Search in This Blog

Showing posts with label MASOGANGE. Show all posts
Showing posts with label MASOGANGE. Show all posts

UWOYA NA MASOGANGE WANAISHI PAMOJA SOUTH, JE KUNANII?


Hili ni swala la kujiuliza...ingawa hadi sasa Uwoya hajasema chochote...Lakini Masogange kupitia ukurasa wake wa INSTAGRAM amekuwa akiweka picha kadhaa za Irene Uwoya wakiwa pamoja huko SAUZI....Sasa katika kumaliza zaidi jana ameka video Irene akiwa anapika....HEHEHEHE

PICHA ZA AGNES MASOGANGE AKIWA NA NJEMBA YAKE KUTOKA SOUTH AFRIKA

MASOGANGE ASEMA ANAOGOPA KAMA UKOMA MUME WA MTU

VIDEO Queen mwenye figa matata Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange’ amesema anaogopa kama ukoma kutembea na mume wa mtu kama wafanyavyo baadhi ya watu.
 
Agnes Jerald ‘Masogange’.
Akizungumza na paparazi wetu, Agnes ambaye hivi sasa amejiingiza kwenye soko la filamu, alisema anaogopa sana kuingia kwenye uhusiano na mume wa mtu ndiyo maana anaona bora aendelee na mpenzi wake wa siku zote kuepuka uhasama.
 
“Sina tabia ya kushobokea kabisa waume za watu,  bora niendelee na mtu wangu wa siku zote na kama tukishindwana basi bora nitafute mwingine lakini awe wangu peke yangu,” alisema Masogange.

MASOGANGE AJIANDAA KWA AJILI YA VIDEO YA TUNDAMAN KWA KUKATA MAUNO OVYOOVYO



Video Queen Agnes Jerald ‘Masogange’akikata mauno.
Stori: Imelda Mtema BAADA ya kujificha muda mrefu tangu atoke mahabusu nchini Afrika Kusini kwa msala wa madawa ya kulevya, Video Queen Agnes Jerald ‘Masogange’ amenaswa ‘live’ akikata mauno huku akipewa kampani na mtoto mdogo nyuma yake.

Agnes Jerald ‘Masogange’ akiwa nyumbani kwa Salma Jabu ‘Nisha’, Kijitonyama jijini Dar
Weekly Star Exclusive  ilimbamba mrembo huyo juzikati nyumbani kwa mwigizaji Salma Jabu ‘Nisha’, Kijitonyama jijini Dar ambapo Nisha alikuwa akipiga makofi na kushangilia wakati Masogange alipokuwa akikata mauno.
“Sijacheza siku nyingi jamani ndiyo maana leo nimejikumbushia mambo yangu ya mjini, kuna vitu vingi sana nilivimisi kama kukutana na watu hivi na kucheka pamoja kwa uhuru,” alisema Masogange.
Wakati akiendelea kukatika, mtoto mdogo ambaye jina lake halikupatikana mara moja mwenye umri uliokadiriwa kama miaka 7, alishangilia na kucheza naye pamoja.

Tangu arejee kutoka Bondeni, Masogange amekuwa shosti mkubwa wa Nisha ambapo mbali na urafiki, wanafanya filamu pamoja iitwayo Betina na Zena.
Kwenye msala wa madawa ya kulevya, Masogange aliachiwa kwa kulipa faini baada ya kuthibitika kuwa mzigo aliokutwa nao haukuwa madawa ya kulevya bali ni ‘material’ ya kutengenezea madawa tofauti.

MASOGANGE KUONEKANA KWA MARA YA KWANZA KWENYE VIDEO YA TUNDAMAN

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Khalid Ramadhani Tundamani anatarajia kumwonyesha kwa mara ya kwanza 'Video queen' Agnes Gerad maarufu Masogange katika video ya wimbo wake wa Msambinungwa.

Akiongea Tundaman alisema ataondoka nchini Januari 5, 2014 kwenda Nairobi kwa ajili ya utengenezaji wa Video hiyo na kwamba ameamua kufanya video hiyo akiwa na Masogange kwani ni msichana anayefanya vizuri katika video nyingi za wasanii pia ana kipaji cha kazi hiyo.

SENGA AWEWESEKA NA MZIGO WA MASOGANGE, ANGALIA HAPA UONE

“Mzigo” wa Agness Masogange ‘wamdatisha’ Senga, Tazama picha hapa
  • “Mzigo” wa Agness Masogange ‘wamdatisha’ Senga, Tazama picha hapa 1
Mwigizaji mkongwe nchini Ulimboka Mwakilasa al-maarufu kama “Senga” alishindwa amenaswa laivu na kamera ya mdau mmoja akishangaa laivu mzigo (wowowo) la mwanadada Agness Masogange wakati wakishoot filamu mpya ya mwanadada Nisha ambayo mwigizaji huyo ameshirikishwa. Tazama picha.

“SIKUTAKA KUWEKA WAZI KAMA NIPO DAR KWA SABABU ANAWAOGOPA SANA MAPAPARAZI.” MASOGANGE

VIDEO Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ ambaye alipata soo la kukamatwa na malighafi haramu aina ya Ephedrine Julai 5, mwaka huu nchini Afrika Kusini amejaa tele jijini Dar es Salaam, Ijumaa limethibitisha.
Masogange akipozi na Jack Patrick.
Masogange ambaye siku ya tukio alikuwa na nduguye, Melisa Edward baada ya kunaswa na madawa hayo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park jijini Johannesburg nchini humo alihukumiwa kwenda jela miezi 32 au kulipa faini ya shilinghi milioni 4.8 ambapo aliweza kulipa na kuwa huru.
Tangu aachiwe huru, Septemba mwaka huu, msanii huyo akawa hajulikani alipo huku baadhi ya ‘posti’ zake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram zikionesha yupo Tanzania au Afrika Kusini.
Masogange akipozi dukani Bongo.
Jumatatu iliyopita, mida ya saa kumi jioni, paparazi wetu alipigiwa simu na msomaji wa gazeti hili (jina tunalo) akisema amemwona Masogange akiingia kwenye duka la nguo lililopo Sinza Kamanyola, Dar akiwa peke yake.
Paparazi wetu alijipanga kwa kamera na kutia timu kwenye duka hilo ambapo hata hivyo muuzaji alisema aliondoka baada ya kufanya manunuzi ya kawaida.
Jumatano, Masogange alitumbukiza picha kwenye mtandao wake akiwa ndani ya duka hilo na modo maarufu nchini, Jacqueline Patrick.

Jack alipigiwa simu ambapo alikiri kuwa na Masogange siku ya Jumanne kwenye duka hilo. Akasema: “Mimi nilimkuta pale, tukapiga picha tukaachana, basi.”
Kwa kutumia namba yake ya simu ya mkononi, Masogange alipatikana na kukiri yupo Dar lakini akasema hakutaka kuweka wazi kwa sababu anawaogopa sana mapaparazi.

MANGE KIMAMBI AWASHUTUMU GLOBAL PUBLISHERS KWA KUWEKA VIDEO YA DENTI ANAYEDAI KUBAKWA NA KAPUYA!

Baada ya Mange kimambi Kuona hii Video hapo juu Alikuwa na haya ya Kusema:
"Global publishers shame on you........
This is harrassment and unfair treatment ya mlalamikaji....
Hatusemi kama anaongea ukweli au kama ni muongo ila kwa jinsi mnavyomfanyia aiseeeeee
ingekuwa ni mimi na kesi ningeachana nayo especially coz kesi yenyewe ni ya kubakwa.
Alafu mnamtishia na kumtoa picha yake bila kuziba sijui nini na hatowafanya chochote...
Kwa kweli nimejisikia vibaya sana, sijui kama huyu binti ni muongo au kama ni mkweli ila Global wanataka kummaliza confidence yooooote......
VERY UNFAIR............
Hivi hawawezi tu kumuhoji mlalamikaji wakamsikiliza kama jinsi walimvyomuhoji Kapuya wakaandika alichosema  Kapuya.
wao wana mjudge mlalamikaji kama nani? Unajua mtu muongo ukimpa chance ya kujieleza kiurefu na kiundani huwa anajifunga kitanzi mwenyewe.
Sasa kama lengo lao lilikuwa kumuonyesha huyu binti ni tapeli wameshindwa sana sana wametuonyesha kuwa binti anaonewa na kunyanyaswa.
Kweli hizi nchi zetu ni tofauti sana na nchi zilizoendelea
nchi zilizoendelea yani hata kama huyo binti angekuwa muongo magazeti yooote yangekuwa on Kapuya's case yani uongo wa huyo binti ungekuja kujulikana mahakamni
ila nchi zetu za kimaskini magazeti yanamkandamiza maskini  mwenye nazo anatetewa....
Nchi za wenzetu ni guilty till proven innocent...lol.......
Yani hii kitu ingeplay very differently nchi zilizoendelea......ila kwetu binti keshasulubiwa na kuaibishwa kuwa ni tapeli wanamtajia na watu aliowatapeli mwenyewe anasema hawajui bado wanamlazimisha.....
Sasa huu ndo ukandamizaji wa wanawake........." Mange

"HUKUMU YA MASOGANGE KUKUTWA NA MALIGHAFI HARAMU NCHI AFRICA KUSINI NI NDOGO SANA" ........SADC

MAKAMANDA wa vitengo vya kudhibiti madawa ya kulevya kwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wamemaliza kikao chao jana kujadili mustakabali wa uhalifu ikiwemo hukumu iliyotolewa kwa Mtanzania Agness Gerald ‘Masogange’ aliyekamatwa na malighafi haramu aina ya Ephedrine, Julai 5, 2013 nchini Afrika Kusini kwamba ni ndogo.
Agness Gerald ‘Masogange’.
Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi Tanzania zimeeleza kuwa makamanda wa nchi hizo 15 walikutana jijini Arusha kuanzia Jumatatu iliyopita lengo kubwa likiwa kutokubaliana na adhabu zinazotolewa na baadhi ya nchi wanachama kwa wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’.
WALICHOJADILI
Kwa mujibu wa chanzo kilicho ndani ambacho kiliomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji, makamanda wa nchi hizo walikuwa na kibarua kizito cha kujadili mbinu mbalimbali za kukabiliana na uhalifu pamoja na hukumu inayotolewa kwa watu wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na unga.
“Walijadili matukio mengi ya uhalifu likiwemo suala la madawa ya kulevya, wakajadili mbinu za kukomesha biashara hiyo haramu ili waweze kupata suluhisho la kudumu,” kilisema chanzo hicho.                                                                                   Kamanda Nzowa. WATAKA HUKUMU KWA NCHI WANACHAMA IWE MOJA
Ilidaiwa kuwa, malighafi aliyokamatwa nayo Masogange na mwenzake kwa nchi nyingine kifungo chake kinafanana na kile cha mtu aliyekamawa na madawa ya kulevya, lakini kwa Afrika Kusini ni cha chini sana.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, miongoni mwa masuala yaliyokuwepo kwenye ajenda ni pamoja na umoja katika suala zima la hukumu hususan kwa watuhumiwa wa madawa ya kulevya kwani kumekuwa hakuna uwiano baina ya nchi moja na nyingine ndani ya Jumuiya hiyo.
Rais Dk. Kikwete.
“Tumeona ilivyokuwa kwa Masogange, nchi nyingi zimepinga kabisa ile hukumu kwani ilikuwa haifanani na kosa husika. Mtu anatozwa faini ya shilingi milioni nne na laki nane (Sh. milioni 4.8) kitu ambacho hakiingii akilini kabisa, makamanda wengi wameonesha kupinga hukumu ile,” kilisema chanzo hicho.
MASOGANGE AJIFICHA
Wakati makamanda wa nchi hizo wakimaliza kikao chao, habari zenye utata zimesambaa kwamba, Masogange alitua Bongo katikati ya mwezi uliopita lakini anaishi Dar au Mbeya kwao kwa kujificha.
Baadhi ya watu, wakiwemo marafiki zake wamekuwa wakisema kwa mkato staa huyo yupo Dar huku wengine wakisema baada ya kutua Dar alikwenda kwao Mbeya kwa sababu hataki kujulikana kuwa amesharudi Bongo.
Mwenyewe anapopatikana kwenye simu na kuulizwa amekuwa akijibu bado yupo Afrika Kusini lakini siku yoyote atatua Dar.
NZOWA ATOA UFAFANUZI
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alipoulizwa kwa njia ya simu juzi kuhusu mkutano huo alijibu kuwa yupo safarini kikazi akiwa katika mazingira mazuri atatoa ufafanuzi.
“Nipo safarini kikazi, naomba unitafute siku nyingine nitakupa ufafanuzi mzuri sana,” alisema Kamanda Nzowa ambaye naye ilidaiwa alikuwepo kwenye kikao hicho.
Mellisa Edward.
KUMBUKUMBU
Masogange na Mellisa Edward walikamatwa Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park jijini Johannesburg  nchini humo wakidaiwa kuingiza madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
Hata hivyo, mahakama kuu nchini humo ilidai madawa hayo si ya kulevya bali ni malighafi haramu iitwayo Ephedrine ambapo kwa sheria za Afrika Kusini mtu akipatikana na hatia ya kuyaingiza nchini humo ni kifungo cha miezi 32 jela au faini ya shilingi milioni 4.8 kama alivyohukumiwa Masogange ambayo ni ndogo.

HUKUMU YA MASOGANGE.. MCHEZO UMECHEZWA!

“Hivi jamani, hiki sasa ni kiini macho. Tuliambiwa lakini watatoka tu. Mamlaka ya mapato kule Sauzi waliona ni madawa ya kulevya, mahakama ikaona ni kemikali hatari, mnadhani nani mkweli hapo?”
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe wakati akionyesha picha ya Masogange kwa wanahabari.

 VIDEO Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ na shosti yake, Melissa Edward wapo huru kufuatia kesi iliyokuwa ikisikilizwa nchini Afrika Kusini ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine ya Sh. bilioni 6.8, lakini baadhi ya wadau nchini wanasema kuna mchezo umechezwa, Ijumaa Wikienda limebaini mambo ya kushangaza nyuma ya pazia.
Masogange na Melissa walikamatwa Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park jijini Johannesburg nchini humo. Wawili hao wameishi mahabusu kwa saa 1824.

MMOJA HURU, MMOJA AHUKUMIWA
Uhuru wa Masogange ni baada ya Mahakama ya Kempton jijini Johannesburg kumtia hatiani kwa kuingiza kemikali hatari nchini humo, akatakiwa kulipa faini ya randi 30,000 (Sh. milioni 4.8 za Bongo) au kifungo cha miaka 2 jela.
Melissa yeye hakukutwa na hatia kwa vile ilibainika mizigo aliyokutwa nayo aliombwa na Masogange amsaidie kubeba baada ya kukutana ndani ya ndege ya Shirika la South Africa Airlines.

Agnes Gerald Waya ‘Masogange’.
KUMBE SI CRYSTAL MATHAMPHETAMINE
Habari kutoka nchini humo zinasema mdhamini wa Masogange (jina halijapatikana) alipigana kuhakikisha staa huyo na nduguye ambaye amezaliwa naye kwa mama mkubwa wanakuwa huru na kurejea Bongo.
Katika kupigana huko, mdhamini huyo alifurahia matokeo ya uchunguzi wa mkemia mkuu wa serikali ya nchi hiyo kuyaona madawa hayo kuwa si Crystal Methamphetamine bali ni Ephedrine ambayo si unga ila ni kemikali hatari ambayo ikichanganywa na dawa nyingine hupatikana unga halisi.
Kwa Bongo madawa hayohayo ni unga na tayari watu wengi wapo korokoroni kwa kukamatwa nayo akiwemo aliyekuwa rafiki wa marehemu Steven Kanumba, Saada Ally.
Katika hilo, mtu anayekamatwa na madawa hayo nchini humo hushtakiwa kwa kosa la kuingiza kemikali hatari. Serikali ya Afrika Kusini ilipiga marufuku kuingizwa nchini humo kwa madawa hayo na adhabu yake iko wazi.
“Yule mdhamini alipojua mkemia mkuu amesema yale si Crystal Methamphetamine bali ni Ephedrine aliitumia nafasi hiyo kucheza na mwanasheria ambapo kifungo chake kinajulikana,” alisema mtoa habari wetu mmoja.

Mangunga.
MSEMAJI WA ‘TRA’ YA SAUZ AINGIA SHAKA
Habari zinasema kuwa, kufuatia taarifa za mahakama kwamba mzigo huo si Crystal Methamphetamine bali ni Ephedrine Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini (SARS), Marika Muller alisema kuwa timu yake ina uhakika wa asilimia mia moja kwamba, mzigo wote wa Masogange na Melissa walioukamatwa  nao ni madawa ya kulevya aina ya Crystal Meth.
Muller akatoa la moyoni akisema kwamba, kama mahakama imekubaliana na matokeo ya uchunguzi wa mkemia mkuu wa nchi hiyo, yeye hana la kusema kwa kuwa uamuzi wa korti ni wa mwisho.

KAMANDA NZOWA ANYOOSHA MIKONO
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Kamanda wa Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa ambapo alipoulizwa juzi kama serikali ina mpango wa kumkamata Masogange atakaporejea nchini ili awataje waliomtuma, alisema:
“Sasa kama wameachiwa kule, sisi tutawakamataje? Hatuna sababu ya kufanya hivyo, kesi ilisikilizwa kule mahakama ikafikia ilipofikia, basi tena! Ila tutafuatilia chini kwa chini mtandao huo.”

Melissa Edward.
MCHEZO UMECHEZWA
Jijini Dar es Salaam, baadhi ya wasomaji walipozungumza na gazeti hili juzi walitilia shaka kuwepo kwa mazingira ya kuchakachuliwa kwa madawa hayo.
Walisema kuwa, ilikuwaje SARS iwakamate akina Masogange na kugundua walibeba Crystal Meth (unga) halafu mahakama iseme ni Ephedrine (kemikali hatari)?
“Hivi jamani, hiki sasa ni kiini macho. Tuliambiwa lakini watatoka tu. Mamlaka ya mapato kule Sauzi waliona ni madawa ya kulevya, mahakama ikaona ni kemikali hatari, mnadhani nani mkweli hapo?” alihoji msomaji aliyejitambulisha kwa jina la Aunt Elizabeth, mkazi wa Mbezi Beach, Dar.
Wengine walitupia kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na Twitter wakidai hivyohivyo kwamba kuna mchezo umechezwa.
“Kwanza wamekamatwa Julai 5, mwaka huu. Kesi imeisha katikati ya wiki iliyopita, hata miezi mitatu haikufika. Hapa Bongo, yule mama Leila (Mwanaidi Mfundo) na wenzake walikamatwa 2011 kwa unga huohuo, kesi yao bado ipo Mahakama Kuu, Dar hadi leo,” alisema Samuel Msalanda wa Ilala, Dar.
Wengi walionesha kutilia shaka hukumu hiyo kutokana na mitazamo yao lakini Mahakama ya Kempton jijini Johannesburg, Afrika Kusini ndivyo ilivyoamua.

Kamanda Nzowa.
MASWALI TATA
Ukiachana na mitazamo na ukweli ulivyo, bado kuna maswali tata ambayo utatuzi wake unakuwa mgumu kulingana na kesi yenyewe kuanzia kutajwa, kusikilizwa hadi hukumu ilikuwa nje ya Tanzania.
Je, mwenyewe Masogange alipokuwa akisafirisha dawa hizo alijua ni kemikali hatari ambayo ni mali ghafi ya madawa ya kulevya?
Iwe ni kemikali au la! Alitoa wapi mali ghafi hiyo na alikuwa akimpelekea nani kule Afrika Kusini?
Ni kigogo au mtu gani aliyeratibu safari hiyo mpaka Masogange akafanikiwa kupita kwenda Afrika Kusini?
Nani alimpeleka Masogange hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)?
Kituo cha kwanza cha Masogange kuondokea kwenda JNIA kilikuwa wapi? Inawezekana ni nyumbani kwake ambapo alilala na mizigo yote ile?
Kama mahakama imebaini Masogange hakuingia Afrika Kusini  na unga, vipi kuhusu wale  wafanyakazi wa  JNIA walioachishwa kazi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kwa kuzembea Masogange akapita na ule mzigo?
Yupo wapi Nassoro Mangunga aliyetajwa na Dk. Mwakyembe kuwa alifanikiwa kutoroka na mabegi matatu ya unga kule Sauzi?


CREIDT: GPL

WASEMAVYO WANASHERIA KUHUSIANA NA HUKUMU YA KUMWACHIA HURU MASOGANGE


Taarifa ya kuachiwa huru kwa Agnes Gerald aka Masogange na mdogo wake Mellisa Edward imepokelewa kwa mshangao mkubwa na Watanzania wengi.
Agnes-2
Si kwasababu hawawapendi wasichana hao na kwamba wangependa wafie jela, bali ni kitokana na namna ambavyo kesi yao ilivyokuwa ikionekana kubwa na jinsi ilivyokuwa ikitawala vichwa vya habari vya magazeti ya Tanzania.
Kukamatwa na mabegi 6 yenye madawa ya kulevya aina ya Methamphetamine na yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 6 si kosa la kawaida. Wengi walikuwa wakiamiani kuwa, maisha ya wasichana hao yameshaharibika na ni ngumu kurudi uraiani mapema.
Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela kwa miezi 30 (miaka miwili na miezi mitano) au alipe faini ya R30, 000 (sawa na Sh4.8 milioni. Naye Melissa ameonekana hana hatia kwakuwa alidaiwa kumsindikiza tu dada yake aliyemuomba amsaidie kubeba mzigo huo.
Pia imeonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya, bali ni kemikali aina ya ephedrine. Walibeba kemikali hizo kwenda kufanyia? Hilo ni swali gumu kulijibu.
Uamuzi wa mahakama hiyo na kubadilika kwa maelezo, haujawashangaza tu Watanzania bali pia Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS), Marika Muller aliyelieleza gazeti la Mwananchi kuwa timu ya SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5 ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine. Hata hivyo kemikali hiyo ya Ephedrine ina mfumo wa molecule sawa na madawa ya kama phenylpropanolamine na methamphetamine.
Kwahiyo hata kama alikamatwa na kemikali, bado si kitu cha kawaida kwa msichana tu anayejulikana kuwa ni video vixen kusafirisha bidhaa kama hiyo.
Ili kupata uelewa zaidi kuhusu masuala ya sheria, nimezungumza na Sillas John, mwanafunzi wa sheria katika chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino ambaye ameeleza jinsi kesi za dawa za kulevya zilivyo.
“Huwa inategemea na sheria ya nchi hiyo inasema nini, maana mahakama yenyewe inaongozwa tu na sheria inasema nini,” anasema Sillas.
“Kama kwenye kifungu cha sheria ya Afrika Kusini inasema kwamba mtu yeyote akikamatwa na madawa ya kulevya, haijalishi kiasi gani, atafungwa miaka sita au faini ya milioni 4, basi mahakama haina choice hata kama ingekuwa ni madawa ya kulevya ya trillion 10. Kwasababu kisheria, ukisoma hata katiba yetu ya Tanzania ibara kama ya 13, inasema kwamba mtu yeyote hatapata adhabu ya kosa ambalo amelitenda kipindi ambach hilo kosa halikuwa ni kosa kisheria.
Kwahiyo sheria zimetungwa miaka ile ambapo milioni 4 ilikuwa ni hela kubwa. Katika hali ya kawaida watu wako too emotional ila hawajui upande mwingine wa sheria.”
Sillas amesema hata Kamishna Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Geofrey Nzowa ambaye ameshangazwa na adhabu ndogo iliyotolewa kwa wasichana hao licha ya kukamatwa na mzigo wenye thamani ya shilingi bilioni 6.8, haijui vizuri sheria.
“Hiyo hukumu imetolewa kwa mujibu wa sheria,” anasema Sillas. Ni ninyi wananchi mnatuchagulia bunge ambalo linatutungia sisi mahakama sheria za kuapply. Leo, any traffic offence Tanzania unaweza ukagonga mtu na akavunjika miguu ukalipa shilingi elfu 20.
Tatizo linakuja kwamba watu wanaona athari za madawa ya kulevya lakini hawalishawishi bunge lao kubadilisha sheria, sasa unategemea mahakama itafanyaje? Kwa sababu kweli haiingii akilini kutoa adhabu ya milioni 4 wakati kosa ni la bilioni 6, milioni 4 ni nini? Lakini ni kwa mujibu wa sheria. Hatoshtakiwa mtu kwa kosa ambalo halijaandikwa kisheria na hatuwezi kutoa adhabu kwa mtu yeyote kwasababu tu amefanya kosa ambalo sasa hivi linaonekana kubwa.
Maana ya jinai kisheria, ni kile kitu ambapo sheria inasema hii ni jinai. Na maana ya adhabu kisheria sio wananchi wanasemaje, ni ile sheria inaposema kwamba ‘adhabu ya kosa hili ni hii’. Makahaka haiwezi kujitungia sheria, haina mamlaka hayo.”

MASOGANGE KUSHTAKIWA TENA TANZANIA

WAKATI wasichana wawili wakitanzania waliokuwa wakiendelea kusota lumande nchini Afrika Kusini kwa tuhuma za kuingia kemikali zinazotumika kutengenezea za dawa za kulevya wakiachiwa huru baada ya kulipa faini ya  R30,000 (Sh4.8 milioni), Jeshi la Polisi nchini Tanzania imepanga kuwatia hatiani mara tu baada ya kuwasili nchini. Taarifa za ndani zilizonaswa na zinadai kwamba Agnes Gerald, maarufu Masogange na mwenzake Melissa Edward, wanaandaliwa shtaka la kusafirisha dawa hizo nje ya nchi na kuchafua jina la Tanzania.  
"Hatua hiyo inachukuliwa dhidi yao kwakuwa sheria za Afrika Kusini zinatofautiana na sheria za Tanzania na ndiyo sababu hata  Kamishna Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Geofrey Nzowa alikwenda nchini Afrika Kusini kufuatilia suala lao," kilisema chanzo hicho. Kwa upande wake Nzowa alipoulizwa alisema mzigo walioubeba Masogange na mwenzake haukuwa dawa za kulevya bali ni kemikali za dawa za kulevya.

                                                                                                        Masongange
Hata hivyo Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS), Marika Muller alieleza kuwa timu ya SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5 ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine. Wakati Masogange akitozwa faini hiyo mwenzake, Melissa Edward ameachiwa huru na mahakama hiyo, baada ya kukosekana ushahidi wa kumtia hatiani.
Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai cha Afrika Kusini(Hawk), Kapteni Paul Ramaloko akizungumza na Habarimpya.com mjini hapa jana alisema kwamba uchunguzi wa kisayansi uliomalizika jana umeonyesha kwamba watanzania hao hawakubeba dawa za kulevya, bali walibeba kemikali aina ephedrine ambazo pia hutumika kutengenezea dawa mbalimbali zikiwemo dawa za kulevya ambapo wakati mwingine hutumiwa na madaktari wakati wa upasuaji.
Kwa upande wa Melisa Kapteni Paul Ramaloko alisema kwamba Mahakama ilibaini kuwa, hakuwa na kosa baada ya uchunguzi kuonyesha kuwa alimsindikiza mwenzake katika safari hiyo na kwamba hakuhusika moja kwa moja katika tukio hilo. “Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu kumsaidia kubeba baadhi ya mabegi, lakini hayakuwa yake. Mizigo yote iliandikwa jina la Agness Gerald na si Melissa,” alisema Kapteni Ramaloko.

Mahakama  Kuu ya Gauteng iliyoko eneo la Kempton Park jijini Johannesburg Afrika Kusini iliyokuwa ikiendesha kesi ya Masogange.
Kapteni Ramaloko alifafanua kwamba utetezi wa Melisa ulikubaliwa na Mahakama baada ya kujitetea kwamba walikutana na Agness ndani ya ndege na baada ya kuteremka, Masogange akamwomba amsaidie kubeba mizigo hiyo, kwani ilikuwa mikubwa. Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali zozote ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la jinai kisheria, hivyo mahakama iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela kwa miezi 30 (miaka miwili na miezi mitano) au alipe faini ya R30, 000 (sawa na Sh4.8 milioni).
Hata hivyo, Kapteni Ramaloko alisema mdhamini wa Masogange alilipa nusu ya fedha na kwamba zinazobaki amalizie baadaye. Alisema kutokana na kutomalizia kulipa fedha hizo ataendelea kubaki nchini humo hadi atakapomaliza kulipa nusu ya faini iliyobaki. Masogange na mwenzake walipokamatwa na SARS ilielezwa walikuwa wamebeba dawa za kulevya aina ya Methamphetamine, lakini Mahakama juzi ilithibitisha walikamatwa na kemikali aina ya Ephedrine, ambayo siyo dawa za kulevya.

AGNES MASOGANGE NA MELISSA WAACHIWA HURU AFRIKA KUSINI BAADA YA KULIPA FAINI YA SHILINGI MIL 4.8


Melisa & Agnes
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi la leo, Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, nchini Afrika Kusini imemwachia huru mrembo huyo baada ya kulipa faini ya R30,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni 4.8 za Tanzania, kubeba kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya.
Naye Melissa Edward ameachiwa huru na mahakama hiyo, baada ya kukosekana ushahidi wowote wa kumtia hatiani.
Habari hiyo kwenye gazeti la Mwananchi inaeleza kwa urefu:
Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai cha Afrika Kusini(Hawk), Kapteni Paul Ramaloko alisema Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya, bali kemikali aina ya ephedrine.
Mahakama hiyo ilibaini kuwa, Melissa hana hatia kwa kuwa ilionekana kuwa amemsindikiza Masogange, ambaye alimwomba amsaidie kubeba mzigo huo.
“Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu kumsaidia kubeba baadhi ya mabegi, lakini hayakuwa yake. Mizigo yote iliandikwa jina la Agness Gerald na si Melissa,” gazeti la Mwananchi limemnukuu Kapteni Ramaloko.
Alisema, Melissa alijitetea kuwa hakuwa amesafiri pamoja na Masogange bali walikutana ndani ya ndege na Masogange alimwomba amsaidie kubeba mizigo hiyo, kwani ilikuwa mikubwa.
Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali zozote ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la jinai kisheria, hivyo mahakama iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela kwa miezi 30 (miaka miwili na miezi mitano) au alipe faini ya R30, 000 (sawa na Sh4.8 milioni).
Hata hivyo, Kapteni Ramaloko alisema mdhamini wa Masogange alilipa nusu ya fedha na kwamba zinazobaki amalizie baadaye.
Alisema kutokana na kutomalizia kulipa fedha hizo ataendelea kubaki nchini humo hadi atakapomaliza kulipa nusu ya faini iliyobaki.
Masogange na mwenzake walipokamatwa na SARS ilielezwa walikuwa wamebeba dawa za kulevya aina ya
Methamphetamine, lakini Mahakama juzi ilithibitisha walikamatwa na kemikali aina ya Ephedrine, ambayo siyo dawa za kulevya.
Wakati Kamishna Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Geofrey Nzowa alipoulizwa na Mwananchi Jumamosi juzi alisema mzigo walioubeba Masogange na mwenzake haukuwa ni dawa za kulevya bali ni kemikali za dawa za kulevya, lakini Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS), Marika Muller alieleza kuwa timu ya SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5 ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine.
Jana, Muller alipoambiwa kuwa Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kulipa faini na mmoja kuachiwa huru kwa kuwa Mahakama imeridhika kuwa hazikuwa methamphetamine bali kemikali aina ya Ephedrine, alirudia tena na kueleza kuwa, mamlaka hiyo ina uhakika na kazi yake na iwapo mahakama imewaachia huru basi yeye hana la kusema zaidi.
“Kazi yetu kubwa ni kukamata mizigo haramu inayopitishwa uwanja wa ndege, kama Mahakama imeona kuwa si dawa za kulevya, hatuna la kuongeza. Kikubwa tumemaliza kazi yetu,” alisema Muller kwa kujiamini.
Hata hivyo, Nzowa jana akizungumzia kuachiwa huru kwa Watanzania hao, alionyesha kushangazwa jinsi Mahakama ilivyotoa adhabu ndogo.
“Hii ni ajabu sana. Kama watu wamebeba mzigo wenye thamani ya Sh6.8 bilioni wanapigwa faini ya milioni nne, hawataogopa kufanya hiyo biashara. Hao watu ni hatari sana,” alisema Nzowa.
Alipoulizwa iwapo wakirudi Tanzania wanaweza kushtakiwa, Nzowa alisema kitengo chake hakitaweza kuwashtaki tena kwa sababu wanaweza kujitetea kuwa tayari walishahukumiwa, isipokuwa Mwendesha Mashtaka aliyekuwa akisimamia kesi yao anaweza kukata rufaa.
“Iwapo Mwendesha Mashtaka wa huko akikata rufaa kwa kuona adhabu aliyopewa mhalifu huyo ni ndogo, anaweza kufanya hivyo,” alisema Nzowa.
Nzowa alisema, inasikitisha kuwa wakati mapambano ya biashara hiyo yakiwa yanaendelea Tanzania, watuhumiwa hao wanaachiwa.
“Adhabu waliyopewa ni ndogo hasa wakati huu ambao Tanzania tunachafuka kwa tuhuma hizi. Lazima kitu kifanyike kubadili hali halisi hapa nchini,” alisema.
Nzowa alieleza kuwa alikwenda Afrika Kusini tangu Septemba Mosi kuwahoji wasichana hao ambao hata hivyo hawakuweza kusema lolote la kuisaidia polisi.
Masogange aliandika kwa maandishi kuwa ni kweli mzigo ulikuwa wa kwake, lakini akasema mdogo wake, ambaye ni Melissa, hajui lolote na alikuwa amemsaidia.
Julai 5, mwaka huu Masogange na Melissa walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo wakidaiwa wamebeba kilo 150 zilizodaiwa kuwa ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine zenye thamani ya Sh6.8 bilioni.
Dawa hizo zilizokuwa zimepakiwa katika mabegi makubwa sita, zinatajwa kuwa ni kiwango kikubwa kukamatwa katika historia ya SARS ndani ya uwanja huo unaotumiwa na mataifa makubwa duniani.
Taarifa za kukamatwa kwa wasichana hao zilipamba kurasa mbalimbali za magazeti ndani na nje ya Tanzania, jambo lililosababisha Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kuchukua hatua za kuusafisha Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.
Baada ya uchunguzi wa Dk Mwakyembe ambao ulibaini kuwapo mchezo mzima uliochezwa wakati Masogange na Melissa walipokuwa uwanja wa ndege.
Agosti 17 alitoa agizo la kufukuzwa kazi, Koplo Juliana Thadei, Jackson Manyoni, Yusuph Daniel Issa, Koplo Ernest na Mohamed Kalugwan.
Mwakyembe alisema katika hali isiyokuwa ya kawaida mfanyabiashara ambaye hakuwa na tiketi ya kusafiri siku hiyo, baadaye alibadili mawazo hapohapo na kuamua kuondoka siku hiyo kwenda Afrika Kusini na kulipia faini ya dola 60 (Sh96, 000) ili kupata tiketi.
Pia Mwakyembe aliliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kumkamata mfanyabiashara anayedaiwa kumsaidia Masogange kusafirisha dawa za kulevya ambaye alitoweka na mabegi matatu ya dawa hizo huko Afrika Kusini.

MASTAA BONGO WAMFANYIA SHEREHE YA BIRTHDAY AGNESS MASOGANGE HUKU AKIWA JELA SOUTH AFRICA


So guys kama mnavyojuajuz ilikuwa birthday ya Miss FineAss AGNES MASOGANGE, Na kwakutambua mchango naurafiki wao Jackline Wolper akaamua kuangusha boonge la dinner kwa ajili ya kusherehekeasiku ya kuzaliwa ya kipenzi chao uyo ambaye yuko jela kwa tuhuma za madawa ya kulevya huko South Africa... hivi ndivyo hali ilivyokuwa...
Enjoy!!

MASOGANGE AZIDI KUBAINIKA, SASA HUENDA AKAFUNGWA MIAKA 20 AU KIFUNGO CHA MAISHA

BAADA ya kukamatwa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini, msanii anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wa bongo fleva, Agnes Jerald 'Masogange' na mwenzake Melisa Edward, ukweli umeibainika kwamba dawa walizokamatwa nazo ni za kutengenezea dawa za kulevya, ambazo hazipatikani nchini na hazina matumizi yoyote.Kupitia taarifa rasmi zilionesha kuwa, Chemical bashirifu ndiyo aina ya dawa walizokamatwa nazo nchini humo, ambapo wasanii hao walikamatwa nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.Akizungumza ofisini kwake Dar es Salaam leo Kamishina wa Tume ya Kuratibu na Kuthibiti Dawa za Kulevya nchini, Christopher Shekiondo alisema kwamba kwa mujibu wa sheria za nchi, dawa walizokamatwanazo wasichana hao zinatumika kutengenezea dawa za kulevya, ambapo adhabu yao ni sawa na mtu aliyekamatwa na dawa za kulevya.Wasichana hao walikamatwa Julai 5, mwaka huu nchini humo wakiwa shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya sh. bilioni 6.8 wakitokea Tanzania.Shekiondo alisema dawa walizokamatwa nazo hazitumiki moja kwa moja kama dawa, bali zinatumika kutengenezea dawa za kulevya hivyo kwa mujibu wa sheria, adhabu zao zinakwenda sambamba na waliokamtwa na dawa za kulevya."Dawa hizo hazitumiki moja kwa moja bali zinatumika kutengenezea dawa za kulevya, hivyo kama taarifa tulizopata ni sahihi juu ya aina ya dawa walizokamatwa nazo na dawa hizi hazitumiki sana nchini, bali zinatumika Afrika Kusini, Asia pamoja na Ulaya," alisema Shekiondo.Alisema kwa mujibu wa sheria za nchi, mtu anayekamatwa na dawa hizo mara nyingi hukumbwa na adhabu ya kuhukumiwa miaka 20 au kifungo cha maisha.Akielezea kuhusu wasichana hao wawili kupanda kizimbana juzi, Kamishina huyo aliweka wazi kuwa hadi sasa hawajapata taarifa zozote rasmi, zaidi ya kupokea zile za awali za kushikiriwa na Jeshi la Polisi Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi.Kamishina huyo alisema inaonesha Watanzania wengi wamekamatwa na dawa za kulevya nchini Brazil ambao idadi yao inafikia 109, ambapo wengi wao wameshahukumiwa.Alisema watu hao wamekamtwa nchini humo, wakiwa na dawa aina ya cocain kwa ajili ya kusafirisha nchi nyingine, huku baadhi yao wamehukumiwa kunyongwa pamoja na kifungo cha maisha, ingawa idadi kamili ya watu hao bado haijafika rasmi."Tumepokea taarifa jumla ya Watanzania 109 wamekamtwa nchini Brazil, ingawa bado tunasubiri kujua ni wangapi waliohukumiwa kifo, pamoja na kifungo cha maisha," alisema Shekiondo.Aliongezea kuwa baadhi ya nchi nyingine, ambazo Watanzania wanakamatwa na dawa hizo za kulevya wakiwa wanasafirisha ni China vijana 34, Kenya 30, Pakistani 16, Falme za Kiarabu ikiwemo Dubai 14,  pamoja na nchi nyingine kama Japan, Argentina, Msumbiji, Afrika Kusini, Ureno, pamoja na Uingereza.Akizungumzia hukumu ambazo zimeshatolewa baadhi ya nchi walizokamatwa Watanzania hao,, Kamishina huyo alisema Brazil ambayo ndiyo Watanzania wengi wamekamatwa idadi kamili, bado hawajapata ingawa Kenya tayari wapo waliohukumiwa kifungo cha maisha, huku wengine wakiwa wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 hadi 40, nchi China wapo waliohukumiwa kifo na kifungo cha maisha.Shekiondo alisema Tanzania kwa sasa inajulikana kama ni njia ya kusafirisha dawa hizo.Alisema kuna baadhi ya watu wanatumia maji kusafirisha dawa hizo, yaani meli, jahazi pamoja na mitumbwi, hivyo wana mikakati ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu udhibiti wa matumizi ya dawa za kulevya.

WALIOMRUHUSU MASOGANGE APITE NA 'UNGA' AIRPORT NI HAWA!

HAKUNA sababu ya kumkamata ‘mchawi’  kwenye skendo ya Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ kudaiwa kukamatwa na madawa ya  kulevya nchini Afrika Kusini wakati ukweli upo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Watu mbalimbali ambao wamesoma sakata hili kwenye vyombo vya habari, walitoa maoni yao wakisema kuwa watu wanaotakiwa kuwajibishwa ni waliokuwa uwanjani hapo siku Masogange aliposafiri na kuruhusu mizigo ya mrembo huyo na mdogo wake, Melisa Edward ipite bila ukaguzi makini.

“Kuna uwezekano kabisa wa kuwajua watu hao,” alisema msomaji wetu, Mbande Kinaka, mkazi wa Kariakoo, Dar.
Risasi Jumamosi lilimtafuta Mkuu Kitengo cha Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Kamanda Godfrey Nzowa, alipopatikana na kuulizwa namna ya kuwabaini waliomruhusu Masogange akapenya na mzigo airport, alisema lazima watawapata.


Taarifa tulizozipata zinasema Agnes na mdogo wake Melisa Edward  waliondoka nchini Julai 5, mwaka huu kwenda Afrika Kusini.

HATIMAYE AGNES MASOGANGE AKUBALI AMEKAMATWA HUKO S.AFRICA

HUKU skendo ya kunaswa akiwa na madawa ya kulevya ikiendelea kumtesa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ anatarajiwa kupandishwa kortini nchini Afrika Kusini leo kujibu shitaka ambalo mwenyewe hajaliweka wazi, Ijumaa linakupasha.

Agnes Gerald ‘Masogange’.
AWALI YA YOTE
Mwishoni mwa wiki iliyopita, habari ya mjini ilikuwa Masogange kanaswa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini.
Habari zilisambaa kwamba sanjari na Masogange, mwingine aliyenaswa naye ni mdogo wake (mtoto wa mama yake mdogo Agnes) aitwaye Melisa Edward.
Kwa mujibu wa habari hiyo ya mjini, wawili hao walinaswa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oriver Tambo uliopo Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania wakiwa na ‘mzigo’ wa kilo nyingi aina ya ‘crystal methamphetamine’ wenye thamani ya shilingi za Kitanzania bilioni 6.8!


IJUMAA LAANZA KUSAKA UKWELI
Baada ya kunasa habari hiyo, Ijumaa liliingia mzigoni kuusaka ukweli ambapo hata hivyo, madai hayo yalikuwa yakijifungafunga sana.
Mtu mmoja wa karibu na Masogange alipoulizwa kuhusu ukweli au uongo wa habari hiyo alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli Agnes amekamatwa akiwa na madawa ya kulevya kule Sauzi. Lakini si yenye thamani hiyo ya bilioni sita bali ni milioni arobaini tu. Hata hivyo, ameachiwa kwa dhamana ila paspoti yake imezuiliwa.
“Nadhani kuna mambo yanawekwa sawa ikiwezekana atarudi nyumbani.”
JIJINI DAR, KAMANDA WA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA ANENA
Jumatatu iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliviambia vyombo vya habari kuwa, Watanzania wawili walikamatwa nchini Afrika Kusini na mamlaka ya mapato wakiwa na madawa ya kulevya kutoka Tanzania yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
Kamanda Nzowa aliwataja Watanzania hao kuwa ni Agnes Gerald ambaye ana miaka 25 na Melisa Edward mwenye miaka 24. Alisema wawili hao baada ya kukamatwa na chombo hicho walikabidhiwa kwa polisi ambapo mahojiano yanaendelea.
 
IJUMAA LAMWIBUKIA KAMANDA NZOWA
Baada ya Kamanda Nzowa kuwataja kwa majina wawili hao Jumatatu iliyopita, siku iliyofuata, Ijumaa lilipiga hodi kwenye ofisi za kamanda huyo kwa lengo la kutaka kujua kama Agnes Gerald aliyemtaja jana yake ni Masogage au majina yanafanana tu.
Kamanda huyo hakuwepo ofisini kwake asubuhi hiyo na kwa mujibu wa wasaidizi wake, alikuwa kwenye kikao cha dharura kwenye Ofisi za Polisi wa Kimataifa ‘Interpol’.
APIGIWA SIMU
Ilibidi Ijumaa limsake kwa njia ya simu ya kiganjani kwa mara kadhaa. Alipopokea akaulizwa kuhusu Agnes Gerald aliyemtaja kama ni Masogange yule staa.
Kamanda Nzowa: “Eee, mimi siwezi kusema ni huyo, ninachojua ni Agnes Gerald tu basi. Sasa kama ni Masogange mimi sifahamu lolote.”
 
 
JUMANNE USIKU SIMU KUTOKA SAUZI
Mpaka hapo, timu nzima iliyokuwa ikifuatilia habari hiyo haikuona ukweli wa Agnes Gerald kuwa ni Masogange na kwa vile siku zote Global Publishers inasimamia utafiti kabla ya kuandika habari iliamua kuiweka pembeni kwanza ili kuendelea kuichimba.
Saa 2:14 usiku wa siku hiyo, Ijumaa lilipokea simu yenye kuashiria wito (code number) ni ya nje na kabla haijapokelewa, ilibainika ni ya Afrika Kusini.
Ijumaa: Haloo.
Sauti: Haloo, mimi Masogange.
Ijumaa: Mambo Agnes, pole sana na mkasa uliokupata bwana, pole sana.
Agnes: Kwanza naumizwa sana na maneno ambayo watu wanazidi kuyaeneza sehemu mbalimbali bila kuwa na uhakika wowote, mimi sikukamatwa kwa sababu ya madawa ya kulevya.
“Mkasa nilioupata siyo ambao watu wanaueneza kwenye mitandao mbalimbali na katika vyombo ya habari.”
Ijumaa: Kwa hiyo madai ya kukutwa na madawa ya kulevya si ya kweli?
Agnes: Kweli nilikamatwa huku kwa matatizo f’lan ila siyo ishu ya madawa kama watu wanavyosambaza.
Ijumaa: Ni tatizo gani sasa?
Agnes: Unajua sipendi tena kuwapa watu faida ila lilikuwa ni tatizo la kawaida, nilikamatwa na baada ya hapo nilitoka na niko huru. Nasubiri tu kwenda mahakamani Ijumaa (leo) mara moja kisha n’tarudi Bongo.
Ijumaa: Mh! Sasa Egg, mbona huku mpaka viongozi wa polisi wamesema ni madawa?
Agnes: Hapana, siyo, ipo ishu ndogo tu.
Ijumaa: Haya pole sana kwa misukosuko.
Agnes: Asante sana, nitakuja huko siku si nyingi.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger