Agnes Jerald ‘Masogange’.
Akizungumza na paparazi wetu, Agnes ambaye hivi sasa amejiingiza
kwenye soko la filamu, alisema anaogopa sana kuingia kwenye uhusiano na
mume wa mtu ndiyo maana anaona bora aendelee na mpenzi wake wa siku zote
kuepuka uhasama.“Sina tabia ya kushobokea kabisa waume za watu, bora niendelee na mtu wangu wa siku zote na kama tukishindwana basi bora nitafute mwingine lakini awe wangu peke yangu,” alisema Masogange.