MWENYEKITI wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Freeman Mbowe amemkaribisha Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye kujiunga
na chama chake ili kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa.
Mbowe alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa sherehe za ufunguzi wa
jengo jipya la ibada zilizofanyika katika Kanisa la Kiinjili la
Kilutheli Usharika wa Lole Mwika na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali
wa serikali na kanisa ambapo Sumaye alikuwa mgeni rasmi.
Alisema hoja ya rushwa inayozungumzwa na Sumaye ambayo CHADEMA imekuwa
mstari wa mbele kuipiga vita ina msingi, hivyo viongozi wengine
wanapaswa kumuunga mkono na kuliomba kanisa lizidi kuwaombea viongozi wa
aina hiyo ili wazidi kupaza sauti zao bila hofu.
“Ndugu zangu hoja ya rushwa iliyozungumzwa mahali hapa na Sumaye ni hoja
ya msingi sana, haki katika taifa hili ni bidhaa adimu na wale
wanaotetea haki katika taifa hili wengine wanailipa kwa gharama ya
maisha yao,” alisema.
Alisisitiza kuwa ni vyema viongozi wakawa na mipaka ya vyama vyao vya
siasa na kuwa na lengo moja la kusimamia hatma ya taifa kwa kupigania
haki bila uwoga ili kuepusha mateso kwa wananchi.
“Viongozi wote kama tukaamua kusimamia hii hoja bila ya kuona huyu yuko
chama gani, yule yuko chama gani, tukafanya hili suala la rushwa ni la
taifa, basi tunaweza kupiga hatua, na kama hatutasahau mipaka ya vyama
vyetu hakika nchi hii bado wananchi wa kawaida wataendelea kuteseka
sana,” alisema.
Mbowe aliomba kanisa lisaidie katika suala hilo ili kuepusha taifa
kupasuka kutokana na viongozi kuweka itikadi mbele na kusahau kuwa siasa
ni masuala yanayopita.
Alisema hivi sasa vyama vya siasa vimetafsiriwa kama vyombo vya
kugombanisha watu, huku baadhi ya viongozi kwa makusudi wakisahau kuwa
vyama vya siasa ni vyombo vya uchaguzi vinavyotumika kupata viongozi.
“Tunauana kwa mabomu, tunauana kwa risasi, tunafungana kwa ajili ya
siasa, siasa ni kazi ya kupita, kama Mungu amemuandika mtu kuwa na
uongozi atapata uongozi bila ya kujali yuko chama gani, kwa hiyo niombe
kanisa lifanye suala la uchaguzi kuwa ajenda ya kudumu ya kanisa,”
alisema.
Akizungumzia mwaka mpya 2014, Mbowe alisema ni mwaka wa kutisha kwa watu
ambao wapo katika siasa adhimu (active politics) wanaoona namna siasa
zinavyobadilika na kuwa ni mambo ya kutishia uhai wa watu.
“Huu ni mwaka wa majaribu makubwa na tunaliomba kanisa lisikae mbali,
kanisa lina wajibu mkubwa wa kutusaidia wanasiasa maana tunapokuwa ndani
ya nyumba za ibada kama hizi kwa kiwango fulani tunaheshimiana,”
alisema.
Showing posts with label CCM. Show all posts
Showing posts with label CCM. Show all posts
WAUZA UNGA WATATU AMBAO NI WABUNGE KUPITIA CCM WAJISALIMISHA, SOMA ZAIDI
Katika mahojiano maalum na NIPASHE Mwenyekiti wa Kamati ya maadili na
haki za binadamu kwa jamii nje na ndani ya madhehebu ya dini, Mchungaji
wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste, William Mwamalanga, alitoa
taarifa hizo.
Alieleza kuwa wabunge hao (majina yanahifadhiwa) ni wa viti maalum kutoka mikoa ya Mbeya, Dar es Salaam na Mara.
Alisema mbali ya wabunge wamo viongozi wa dini na mfanyabiashara maarufu ambaye alikuwa akisafirisha mihadarati mkoani Mbeya.
Mchungaji huyo alisema kujisalimisha huko kunatokana na kamati hiyo
mwezi Oktoba mwaka huu kuwataka vinara 61 wakiwemo wabunge hao
kujisalimisha kwa ridhaa zao kwa Rais Jakaya Kikwete kama njia ya kutubu
makosa yao.
Kinyume na hapo kamati hiyo iliweka wazi uamuzi uliofikiwa kuwa ni
kuwapeleka watu hao katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) iliyoko
jijini Hague nchini Uholanzi ili sheria kuchukua mkondo wake.
Mchungaji Mwamalanga alisema kamati ilitoa muda wa miezi miwili ambayo inaisha mwezi huu.
Alisema kutokana na ukaidi huo majina ya watu 56 ya wale ambao
hawajajisalimisha ifikapo Januari 15 mwakani yatakabidhiwa rasmi kwenye
taasisi za kupambana na dawa za kulevya Umoja wa Mataifa ili wafikishwe
ICC.
“Novemba 15, mwaka huu tuliyaingiza majina 61 kwenye mtandao wa
taasisi hizo, baada ya hawa watano kuja kwetu, tulipeleka mrejesho kwa
taasisi hizi kuwa tumewatoa ingawa nao hawakuenda kwa Rais,” alisema na
kuongeza:
“Baada ya kuyaingiza majina haya kwenye taasisi hizi, uchunguzi wa
taasisi hizi ulibaini watu hawa ni kweli wanajihusisha na biashara hii,
sasa tunachofanya hivi sasa ni kuyakabidhi majina ya wale waliokaidi ili
hatua zaidi ziweze kuchuliwa,” alisema.
Alisema kwa sasa kamati ipo katika hatua ya mwisho ya kufanya kazi ya
kukusanya majina ya watu waliofariki kwa dawa za kulevya nchini kama
ushahidi kwenye kesi hiyo.
Alisema majina hayo wanayakusanya kupitia kwenye hospitali na kwa ndugu wa marehemu waliofariki kutokana na dawa ya kulevya.
Alitaja baadhi ya takwimu walizokusanya za vifo vya baadhi ya watu
waliofariki na dawa hizo kwenye mikoa na wilaya kuwa ni Mbeya 38,
Kinondoni 67, Dodoma 19, Tanga 41, Lindi saba.
Mchungaji Mwamalanga alisema baadhi ya takwimu hizo ni za mwaka mmoja na nyingine miaka mitatu iliyopita.
Aliongeza kuwa wanaendelea na zoezi la kukusanya takwimu hizo kwenye maeneo mengine.
Kuhusu wale waliojisalimisha kwao ambao gazeti hili inayo majina yao,
Mchungaji huyo alisema kamati imewawekea ulinzi wa siri wa kuifuatilia
mienendo yao ili kubaini kama wameacha au la kama walivyokiri kwao.
Mchungaji Mwamalanga, alisema moja ya masharti waliyotoa kwa watu hao
watano ni kutoa ushirikiano utakaowezesha kukamatwa wale wanaoendelea
na kuingiza au kusafirisha nje ya nchi dawa hizo.
Alisema tayari watu hao wameshatoa ushirikiano na kuwezesha kukamatwa
watu kadhaa waliokuwa wakisafirisha dawa hizo kwenda nchi nyingine
duniani.
Alisema watu hao waliwatajia mbinu ambazo hutumika kusafirisha dawa
hizo kuwa ni baadhi wamekuwa wakizihifadhi kwenye ‘uume bandia’ na
kwenye midoli.
“ Walitueleza kuwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki na zile za
Maziwa Makuu, wafanyabiashara wamebadilisha mbinu za usambazaji wa dawa
hizi ambapo njia hizo ndizo hutumika, ukimuona mwanamke kabeba mdoli
wengine huwa wamebeba dawa hizi,” alisema.
Pia alisema watu hao waliwaeleza mbinu nyingine ni dawa kusafirishwa
kupitia kwa baadhi ya wafadhili wanaoshughulika na mambo ya afya.
Mchungaji Mwamalanga amewaasa vinara hao kuzitumia sikukuu za mwisho
wa mwaka huu kujisalimisha wenyewe ili ifikapo mwakani taifa liache
kuzungumzia suala hilo.
“Tunawaomba wajisalimishe wenyewe, wanadhani sisi tunafanya mzaa
lakini tunawaambia kuwa, watekeleze yale tuliyowataka,” alisema.
Mkutano ambao uliibuka na maamuzi ya kuwafikisha vinara hao ICC
ulifanyika siku mbili kuanzia 21 Oktoba mwaka huu na kuhudhuriwa na
viongozi wa dini wa madhehebu ya Kiislam na Kikristo 134 kutoka Bara na
Visiwani.
CHANZO: NIPASHE
Wamejisalimisha kwenye tume ya kidini iliyoundwa baada ya kuambiwa
watapelekwa ICC The Hague. Hawajatajwa kwa majina lakini wote ni wabunge
wa viti maalum kutoka CCM mikoa ya Mbeya, Dar es Salaam na Mara.
MWENYEKITI WA CCM AJIUNGA NA CHADEMA, MCHKI HAPA
YALIYOJIRI KWENYE MKUTANO WA CHADEMA KIBONDO, KIGOMA
Askari
wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kwa kushirikiana na wananchi,
wakimdhibiti mmoja wa vijana waliofanya fujo katika mkutano wa hadhara
wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.
Willibrod Slaa, uliofanyika katika kijiji cha Mabamba wilayani Kibondo
mkoani Kigoma. (Picha na Joseph Senga)
Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod
Slaa, akipokea kadi ya uanachama, kutoka kwa liyekuwa Mwenyekiti
Kitongoji cha Mtaa wa Shule katika Kijiji cha Mabamba kupitia CCM,
Sevelino Damian, ambaye amehemia Chadema, wakati wa mktano wa hadhara
uliofanyika kijijini hapo.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod
Slaa, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Community
Center mjini Kibondo.
CHADEMA YAIONA CUF NI KIBARAKA WA CCM, SOMA KUJUA UKWELI
BAADHI ya wafuasi cha Chadema, jana nusura waanzishe fujo kwenye mdahalo wa kujadili demokrasia na migogoro ndani ya vyama vya siasa, baada ya mmoja wa washiriki kutamka kuwa, CCM itaendelea kuongoza nchi endapo vyama vya upinzani vitaendelea kuwa na migogoro hivyo kuzidi kividhoofisha.
Kauli hiyo, licha ya kutaka kusababisha fujo, iliwafanya baadhi ya wafuasi wa Chadema kutoka nje ya ukumbi.
Rehema Mwenda wa Chama cha Wananchi (CUF), ndiye aliyepasua ukweli huo uliowakera baadhi ya wafuasi wa vyama vya upinzani, baada ya kusisitiza migogoro katika vyama haina faida zaidi ya kuvidhoofisha, huku CCM ikizidi kujipanga na kuonya kuwa, migogoro ikiendekezwa ni sawa na kuipa CCM fursa ya kuendelea kuongoza nchi.
Katika mdahalo huo ulifanyika jijini Mwanza ilizuka sintofahamu wakati mtoa mada ya “Hali ya Siasa - Tulikotoka, Tulipo na Tuendako”, Habibu Change alipokuwa akiwasilisha mada yake na kudai kuwa ndani ya Chadema kuna mgogoro, kauli iliyopingwa na Wana-Chadema na wengine kutoka nje kabisa ya ukumbi wa mjadala.
Akichangia katika mdahalo huo, Shaban Ironga alisema migogoro ndani ya vyama vya siasa imekuwa ikidumaza demokrasia ya kweli na mawazo ya kweli kutokana na maamuzi ya wachache na faida ya wachache.
“Demokrasia ya kweli hujengwa na wanachama kuanzia ngazi ya chini na kwamba wapo waliogombana na kupoteza ndugu zao kutokana na vyama hivi lakini leo wanaonekana sio watu ndani ya vyama kutokana na ubinafsi na maamuzi ya wachache,” alisema.
Aidha Ironga aliwataka wanachama wa vyama vya siasa vya upinzani kuamka na kuacha kutumika na viongozi kwa ajili ya maslahi yao kwani wamekuwa wakipoteza nguvu zao huku wanzao wakiendelea kunufaika.
Awali akitoa mada ya kwanza ya demokrasia na migogoro ndani ya vyama vya siasa, Jimmy Luhende alisema hakuna siasa ya kupendana kwenye mapambano na kwamba wakitokea marafiki ujue wanaanza kupotosha jitihada za mapambano.
Mdahalo uliokuwa ukijadili migogoro ndani ya vyama vya siasa inakuza demokraia au la, uliandaliwa na Asasi ya Jitambue Foundation ambapo walilazimika kuita mabaunsa ili kudhibiti vurugu zilizotaka kujitokeza.
-Habari Leo
-Habari Leo
JANUARI MAKAMBA AELEZA KWA NINI ANAWEZA KUGOMBEA URAISI 2015, SOMA HAPA UJUE SABABU
NAIBU waziri
wa Wizara ya Mawasiliano sayansi na teknolojia, January Makamba, ambaye pia ni Munge wa Jimbo la Bumbuli, ametumia
dakika 17 kueleza kwanini anaweza kuwania nafasi ya Urais mwaka 2015 kupitia
Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Alitumia
muda huo baada ya mmoja wa waadhiri wa vyuo na vyuo vikuu mkoani Mbeya kutaka
kujua uhalisia wa uvumi kuwa yeye ni miongozi mwa vijana wa CCM ambao wanatajwa
kuwa watawania nafasi hiyo.
Makamba
alisema kuwa, makundi ya watu wa rika mbalimbali wameendelea kumshawishi
kuwania nafasi hiyo mwaka 2015 na kumtaka atafakari na kuchukua hatua.
Alisema kuwania
nafasi hiyo ni jambo kubwa sana hasa wakati huu ambao yeye anakerwa na matumizi
ya fedha yenye lengo la kupata uongozi.
‘’Nakerwa
sana na matumizi ya fedha kutafuta uongozi jambo ambalo linawanyima fursa watu
wenye vipawa vya uongozi kutuongoza, mimi sina hela, lakini kadri siku
zinavyozidi kwenda watu wanazidi kunifuata’’alisema Makamba.
Alisema
kabla hajachukua hatua ya kutamka kuwa atagombea, anaendelea kutafakari kama
kazi yenyewe ataiweza au la kwasababu kazi ya kuwa Rais si kazi yeye na familia
yake bali ni ya kuwatumikia watanzania.
‘’Natafakari
kuwa je! Ninaweza kuungwa mkono na watu wote Tanzania? Isije ikawa ni kikundi
cha ndugu au marafiki pekee ndiyo wanakuunga mkono, Urais siyo wa Bumbuli tu’’
alisema Makamba.
Aliongeza
kuwa tafakuri yake ni kwamba akijiridhisha kuwa atapata wapi fedha za kuendeshea
nchi katika utawala bora, elimu na mambo mengine, atatamka rasmi kuwa anagombea
nafasi hiyo kubwa na ya heshima.
‘’Ni rahisi
kusema kuwa unataka kugombea, lakini ni lazima ujiulize maswali kadhaa yakiwemo
kuwa je unaweza kuwaridhisha watanzania kimwili, kiakiri, kifikra na kuwa na
fikra za kubadili nchi kuwa kwanini tumeshindwa mahala fulani na tunawezaje
kuziba mapengo hayo. Hivyo mimi bado natafakari’’ alisema Naibu Waziri huyo.
Katika
kongamano hilo lililolenga kuwakaribisha wanafunzi ambao ni wanaCCM wa mwaka wa
kwanza katika vyuo hivyo, Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary
Mwanjelwa alitoa mada ya asilimia hamsini kwa hamsini ya uogozi kwa wanawake.
Alisema ili
kufikia kiwango hicho cha Hamsini kwa hamsini, ni lazima wanawake waache
kuchukiana na jamii iwape nafasi wanawake katika nafasi za kiungozi.
‘’Wanawake
ndiyo wapiga kura wakubwa na Tanzania takwimu zinaonesha kuwa wanawake ni
asilimia 52, lakini wanawake tuna tatizo la kutoungana mkono na kuchukiana’’
alisema Dr. Mwanjelwa.
Mkuu wa
wilaya ya Mbeya, Dr. Norman Sigalla, alitoa mada ya ukosefu wa ajira kwa wasomi
ambapo alisema kuwa wasomi wengi hawafanikiwi kwasababu wanachagua kazi za
kufanya.
‘’Hakuna
serikali yeyote duniani ambayo inaajiri wasomi wake wote, na ukiangalia
wafanyabiashara wakubwa zaidi ya asilimia 86 hawana elimu ya kidato cha sita
ama shahada’’ alisema Dr. Sigalla.
KATIBU WA CHADEMA AVUA MAGWANDA YA CHADEMA NA KUVALISHWA MAVAZI YA CCM MBELE YA WANANCHI, NI IMETOKEA CHUNYA MKOANI MBEYA
Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Bryson
Mwasimba akionbyesha kadi yake ya chama hicho, kabla ya kumkabishi
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto), alipotangaza kuhamia
CCM, leo jioni katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Kata
ya Lupa, wilayani humo.
Bryson Mwasimba kutoka Chadema akikabishi kadi yake kwa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
"Sasa Nataka kuungama dhambi nilizowafanyia ndugu zanguni wakati nikiwa Chadema, Niliwadanganya mengi nanyi mkaniamini. Sasa naungama kwenu mnisamehe, Lakini mjue kwamba wenye lawama kubwa ni Chadema kwa sera zao za kuhimiza wanachama na viongozi wake kuwa waongo. Sasa kabla sijaendelea kusema yaliyo safi naomba kwanza nilivue gwanda hili la Chadema maana linaninajisi", alisema Bryson, akiwa jukwaani baada ya kutangaza kuhamia CCM kwenye mkutano huo.
"Sasa ngoja nilivulie mbali hili kwanda nibaki huru", akasema Bryson wakati akilivua gwanga lake la Chadema, huku akiwa ameshikilia mdomoni kadi yake mpya ya CCM aliyokabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kushoto).
Baada ya kulkivua gwanda, Bryson akavaa shati la kijani la CCM.
Kisha akazungumza ya moyoni, huku akimtwisha mzigo wa Lawama Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, kwamba amekuwa akimtumbukiza kwenye madeni mbalimbali kwa kutumia huduma kisha kusepa bila kulipa. Wakati akisema hayo Nape alikuwa upande wa kulia akimtazama na kumsikiliza kwa makini sana
Ikawa nderemo na hoi hoi Bryson akabebwa na wana CCM kwa furaha
KABLA YA HAPO KINANA ALIKAGUA UJENZI BARABARA YA CHUNYA HADI TABORA INAYOJENGWA NA KAMPUNI YA CCCC YA CHINA
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na wasaidizi wake, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakikagua sehemu ya ujenzi wa barabara inayoenda hadi Tabora, unaofanywa na Kampuni ya Kichina ya CCCC, wakati Kinana na msafara wake walipokuwa wakipita katika eneo hilo, akiwa njiani kwenda wilayani Chunya, leo
Baadhi ya maeneo yanajengwa kwa uhodari mkubwa kiasi kwamba kupita ni lazima kuruka, Hapa Katibu wa NEC, Itukadi na Uenezi akiruka kutoka upande mmoja kwenda mwingine wa eneo hilo linalojengwa.Nyuma yake ni Kinana ambaye naye alimfuata Nape pia kwa kuruka eneo hilo
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiruka eneo hilo
Kazi ya kuopasuka milima na kuweka sawa inapopita barabara hiyo, ikiendelea
MIKUTANO NA SHUGHULI NYINGINE ZA KINANA WILAYANI CHUNYA
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itukadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwaslimia wananchi, baada ya msafara wa Kinana kuwasili wilayani Chunya
Kinana akiwasalimia wananchi baada ya kusimamia msafara wake akiwa njiani kwenda Chunya
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua shina la wakereketwa wajasiriamali wa CCM katika kituo cha mabasi mjini Chunya.
Kisha akakabidhi kazi za CCM kwa wanachama wapya 100 kwenye shina hilo
Kinana akihutubia baada ya kizindua shina hilo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsikiliza Kijana, Frank Mwapololo, ambaye ni mmoja wa wachimbaji wadogo katika machimbo ya mafunzo kwa ajili ya wachimbaji wadogo, yaliyopo Chunya, alipozungumza na wajasiriamali wa mradi huo, Nov 30, 2013, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia sahihi ya kuzitatua, mkoani Mbeya.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (wapili kulia) akimrekebishia sawasawa vazi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, baada ya wazee wa Kata ya Lupa, wilayani Chunya, kumvalisha vazi la wazee wa Kata hiyo, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia sahihi ya kuzitatua, mkoani Mbeya
Katibu Mkuu wa CCM akiwahutubia wananchi wa Kata ya Lupa,

LEMA AISHANGAA CCM KUKITAKIA MAMBO MEMA CHAMA CHAKE
Godbless Lema
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), ameeleza kushangazwa
na jitihada za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutaka Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Zitto Kabwe asichukuliwe hatua zaidi kwa madai ya kukinusuru
chama kisisambaratike.
Lema alitoa kauli hiyo juzi wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kilombero.
Alisema kuwa CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani kinachowanyima CCM
usingizi, walipaswa kufurahia kusambaratika kwao, lakini cha kushangaza
viongozi wa chama tawala wamekuwa wakiwaasa wasimfukuze Zitto.
“Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba, Katibu wa Itikadi
na Uenezi, Nape Nnauye wanalia wakitaka tupatane. Mbunge wao wa Kigoma
Mjini, Peter Serukamba naye analia kuwa CHADEMA tumefanya vibaya,
tumrudishe Zitto.
“Sisi tunawauliza tukifanya vibaya ni faida kwao, kwanini wanalia.
CCM wanalalamika CHADEMA hatuna demokrasia, ni chama cha kibabe,
tumemwonea Zitto, kwamba tutapasuka. Hivi tukipasuka wao wataimarika sasa
wanalia nini badala ya kufurahi?” alihoji Lema.
Naye Mwenyekiti wa madiwani wa Jiji la Arusha, Doita Isaya alikemea
tabia ya baadhi ya walimu kuacha kufundisha ipasavyo muda wa kazi ili
baadaye wafanye hivyo kwenye masomo ya ziada ya kujiingizia kipato.
Mwenyekiti wa Wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro alisema kipaumbele cha
kwanza cha CHADEMA ni elimu, ndiyo sababu kwa kipindi cha miaka mitatu
walichoongoza halmashauri wameisimamia ipasavyo na kuhakikisha madarasa
51 yanajengwa.
SAKATA LA KUBAKA: KAPUYA AACHIWA MANYOYA NA CHAMA CHAKE
Chama Cha Mapinduzi (CCM) nacho kimeibuka na kueleza kushangazwa na kitendo cha mbunge huyo kuikana namba yake ya simu 0784 993 930 wakati ipo hata kwenye kitabu cha wageni cha chama hicho alichokisaini mwenyewe mkoani Dodoma.
Prof. Kapuya ambaye amewahi kushika nyadhifa kadhaa za uwaziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu na Nne, tayari amefunguliwa jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, tangu Novemba 24 mwaka huu.
Jalada hilo lilifunguliwa na mwanafunzi huyo anayedaiwa kubakwa na kutishiwa kuuawa, lakini Jeshi la Polisi limekuwa likishughulikia suala hilo katika namna ya kumlinda mtuhumiwa.
Siku moja baada ya jalada hilo kufunguliwa, Kapuya alidaiwa kutimkia nchini Sweden, lakini taarifa za uhakika zinasema kuwa alirejea nchini Alhamisi na amekuwa akiishi kwa kujificha huku polisi wakidai kuendelea kumsaka.
Ni katika danadana hizo, uongozi wa Bunge umesisitiza kuwa suala hilo ni jinai na linapaswa liende katika mkondo wa kisheria.
Akizungumza na gazeti hili wiki hii, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alikiri kulifahamu jambo hilo akisema kuwa walipomsikiliza mtoto huyo waliona ni suala ambalo linahitaji kushughulikiwa kisheria kwa kuwa ni jinai.
“Suala la binti huyo lilifikishwa kwangu kupitia msaidizi wangu ambaye alisikiliza hoja na rai yake na kushauriwa kuwa hilo ni suala la jinai na linapaswa liende katika mkondo huo.
“Hata hivyo, binti huyo alitambulishwa kwa spika kama kiongozi wa wabunge na kuelekeza kuwa tumshauri alifikishe katika mamlaka husika,” alisema Dk. Kashililah.
Chanzo chetu cha habari kilithibitisha kuwa binti huyo alikutana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Oysterbay (OCD) na OC-CID wake na kutoa maelezo ya awali kabla ya viongozi hao kumruhusu ayaweke malalamiko yake katika maandishi kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alikiri polisi kufungua jalada hilo na kuongeza kwamba hivi sasa wanafanya uchunguzi kubaini kama ujumbe ulio katika simu ya binti anayedai kubakwa na kutishiwa maisha unatoka katika simu ya mbunge huyo.
Lakini tangu kufunguliwa kwa jalada hilo, mtuhumiwa huyo ameendelea kubaki uraiani bila kuhojiwa, huku akiendelea kuwapa vitisho watoto hao, kusafiri nje ya nchi na kurejea kupitia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere bila kukamatwa.
Awali Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema hawana shamba mjini, kazi yao ni kukamata wahalifu na kuwa wangemsaka popote mtuhumiwa huyo ikiwa taarifa itafikishwa rasmi polisi.
Kwa siku tatu sasa jeshi hilo limekuwa likitupiana mpira kuhusu kumkamata na kumhoji mtuhumiwa huyo.
Wakati Kamanda Wambura akijitetea kuwa yuko mkoani Arusha, Kamishna Kova naye anadaiwa yupo nchini China, huku Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini, Isaya Mungulu akisema hadi jana alikuwa hana taarifa, hivyo kuomba muda zaidi ili leo aweze kutolea ufafanuzi.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Mungulu alikuwa na taarifa tangu Kapuya anarejea nchini akitokea nje kwa ndege ya Shirika la Qatar ingawa yeye hakuwa tayari kufafanua suala hilo.
CCM wamuumbua
Kada wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Dodoma ambaye aliomba kuhifadhiwa jina, amemuumbua Prof. Kapuya akisema namba ya simu aliyoikana na kudai kuwa alishaigawa miezi sita iliyopita ndiyo hiyo aliiandika mwenyewe kwenye kitabu cha wageni.
Akiwa mjini Dodoma kama kamanda wa UVCCM, Kapuya alitembelea tawi moja na kusaini kitabu cha wageni ambapo mwisho wa saini yake aliandika namba hiyo ya simu ambayo pia imeandikwa kwenye kitabu cha orodha ya wabunge.
Kada huyo alisema kuwa alishitushwa kusikia Prof. Kapuya anaikana namba 0784 993 930 ambayo imekuwa ikiandikwa na gazeti hili kuwa ndiyo imekuwa ikitumika kutuma ujumbe wa vitisho kwa binti anayedaiwa kumbaka.
Alisema kuwa anampa ushauri wa bure Prof. Kapuya asijaribu kujiaibisha kwa kuikana namba hiyo kwa sababu hata kwenye moja ya vitabu vya wageni aliiandika na kusaini kwa mkono wake.
“25.6.2013 Alhaj Prof. Juma Athuman Kapuya, Mbunge wa Urambo Magharibi, Mjumbe wa NEC-CCM Taifa, Kamanda wa UVCCM (M) Tabora, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Juhudi zako zibarikiwe na Mungu 0784993930 CCM Oyee,” aliandika Kapuya katika kitabu kile.
MSAFARA WA MWENYEKITI UVCCM WAZUIWA KWA WAWEKEWA MAGOGO HUKO MKOANI PWANI
Polisi
mkoani Pwani inachunguza kundi la watu linalodaiwa kuweka magogo
barabarani kuzuia msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM
(UVCCM) taifa, Sadifa Juma Khamis (MB) katika eneo la Tondoroni,
wilayani Kisarawe, mkoani humo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, alisema atazungumzia suala hilo baada ya kupata taarifa kamili.
Kwa
mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kundi hilo liliweka magogo
hayo jana usiku katika barabara ya kati ya eneo la Mpuyani katika njia
panda ya barabara iendayo vijijini kuingia barabara kuu ya Morogoro.
Mashuhuda
wa tukio hilo walisema katika nyakati tofauti kundi hilo lilianza
kuzuia msafara huo kwa kutaka kushinikiza dai la mgogoro wa mipaka kati
ya eneo la Jeshi la Wananchi wa Ulinzi Tanzania (JWTZ) na makazi ya watu
katika eneo la Tondoroni, wilayani humo.
Watu
hao ambao idadi yao haikuweza kufahamika walidaiwa kutishia kuchoma
moto magari ya msafara huo wa mwenyekiti wakati alipotaka kushuka na
kuzungumza nao na kuamua kujisalimisha kwa kuingia ndani ya gari na
kurudi Kisarawe.
Mwenyekiti
huyo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Donge, Tanzania Visiwani mapema
akiwahutubia wananchi wa Kisarawe aliwataka kudumisha amani kwa
kukiweka Chama Cha Mapinduzi madarakani. “Amani ikivurugika hakuna
atakayekuwa salama, hata askari nao hawatokuwa salama”.
Akiongea
na viongozi wa CCM na UVCCM katika jengo la ofisi za CCM wilaya,
aliwataka wanachama hao kuvunja makundi ya kampeni kwa kuwa hayana tija
kwa sasa, isipokuwa wakati wa kampeni za uchaguzi.
Alisema kuwa Muungano wa Tanzania ni muhimu hivyo changamoto zilizomo ndani yake zitafutiwe muafaka kwa njia ya amani.
Alisema
kuna baadhi ya watu wakorofi ambao wanadai muungano uvunjwe hasa
kutoka Pemba wakidai kuwa kisiwa hicho ni chao wakati visiwa hivyo vya
Pemba na Zanzibar havina wenyewe na watu walioko huko wametokana na
biashara ya utumwa na wengi wao walitoka upande wa Tanzania Bara wa
makabila mbalimbali.
Wakati huo huo, mwenyekiti huyo alimsimika mwandishi wa siku nyingi,
Abubakar Mlawa kuwa kamanda wa UVCCM wilayani humo na wengine 15
wakiwamo madiwani kuwa makamanda wa UVCCM wa kata zao.
CHANZO: NIPASHE
KATIBU MWENEZI WA CHADEMA AKATAA KUNUNULIWA NA ILI AJIUNGE NA CCM, ASEMA YEYE NI CHADEMA DAMU, WANACHAMA WENGINE WANUNULIWA KWA 300,000/=
KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Adam Ngalawa, juzi alipatwa na fedheha kubwa baada ya Katibu Mwenezi wa CHADEMA, Tawi la Bulyanhulu, Kata ya Kakola, Philemon James, kukataa hadharani mpango wa kununuliwa ili ajiunge na chama hicho.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu jana, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Bulyanhulu, Emmanuel Gombega, alisema mkakati wa viongozi wa CCM katika eneo hilo kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa, kuwashawishi wanachama wa CHADEMA kwa fedha ulianza muda mrefu katika eneo hilo.
Alisema kuwa wiki moja iliyopita walifanikiwa kumshawishi James na mwanachama mwingine wa CHADEMA kwa kuwapatia kiasi cha sh 300,000 kwa lengo la kuangamiza nguvu za chama hicho cha upinzani katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa Gombega, baada ya viongozi hao kukubaliana na James, waliandaa mkutano wa hadhara na kumualika Katibu wa CCM mkoa kwa ajili ya kumpokea mwanachama huyo wa CHADEMA mwenye na nguvu za ushawishi kwa wananchi wa Bulyanhulu.
“Kila hatua waliyokuwa wakifanya, James alikuwa anafikisha taarifa kwa uongozi wa CHADEMA, tukamueleza sasa ni wakati wa kula fedha zao na kuwakataa hadharani,” alisema Gombeza.
Aliongeza kuwa kabla ya mkutano uliohutubiwa na Ngalawa, walifanya kazi ya kuwashawishi wananchi wahudhurie kwa wingi wakijua kitakachotokea.
Baada ya katibu huyo wa mkoa kumaliza kuhutubia, mshereheshaji katika mkutano huo alimuita James jukwaani kwa lengo la kurudisha kadi ya CHADEMA na kukabidhiwa ya CCM.
James alipanda jukwani na wafuasi na viongozi wa CCM kumvisha shati pamoja na khanga za chama chao.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo wa CHADEMA, baada ya James kuvishwa vitu hivyo, aliwaomba viongozi walio jukwaani wampatie kipaza sauti na watulie kumsikiliza.
Ndipo akawaeleza kuwa suala la kuwa katika chama chochote ni hiyari ya mtu na siyo ushawishi wa fedha.
“Baada ya kuwaeleza hivyo, akavua zile sare na kuwaambia hawezi kuondoka CHADEMA na kusaliti mageuzi, hali iliyomfanya Mwenyekiti wa CCM wa tawi aanguke chini kwa kuchanganyikiwa huku katibu wa mkoa, akilaumu kwa namna viongozi wake walivyoandaa mkutano wa kumfedhehesha,” alisema.
Tanzania Daima iliwasiliana na Ngalawa kuthibitisha tukio hilo la chama chake kuwanunua wapinzani, ambapo alikiri kufanya mkutano wa hadhara katika eneo.
Pia alikiri James kupanda jukwaani huku akikanusha kuwapo kwa mkakati wa kuwanunua wanachama wa vyama vingine wajiunge na CCM.
“Ni kweli nilikuwa Kakola na mmoja wa wananchi aliomba kipaza sauti akauliza maswali, lakini hakuna mtu aliyeshawishi kuwanunua wanachama wa vyama vingine, na hata huyo unayemsema hana hadhi ya kununuliwa,” alisema Ngalawa.
Alipoulizwa sifa za wanachama wa vyama vingine wanaopaswa kununuliwa, Ngalawa alisema CCM hakina utaratibu wa kuwanunua wananchi.
CHADEMA YAISHINDA CCM KWENYE UCHAGUZI WA UNAIBU MEYA ARUSHA
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeibuka kidedea katika
uchaguzi wa Naibu Meya wa Jiji la Arusha, huku kikisisitiza msimamo
wake wa kutomtambua Meya wa jiji hilo, Gaudency Lyimo (CCM).
Ushindi wa CHADEMA ulikuwa wa mteremko baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuacha kuweka mgombea huku mgombea wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Michael Kivuyo naye akijitoa siku moja kabla ya uchaguzi.
Hata hivyo, mshindi wa kiti hicho, Diwani wa Kata ya Daraja Mbili, Prosper Msofe, aliibua mzozo kwa madiwani wa CCM baada ya kutangaza msimamo huo wa CHADEMA kutomtambua meya.
Uchaguzi huo ulifanyika jana wakati wa kikao cha mwisho wa mwaka cha Baraza la Madiwani ambapo kulitanda ulinzi mkali wa polisi waliovalia kiraia, Usalama wa Taifa na wale wa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Kufanyika kwa uchaguzi huo, kumekata kiu ya wananchi wengi wa jiji hili, hasa kwa kuzingatia kwamba nafasi hiyo imekuwa wazi tangu Desemba 2010 baada ya uchaguzi uliofanyika awali kwa kumweka madarakani Lyimo, kudaiwa kuwa haukukidhi vigezo kisheria.
Hatua hiyo, ilimlazimu naibu meya aliyekuwa amechaguliwa kushika nafasi hiyo, Kivuyo (TLP) kujiuzulu.
Katika uchaguzi huo wa jana, Msofe aliibuka mshindi baada ya kupata kura 25 za ndiyo na mbili za hapana huku moja ikiharibika hali inayodhihirisha wazi kuwa madiwani wa CCM pamoja na wabunge wao nao walimchagua.
Habari toka ndani ya kikao hicho, zinadai kuwa mara baada ya Msofe kutangazwa kuwa naibu meya, alimweleza meya kuwa hamtambui kwani taratibu zilizotumika kumweka kwenye kiti hicho hazikuwa halali.
Akizungumza na Tanzania Daima nje ya kikao, Meya Lyimo alikiri kutolewa kwa kauli hiyo huku akidai kuwa inashangaza kwani yeye ndiye aliyesimamia uchaguzi uliomweka naibu meya huyo madarakani sasa inakuwaje asimtambue.
Alisema kuwa hakuna uchaguzi mwingine wa meya kwa sasa kwani sheria iko wazi kuwa uchaguzi hufanyika kila baada ya miaka mitano wanapochaguliwa madiwani wengine.
Katika uchaguzi wa kamati za kudumu za Mipango Miji, Mazingira na Ujenzi, Diwani wa Moshono, Paul Matthysen (CCM) aliibuka mshindi kwa kupata kura 11 dhidi ya moja aliyopata Diwani wa Elerai, Injinia,Jeremiah Mpinga ambapo kamati hiyo inaundwa na madiwani watano wa CHADEMA na sita wa CCM.
Uenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya ulichukuliwa na Diwani wa Ngarenaro, Doita Isaya (CHADEMA) aliyepata kura tisa dhidi ya mbili alizopata Diwani wa Kata ya Engutoto, Elibariki Marlley (CHADEMA).
Wakizungumza na waandishi wa habari, Matthysen aliahidi kusimamia shughuli za kamati hiyo ipasavyo kwa kuhakikisha watendaji wanazingatia sheria kwa kuhakikisha hakuna ujenzi holela utakaoendelea kwenye Jiji la Arusha wala biashara zinazofanyika pembezoni mwa barabara za waenda kwa miguu na magari.
Naye Isaya aliahidi kufanya kazi kwa karibu na wanakamati wenzake pamoja na wakuu wa shule ili kuhakikisha watoto wanapatiwa elimu bora sanjari na kuwapunguzia wazazi mzigo wa michango mingi isiyo na tija.
Wakati huohuo, CHADEMA kimedai kuwa CCM haikusimamisha mgombea kwenye nafasi ya naibu meya kwa kuhofia kushindwa kutokana na kuwa na idadi ndogo ya madiwani.
CHADEMA walikuwa 15 huku wale wa CCM wakiwa 13 kutokana na mbunge wa viti maalumu, Namelock Sokoine kutohodhuria.

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA ASHIRIKI UJENZI WA NYUMBA ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MCHOTEKA KATIKA ZIARA YA CCM WILAYA YA TUNDUMA MKOANI RUVUMA.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa moja ya nyumba za walimu wa shule ya Sekondari Mchoteka,wilayani Tunduru.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa kata ya Mbesa ,kijiji cha Mbesa wilayani Tunduru ,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya mkoa wa Ruvuma ambayo ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk Asha-Rose Migiro kujenga daraja la mto Munjapu wilayani Tunduru.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyeshwa jinsi barabara itakavyokuwa baada ya kukamilika kwa daraja la mto Munjapu,lililopo kijiji cha Mnemasi, Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha chama,kusimamia ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 katika mkoa wa Ruvuma akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa kwenye kijiji cha Mchoteka kwa staili ya aina yake ya kukimbia mchaka mchaka mapaka kwenye miradi ya ujenzi wa madarasa,maabara na nyumba za walimu katika shule ya Sekondari ya Mchoteka wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akishiriki uchimbaji wa msingi wa vyumba vya maabara ya shule ya sekondari Mchoteka wilayani Tunduru.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na umati wa wananchi wa kijiji cha Mchoteka wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Mchoteka waliofurika kutaka kumsikiliza, Katibu Mkuu alikuwa na ratiba ya kuonana na kumsalimia balozi wa nyumba kumi lakini kwa namna wananchi walivyojaa ilibidi ahutubie wananchi kwanza kabla ya kuonana na Balozi wa nyumba kumi.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa KImataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mchoteka wilayani Tunduru.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mchoteka waliojitokeza kwa wingi kuja kuwapokea viongozi wao wa kitaifa.
Babu Akuilaya (Babu Mkuu) kama heshima aliyopewa na Machifu wa Mchoteka,Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na wananchi wa kijiji cha Mchoteka na kuwashukuru kwa heshima waliyompa.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa CCM ambapo zaidi ya wanachama 100 wamejiunga na CCM katika kata ya Mchoteka.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata mapokezi mazuri wakati akiwasili katika kata ya Nalasi,kijiji cha Nalasi wilaya ya Tunduru.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiimba na akina mama wakazi wa kata ya Nalasi waliojitokeza kwa wingi kuupokea ugeni .
Umati wa wakazi wa Kijiji cha Nalasi ukiwa umejaa kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara katika mkoa wa Ruvuma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Nalasi, wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma ambao walijitokeza kwa wingi kumsikiliza .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Mkina kijiji cha Mkina ,wilya ya Tunduru mkoa wa Ruvuma.
Baadhi ya wananchi wakisikiliza hotuba za viongozi wao wa CCM Taifa wakiwa juu ya miti.
Sehemu ya wakazi wa kata ya Mkina wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya mikoa ya Ruvuma na Mbeya.Wananchi hao wamemueleza Katibu Mkuu wa CCM kuwa hawapo tayari kuuza korosho kwa mkopo,pia hawapo tayari kupangiwa bei na wanunuzi, wananchi hao waliitupia lawama bodi ya korosho pamoja na vyama vya ushirikia kwani vimeonekana havina msaada kwa wakulima.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mkina wilayani Tunduru mkoani Ruvuma ,Katibu Mkuu aliahidi kushirikiana nao katika kuhakikisha tatizo la zao la Korosho linapatiwa ufumbuzi kwani ni zao pekee linaloweza kuinua uchumi wa eneo hilo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha moja ya leseni za dereva wa Boda Boda ambazo zilitolewa baada ya madereva hao kupata mafunzo ya kuendesha na ya usalama barabarani yaliosimamiwa na mbunge wa Tunduru Kusini Mtutura Abdallah Mtutura.
Subscribe to:
Posts (Atom)