Oooh! Nooh! Wakati akimpa mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ gari la
Sh. milioni 38 huku akitawanya mamilioni ya fedha kwenye matukio
mbalimbali, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
anadaiwa kunyemelewa na laana kufuatia baba yake, Abdul Jumaa kuugua na
kuvimba miguu bila msaada wowote.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa, baba wa staa huyo anayeishi
Magomeni-Kagera jijini Dar, amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvimba
miguu na hakuna msaada wowote anaoupata kwani chanzo cha mapato
anachokitegemea ni kodi tu ya nyumba ambayo anaipata kutoka kwa
wapangaji wachache alionao.
BOFYA HAPA KUKISIKIA CHANZO
“Yaani tunashangaa
kusikia Diamond ana fedha nyingi, juzikati tuliona katika gazeti
kamnunulia mama yake gari la milioni 38 (Toyota Lexus-Harrier) sasa kwa
nini asimthamini baba yake hata kidogo?
“Ukweli ni kwamba baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba.
“Amekuwa akilalamika mara kwa mara lakini Diamond hatujawahi
kumuona,” kilinyetisha chanzo hicho na kuongeza:“Juzikati hapa baba
Diamond alishikika kwelikweli miguu, akaugulia mwenyewe ndani pasipo
kuwa na msaada wowote tena nasikia mzee huyo hataki hata kuongelea
lolote kuhusu Diamond maana haoni umuhimu wa kufanya hivyo wakati
amemsusa muda mrefu sana.”
MATIBABU HAYAZIDI MILIONI
Katika aya nyingine,
chanzo hicho kilidai kwamba ugonjwa wa miguu ambao unamsumbua mzazi
huyo, gharama za matibabu haziwezi kufikia hata shilingi milioni moja za
madafu achilia mbali mamilioni anayoyatapanya staa huyo.
“Ingekuwa tatizo kubwa sana, hapo sawa, kwa sababu miguu huwa
inamvimba lakini akipata dawa za kutumia huwa inarudi katika hali ya
kawaida, kwa nini lakini anamfanyia hivyo baba yake? Amemkosea nini?”
Kilihoji chanzo hicho.
UTAJIRI WAKE WAANIKWA
Wakati chanzo hicho
kikiweka nukta hapo kwa muda, mapaparazi wetu walipewa malalamiko
mengine kutoka kwa jirani mmoja wa baba Diamond ambaye alimsihi amsaidie
mzazi wake kwani anaamini uwezo anao kupitia kumbukumbu ambazo Diamond
mwenyewe alizithibitisha kupitia vipindi mbalimbali vya runingani kama
Take One na Spora Show vya CloudsTV.
Pia kwenye vyombo vingine vya habari zikiwemo redio na magazeti pendwa ya Global Publishers.
Jirani huyo alidai kwamba mwaka jana Diamond alitangaza kuwa ana
utajiri wa Sh. bilioni moja ikiaminika kwamba mwaka huu umeongezeka mara
dufu.
“Nakumbuka mwaka jana kupitia Kipindi cha Spora Show na kile cha Take
One, Diamond alikiri kuwa ana mkwanja usiopungua bilioni moja, hiyo
ilikuwa kwa mwaka jana, sasa mwaka huu unadhani atakuwa na shilingi
ngapi? Aache hizo bwana, amsaidie baba yake hata kwa kumpa mtaji mdogo
wa biashara ambao unaweza kumsaidia,” alisema jirani huyo.
MATANUZI YA DIAMOND, WEMA
Katika kuendelea
kuichimba habari hiyo, mapaparazi wetu walinasa malalamiko kutoka kwa
jirani mwingine wa mzazi huyo ambaye alieleza masikitiko yake kwa
kulinganisha starehe ambazo staa huyo anazifanya na asali wake wa moyo,
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na maisha halisi ya baba yake.
“Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa habari za mastaa, naona kila siku
kwenye vyombo vya habari jinsi gani Wema na Diamond wanavyotumia fedha
nyingi katika masuala ambayo hayana ulazima kiivyo.
“Sisi kama
majirani hatupendezwi na hali hii, angekuwa anakuja angalau siku
mojamoja kumuona baba yake kuliko kila siku kumhudumia mama yake pekee,”
alisema jirani huyo.
TATIZO NI NINI?
Mapaparazi wetu waliingia
mzigoni kusaka kiini halisi kwa nini Diamond amwage fedha nyingi kwa
mama yake pasipo kumkumbuka japo kiduchu baba yake ambapo ilielezwa kuwa
staa huyo wa Mdogomdogo hakuwa na ugomvi wowote na mzazi wake huyo.
“Kama ni ugomvi ulikuwepo kati ya mama na baba lakini Diamond
hahusiki, tunashangaa kuona kama staa huyo naye anaweza kumsusia baba
yake,” kilieleza chanzo na kuongeza:
“Mbaya zaidi nasikia Diamond amekuwa mzito kupokea simu za baba yake,
sasa huoni kama siyo jambo la busara, mzazi ni mzazi tu hata iweje. Kwa
mtazamo wangu kinachofuata ni laana.
“Kuna mifano ya watu wengi ambao waliingia kwenye laana za wazazi wao
na wakajikuta kama siyo kufulia kama (wanatajwa mastaa waliofulia wa
muziki Bongo) au hata kukutwa na umauti.
“Jambo hili si la
kibinadamu tu, kwa wale wanaosoma vitabu vitakatifu watakuwa na mifano
mingi ya watu waliowakosea wazazi wao wakalaaniwa.”
BABA DIAMOND ANASIKITISHA
Ijumaa lilipomtafuta
baba Diamond kwa njia ya simu aliongea maneno ya kusikitisha huku
akikataa katakata kumzungumzia kijana wake huyo.
“Jamani naomba mumuache Diamond na maisha yake, sitaki kabisa kusikia
habari zake maana hata nikiongea naonekana najipendekeza kwake.
“Namshukuru Mungu, kama ni kuumwa kwa sasa naendelea vizuri na maisha yangu, niacheni nipumzike,” alisema mzee huyo kwa unyonge.
DIAMOND ANASEMAJE?
Alipotafutwa Diamond ili
kumsikia anazungumziaje madai hayo, simu yake iliita bila kupokelewa.
Tunaamini atasoma habari hii hivyo si vibaya akatutafuta ili afunguke
kwa upande wake.
MAONI YA MHARIRI
Diamond ni staa mkubwa kwa sasa
ndani na nje ya Bongo, uwezo alionao kifedha unapaswa kuendana na
baraka za wazazi wa pande zote mbili. Vitabu vya Mungu vinatufundisha
kwamba wazazi ndiyo Miungu wetu hapa duniani hivyo hata kama kuna kosa
amefanya, mzazi atabaki kuwa mzazi tu. Hatutakiwi kumkosoa!
Showing posts with label WASANII. Show all posts
Showing posts with label WASANII. Show all posts
STEVE NYERERE AWAFUNGUKIA WANAOMZUSHIA KUWA YEYE NI SHOGA

Mwenyekiti wa bongo movie Unity, Steve Nyerere amechukizwa na watu wanaotumia mitandao vibaya na kwa kumzushia kuwa ni shoga.
Steve Nyerere kupitia akaunti yake ya facebook ameandika:
Napenda kuchukua fursa hii kuongea
machache na kama mtaboa mtu naomba samahani najua binadamu tumezaliwa
tofauti sana kuna wale wanaogopa zambi na kunawale wanopenda zambi mimi
daima nasema izo ni changamoto tuuu ok nimepata taarifa umu umu kwenye
mitandao yetu ya kijamiii hususani huuu kwamba kuna binti anaitwa zainab
ananichafua na kuniandika mambo ambayo ayana tija kwangu.
Nazani ata kwake kwamba mimi shoga
anauhakika hahahahaha nimecheka sana kupata izi taarifa nataka kuwapa
taarifa ndugu zangu kuna msemo unasema mti wenye matunda ndio unaopigwa
mawe na mkanya mara moja aache mara moja kwani naimani anapoteza muda tu
habari hizo si zakweli kabisa ila namtakia laheli kwahili jambo
analonitendea mimi nasema namwachia mola akumbuke nafamily mke na watoto
mama dada zangu kiukweli najisikia vibaya sana mi nasema asante”.
Baada ya kuandika kauli hiyo, Steve Nyerere ameuambia mtandao wa bongo5 kuwa kuna watu wameamua kumchufua baada ya kujionyesha wazi kwenye siasa.
“Watu wananitumia meseji mbaya, eti mimi nimetumwa na viongozi, mara sijui mimi ni shoga, jamani hakuna mambo kama hayo, nawataka watanzania wajue hayo ni mambo za uzushi, sijui ata yametoka wapi” Alisema Steve Nyerere
JACKLINE WOLPER AFUNGUKA YOTE KUHUSU YEYE NA NEY WAMITEGO SOMA HAPA KUJUA ALICHOSEMA PATA STORI HAPA
FLORA MBASHA NA MUMEWE BADO NDOA YAO IPO KATIKA VURUGU KUBWA
Imebainika
kwamba waimbaji wa muziki wa Injili nchini, Flora Mbasha na
mumewe, Emmanuel Mbasha hawajapatana kama ilivyodaiwa awali na
taarifa zinasema kuwa mwanadada huyo ameanza maisha yake
kivyake kwa kupanga nyumba nyingine mbali na mumewe….
Habari
za kuaminika toka ndani ya familia ya Flora zinasema kuwa
msanii huyo amekuwa na wakati mgumu wa kumsamehe mumewe
kutokana na tabia zake chafu ambazo zimekuwa zikiutesa moyo
wake na sasa anang’ang’ania kumchukua mwanaye…..
“Hivi
karibuni iliripotiwa kuwa wanandoa hao wamepatana lakini ukweli
ni kwamba hakuna kitu kama hicho,mwanamke amepanga chumba chake
hapa Dar es Salaam na kumwachia kila kitu mumewe ambaye sasa
ana haha kumchukua mwanaye ili aishi naye,” kilisema chanzo cha habari.
Lakini
upande wa pili, mume wa msanii huyo hivi karibuni alieleza
kuwa ugomvi baina yao ulianza kutokana na kuchepuka kwa mkewe,
huku akipeleka shutuma kwa mchungaji wa kanisa la ufufuo na
Uzima, Josephat Gwajima ambaye ni maarufu kwa vitu ambavyo ni
tofauti na huduma zake….
Emmanuel
Mbasha tayari alishatoa waraka wa wazi kwenda kwa mchungaji
huyo, akimtaka kukaa mbali na ndoa yake jambo ambalo bado
halina mrejesho chanya kwani wawili hao Flora na Gwajima
wameendelea kufanya kazi pamoja kitu kinachopelekea Emmanuel
kuona bado kuna kitu kinaendelea kati yao….
Kutokana
na hali hiyo, mume wa Flora amekuwa mgumu kumtoa mtoto wake
akihofia kulelewa na mtu ambaye kwake anamchukulia kama adui
wa familia yake…
“Imekuwa
ngumu sana kwa Emmanuel kumwachia mtoto wake katika hali hii,
hata kama ni wewe unamuachiaje mtoto wako kipenzi aende kwa
mwanamke ambaye ni msaliti,” alisema ndugu wa karibu wa
Emmanuel Mbasha
MARTIN KADINDA AFUNGUA NA KUELEZA UKWELI KAMA YEYE NI SHOGA AU LA, TWENDE PAMOJA HAPA
Mbunifu
wa mavazi nchini, Martin Kadinda amesema kuwa amekuwa akikutana na
changamoto kutoka kwa wanaume wengi wanaodhani kuwa yeye ni shoga na
kufikia hatua ya kumtumia ujumbe wa kumtaka kimapenzi.
“Kila mtu anakuwa na maswali yake anaya-raise kutokana na anacho kifikiria katika akili yake, Watanzania tunatabia ya ku-create situation katika akili zetu halafu we want everybody to accept.Kwamba mtu tu anaamka asubuhi may be ana matamanio na wewe anaanza ku-raise hilo swali aone jibu litakuwa ni nini. Wapo wengi (wananitamani) wako hivyo, facebook, Instagram mtu atakutumia namba yake, hakwambii lakini unaona kabisa huyu, nakukubali sana I wish siku moja uje nyumbani kwangu au can I come to your place, mimi sitakagi hata kwenda huko najua nitajiuliza imekuaje mpaka imefikia hivi, basi nasema sawa. Kwa sababu mimi facebook nakuwa mkweli sijawahi kujibu mtu tangu 2012, I have a person huwa anazipitia, akiulizia mtu maswala modelling mpe namba ya fulani, mambo mengine binafsi usiwajibu achana nao, kwa sababu mara ya kwanza nilikuwa ninadhani I should meet these people talk to them this is not right but nikaona unapoanza kuwa unajihusisha ndipo unapojikuta unaanza kuingia bila kujua” Martin Kadinda aliambia Sporah Show.
Pia Martin amesema kuwa ana mpenzi wake ambaye hapendi kumuweka wazi ili kulinda heshima yake.
“Ukishakuwa maarufu na mtu wa karibu yako atakuwa maarufu, she’s not already kwa hiyo kitu yakuingia kwenye hiyo cycle kila siku wanamuona kwenye magazeti kwenye Instagram haiko hivyo. Ndiyo maana hata nikiweka picha yake Instagram nitaweka picha yake moja kwa miezi sita, yupo hata ukitaka kumuona kwenye Instagram yangu yupo, first lady wa martin huyu, lakini cycle yake na maisha yake siyo mtu wa kukaa kwenye media nadhani ni kwa sababu ya future ya kazi atayokuja kuifanya kwaiyo anajitaidi kuwa pembeni… Mara ya kwanza alishawahi kuniuliza alipita kwenye comment za watu kwenye blog fulani akasoma, akaniambia najua hii ni Watanzania walivyo, as long nakutambua mwanaume wangu ni mtu wa namna gani I don’t care about these people” Alimaliza Martin
HAPPYNESS MAGESE ANAHALI MBAYA SANA, SASA AKOJOA KWA KUTUMIA MIPIRA
Happiness
Magese anasihi wanawake kucheki afya zao mara kwa mara wasije wakakutwa
na tatizo kama lake la ugumba ambalo limeharibu na kibofu chake na
kupelekea hata kushindwa kukojoa kwa njia ya kawaida na badala yake
anatumia mipira, ni vema kuchek afya mara kwa mara.
HII NDIO HEKAHEKA INAYOMHUSU MAMA WA DIAMOND PLATNUMZ
JAMAA ANAVYOMFAIDI WEMA, LAITI KAMA DIAMOND ANGEMFUMA... MMMH SIJUI INGEKUWAJE
Wema Sepetu na Kajala wakibadilishana mawazo huku burudani ya Skylight Band ikiendelea.
Benny Kinyaiya, William Malecela na Wema Sepetu.
Pichani juu na chini ni Wema Sepetu akimpagawisha Sam Mapenzi wa Skylight Band
Sam Mapenzi akimwimbia Wema Sepetu ndani kiota cha Thai Village kilichopo Masaki jijini Dar Juma lililopita.
Maimatha
wa Jesse akishow love na marafiki alipotinga kwenye kiota cha Thai
Village kuanza week end yake na burudani za Skylight Band
RAY C APIGWA VIBAYA NA CHID BENZI
evu! Rapa
mwenye ‘swagger’ za Ja-Rule Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’, anadaiwa
kukwaa kisanga kingine kibaya baada ya kukurupuka kutoka nyumbani kwake
na kwenda kumvamia staa mwenzake, Rehema Chalamila ‘Ray C’ nyumbani
kwake anapoishi na kumtwanga makonde ikiwa ni siku chache tangu jamaa
huyo apate msala mwigine wa aina hiyo.
TUJIUNGE NYUMBANI KWA RAY C
Ilidaiwa kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita nyumbani kwa Ray C, Changanyikeni jijini Dar es Salaam ambapo ilisemekana kwamba Chid Benz alimvamia mishale ya saa 4:00 usiku kwa gia ya kumsaka mzazi mwenzake aliyemtaja kwa jina moja la Mariam.

CHID BENZ ATAKA KUMUONA MWANAYE
Ilidaiwa kwamba Chid Benz alisema kuwa alizungumza na mpenziye huyo kwamba alitaka kwenda kumuona mwanaye ambapo Mariam alimjibu kwamba kwa muda huo alikuwa nyumbani kwa Ray C Changanyikeni.
Ilidaiwa kwamba Chid Benz alisema kuwa alizungumza na mpenziye huyo kwamba alitaka kwenda kumuona mwanaye ambapo Mariam alimjibu kwamba kwa muda huo alikuwa nyumbani kwa Ray C Changanyikeni.
UNGA WATAJWA
Sosi wetu alidai kwamba baada ya kujibiwa hivyo, Chid Benz alianza kulalama na kumwambia anamfuata palepale kwa nini usiku ule alale kwa Ray C, wakati ana uwezo wa kwenda nyumbani au amekwenda kwa staa huyo ili kunywa dawa zao za kuondoa sumu ya madawa ya kulevya ‘unga’, jambo ambalo jamaa huyo siku zote huwa hataki hata kulisikia masikioni mwake.

CHID BENZ AWAVAMIA
“Huwezi kuamini baada ya muda kama wa saa moja, Ray C na Mariam wakiwa ndani wakitazama TV, ghafla mlango ulisukumwa kwa nguvu kisha akaingia Chid Benz na kumdaka Mariam na kuanza kumshushia kipigo.“Yaani huo mshtuko walioupata walidhani wamevamiwa na Al-Shabaab.

KIBAO CHAMGEUKIA RAY C
“Mungu mkubwa kwa sababu Mariam alifanikiwa kuchoropoka na kukimbilia chumbani ndipo kibao kikamgeukia Ray C.
“Mungu mkubwa kwa sababu Mariam alifanikiwa kuchoropoka na kukimbilia chumbani ndipo kibao kikamgeukia Ray C.
“Ray C akiwa anashangaa ghafla naye alipokea kipigo kikali kutoka kwa Chid na kumsababishia majeraha mbalimbali mwilini.
RAY C AKIMBILIA KWA MAJIRANI
“Baada ya kuona maji yanazidi unga, Ray C alitafuta upenyo na kukimbilia kwa majirani huku akipiga kelele za kuvamiwa, mara moja majirani waliambatana naye mpaka nyumbani kwake.
“Walipofika Chid Benz alikuwa ametumia staili za kininja kwa kuruka geti na kutokomea kusikojulikana huku akiwaacha Ray C na Mariam wakiangua vilio kwa kipigo kikali walichopokea.

RAY C AVUJA DAMU
“Ray C aliumia mkono na mguu ambao ulionekana ukivuja damu. Mariam alikuwa akililia mbavu zake kuchakazwa kwa makonde mazito na upande mwingine baadhi ya vyombo vya ndani vikionekana kuvunjwa na vingine kusambaratishwa kufuatia tafrani iliyozuka muda mfupi baada ya Chid Benz kutia maguu nyumbani hapo,” chanzo kilishusha madai hayo mazito.

RAY C ATIRIRIKA SAKATA LILIVYOKUWA
Akizungumzia na gazeti hili Alhamisi iliyopita juu ya sakata hilo, Ray C alisimulia mkasa mzima: “Kweli Chid Benz alikuja nyumbani kwangu na kunivamia.
Akizungumzia na gazeti hili Alhamisi iliyopita juu ya sakata hilo, Ray C alisimulia mkasa mzima: “Kweli Chid Benz alikuja nyumbani kwangu na kunivamia.
“Alinipiga vibaya sana na kuvunja baadhi ya vitu vya ndani kwangu, jambo
ambalo lilinishangaza zaidi ni namna alivyopafahamu nyumbani kwangu
hadi kuja kunifanyia fujo nikiwa na mzazi mwenzake, Mariam ambaye
nilitoka naye ofisini kwangu.
“Ujue jana (Jumatano) tulikuwa na kazi sana ofisini kwangu mimi na
Mariam, sasa kutokana na kubanwa na kazi kweli muda ulienda sana hivyo
nikamwambia Mariam akalale kwangu.
“Kwa kuwa muda ule ilikuwa ngumu kwenda kwao Mbezi Beach, Mariam alikubali na tulikwenda wote nyumbani kwangu.
“Kwa kuwa muda ule ilikuwa ngumu kwenda kwao Mbezi Beach, Mariam alikubali na tulikwenda wote nyumbani kwangu.
“Huko nyuma Mariam alikuwa mwathirika wa madawa ya kulevya lakini baada
ya kusikia mimi nimeacha, naye aliachana nayo na kuanza kutumia dawa za
kuondoa sumu.
“Tumeendelea kutumia naye dawa na sasa ameshapona kabisa hivyo kuna
baadhi ya kazi nimekuwa nikimshirikisha kunisaidia kwenye ofisi yangu.
Pia alishawahi kumshawishi Chid Benz ili aje kutumia dawa lakini jamaa
alikataa na kumfanyia vurugu sana huku akimkataza kuwa na mimi kwa madai
mimi ndiyo namfanya amwambie kuachana na utumiaji dawa za kulevya.
“Sasa jana alipojua hivyo nadhani Chid Benz alikuja kutimiza dhamira yake ambayo siku nyingi alikuwa akiahidi kunipiga.”
SOO LIPO POLISI
Ray C alisema baada ya tukio hilo alikwenda kuripoti kwenye Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Kinondoni na kufunguliwa jalada la kesi ambapo Chid Benz anasakwa na polisi.
Ray C alisema baada ya tukio hilo alikwenda kuripoti kwenye Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Kinondoni na kufunguliwa jalada la kesi ambapo Chid Benz anasakwa na polisi.
Juhudi za kumpata Chid Benz hazikuzaa matunda kwani simu yake haikuwa
hewani hivyo jitihada zinaendelea na kama ana ufafanuzi au utetezi
anaweza kutupigia.
CHID BENZ NI TATIZO?
Chid Benz anadaiwa kuwa ni tatizo kwani tukio hilo la Ray C amelifanya wakati akiwa na tukio la pili kwa wanawake kwani kwenye Mahakama ya Mwanzo, Ilala ana kesi mbichi aliyoshitakiwa kwa kosa la kumpiga mrembo aitwaye Mwanaisha.

Mbali matukio hayo pia Chid Benz ana rekodi ya kukorofishana na wasanii wenzake kama Kalapina na marehemu Ngwea.
KWELI JINI KABULA NI MALAYA WAKUTUPWA, ANGALIA USHENZI ALIOSEMA KUHUSU MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI NA VIMINI VYAKE
STAA wa sinema za Kibongo, Miriam Mjolwa ‘Jini
Kabula’ amecharuka baada ya kukosolewa juu ya mavazi ya mitego, vimini,
anayovaa ndani ya mwezi wa Ramadhani.
Baada ya majirani wanaofunga kufikisha malalamiko, paparazi wetu alimvutia waya Jini Kabula na kumsomea mashtaka hayo ambapo alisema kuwa alikuwa lokesheni siku waliyomuona lakini pia hahofii sana kwani mwezi huo haumuhusu.
“Hao wanaweka chumvi tu mimi sikuwepo huko mtaani nilikuwa lokesheni tangu mwezi uanze, na hata kama nitavaa nguo za ajabu, mwezi huu haunihusu nitavaa vyovyote nipendavyo,” alisema Jini Kabula.

KAJALA: WEMA NI MNAFIKI NA PIA NI KIGEUGEU
Akizungumza kwa kujiamini mbele ya waandishi wetu, juzi Jumatano pande wa Mikocheni jijini Dar es Salaam, Kajala alisema: “Wema ni mnafiki kabisa. Upatanisho wetu ni wa uongo. Mimi moyoni nimeondoa kinyongo lakini mwenzangu naona kama bado ana donge moyoni.”
Kajala alisema hayo alipoulizwa na Risasi Jumamosi, sababu ya kutoonekana kwenye tukio la futari lililofanyika nyumbani kwa mama mzazi wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ambaye ni mkwe wa shosti wake huyo.
Katika tukio hilo, mama Diamond alifanyiwa sapraizi ya nguvu alipokabidhiwa gari kali aina ya Toyota Lexus Harrier kama zawadi ya bethidei yake, ambayo ilitolewa na meneja wa Diamond, Babu Tale kwa niaba ya mwanamuziki huyo ambaye alikuwa safarini nchini Marekani.
“Tunakubaliana kuwa kitu kimoja lakini mwenzangu anaonekana ana kinyongo. Hebu angalia, anawezaje kuacha kunialika kwenye shughuli muhimu kama ile kama kweli tumepatana? Mbona amealika watu wengi lakini mimi ameniacha? Wema aache unafiki bwana.
“Mbaya zaidi, hivi juzi tu ameweka picha ya msichana mmoja anayekaa China, huyu mdada anaitwa Sabrina, niliwahi kugomabana naye, lakini yeye amemuweka Instagram na kumwandikia maneno kibao ya kumsifia akim-wish happy birthday, hapo si kama ananisimanga? Wema si mkweli,” alisema Kajala.
Akizungumzia ishu hiyo, siku ya tukio Wema alisema: “Ukiniuliza kuhusu Kajala kutokuwepo hapa, kwa kweli utakuwa kama unanichanganya tu maana leo sijashika simu muda mrefu sana.
“Hata ujio wangu hapa nilikurupushwa, ndiyo maana sijakumbuka kumuita Kajala, lakini tuko vizuri na mara ya mwisho tumeongea jana (Jumapili) usiku tu,” alisema Wema.
MZIMU WA RECHO WAZIDI KUWATESA WASANII, SSA NI ZAMU YA SAGUDA
WAKATI Arobaini ikitarajia kufanyika jana, mchumba wa marehemu Sheila Haule ‘Recho’, George Saguda ameeleza kuwa bado aliyekuwa mchumba wake huyo anamtesa kwa kumtokea mara kwa mara.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Saguda alisema marehemu amekuwa akimtokea akiwa usingizini na kumsisitiza kuhusu kazi.“Najitahidi sana kuondoa mawazo juu yake lakini bado ananitokea, sijui hali hii itaisha lini,” alisema Saguda.
Recho kabla hajapatwa na umauti, walizalisha filamu mbili katika kampuni yao ya Sara Entertainment ambazo ni Vanessa na Fedheha ambayo imetoka hivi karibuni.
MFUNGO WAMBADILI JOHARI MAVAZI, MWEZI HUU HAVAI TENA VIMINI
MWIGIZAJI wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’
amesema amewaunga mkono Waislamu kwa kuvaa mavazi ya kujistiri na
kuziba sehemu kubwa ya mwili kuheshimu mwezi wa Ramadhani.
Akipiga stori mbili tatu na paparazi wetu, Johari alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu dini zote ni za Mungu na kwa kuwa ni kipindi cha Ramadhani, amebadilika kwa kila kitu.
“Kipindi hiki ni cha kumrudia Mungu, nimeacha kila kitu kibaya kwa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na nimeamua kutulia ili nipate muda mwingi wa kuomba,” alisema Johari.

DIAMOND NI MWIZI, KANIIBIA WIMBO WANGU, HAYA NI MAENO YA WABABA
Malalamiko
ya wasanii kuibiana au kupigana kanzu kwenye kazi zao yaliripotiwa sana
mwaka jana na mwaka huu mambo yalikuwa shwari, lakini baada ya kuvuka
nusu ya mwaka yameibuka tena.
Mshiriki wa shindano la kuimba la Bongo Star Search (BSS) , Wababa amewatuhumu maswaiba wa ‘Muziki Gani’ Nay wa Mitego na Diamond Platinumz kwa kumuibia kazi zake kwa wakati tofauti.
Akiongea kupitia Friday Night Live ya East Africa TV, Wababa amesema Diamond amemuibia wimbo wake ambao alikua anaiita ‘Kitorondo’ na kwamba aliibadilisha jina baadae.
“Kiukweli kuhusu Diamond, mimi mwenyewe nimetumiwa hiyo ngoma ambayo ameitoa, nimeiskiliza jinsi ilivyo kuanzia idea, mwendo, style ambazo anafanya. Ambayo ameibadilisha jina tu baada ya ya kwamba ilikuwa mitandaoni nilikuwa nimemfatilia ilikuwa inaitwa Kitorondo mwezi mmoja kama uliopita. Kwa hiyo nilishindwa kulalamika kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa analalamika kuwa imevuja. Kwa hiyo sikuona sababu ya kuongea kitu kwa sababu haikuwa official. Kwa hiyo sikuwa na sababu ya kucomplaini kwa sababu haikuwa official, lakini mpaka jana ina maana ilikuwa serious kama biashara.” Ameeleza Wababa. Wababa
Alipoulizwa ni wapi ambapo Diamond aliusikia wimbo huo, amesema huo ni wimbo wake alioutoa miaka minne iliyopita akiwa na Dogo Asley na aliuweka kwenye mtandao wakati anatumia jina la Nurdi, kabla hajaanza kutumia jina la Wababa aliposhiriki BSS. “Ni nyimbo ambayo iko mtaani na watu wengi wanaielewa. Kwa hiyo sijaelewa..” Kwa upande mwingine, Wababa amedai kuwa alifanya kazi na Nay wa Mitego katika studio za Mazoo lakini baaadae Nay alirudi studio na kuongea na Mazoo kutaka kuunua wimbo huo kwa shilingi milioni moja bila kumshirikisha Wababa.
“Hivi karibuni nimefanya ngoma mpya na Nay wa Mitego, ni ngoma ambayo ilikuwa iko paid kwake pamoja na studio. Lakini kitu cha kushangaza ni kwamba siku mbili baada ya kufanya kazi nikapigiwa simu na producer akaniambia kwamba jamaa amerudi tena kwa ajili ya kutaka kununua wimbo kwa milioni moja, auchukue wimbo aende akaufanye sehemu nyingine. Baada ya hapo hata mahusiano yangu na mshikaji yamekuwa sio mazuri. Ukimpigia simu anakwambia yuko busy kuna kazi anafanya atanicheki, hadi kufikia leo sielewi.”
Nay alipigiwa simu lakini hakuwa anapatikana kwa muda huo.

UWOYA NA MASOGANGE WANAISHI PAMOJA SOUTH, JE KUNANII?
Hili ni swala la kujiuliza...ingawa hadi sasa Uwoya hajasema chochote...Lakini Masogange kupitia ukurasa wake wa INSTAGRAM amekuwa akiweka picha kadhaa za Irene Uwoya wakiwa pamoja huko SAUZI....Sasa katika kumaliza zaidi jana ameka video Irene akiwa anapika....HEHEHEHE
SIRI YAFICHUKA, WEMA NA DIAMONDA SASA NI ......
IN THE NAME OF #INSTAGRAM
ONE
OF WEMA'S FAN COME WITH A DOUBT CONCERNING A RING WHICH SEEMED ON THE
WEMA'S COURT FINGER SO THE QUESTION COMES DOES WEMA SEPETU TAKE IT FOR
DECORATION OR NEAR TO MARRIAGE??
POWER TO YOU!!
" ONE OF WEMA'S FAN COME WITH A DOUBT CONCERNING A RING WHICH SEEMED ON THE WEMA'S COURT FINGER SO THE QUESTION COMES DOES WEMA SEPETU TAKE IT FOR DECORATION OR NEAR TO MARRIAGE?? POWER TO YOU!!
" ONE OF WEMA'S FAN COME WITH A DOUBT CONCERNING A RING WHICH SEEMED ON THE WEMA'S COURT FINGER SO THE QUESTION COMES DOES WEMA SEPETU TAKE IT FOR DECORATION OR NEAR TO MARRIAGE?? POWER TO YOU!!
WASTARA: NIMEGUNDUA WANAUME WENGI WANATAKA KUNIVUA CHUPI TU
Msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma amefunguka kuwa tangu mume wake
Juma Kilowoko ‘Sajuki’ afariki dunia, wamekuwa wakijitokeza wanaume
kibao wakitaka kumuoa lakini amegundua wengi wana nia ya kunitumia tu.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Wastara alisema kama mwanamke amekuwa akitamani kumpata mwanaume wa kumfariji lakini kinachomchanganya ni sampuli ya wanaume wanaotuma maombi kwake.
“Mpaka sasa wameshanitokea wanaume zaidi ya kumi lakini wengi wao nawaona wananitaka ili kujua nini nilichonacho na wengine wananifuata wakidhani watapata mali na si mapenzi ya dhati.
“Kimsingi wanataka tu kujua Sajuki alidata na nini kwangu, mimi siko hivyo. Siwezi kumruhusu mtu aingie kwenye maisha yangu kwa masilahi yake. Ninayemhitaji namjua moyoni na ipo siku nitampata kwani siangalii mfuko wa mtu, naangalia tabia,” alisema Wastara.

Subscribe to:
Posts (Atom)