BAADA ya kuzagaa kwa habari kuwa viongozi wa kamati ya uchaguzi wa
Klabu ya Bongo Movie wamebwia rushwa, Mayasa Mrisho ‘Maya’ ameibuka na
kukanusha taarifa hizo.
Mayasa Mrisho ‘Maya’.
Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo uliofanyika Jumamosi
iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar na
kumtangaza Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ kushinda nafasi ya uenyekiti,
baadhi ya wasanii waliibua minong’ono kuwa kamati ya uchaguzi ‘ilipozwa’
ili kupindisha matokeo.
“Hatukuchukua rushwa kutoka kwa mtu yeyote, uchanguzi ulikwenda
vizuri na kila kitu kipo katika rekodi, anayetaka kuonyeshwa mfumo mzima
wa kura atuone,” alisema Maya.