofolewa kiungo hicho kisa kikidaiwa kuwa ni hawara yake.
Tukio hilo lilitokea Desemba 16, mwaka jana ambapo mwanamke huyo alidai kuwa alikuwa akizungumza kwa simu na mfanyakazi mwenzake ambaye anauza naye chakula maeneo ya Mlango Mmoja jijini hapa kabla ya mumewe kumvamia na kumpiga.
Kwa huzuni, Consolatha aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa baada ya mumewe kumpiga yeye aliamua kupigana naye kisha kumchania ‘boksa’ na kusababisha viungo vyake vya uzazi kubaki wazi.
Alisema wakati timbwili likiendelea, ghafla alitokea mama mwenye nyumba akifuatana na mwanamke aliyemtaja kwa jina moja la Hawa na kumg’ata sikio lake hadi akalinyofoa na kulitema.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mume wa Consolatha aliyejitambulisha kwa jina moja la Athuman alidai kuwa siku ya tukio alimuona mkewe akiongea na simu usiku jambo ambalo halikuwa kawaida yake na alipomuuliza alikata simu na kwenda kuongelea nje ya nyumba.
Aliongeza kuwa, alimfuata nyumanyuma na kupata wasiwasi kutokana na mada zilizokuwa zikiongelewa ndipo alipomnasa kofi mkewe aliyekimbilia kumchania boksa yake.
Athuman alisema kuwa mama mwenye nyumba alipoona ugomvi huo unazidi ndipo alipowaita majirani walioingia wakiwa na huyo Hawa aliyedaiwa kumg’ata mkewe.
“Wakati mimi natafuta khanga ili nijistiri ndipo nilipoona mke wangu ameloa damu huku kipande cha sikio lake kikiwa chini kabla ya kuliwa na mbwa, sijui kwa nini Hawa aliingilia ugomvi wetu,” alisema Athuman huku kukiwa na madai Consolatha alikuwa akizungumza na mume wa Hawa.
Baadaye sakata hilo lilipelekwa kwa mwenyekiti wa mtaa na watu hao kutakiwa kuripotiwa Kituo cha Polisi cha Nyakato (Mwatex) ambapo jalada la kesi lilifunguliwa kwa NY/RB/8709/2013 KUPIGANA HADHARANI wakisubiri sheria kuchukua mkondo wake.
HABARI NA MATUKIO BOFYA HAPA
GPL