Wadau nipo njia panda naombeni ushauri wenu, nimefanya kosa kubwa na nalijutia
Tafadhali naomba ushauri badala ya kunituhumu
Mwezi nilikuta na demu mmoja tulisoma
naye chuo kitambo alikuwa demu wangu for time being, so baada ya miaka
kadhaa tukaja kukuta sehemu, shetani akanipitia nikavunja amri ya sita
naye
Baada ya kurudi home nikagundua sina pete, nikajaribu kukumbuka nilipoiweka sikupata majibu
Baada ya siku kadhaa yule demu akzidi
kunisumbua na kutaka niwe karibu naye sana lakini nikaona si vyema maana
anaweza kusababisha mtafaruku kwa ndoa yangu
Baada ya kuona nampotezea akaniambia
sasa unajifanya mjanja pete yako ni nayo na nahitaji sh 500,000 cash ama
sivyo naharibu kwa mkeo kwamba pete ninayo na ulinikopa.
Kibaya zaidi wife aliniuliza pete
umepeleka wapi nikadanganya nimeisahau ofisini nilikuwa nafungua printer
sasa pete ikawa inani disturb nikaivua , nilipoenda jumatatu
nikamwambia nahisi wahudumu wa usafi wameiiba maana siiona pale
nimeiweka naendelea na uchunguzi.
Mwanzo nilimpuuzia lakini mshenzi yule
kapeleleza hadi wife anapofanya kazi na kapata simu yake, juzi kampigia
kamwambia "naomba mkumbushie mumeo deni langu mimi xxxxx nampigia
simpati" halafu akakata simu.
Niliporudi wife kanibana nikamwambia ni
mambo ya kazi tu akataka kujua no yake kaipataje, nikazuga zuga na ubabe
wa kiume yakaisha
Nikipiga akili nimuendee Polisi naona kama kitanuka na wife atajua
Nikifikiria kumlipa akili hainipi kabisa....kilo tano?
Sijui nimueleze wife ukweli?
Nimejaribu kumpiia simu na kumbembeleza kagoma anachohitaji ni kilo tano au aniharibie kwa wife
Tafadhali ushauri wakuu lawama na madongo hayatanisaidia