Search in This Blog

Showing posts with label MIKASA. Show all posts
Showing posts with label MIKASA. Show all posts

AFUNGWA MIAKA 2 JELA BAADA YA KUMNYONYESHA MTOTO WA JIRANI BILA RIDHAA,TAZAMA MKASA MZIMA

MWANAMKE mmoja raia wa Zimbabwe aliyenyonyesha mtoto wa jirani bila ruhusa anakabiliwa na kifungo cha karibu miaka miwili kwa kumwambukiza mtu  HIV kwa  kukusudia kwa  kuwa  yeye  ni  mwathirika.
Annie Mpariwa, 39, alifikishwa mbele ya mahakama ya Gaborone  wiki iliyopita  na kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 24 kuruhusu kipimo cha pili cha HIV kufanyiwa mtoto huyo.
 
Matokeo ya kwanza ya mtoto huyo yalionyesha hana virusi ilhali ya mama huyo yalikuwa na virusi. 

Mpariwa alikamatwa wiki jana kwa mashtaka ya usumbufu na iwapo mtoto huyo atapatikana na virusi,  mashtaka hayo yatazidishwa hadi 'kumwambukiza mtu mwingine HIV kimakusudi.’ 

Mama wa mtoto huyo wa miezi 14, Nyasha Mironga, alisema kumwona mwanawe akinyonyeshwa na jirani wake lilikuwa ni jambo lililomshtua sana. 

Kisa hicho kimetokea baada ya kupitishwa kwa sheria mpya ya HIV/Aids inayotoa adhabu kali zaidi kwa wale wanaowaambukiza wengine HIV

BINTI WA MIAKA 16 ASIMULIA RAHA YA NDOA BAADA YA KUOLEWA

Stori: Denis Mtima na Chande Abdallah

BINTI wa miaka 16, Husna amefungukia ndoa yake na mwanaume anayetajwa kwa jina la Juma na kudai anafurahia ndoa yake, Risasi Jumamosi lina mkanda mzima.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»
Akizungumza na waandishi wetu, Mbande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Husna alisema aliolewa na mwanaume huyo Julai mwaka huu, mkoani Lindi na mwezi uliopita walihamia Dar.
Alipohojiwa kwa nini alikubali kuolewa akiwa na umri mdogo, alisema kwamba alikosa kazi ya kufanya.
 
Binti huyo aliwashangaza waandishi na polisi pale alipodai kwamba yeye si mtoto mdogo kwani ana mdogo wake mwenye umri wa miaka 15 ambaye ameolewa na amezaa mtoto hivyo yeye asikodolewe macho. “Mbona mdogo wangu ana miaka 15 ameolewa. Mimi siyo mtoto mdogo ninaijua raha ya ndoa yangu,” alisema Husna.
 
Waandishi wetu walipotaka kujua kama huwa anapatwa na maumivu anapokutana na mumewe,  alisema anajisikia kawaida kwani alianza mapenzi tangu akiwa shuleni.
Kama vile haitoshi, binti huyo alisema kuwa huwa anawashangaa hata polisi ambao wanajaribu kulifuatilia suala hilo. Hata hivyo, Husna alisema kuwa angependa kuendelezwa kimasomo kama akipatikana mfadhili na kuachana na mumewe huyo.
 
“Nipo tayari kuachana na mume wangu na kwenda kusoma kwa kuwa umasikini ndiyo uliochangia kuolewa mapema,” alisema. Awali waandishi wetu walipewa taarifa za kuwepo mwanaume aliyeoa mtoto mdogo na majirani wa wanandoa hao na kuwataka kulivalia njuga suala hilo.

”Tunashangaa mwanaume amemuoa binti mdogo sana yaani sawa na mwanaye kabisa. Muda mwingi binti anachezea michanga na watoto wengine. Sijui kamtoa wapi?” alisema mmoja wa majirani hao.

Baada ya kufanyia uchunguzi jambo hilo. Waandishi wetu walibaini nyumba wanayoishi wanandoa hao, ndipo Septemba 14 mwaka huu, waandishi wetu walivamia nyumba hiyo wakiwa na askari ili kumtia nguvuni mwanaume huyo ambaye kwa mujibu wa majirani aliambiwa na watu wake wa karibu na kutoroka eneo hilo.

Akizungumza na waandishi wetu kuhusiana na tukio hilo, Mwakilishi wa Mtandao wa Wanawake Kanda ya Kipolisi Temeke, Eva Michael alisema kuwa wazazi wengi wenye mabinti wadogo hawajui sheria zinazowahusu kama ilivyo kwa Husna ambaye anaona kuolewa katika umri wake ni jambo sahihi kwake.

“Kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 2009 hairuhusiwi mwanamke kuolewa chini ya miaka 18, kwani huo ni kama ubakaji. Watu bado wanaitambua sheria ya mwaka 1971 inayoruhusu mwanamke kuolewa kuanzia umri wa miaka 14, sheria ambayo imeshabadilishwa, kwa hiyo mume wa Husna anachukuliwa kama mbakaji,” alisema mwanaharakati huyo.

Akibainisha jinsi ya kushughulikia suala la Husna, Bi. Eva alisema kuwa atashirikiana na watu wa Ustawi wa Jamii watakaomjenga kisaikolojia na kumpa hifadhi ya muda kabla ya kuwapata wafadhili watakaojitolea kumsaidia.

Mume wa Husna bado anatafutwa na polisi na amefunguliwa kesi katika Kituo cha Polisi Mbagala Kizuiani yenye  namba, MBL/RB/9435/13

VIDEO:FUNDI CHEREHANI AZUA BALAA LA MWAKA, ACHEZEA KICHAPO BAADA YA KUFUMANIWA NA MTEJA WAKE:

NI SAHIHI FEZA KUISHI BOTSWANA NA ONEAL – MAJIBU YA BLOG YA NCHINI HUMO ILIYOMWAMBIA ‘GOME HOME’


Mwandishi wa kike, Galaletsang Molabi wa blog changa ya Botswana, 1980sumn ameandika makala kumtaka Feza Kessy arudi nyumbani kutumia jina alilolipata baada ya kushiriki shindano la Big Brother Brother The Chase.
“Lini Feza ataenda nyumbani kuutumia umaarufu wake wa BBA?” anauliza mwandishi huyo.
“Siulizi swali hili kwasababu mimi ni hater wa ‘Oneza’ kama wengine wanavyoweza kuhisi. Nauliza kwasababu, ndani yangu kama mfanyabiashara, napenda afanikiwe.”
Molabi anasema inamshangaza hadi sasa kuona Feza hayupo kwao (Tanzania) kutumia umaarufu wake kujikuza kimuziki.Amesema hivyo kwasababu, mpenzi wake Oneal amekuwa akitengeneza hela nzuri baada ya shavu la BBA ambapo amekuwa akipata mialiko kwenye club nyingi hata za Afrika Kusini kama Dj.
Anauliza pamoja na Feza kuwa pembeni ya Oneal muda wote, mpaka sasa hawajaweza kupata show na kutumbuiza ama kwa kulipwa kutokana na appearance yake sehemu. Mwandishi huyo anasema alitegemea kuona Feza anatumia muda huu nyumbani kupromote zaidi wimbo wake lakini ameendelea kukaa Botswana wakati Oneal akilikuza tu jina lake.
“Nafikiria tu kiasi cha fedha ambacho angekuwa akikiingiza sasa hivi kwa kutumbuiza nyimbo zake kwa watu wa nchi yake, kuendeleza career yake ya muziki wakati chungu cha BBA kingali cha moto,” anasema.
“Kwa upande mwingine, vipi kuhusu mashabiki wake wa Tanzania? Lini watapata nafasi ya kumshangilia. Walimpigia kura, walimuunga mkono na tunaweza kuhisi kuwa walikuwa wakingoja kwa hamu kumuona nyota wao. Bahati mbaya hawakuweza kupata nafasi hiyo kutoka kwake. Hao ni watu walio nyuma yake. Naamini penzi lingesubiri kwa miezi mitatu. Penzi linaweza kuishi lenyewe hivyo umbali sio issue hapa.”
“So if you see sweet beautiful Feza on the streets of Gabs, please tell her to ‘go home Fezaaaa,” alimalizia mwandishi huyo.
Mtazamo wangu
Kwa namna fulani mwandishi amezungumza masuala ya muhimu ambayo Feza anahitaji kuyazingatia japo ntaeleza pia ni kwanini ni sahihi kwa Feza kuwa Botswana.
Kwanini Mwandishi ana point:
Ni kweli baada ya Feza Kessy kurudi kutoka Big Brother, hajawapa nafasi ya kutosha mashabiki wake kumfahamu zaidi.
Alipochaguliwa Big Brother, Feza Kessy hakuwa na jina kubwa kihivyo. Waliokuwa wakimfahamu ni wale waliofuatilia mashindano ya Miss Tanzania, mwaka 2005/2006 alipokuwa Miss Dar City Center. Kwa wengi, Feza Kessy lilikuwa jina geni kabisa. Na hata jina lake lilipotajwa kuwa ataiwakilisha Tanzania kwenye shindano hilo, wengi waliuliza ‘Feza ndio nani?’ Kwa muda mfupi baada ya kukaa wiki chache tu kwenye jumba la Big Brother, jina lake likawa kubwa na tayari akaingia kwenye klabu ya mastaa wa Tanzania. Ni kweli, Feza alikuwa mshiriki mwenye nguvu kwenye The Chase na Afrika ilimpenda.
Alipokuja Tanzania baada ya kuondolewa, alipaswa kutumia muda kuconnect na mashabiki wake kwa namna nyingi. Ikumbukwe kuwa video ya wimbo wake Amani ya Moyo, ilitoka wakati tayari yupo BBA. Maana yake ni kuwa, alipaswa kuipromote baada ya kuja, hasa kwa kufanya interview nyingi za TV, kama kweli muziki ndicho kitu anachotegemea kimwekee chakula mezani (aliwahi kusema hivyo). Hata hivyo, muda na nafasi wa kufanya hili bado upo.
Naamini pia, kama angekuwa Tanzania, huenda angepata shavu la kutumbuiza kwenye baadhi ya show za Fiesta ama Kili Tour, ingewezekana kabisa.
Kwanini Feza Kessy yupo sahihi kukaa Botswana?
Kuweka mizizi ya penzi lake na Oneal
Hakuna ubishi kuwa, wakiwa na penzi changa mikononi mwao, Oneal na Feza walihitaji muda wa haraka kujuana zaidi nje ya maisha ya Big Brother ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa nusu kweli na nusu kuigiza. Imani ya Molabi kuwa ‘mapenzi yangesubiri kwa miezi mitatu’ haina uhalisia. Kabla hata ya Oneal kwenda BBA, jina lake nchini Botswana lilikuwa kubwa na baada ya kurejea kutoka BBA, limekua maradufu. Hiyo ina maana kuwa, Oneal alijikuta yupo katikati ya vishawishi vingi kutoka kwa wasichana wengi warembo wanaotaka nafasi kwenye moyo wake. Ilikuwa ni muhimu Feza ajuane na Oneal mapema iwezekanavyo kisha mengine ndio yafuate. Ilikuwa muhimu kwake kwenda kuweka ngome nzito kulilinda penzi la Oneal.
Malengo ya Feza Kessy ya kuwa mwanamuziki wa kimataifa
Baada tu ya Feza kutoka BBA, alihama kutoka kuwa muimbaji wa Tanzania pekee na kuwa muimbaji mwenye sura ya Afrika.
BBA imempa exposure kubwa zaidi ambayo hatakiwi kuitumia Tanzania tu. Na kwa muziki wa Feza, kama akitegemea soko la Tanzania tu, si rahisi ukampa kile anachotaka (tunajua aina ya muziki unaofanya vizuri kiuchumi Bongo).
Ni vizuri anapokuwa Botswana kwa mchumba wake kwakuwa tayari anakuwa jirani na kitovu cha muziki wa Afrika, Afrika Kusini. TV zote kubwa za Afrika ziko huko. Akiwa jirani na huko, ni rahisi kwake kupata endorsements za ukweli na hata mashavu mengine makubwa, kuliko akiwa Tanzania.
Hata kama Feza akiamua kuhamia kabisa Botswana, hakuna tatizo kwakuwa atakuwa karibu na mchumba wake na hatokuwa mtu wa kwanza kumfuata mchumba wake kwao.
So kama kuna mtu atamuona Feza, amwambie asiwe na shaka, maisha ni popote.

HALI NI MBAYA PICHA ZA NUSU UCHI ZAHAMIA KWA WENYE BLOG TAZAMA HAPA ZA HUYU BLOGER

Ama kwa hakika wadau nahisi bado hali si swari kwa taifa letu haswa kwa hii hali inayoendelea kuteka akili za wasichana kwa wavulana kwa kujipiga picha za utupu ambazo baadae huwa ni aibu na fedheha kwa familia zao huku wao wakiwa hawana jipya zaidi ya heshima zao kushuka

Kusema kweli haya mambo kwetu bado ni mageni tofauti na mataifa mengine ambapo hicho ni kitu cha kawaida na mtu hulipwa pesa nyingi sana kupiga picha za namna hiyo.
 Mwanadada aliyewahi kutengeneza kichwa cha habari gazetini akidai kubakwa na mbunge wa CHADEMA mheshimiwa Godbless Lema ambaye ni blogger pia Flora Lyimo a.k.a Mbuta Nanga ametengeneza kichwa cha  habari kwa mara nyingine tena baada ya kujipiga picha za uchi na kutupia kwenye blog yake.
Mara baada ya kutumia picha hizi mwadada huyu alijisifu na kujigamba kuwa yeye ni African qeen na anajiamini!.
Kwa upande mwingine anaweza kuwa sawa kwa imani yake ila kwa maadili ya nchii hii nadhani sio sahihi kupiga picha kama hizo thesuperstarstz imehangaika toka asubuhi kumsaka dada yetu huyo bila mafanikio ila bado tunaendelea kumsaka ili kujua kulikoni na mara tutakapompata kama mwana bloger mwenzetu tutaongea nae ili kujua zaidi

ANGALIA PICHA ZAIDI HAPA CHINI

Haya mdau mambo ya dada zetu hayo

PETE YA NDOA IMENIPONZA....NDOA IPO HATARINI

Wadau nipo njia panda naombeni ushauri wenu, nimefanya kosa kubwa na nalijutia
Tafadhali naomba ushauri badala ya kunituhumu


Mwezi nilikuta na demu mmoja tulisoma naye chuo kitambo alikuwa demu wangu for time being, so baada ya miaka kadhaa tukaja kukuta sehemu, shetani akanipitia nikavunja amri ya sita naye


Baada ya kurudi home nikagundua sina pete, nikajaribu kukumbuka nilipoiweka sikupata majibu

Baada ya siku kadhaa yule demu akzidi kunisumbua na kutaka niwe karibu naye sana lakini nikaona si vyema maana anaweza kusababisha mtafaruku kwa ndoa yangu


Baada ya kuona nampotezea akaniambia sasa unajifanya mjanja pete yako ni nayo na nahitaji sh 500,000 cash ama sivyo naharibu kwa mkeo kwamba pete ninayo na ulinikopa.


Kibaya zaidi wife aliniuliza pete umepeleka wapi nikadanganya nimeisahau ofisini nilikuwa nafungua printer sasa pete ikawa inani disturb nikaivua , nilipoenda jumatatu nikamwambia nahisi wahudumu wa usafi wameiiba maana siiona pale nimeiweka naendelea na uchunguzi.


Mwanzo nilimpuuzia lakini mshenzi yule kapeleleza hadi wife anapofanya kazi na kapata simu yake, juzi kampigia kamwambia "naomba mkumbushie mumeo deni langu mimi xxxxx nampigia simpati" halafu akakata simu.

Niliporudi wife kanibana nikamwambia ni mambo ya kazi tu akataka kujua no yake kaipataje, nikazuga zuga na ubabe wa kiume yakaisha


Nikipiga akili nimuendee Polisi naona kama kitanuka na wife atajua

Nikifikiria kumlipa akili hainipi kabisa....kilo tano?

Sijui nimueleze wife ukweli?


Nimejaribu kumpiia simu na kumbembeleza kagoma anachohitaji ni kilo tano au aniharibie kwa wife

Tafadhali ushauri wakuu lawama na madongo hayatanisaidia

WAUAWA WAKIJARIBU KUMTETEA MWANAMKE ALIYEKUWA AKISUMBULIWA

Baadhi ya waandamanaji kwenye ghasia hizo zilizokatisha uhai wa watu 19.
Vurugu zilizoambatana na ghasia zimeua watu 19 kaskazini mwa India baada ya makundi ya Wahindu na Waislamu kushambuliana kwa bunduki na visu kutuliza makelele ya matusi mtaani.

Ghasia hizo zilianza kwa mauaji ya wanakijiji watatu ambao walijitokea kumlinda msichana mmoja aliyekuwa akisumbuliwa huko Kawal, Jimbo la Uttar Pradesh wiki iliyopita.
Hasira ilifoka katika eneo tangu tukio hilo, lakini vurugu zinabadilika na kuwa za kutisha Jumapili pale mwandishi mmoja, mpigapicha mmoja wa polisi na wanakijiji kadhaa walipokufa kutokana na vurugu hizo.
Zaidi ya watu ishiri wamekufa kutokana na majeraha yao yaliyotokana na mapigano ya Jumamosi katika wilaya ya Muzaffarnagar, baada ya vurugu kusambaa kwenye vijiji kadhaa vya jirani.
Serikali imeingilia kati kwa kupeleka mamia ya askari kuzima vurugu hizo na kufanya msako wa silaha katika eneo hilo, wakati hali ya hatari ikiwa imeweka huko Uttar Ptadesh, eneo la makazi ya watu milioni 200.
"Amri ya kutotembea usiku imewekwa kwenye maeneo matatu yaliyoathiriwa zaidi na ghasia hizo ya Muzaffarnagar," alisema mkuu wa mambo ya ndani ya jimbo hilo, R.M. Srivastava.
Ghasia zililipuka Jumamosi mchana baada ya maelfu ya wakulima wa Kihindu kufanya mkutano kwenye kijiji cha Kawal kudai haki katika mauaji ya Agosti 27 ya wanaume watatu ambao waliongea pale mwanamke mmoja alipokuwa akisumbuliwa kwa maneno.
Waziri mdogo wa afya jimboni humo, Mohammad Azam Khan, alisema wahudhuriaji hao walikuwa wakihutubia kutaka Waislamu wauwawe kujibu mapigo ya vifo vya wanakijiji hao watatu.
Wakulima hao walishambuliwa wakati wakirejea nyumbani baada ya mkutano huo, ofisa wa juu wa polisi Arun Kumar alisema, akiongeza kwamba washambuliaji hao wanaonesha kuwa walipanga shambulio lao kutokana na kuwa na silaha za 'bunduki kubwa na vitu vyenye ncha kali.'
Milio ya bunduki iliripotiwa kutoka sehemu mbalimbali za kijiji hicho. Ndani ya masaa kadhaa mapigano yakaibuka kwenye vijiji vya jirani, alisema Kumar.
Mtangazaji wa kituo cha habari cha IBN 7, Rajesh Verma alipigwa risasi kifuani wakati akiripoti maandamano ya jumuiya mjini Abupura, na kufariki katika eneo hilo la tukio.
Uttar Pradesh lilikuwa kitovu cha mapigano mabaya zaidi ya jumuiya nchini India Desemba mwaka 1992, baada ya kundi la Hindu kuharibu kabisa msikiti wa Babri uliojengwa karne ya 16 mjini Ayodhya.
Serikali imeonya kwamba India inashuhudia ongezeko la ghasia za jumuiya, huku matukio 451 yakiwa tayari yameripotiwa mwaka huu, kulinganisha na 410 kwa mwaka mzima wa 2012.
Kwa mwezi Agosti pekee ghasia za jumuiya zimeua watu wawili na kujeruhi 22 katika kijiji kimoja huko jimbo la Bihar, mashariki mwa Uttar Pradesh, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya India.

WATOTO 22 WAFARIKI DUNIA BAADA YA KULA CHAKULA CHENYE SUMU

Takribani watoto 22 wamekufa na wengine wengi wanaumwa baada ya kula chakula cha bure shuleni mchana ambacho kulichanganyika na dozi kubwa ya dawa za kuua wadudu, maofisa nchini India walisema jana.

Haikuweza kufahamika mara moja jinsi kemikali hizo zilivyoingia kwenye chakula hicho kwenye shule moja iliyoko mashariki mwa jimbo la Bihar, ingawa mmoja wa maofisa alisema inawezekana chakula hicho hakikuwa kimeoshwa vema kabla ya kupikwa.

Watoto hao, wenye umri wa kati ya miaka 8 na 11, walianza kuumwa juzi muda mfupi baada ya kula chakula cha mchana shuleni kwao huko Masrakh, kijiji kilichopo maili 50 kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo hilo wa Patna.

Mamlaka za shule hiyo haraka zikasitisha kugawa chakula hicho cha wali, soya, dengu na viazi kufuatia watoto hao kuanza kutapika.

Chakula hicho cha mchana, sehemu ya kampeni maarufu ya nchi nzima kuwapatia chakula japo mlo mmoja watoto kutoka familia masikini, kilikuwa kimepikwa kwenye jiko la shule hiyo.

Watoto hao haraka walikimbizwa kwenye hospitali moja mjini humo na baadaye wakapelekwa Patna kwa matibabu, alisema msemaji wa serikali Abhijit Sinha.

Mbali na watoto hao 20 waliokufa, wengine 27 akiwamo mpishi wa shule walipelekwa hospitali, alisema. Kumi kati yao walikuwa katika hali mbaya.

Mamlaka zimemsimamisha kazi ofisa anayeshughulikia mpango wa mlo wa bure kwenye shule na kufungua kesi ya uzembe dhidi ya mwalimu mkuu wa shule hiyo, ambaye alitoroka mara baada ya wanafunzi hao kuanza kuumwa.

P.K. Sahi, waziri wa elimu wa jimbo hilo, alisema uchunguzi wa awali umeonesha chakula hicho kilikuwa na kemikali ya organophosphate inayotumika kuulia wadudu kwenye mazao ya mpunga na ngano.

Inaaminika nafaka hiyo haikuwa imeoshwa kabla ya kupelekwa shuleni hapo, alisema.

Hatahivyo, wanakijiji walisema tatizo linaonekana kuwa upande wa chakula cha soya na viazi, wakaongeza kwamba watoto ambao hawakula chakula hicho walisalimika - ingawa walikula wali na dengu.

Mpango wa chakula cha mchana nchini India ni moja ya mipango mikubwa duniani ya lishe mashuleni.

Serikali za majimbo zina uhuru wa kuamua aina ya chakula na mida ya mlo huo kutegemea hali ya eneo husika na upatikanaji wa chakula hicho.

Kwa mara ya kwanza ilianzishwa kusini mwa India, ambako kulionekana kuwapo wazazi wengi mafukara wasio na uwezo wa kuwapeleka watoto wao shule.

Tangu hapo mpango huo umekuwa ukisambaa nchi nzima na kuwasikia zaidi wa watoto wa shule milioni 120 kama sehemu ya juhudi za kukabiliana na utapiamlo.

Kwa mujibu wa serikali hiyo, karibu nusu ya watoto nchini India wanasumbuliwa na utapiamlo.

Ofisa wa ngazi ya juu aliyechaguliwa wa Bihar, Waziri Mkuu Nitish Kumar, ameamuru uchunguzi ufanyike kuhusu vifo hivyo.

SAKATA LA SISTA WA KANISA KATOLIKI ALIYEBAKWA NA KUNDI LA WANAUME WATATU

Sista aliye mafunzoni ametekwa na kubakwa kwa wiki nzima na kundi la wanaume watatu katika kile kinachohisiwa kuwa ni shambulio la kulipiza kisasi, vyombo vya habari nchini India vimeripoti.

Sista huyo mwenye miaka 22 alidaiwa kutekwa kwenye stesheni ya treni na binamu zake na kisha kushikiliwa mateka na kubakwa kwa zaidi ya siku kadhaa sababu waliishutumu familia yake kwa kifo cha baba yao.

Ni tukio la karibu kabisa katika mfululizo wa mashambulio ya ubakaji nchini India mwaka huu tangu mwanafunzi alipobakwa na kundi la wanaume na kufa kutokana na majeraha yake ya kutisha ndani ya basi la Delhi Desemba mwaka jana.
 
Sista huyo aliwaeleza polisi alikuwa akutane na binamu zake kwenye stesheni ya treni karibu na Chennai, huko Tamil Nadu, kusini mwa India, baada ya kudai kwamba mama yao alikuwa anaumwa.
 
Hatahivyo, anasema alichukuliwa hadi kijiji cha jirani ambako alishambuliwa mara kadhaa.
 
Watuhumiwa hao baadaye walimrejesha kwenye stesheni hiyo na kumwonya asiripoti tukio hilo.
 
Binamu wa mwanamke huyo, Jotindra Sobhasundar mwenye miaka 30, na Tukuna Sobhasundar mwenye miaka 28, walikamatwa Jumapili, kwa mujibu wa ripoti.
 
Mtuhumiwa wa tatu alikamatwa Jumatatu baada ya mfululizo wa makimbizano katika wilaya ya Kandhamal.
Vyombo vya habari za mjini humo vilisema kaka wa Sista huyo alihojiwa kuhusiana na mauaji ya mmoja wa watuhumiwa. 

 
Shambulio hilo lilidaiwa kutokea kati ya Julai 5 na 11 lakini likatangazwa hadharani wiki hii.
Tukio hilo limelaaniwa vikali na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini India.
Kardinali Oswald Gracias, alinukuliwa akisema: "Ubakaji huu wa makundi ni ugaidi wa kimwili na kihisia.
Pia alizishutumu wakala za serikali kwa 'kukwepa wajibu wao'.

FRANK WA BONGO MOVIE ATISHIWA KUULIWA....MUUAJI AAPA KUTIMIZA AHADI YAKE HIYO

MSANII wa Filamu za Kibongo, Mohammed Mwikongi ‘Frank’ amedai kutishiwa kuuawa baada ya kupokea ujumbe mfupi wa meneno ‘sms’ kutoka kwa mtu anayekulikana kwa majina ya Jonathan Lyradu




Frank amesema alianza kupokea meseji hizo tangu mwezi uliopita ambapo Lyradu amekuwa akimtishia kusitisha pumzi yake hapa duniani.
“Mara ya kwanza nilijua amekosea namba, nikamuuliza anamuhitaji nani, lakini akanitumia meseji nyingine na kunitaja jina langu huku akiendelea kunitisha na kunimwagia mvua ya matusi kwa kweli nilimshangaa kwani simjui mtu huyo,” alisema Frank.
Msanii huyo alisema ametoa taarifa katika Kituo Kidogo cha Polisi Tabata na kufungua jalada TBK/RB/2750/13 TAARIFA.
Katika utafiti wa awali uliofanywa na polisi wakati wa kumsaka mtu huyo anayemtishia maisha Frank anaonekana katika mitandao kuwa ni mkazi wa maeneo ya Magomeni, Sinza na Bamaga, Mwenge jijini Dar

"MCHANA TUNAFUNGA, USIKU TUNAJIUZA TUPATE HELA YA FUTARI NA DAKU".....MACHANGUDOA DAR

OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) inayoendeshwa na mapaparazi wa Global Publishers inazidi kufichua ‘madudu’ kwenye jamii, safari hii imekutana na machangu ambao wamecharuka kuendeleza biashara hiyo kwa kisingizio cha kutafuta fedha za kununulia futari. 


‘Askari’ wa OFM, wiki iliyopita alifanya uchunguzi katika viunga mbalimbali maarufu kwa biashara hiyo na kukuta machangudoa wakifanya biashara yao kama inavyokuwa katika miezi ya kawaida.
Maeneo ambayo yalionekana kushamiri zaidi kwa biashara hiyo ni Barabara ya Mwananyamala Hospitali, American Chipsi, Makaburi ya Kinondoni, Viwanja vya Leaders Club, Taasisi ya Moyo, Jolly Club (Masaki), Hospitali ya Agha-Khan, New Maisha Club (Masaki) na Coco Beach.

Idadi kubwa ya wadada hao walipohojiwa na paparazi wetu, walisema wanaendelea na biashara hiyo kwa kuwa ndiyo waliyoizoea kutafutia kipato na wakiiacha, watakufa kwa njaa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Ili kujiridhisha kwa data, paparazi wetu alijifanya mteja na kukutana na machangu wa Makaburi ya Kinondoni ambao walidai wanapenda waitwe ‘scraper’ au vyuma chakavu pasipo kufafanua zaidi, bahati mbaya wakashtukia mchezo:
Changudoa: “We kaka mbona unatuzingua? We ulivyokuja si ulijifanya mteja, kumbe paparazi, sisi hatuwezi kuacha kujiuza kwa kuwa ndiyo kazi tuliyoizoea, sasa tukikaa nyumbani tutapata wapi futari?” alihoji mmoja wa machangudoa.
Paparazi: “Hivi ni kweli nyie mnafunga?”

Changudoa: “Wewe tumia ubongo na maswali yako yanayotia njaa, hata kama sisi tunafunga au hatufungi tuna watu wanaotutegemea majumbani kwetu kuwatafutia futari, sasa tusipohangaika itakuwaje?”
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu waliozungumza na Ijumaa Wikienda, walionesha kukerwa na tabia hiyo na kulaani vibaya kwani mwezi huu ni maalum kwa ajili ya kumrudia mwenyezi Mungu na kuacha dhambi.

MKASA WA DEREVA WA DALADALA ALIYESUSIWA MAITI HUKO MBEYA

* Atoweka nyumbani kwa siku mbili
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Ihanga Kata ya Ilomba Emanuel Mwasibata akiwa amesimamia kikao cha usuruhishi
 Dereva wa daladala Aswile Mwalukoba aliyeshika fimbo baada ya kurejea nyumbani na kuhudhuria kikao cha usuruishi  ambapo alikili kuzaa  na mwanafunzi huyo na kukubali kuzika .
 Daladala iliyobeba mwili wa Marehemu kutoka Uyole.
 Wakazi wa Uyole wakiwa wameshikwa na butwaa baada yakumkosa mwenyeji wao
 Mwili wa mtoto ukiwa umefunkwa na kitenge na kutelekezwa kwenye kiti
 Kulia ni Carolina Kyando akiwa na dada yake baada ya kuleta mwili wa mtoto nyumbani kwa Mwalukoba eneo la Mama John jijini Mbeya
Majirani pande zote mbili wakingojea kujua hatma ya mazungumzo yanayo endelea baada ya Mwalukoba kurejea


******************

Vitendo vya ukatili dhidi ya  watoto na wanawake  jijini mbeya vimeendelea chukua sura mpya  baada ya dereva wa daladala jijini humo kumzalisha mwanafunzi Masomo ya jioni kituo cha Juhudi kilichopo  Ilomba.
.
 Tukio hilo limetokea hivi karibuni  eneo la mama John Mtaa wa Ihanga Kata ya Ilomba ambapo dereva wa daladala aliyefahamika kwa jina la Aswile Mwalukoba (45 ) kutelekezewa wa miezi saba ambaye alikwisha fariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti Mtaa huo Ndugu Emanuel Mwasibata amesema kuwa mgogoro huo umetokana  na dereva huyo kugoma kuuzika mwili huo kwakile alicho dai kuwa hivi sasa haishi na binti huyo kwa muda mrefu sasa.
Kwa upande wake binti huyo aliyefahamika kwa jina la Calorina Kyando amedai kuwa kitendo cha yeye kuuchukua mwili wa mtoto huyo hadi kwa baba yake unatokana   kutelekezwa na bwana huyo kisha kupigwa marakwa mara na kusababishiwa ulemavu wa sikio la kushoto baada ya kung’atwa na mwanaume huyo.
Mwanamke huyo amefafanua kuwa mara baada ya mtoto huyo kufariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospital ya Igawilo jijini humo aliamua kumpigia simu mzazi mwenzie kwa lengo la kumpa taarifa za msiba huo.
Amesema mara baada ya kutoa taarifa hiyo mwanaume huyo alikubali na kumueleza mwanamke huyo kuwa yuko tayari kwa ajili ya mazikoya mtoto huyo ambapo anafanya taratibu za kuwasiliana na ndugu zake walioko Tukuyu Wilayani Rungwe.
Amesema katika siku iliyofuata mwanaume huyo hakupatikana kwa simu ya kiganjani na wala hakuwepo nyumbani kwake anapo ishi eneo la Mama John hali iliyo plelekea baadhi ya majirani na mwanamke huyo kutoka Uyole kusaidiana na kuutoa mwili huo Hospitalini hapo kwa lengo la kufanya taratibu nyingine .
Aidha majirani hao waliamua kuchukua mwili huo hadi nyumbani kwa Mwalukoba ambapo waliuweka kwenye kiti ndani ya nyumba yake huku wakiendelea kumsubiri mwalukoba arudi aliko  ambapo baadaye alirudi nyumbani hapo akisindikiazwa na Mdogo wake aliyefahamika kwa jina Gabriel Mwalukoba hadi nyumbani hapo.
Kitendo hicho cha kurejea kwa mwanaume huyo kilifanya mwenyekiti wa mtaa huo Ndugu Emanuel Mwasibata kuhoji juu ya  kutoweka kwa nyumbani kwakwe kwa muda wa siku mbili huku kukiwa hakuna mawasiliano yoyote.
 Baada ya kikao cha muda mrefu kati ya pande zote mbili mwanaume huyo alikubali kuupokea mwili huo na hivyo kuanza kufanya taratibu za mazishi ambapo mazishi hayo yalifanyika katika makaburi ya Iyela mida saa 12 jioni na kuhudhuriwa na familia zote mbili pamoja na majirani wengine kutoka Uyole na Mama John.

VIDEO:WANAWAKE WA KENYA WAZIDI KUWA WABABE KWA WAUME ZAO...MWAMAUME MWINGINE APIGWA VIBAYA NA MKEWE



 
Ni ngumu kumuona mwanaume akitokwa machozi kama hivi…. hii imetokana na mke wake kumpiga makofi hadharani kwenye mji wa Meru nchini Kenya ambapo Mwanamke huyo alikua anadai jamaa kamkana, japo anasisitiza kwamba ni mume wake na ndio baba wa watoto mapacha akiwemo mmoja alienae mgongoni, Mwanaume alikataa kabisa na kusema hata watoto sio wake.


Taarifa ambayo imerushwa na KTN Kenya, ni kwamba alichotaka Mwanamke ni Mwanaume huyo akubali tu kwamba ni mume wake na pia ndio baba watoto wa mapacha hao… lakini Mwanaume aliapa kabisa kwamba hausiki kwenye upande wowote, hicho ndio kilichompa hasira Mwanamke na kuanza kumpiga na baadae pia kusaidiwa kupiga na Mwanamke aliekua nae.

Kenya imekua kwenye mfululizo wa kesi za Wanawake kupiga waume zao nyumbani na hadharani pale wanapokosana ambapo February 2012 Umoja wa Wanaume Kenya ulitangaza kususia kula majumbani kwa wiki moja na kununua chakula hotelini mpaka Serikali itakapoingilia usawa wa Wanaume na kuhakikisha tabia ya Wanawake kupiga Waume zao inamalizwa.

WEMA SEPETU ASAKWA NA POLISI KWA KOSA LA KUMSHAMBULIA MENEJA WA HOTELI



DIVA wa filamu za Bongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu anasakwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe, Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hotelini, kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga makofi meneja wa hoteli hiyo, Godluck Kuyumbu. Songombingo hilo lilijiri saa tano usiku wa Jumatano iliyopita kwenye hoteli hiyo  iliyopo Kawe Beach, jijini Dar. 

Akizungumza na mwandishi wetu , meneja huyo alisema siku ya tukio majira ya saa nane mchana, Wema alifika kwenye mgahawa wa hoteli hiyo akiwa ameongozana na marafiki zake wapatao kumi.

Meneja huyo akaendelea kusema, ilipofika  saa tano usiku, Wema na marafiki zake  walionekana kuzidiwa na kilevi, wakaanza kufanya fujo kwa kupiga kelele, kitendo kilichowakera wateja waliokuwa katika mgahawa huo, wengi wakiwa ni Wazungu ambao waliondoka kutokana na fujo hizo. 


Aliongeza kuwa mmoja wa marafiki wa Wema ambaye ilidaiwa ni mpenzi wake, aliyejulikana kwa jina moja la D, alichukua glasi na kuipasua chini kwa makusudi huku meneja huyo akishuhudia.


Meneja akasema: Wakati wanaondoka, nilimfuata yule jamaa mpaka nje, nikamuuliza ni kwa nini amevunja glasi kwa makusudi, akanijibu kwa dharau huku akinitukana na kutishia kunipiga, akawa ananiuliza hiyo glasi ni shilingi ngapi kwani ?.
 
Aliongeza kuwa swali lake kwa kijana huyo lilionesha kumkera sana Wema, kwani alitoka kwenye gari na kuanza kumlamba vibao visivyo na idadi meneja huyo huku akimpa maelekezo kwamba akashitaki popote na hawezi kufanywa kitu kwani yeye ana nguvu kwenye nchi hii.


“Niliamua kupiga simu Kituo cha Polisi Kawe, wakaja kuangalia mazingira kisha nikaondoka nao kwenda kufungua kesi kituoni.”
 
Faili la kesi hiyo linasomeka KW/RB5988/2013, SHAMBULIO.

AGNESS MASOGANGE AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA AFRIKA KUSINI

 
HATIMAYE  wale Wanawake wawili walionaswa  na  madawa ya  kulevya  Afrika  kusini wametambuliwa kuwa  ni  mabinti  wa  KITANZANIA .. 

Mabinti  hao  wanadaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Akizungumza na mwandishi wetu  jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.
Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald (MASOGANGE)  ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.
Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.
Jumapili iliyopita mtandao huu  ulipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.
Taarifa hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.
Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.

Baada ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao walikabidhiwa polisi. Tukio hilo linatoka takribani wiki moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni 28, mwaka huu kutangaza kuwa tatizo la dawa za kulenya hivi sasa ni janga la kitaifa nchini.
Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.
Pia alisema katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na hivyo kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.
Pinda alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.
Alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya.

Alisema vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani. 

WATOTO WAWILI WALIOKUWA WAMEPELEKWA "JANDONI" WAMEFARIKI WA AJALI YA MOTO HUKO LINDI


 Lindi- Watoto wawili wamekufa na mmoja wao kunusurika mauti, baada ya kuungua kwa moto uliosababishwa na kibatari kilichounguza nyasi za kijumba walichokuwemo.

Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Lindi, Renata Mzinga amesema ajali hiyo ilitokea mwishoni mwa wiki jana katika


mtaa wa Mitwero, katika kata ya Rasbura ya Manispaa ya Lindi na kuwataja waliokufa kuwa ni Maliki Kasimu (7) na na Selemani Fadhili (5) wakati aliyenusurika ni Juma Abdallah.

Mzinga amesema watoto hao watatu waliofika kwa mzee mmoja wa jadi, walikuwa wakijenga nyumba kwenye michezo yao wakati wakiwasubiri wenzao wafike siku za usoni, tayari kwa shughuli ya jando.

Siku ya tukio, moto huo ulishika nyasi zilizokuwa ndani ya shimo na kuwaka na kuwachoma Maliki na Selemani ambapo mwenzao, Juma alifanikiwa kukimbia na kujiokoa.

Wanakijiji wanasema mwangalizi wa jando hilo alikuwa mbali na eneo la tukio na hivyo kushindwa kuwaokoa

WANAFUNZI WAAMUA KUKESHA BAA WAKINYWA POMBE MARA BAADA YA WALIMU KUGOMA

POLISI wa Kenya wamewakamata zaidi ya wanafunzi elfu moja baada ya kupatikana wakiwa walevi mjini Nairobi wikendi hii. Polisi waliendesha msako katika baa anuai na vilabu vya burudani baada ya kupokea malalamishi kwamba watoto wa shule wamekua wakifurika kwenye burudika tangu mgomo wa walimu uanze.

Taarifa zinasema kwa sasa wanafunzi wengi hawako shuleni baada ya waalimu wa Kenya kugoma wakitaka Serikali kuwalipa marupurupu yao kutokana na ahadi iliyotolewa kwao na Serikali mapema miaka ya themanini. Mgomo huo umeingia wiki ya tatu sasa hali iliyofanya wanafunzi kukosa cha kufanya na hivyo kuanza kwenda kwenye vilabu vya burudani nyakati za usiku. Katika kuzima tabia hii polisi mjini Nairobi mwishoni mwa wiki walifanya msako mkali katika mabaa na sehemu za burudani na kuwanasa watoto zaidi ya 1,000. Polisi walianza kuwa na wasiwasI wakati visa vya unyang’anyi vilipoongezeka katika mji mikubwa nchini Kenya
. Wasiwasi ulizidi wakati walalamikaji walipokuwa wakidai kuwa wanaowapora na kuwapiga kabari ni kundi la watoto wanaodhaniwa kuwa ni wa shule. 

Na mabaa na maeneo ya burudani ilipoanza kufurika polisi wakaona ni wakati muafaka wa kuchukua hatua. Polisi sasa wametoa onyo kwa wenye mabaa nchini kenya kuheshimu sheria za biashara. Baada ya wanafunzi kukosa kurudi nyumbani na wengine kuripotiwa kutoroka katika shule zao za mabweni wazazi walifurika katika vituo mbali mbali vya polisi kujua hatma ya watoto wao.
Lakini wengi wa wazazi waliokuwa wamefurika katika kituo cha polisi cha Central jijini Nairobi walielekeza lawama zao kwa mgomo wa sasa wa walimu unaoendelea. Polisi wanasema mtindo huu mpya wa watoto kutoroka madarasani na kuvamia maeneo ya burudani na ma baa sio tatizo la Nairobi pekee bali limeenea katika miji mingi ya Kenya.
Na kabla mambo hayaja haribika zaidi wazazi wanamtaka rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuingilia kati mgomu huo wa walimu kuhusu mishahara na marupurupu mbalimbali.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger